Tanzanian Embassy in Egypt

Tanzanian Embassy in Egypt

Share

The official page of the United Republic of Tanzania embassy in Egypt.
الصفحة الرسمية ?

Now you can apply for an Online Visa to visit the United Republic of Tanzania (both Tanzania Mainland and Zanzibar) via official website as mentioned below:-

https://eservices.immigration.go.tz/visa. And To visit Tanzania you must take a COVID-19 PCR Test before arrival or departure (a test no more than 72 hours).

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 24/04/2024

RAIS WA MISRI ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA KUTIMIZA MIAKA 60 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Abdel Fattah El Sisi leo tarehe 24/04/2024 ametuma ujumbe maalum kwa kumtuma Afisa kutoka Ikulu Bw. Mohamed Mokhtar kuwasilisha salamu za pongezi za kutimiza miaka 60 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar kwenda kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Mohamed Mokhtar alipokelewa na Bw. Rashid S. Haroun (Kaimu Balozi) na Bi. Nimpha E. Marunda (Mwambata Utawala) katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri.

Nae Mhe. Rashid S. Haroun alizipokea salamu hizo kwa niaba ya Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Misri Mej. Gen. Richard M. Makanzo na kutoa shukurani kwa niaba yake.

Aidha, katika yaliyojiri wakati wa kupokea ujumbe huo ni pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza mahusiano mema na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Misri na kuzidi kuuimarisha katika nyanya zilizopo za kisiasa, kiuchumi, kibiashara, kiuwekezaji, utalii, afya,ulinzi na usalama,elimu na michezo.

Ikumbukwe kuwa tukio la Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar lina historia kubwa na muhimu kati ya Tanzania na Misri kwani katika mwaka huo wa 1964 Tanzania pia ilifungua kwa mara ya kwanza ofisi za Ubalozi nchini Misri na Balozi wa kwanza akiwa Mhe. Salim Ahmed Salim, hivyo katika maadhimisho haya Tanzania na Misri zinasherehekea miaka 60 ya ushirikiano.


Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 07/04/2024

Asanteni wanadiaspora

Kwa niaba ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Brig. Jen. Ismail Shajack Ismail (Kaimu Balozi) kwa niaba ya Mhe. Mej. Gen. Richard M. Makanzo Balozi wa JMT nchini Misri anatoa shukurani za dhati kwa Wanadiaspora wote waishio nchini Misri na raia wa mataifa mengine kwa kujitokeza kwao na kujitolea kwao katika kuishangilia na kuisapoti timu ya Simba Sc.

Asanteni sana Wanadiaspora na mashabiki wote wa soka la Tanzania.

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 06/04/2024

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania nchini Misri waiaga Timu ya Simba SC

Leo tarehe 06-04-2024 Brig. Jen. Ismail Shajack Ismail (Kaimu Balozi) pamoja na Maafisa Ubalozi walifika katika Hoteli waliyofikia Timu ya Simba Sc na kuambatana nao hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cairo kwa ajili ya kuagana.

Ikumbukwe kuwa timu ya Simba Sc ilikuwa Misri kwa ajili ya kucheza mechi ya marudiano kati yake na timu ya Al Ahly.

Brig. Jen. Ismail Shajack Ismail akimuakilisha Mhe. Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri Mej. Jen. Richard M. Makanzo aliupongeza Uongozi na timu ya Simba Sc kwa juhudi zinazofanywa na kusisitiza umoja ndani ya timu ikiwa sambamba na kutokata tamaa katika matokeo ya michezo inapokuwa ni hasi.

Mwisho aliwatakia safari njema na matokeo mazuri zaidi katika mashindano ya Kitaifa na ya Kimataifa kwa msimu ujao.


Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 04/04/2024

Ubalozi waipokea timu ya Simba Sc

Siku ya tarehe 03/04/2024 Mhe. Brig. Jen. Ismail Shajack Ismail (Kaimu Balozi) akiambatana na Maafisa wa Ubalozi walifika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo kwa ajili ya kupokea ujumbe na timu ya simba iliyofika nchini Misri kwa ajili ya kukamilisha mechi ya hatua ya Robo Fainali ya CAF Champions League kati yake na timu ya Al Ahly itakayochezwa katika uwanja wa Cairo Stadium siku ya Ijumaa tarehe 05/04/2024.

