23/12/2025
Happy Birthday to our President
Akaunti rasmi ya Facebook ya Wizara ya MAendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Zanzibar
23/12/2025
Happy Birthday to our President
13/12/2025
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimkabidhi cheti cha ushiriki Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ndugu Abeda Rashid Abdala katika ufungaji wa Mafunzo ya Awali kwa Viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha IIT Madras Bweleo Wilaya ya Magharibi " B" Unguja.
06/12/2025
NAIBU KATIBU MKUU ATOA WITO KWA WAANDISHI WA HABARI KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndugu Khatib Mwadini Khatib ametoa wito kwa waandishi wa habari kuongeza juhudi katika kuelimisha jamii kuhusu madhara ya udhalilishaji wa wanawake na watoto na kusema jukumu hilo ni sehemu muhimu ya ulinzi na ustawi wa makundi hayo.
Akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wake kuripoti habari za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Naibu Katibu Mkuu amesema ongezeko la matukio ya udhalilishaji wa watoto na wanawake, ikiwamo unyanyasaji wa kimwili, kingono, kihisia na mtandaoni ni janga linalolikabili taifa na kurejesha nyuma maendeleo ya nchi.
Amesema udhalilishaji wa watoto unaathiri mustakabali wao kwa kuwasababishia msongo wa mawazo, kuharibu afya ya akili, kukosa fursa za elimu na kujiamini, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika kulinda haki zao.
Amesema Udhalilishaji wa watoto kwa njia ya mtandao umeongezeka kwa kasi na kupelekea watoto kukabiliwa na vitisho, maudhi yasiyofaa, upotoshaji na mifano mibaya kupitia mitandao ya kijamii na michezo ya mtandaoni, hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuwa macho na kufuatilia matumizi ya mtandao ya watoto wao.
Amebainisha kuwa katika mafunzo hayo, washiriki wataelekezwa kuhusu Mpango wa Kitaifa wa Mapambano Dhidi ya Ukatili na Udhalilishaji (NPA-VAWC) Zanzibar, unaotekelezwa na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari.
Hatahivyo amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuibua matukio, kuelimisha jamii na kuhamasisha hatua madhubuti dhidi ya ukatili.
Kwa upande wao, wataalamu kutoka wizara na wadau wa maendeleo ya watoto wamesema elimu ya mara kwa mara kwa jamii, uangalizi wa karibu wa watoto, pamoja na kuripoti matukio ya udhalilishaji ni miongoni mwa hatua muhimu za kupunguza vitendo hivyo.
Naibu Katibu Mkuu aliwataka washiriki kutumia mafunzo hayo kuboresha uandishi unaolenga kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali yamefanyika katika ukumbi wa UNWOMEN Kinazini Zanzibar hiyo ukiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku 16 za

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Anna Athanas Paul, pamoja na Naibu Waziri Mhe. Zawadi Amour Nassor na maafisa kutoka wizara wamefanya ziara ya kutembelea Nyumba ya Watoto Mazizini na Nyumba za makazi ya Wazee Sebleni na Welezo. Ziara hiyo imelenga kuangalia maendeleo kusikiliza changamoto zinazowakabili pamoja na kukagua miradi inayoendelea, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha ustawi wa makundi maalum katika jamii.
06/12/2025
Wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Kaskazini Unguja waliofika kupata huduma za Msaada wa Kisaikolojia,Kijamii na Kisheria kuelekea maadhimisho ya siku 16 za harakati za kupiga vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia huko kituo cha walimu (TC) Mkwajuni tarehe 5Disemba,2025
24/10/2025
ZMBF NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII ZANZIBAR WAANDAA MKUTANO WA WADAU KUJADILI MFUMO JUMUISHI WA KIDIGITALI WA TAARIFA NA USIMAMIZI WA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA
Mkutano huu umewakutanisha wadau kutoka wizara mbalimbali, taasisi za serikali na asasi za kiraia (NGOs) kujadili mfumo wa kidijitali unaoendelea kutengenezwa kwa ushirikiano kati ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) na Wizara Ya Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Zanzibar, wenye lengo la kuimarisha ufuatiliaji, uratibu na utoaji wa huduma kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa ZMBF, Bi. Fatma Fungo, amesema mfumo huo utarahisisha ukusanyaji na usimamizi wa taarifa, kuongeza uwajibikaji na kurahisisha utoaji wa huduma kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.
Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Mstahiki Meya Jiji la Zanzibar, Mhe. Mahmoud Mohamed M***a, pamoja na Dkt. Ibrahim Kabole, Mratibu huduma za afya ZPDB, Pia Mkurugenzi wa E-Government Agency Zanzibar (EGAZ), Dr. Said Seif Said, alihudhuria mkutano huo
Mfumo huo unatarajiwa kusaidia Serikali na wadau kupanga mikakati bora ya kulinda haki, heshima na ustawi wa wanawake na watoto Zanzibar.
02/10/2025
02/10/2025
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Abeida Rashid Abdallah ameitaka jamii kuwatunza wazee na kuwathamini Kwani ndio ngao ya Taifa kwa ujumla Katika kuleta maendeleo.
Akizungumza katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani lililofanyika katika ukumbi wa sebleni mkoa wa mjini Magharibi unguja, Bi. Abeida amesema wazee wanayo nafasi kubwa katika kujenga jamii thabiti na endelevu kwa hekima, maarifa na uzoefu walioupata katika maisha yao.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuboresha maslahi ya wazee kwa kuwaongezea kiwango cha pensheni jamii kutoka shilingi 20,000 hadi 50,000 kwa mwezi na kuimarisha huduma katika makaazi ya wazee Sebleni, Welezo na Limbani Pemba ambapo kwa sasa jumla ya wazee 68 wanatunzwa katika makaazi hayo kwa kupata huduma zote muhimu ikiwemo chakula, malazi, mavazi na matibabu.
Bi. Abeida ameipongeza jamii kwa ushirikiano wao katika kushirikiana na mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya Shehia, Wilaya hadi Mkoa, jambo ambalo amesema linasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wazee kwa haraka.
“Ni wajibu wetu kuendeleza mila na tamaduni za Kizanzibari, na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha wazee wanapewa heshima na mapenzi, kwani kuwatunza wazee ni ibada yenye malipo makubwa,” amesema Bi Abeida.
Nae Muwakilishi kutoka Help age ameipongeza wizara kwa kuendelea kuwaunga mkono wazee katika kutatua changamoto zinazowakabili na kuahidi kushirikiana bega kwa bega ili kuona wazee wanapata faraja siku zote.
Muwakilishii wa wazee kutoka jumuiya ya wazee wastaafu Bi Salama Kombo amewataka wazee wenzake kuwa na umoja na mshikamano na kujipenda wenyewe ili kuimarisha ustawi katika maisha yao.
Akiaghirisha kongamano hilo kwa mwaka huu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Khatib Mwadini Khatib amesema kuwa swala la udhalilishaji wa Wazee Zanzibar linazidi kukuwa kila kukicha hivyo amewaomba wadau kuendeleza mashirikiano ili kuweza kulitokomeza kabisa tatizo hilo.
Amesisitiza kurejeshwa kwa heshima na maadili kwa Wazee na kutunzwa ili kuendelea kuneemeka na hekima zao.
Aidha amesema wazee ni hazina ambayo inapaswa kuthaminiwa na kuienzi kwani