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 23/03/2024

Mhe. Balozi atatua kero za Madaktari Bingwa

Mhe. Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri tarehe 22/03/2024 alikutana na Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Vyuo mbali mbali vilivyopo Alexandria kujua maendeleo yao, kupata mrejesho wa mambo mbali mbali waliyomuomba kuwasaidia alipokutana nao Mwezi Januari, 2024.

Pia aliweza kujumuika nao pamoja katika chakula cha pamoja katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika hoteli ya Stegeinberger, iliopo Alexandria.

Nae Bw. Alihussein, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi wanaosoma Alexandria alitoa shukurani kwa Balozi na timu yake kwa ufuatiliaji mzuri wa matatizo yao baada ya kuyafikisha sehemu husika ikiwa ni pamoja na kupunguziwa ada ya masomo kutoka Dola za Marekani 1,500 hadi Dola 300.

Aidha, wamepata mrejesho wa Udhamini kupitia Dr.Samia Superspecialized Scholarship ambapo Wanafunzi waliokosa mwanzo wametakiwa kuomba tena baada ya fursa hizo kutangazwa.

Akitoa nasaha zake kwa Wanafunzi hao, Mhe. Balozi alisisitiza umoja, upendo, bidii na kusaidiana katika masomo yao ili kila mmoja wao afaulu na kuendeleza umoja wao hata wanaporejea Tanzania wakiwa katika majukumu yao Sehemu mbali mbali.

Wanafunzi walioko Alexandria wanasoma kozi za udaktari bingwa katika maradhi mbali mbali na upasuaji, unesi, Maafisa wa Jeshi wanaosoma kozi za Nevi, Maafisa Kadet, ulinzi wa anga, chemical explosive engineering na wanafunzi wa uhandisi wa Environmental Engineering katika chuo cha Egypt-Japan University of Science and Technology (E-JUST).Baadhi ya wanafunzi hao wanatarajia kumaliza masomo yao mwezi Oktoba, 2024.

Wakati huo huo, Mhe. Balozi aliwasihi Madaktari hao bingwa kufanya tafiti na kuwasilisha mapendekezo yao ubalozini juu ya mikakati inayoweza kutumika kupambana na maradhi yasiyo ya kuambukiza k**a vile magonjwa ya Ini, Figo, Kisukari, magonjwa ya Moyo ili kuisaidia Serikali kupambana na kutokomeza kabisa magonjwa hayo nchini Tanzania, magonjwa ambayo yanaonekana kuwa tishio miongoni mwa Vijana wengi nchini Tanzania.

Aliwasihi kutumia vyema taaluma zao kulinda taifa kwa kuwekeza katika afya za Watanzania, rasilimali muhimu katika kujenga uchumi wa nchi, uwekezaji, biashara na kuendeleza uhusiano kwa ujumla. Hii ni kwa sababu Misri imefanikiwa sana kupambana na maradhi ya Ini na wanao ujuzi mkubwa katika sekta ya afya, hivyo ipo haja kuwasaidia Watanzania kwa kuongeza idadi ya wataalamu wanaopata mafunzo nchini Misri pamoja na kuweka mikakati imara kupambana na maradhi mbali mbali nchini Tanzania.

Ikulu Mawasiliano
Wizara Ya Mambo Ya Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 22/03/2024

Mhe. Balozi akutana na Diaspora

Tarehe 21 Machi, 2024 Mhe. Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri alikutana na Watanzania wanaoishi Cairo nchini Misri kwa lengo la kufahamiana na kupeana nasaha.

Hafla hiyo iliyowahusisha Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi, Mapadre na Vijana wanaosoma vyuo na kozi mbali mbali.

Pia, walihudhuria Watanzania mbali mbali wanaoishi Cairo, wanaofanyakazi katika Vyuo Vikuu na Taasisi mbali mbali.

Mhe. Balozi aliwanasihi Watanzania hao kufuata sheria za nchi kwa kuwa na Vibali halali vya kuishi ili kuepuka operesheni k**atak**ata inayoendelea dhidi ya wageni wanaoishi kinyume na sheria kwa kutokuwa na visa na hati za kusafiria.

Aidha, aliwataka kuwa na umoja imara, katiba inayofuatwa kikamilifu na kufanya mikutano kila baada ya muda kujadili mambo mbali mbali yenye maslahi kwao na nchi kwa ujumla.

Aliwasisitiza kufika ubalozini na ubalozi upo kwa ajili yao, kwa shida na raha. Naye Mwenyekiti wa Diaspora waliopo Misri Bw. Fadhili Mansour aliupongeza ubalozi kwa kuwa nao karibu katika shida na raha na kuwakutanisha Watanzania katika hafla hiyo muhimu na kupata chakuka cha pamoja mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alieleza kuwa Hadi sasa Watanzania wawili walik**atwa na Polisi, mmoja amesharejeshwa Tanzania na mwengine yuko kituo cha Polisi akisubiri maamuzi ya vyombo vya usalama, kwa kuendelea kubakia nchini Misri au kurejeshwa Tanzania.

Nae Bw. Haroun Rashid, mlezi wa Diaspora aliwanasihi Watanzania kuhalalisha ukaazi wao na kuacha kujificha, kwani hakutawasaidia.

Hivyo, aliwataka wjitahidi kupata vibali halali vya kuishi na ikishindikana kabisa, ni vyema kufanya uamuzi wa kurejea Tanzania kuepuka msako unaoendelea kwa wageni wanaoishi kinyume na sheria na taratibu za Nchi ya Misri.

Wizara Ya Mambo Ya Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa
Ikulu Mawasiliano

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 28/02/2024

Mhe. Balozi akutana na Uongozi wa Timu ya Yanga pamoja na wachezaji

Mhe. Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri tarehe 28 Februari, 2024 wakati wa jioni amefika uwanja wa Cairo International Stadium, kuangalia mazoezi ya maandalizi ya timu ya Yanga inayotarajiwa kucheza na timu ya Al Ahly ya Misri siku ya Ijumaa tarehe 01 Machi, 2024.

Timu ya Yanga ambayo imeshafuzu kuingia Robo fainali ya Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika imemhakikishia Balozi kupata ushindi mnono katika mechi hiyo.

Aidha, Rais wa Timu ya Yanga, Injinia Hersi Ali Said alimkaribisha Balozi na Maafisa alioambatana nao na aliahidi kufuatilia tiketi za mchezo huo ili Watanzania waliopo Cairo na familia za Maafisa wa ubalozi wafike kwa wingi kushuhudia mchezo huo.

Nae Mhe. Balozi alipata fursa ya kuzungumza na wachezaji na kuwapongeza matokeo mazuri waliyoyapata uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kuwataka waitumie ari hiyo hiyo dhidi ya Al-Ahly siku ya Ijumaa kwa sababu tayari wamejaa hofu kufuatia kiwango kikubwa cha mpira kilichoonyeshwa na Timu ya Yanga, lengo ni kuendeleza heshima ya Tanzania katika mashindano hayo Makubwa Barani Afrika.

instagram.com/p/C357x85iIXY/?img_index=1

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 16/02/2024

TANZANIA NA PALESTINA KUIMARISHA ZAIDI UHUSIANO NA USHIRIKIANO

Tarehe 15/02/2024 Mhe. Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri alimtembelea Mhe. Diab Allouh, Balozi wa Palestina nchini Misri kwa lengo la kujitambulisha rasmi pamoja na kuimarisha uhusiano.

Aidha, ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Tanzania na Taifa la Palestina ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara na uwekezaji katika kuimarisha Viwanda, Kilimo, utalii, sekta ya uchukuzi pamoja na madini.

Mhe. Balozi alifahamisha kwamba uhusiano baina ya Tanzania na Taifa la Palestina ni wa kihistoria wakati wa harakati za ukombozi ambapo Tanzania ililitambua Taifa la Palestina mapema sana.

Mhe. Balozi Richard Makanzo alimfahamisha Balozi Diab uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania pamoja na rasilimali nyingi za madini, maliasili za maji ya kutosha kusaidia uwekezaji katika kilimo, uwepo wa vivutio vingi vya utalii ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, wanyama pori wanaohama kutoka Tanzania kwenda Kenya na kurejea Tanzania pamoja na fukwe nzuri za Bahari ya Hindi katika Visiwa Vya Zanzibar, inayozungukwa na Hoteli kubwa za kisasa.

Naye Balozi Diab Allouh alitoa shukurani zake kwa kutembelewa na Balozi Richard na kusema kuwa Ubalozi wa Palestina daima unathamini haja ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Tanzania na kwamba uko tayari kushirikiana naye akiwa ni Balozi wa Tanzania nchini Palestina mwenye makazi yake Cairo nchini Misri.

Aidha, Ubalozi uko tayari kushirikiana na Tanzania katika kila sekta na kwamba uratibu utafanywa kufanya ziara na kundi la Wafanyabiashara kutoka Palestina kwenda Tanzania.

Kisiasa, Balozi Diab aliiomba Tanzania kuendelea kuiunga mkono Palestina katika majukwaa ya Kimataifa ili kufikia lengo la utatuzi wa mgogoro unaoendelea na hatimae kufikia suluhisho la kuundwa kwa mataifa mawili, Taifa la Palestina na Taifa la Israel kwa kuzingatia mipaka ya mwaka 1948 ambapo Jerusalem ya Mashariki itakuwa ndio mji Mkuu wa Palestina.

Ikulu Mawasiliano
Wizara Ya Mambo Ya Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 07/02/2024

MISRI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Tarehe 07 Februari, 2024 Mhe. Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri alifanya mazungumzo na Profesa Saad Mousa, Msimamizi wa Mahusiano Kutoka Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Kusimamia Marufuku ya Mimea ili kuimarisha uhusiano na ushirikiano pamoja na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Wizara ya Kilimo ya Tanzania na Wizara ya Kilimo ya Misri.

Profesa Saad alisisitiza haja ya kuhuisha na kutekeleza kikamilifu Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) iliyotiwa saini mwaka 2018 katika sekta ya kilimo kupitia Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC).

Pia, alieleza haja ya kuhuisha MoU 2 katika sekta ya Kilimo zilizotiwa saini ili kuongeza wigo wa mashirikiano katika sekta ya mifugo, vifaa vya kilimo, umwagiliaji maji, uvuvi na mafunzo ya aina mbali mbali kutoa fursa ya Maafisa wa kilimo kutoka Tanzania, Bara na Zanzibar kunufaika na fursa hizo.

Alieleza kuwa Jumla ya Wanafunzi 10 hadi 15 hupata mafunzo ya kozi fupi nchini Misri kila mwaka katika sekta ya Kilimo na Uvuvi.

Aidha, alieleza mafunzo yanayotolewa na wataalamu wa Kilimo kutoka Misri huko Zanzibar kupitia shamba la pamoja liloanzishwa mwaka 2003.

Naye Mhe. Mej. Jen. Richard M. Makanzo alitoa shukuran kwa mashirikiano mazuri yaliopo baina Tanzania na Misri katila sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na Kilimo.

Alisisitiza haja ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano uliopo kwa kuimarisha sekta ya uvuvi, ufugaji wa Samaki na kilimo cha mazao mbali mbali kwa uwekezaji wa Viwanda na mashamba makubwa kuunga mkono Juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mradi ' ‘Building a Better Tomorrow Initiatives' ili kujenga fursa nyingi zaidi za ajira kwa vijana.

Alizungimzia mazingira mazuri ya uwekezaji yaliopo Tanzania, ardhi nzuri ya kilimo, vyanzo mbali mbali vya maji kwa kilimo cha umwagiliaji, pamoja na rasilimali za madini, vivutio vya utalii k**a mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro na fukwe nzuri za bahari ya Hindi katika visiwa vya Zanzibar ili kuvutia Wawekezaji.

Pia uwepo wa mifugo mingi Tanzania ni miongoni mwa fursa ambayo Misri inaweza kuitumia kikamilifu katika kuimarisha biashara baina ya Misri na Tanzania.

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 07/02/2024

SEKTA YA AFYA NCHINI TANZANIA KUIMARIKA ZAIDI

Tarehe 06 Februari, 2024 Mhe. Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri akiwa na Timu ya wakaguzi wa Dawa na Vifaa Tiba kutoka Tanzania Medicines and Medical Devices Authority (TMDA) waliopo Misri kwa kazi ya ukaguzi wa viwanda vya dawa, alihudhuria kikao maalum cha ushirikiano na Egyptian Drugs Authority (EDA) ili kwa pamoja kujenga uhusiano na ushirikiano katika udhibiti wa dawa na vifaa tiba ili kufanyakazi kwa pamoja, kubadilishana uzoefu na mafunzo kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa.

Mkutano huo uliowakutanisha Maafisa watendaji Wakuu wa Viwanda vya dawa nchini Misri, kiliongozwa na Dr. Ali Ghamrawy, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa nchini Misri (EDA) akiwa na Maafisa Waandamizi wa Mamlaka hiyo, Mhe. Mej. Gen. Richard M. Makanzo naye akiwa na Bw. Adam M. Fimbo, Mkurugenzi wa TMDA anayeongoza timu ya Wakaguzi kutoka Tanzania wanaokagua viwanda vya dawa nchini Misri.

Uongozi wa TMDA umewasilisha nakala ya awali (draft) ya Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) baina ya TMDA na EDA hatua ambayo itasaidia kuharakisha kazi ya usajili wa dawa zinazozalishwa Tanzania kuingia Misri na zile zinazozalishwa Misri kuingia Tanzania, soko la Afrika Mashariki na SADC kwa ujumla.

Aidha, ushirikiano huo utafungua milango ya uwekezaji wa viwanda vya Dawa kwa wingi nchini Tanzania kutoka kwa wawekezaji kutoka nchini Misri.

Jumla ya viwanda vya dawa 200 vimesajiliwa nchini Misri vinavyotosheleza soko la ndani la asilimia 94 na sasa vinahitaji kuongeza uzalishaji kukidhi soko la Tanzania, Soko la Afrika Mashariki na SADC kwa ujumla.
Ikulu Mawasiliano

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 05/02/2024

UTEKELEZAJI DIPLOMASIA YA UCHUMI WAZIDI KUIMARIKA

Tarehe 05/2/2024 Mhe. Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri alifanya ziara kuitembelea Taasisi ya Arab Organization for Industrialization (AOI) katika mji wa Nasser City, Cairo.

Taasisi hiyo ni mkusanyiko wa Makampuni 14 ambayo 7 kati ya hayo yapo chini ya Jeshi la Misri na mengine 7 yaliyobakia yanamilikiwa na watu binafsi.

Taasisi ya AOI inajihusisha na uzalishaji na uunganishaji wa Magari ya Kijeshi, Polisi, zimamoto, magari ya kusafirishia fedha, magari yenye ofisi zinazotembea (mobile offices), vifaa vya kijeshi k**a vile Ndege Nyuki (drones), vifaa vya kilimo pamoja na vifaa vya matumizi ya nyumbani k**a vile majokofu, Televisheni, vipoza hewa, mashine za kufulia na kadhalika.

Lengo la ziara hiyo ni kimarisha uhusiano na Taasisi ya 'AOI' na kuona utendaji wa Taasisi hiyo na vifaa vinavyozalishwa na Makampuni yaliopo chini ya Taasisi hiyo.

Viongozi wa Taasisi ya Arab Organization for Industrialization wanatarajia kufanya ziara nchini Tanzania kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Wizara, Taasisi na Makampuni mbali mbali ya Tanzania kujadili namna bora ya kushirikiana kibiashara, kubadikishana bidhaa na kadhalika.

Ikulu Mawasiliano

Photos from Tanzanian Embassy in Egypt's post 31/01/2024

Mhe. Balozi ashuhudia zoezi la Ukaguzi wa Kiwanda cha Global Pharmaceutical Group (GPI)

Tarehe 31 Januari, 2024 Mhe. Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri akiwa na Wakaguzi kutoka Tanzania Medical and Drug Authority (TMDA) ameshiriki ukaguzi wa kiwanda cha Global Pharmaceutical Group ( GPI) kilichopo Mji wa 6th October City, nje kidogo ya Mji wa Cairo.

Kiwanda hicho kinaongozwa na Dr. Peter Makram Mehany, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mwendeshaji kilianzishwa 2009 na kuanza uzalishaji mwaka 2010 kwa uzalishaji wa dawa za sindano pekee zaidi ya bidhaa 150.

Kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda 10 bora nchini Misri kwa utengenezaji dawa kwa matumizi ya Binaadam nchini Misri.

Ukaguzi huo unafanyika ikiwa ni hitajio la kisheria kabla dawa za kiwanda hicho kuingia katika soko la Tanzania.


Want your business to be the top-listed Government Service in Al `Ajuzah?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Al `Ajuzah

Opening Hours

Monday 9am - 5pm
Tuesday 9am - 5pm
Wednesday 9am - 5pm
Thursday 9am - 5pm
Friday 9am - 5pm