22/06/2020
Mambo 8 kuhusu hadithi,simulizi ama kitabu chochote. Share na wengine wapate maarifa!
Equator story ni website ambayo inakurusu kusoma na kuandika story kwa njia rahisi. Tembelea equatorstory.com unda account na uanze ku enjoy!
22/06/2020
Mambo 8 kuhusu hadithi,simulizi ama kitabu chochote. Share na wengine wapate maarifa!
15/06/2020
MY SOULMATE EPISODE 3
PRODUCED BY : EQUATORSTORY SPECIAL
Tulipoishia
Angela : “Hey mtumishi twende tukale ama ndo upo kwenye mfungo!?.”.Kabla ya Nickson haja jibu alimwangalia Stela akagundua stela alikuwa ana waaangalia tena kwa uso uliofura.
Tuendelee sasa.
Ni ndani ya ofisi ya Matumizi App Company. Angela amesimama mbele ya meza ya kazi ya Nickson akiwa amevalia style ya kipekee mabuti yaliofika karibu kidogo na magotini suruali ya jeans alio chomeka kwenye viatu vyake vya brown iliopauka ikiwa na vinakshi kidogo vya urembo wa k**a manyoya meupe kwa juu. Na blauzi yake ambayo haijambana saaaana ya rangi ya njano . Angela ni mdada flani mwembamba size yani sio njiti sana lakini hivo anao ka unene flani hivi. Ana ngozi ya maji kunde . Alionekana akisimama kwa shauku akingojea jibu la Nickson.
Nickson : “Ah leo roho ameniambia anataka Kunena na mimi so sili leo ntafunga mpaka nimsikie roho.”Nickson alijibu hivyo kwa sauti ya kukwaruza ikiwa ni mithili zile za wa injilisti mashuhuri unaowajua . Kwa akili sana ili aweze kumpotezea Angela. Angela alicheka na kutoka ofisini humo na wafanyakazi wengine wawili wa humo humo ofisini.
Basi ilikuwa ndo muda wa lunch kila mmoja alitoka ofisin kwenda kula kulingana na hapetait yake na mfuko wake unavyosema. Nickson akaangalia kushoto na kulia akaona wengi wamepungua hata Stela hakuwepo maeneo hayo basi aka nyanyua begi lake na kuelekea jikoni akachukua maji akaweka ndani ya heater ya kupashia maji ili aweze kutengeneza chai. Wakati anangojea maji yachemke akawa anawaza situation yake ya kimapenzi . Akajisemea ingekua naweza kubadilisha wapenzi ninge mbadilisha Stela ili nipewe Angela maana ana nivutia sana kwa tabia zake na uzuri wake anavaaaga style flani ivi inakufanya usahau hata ulichokuwa unafanya yani ni mcheshi na tunapatana sana. Lakini Nickson akajiambia moyoni kwamba ni wengi sana wamejaribu kumtongoza Angela hapo ofisini kasoro yeye tu na hao wote walio mtongoza amewakataaa hata akiwemo Mr Sambeke pamoja na hela zake. Aliwaza kwamba kuliko ampoteze Stela alafu avunje urafiki wake na Angela awe kwenye kikundi cha waliokataliwa na Angela bora abaki na Stela wake. Basi mara baada ya maji kupata moto aka toa tambi alizopika asubuhi na kutengeneza chai akala na tambi zake akatoka mapema kwenda kukaa kwenye meza yake maana hataki watu wamu ulize maswali mengi sana. Nickson akakaa mezani kwake akiwa na earphones zake kaweka mziki kwenye simu yake akawa anasikiliza nyimbo azipendazo. Mara ghafla akatikiswa bega kuhamaki ni Boss Sambeke ndo ameingia.
Nickson : “Shkamooo boss”. Nickson alisema huku akitoa headphone masikioni haraka.
Boss : “Marahaba Nickson unafanya kazi kweli!?”. Boss wake aliuliza akiwa na mashaka maana hakuwa ofisini tokea asubuhi.
Nickson : “Ndio Boss nafanya kazi hapa nipo kwa ajili ya kazi boss.”.
Boss : “Kwani sijui hapa upo kwa ajili ya nini hujui kwamba hata kukaa bure ni kazi?” Boss aliuliza hivi kwa sauti ya hasira kidogo .
Nickson : “Ndio Boss najua lakini hapa nlikuwa nafanya kazi ulioniajiri kufanya boss.” Nickson alijibu hivyo akiwa anajua tu ndo kawaida ya boss wake ndo hivyo inabidi amzoe tu.
Boss : “Sasa yerro kuna mabadiliko ile presentation nilio waambia itafanyika kesho kutwa ita fanyika kesho saa nne kwahyo naomba uache kila kitu unafanya umalizie hiyo presentation kabla hujaenda.”
Nickson : “Lakin boss mda huatato……” Boss akamkatisha.
Boss : “Acha uzembe kila mmoja ana masaa 24 na wengine wanafanikiwa sasa wewe una shindwaje kwa mfano!?”. Boss alisema hivi huku waliokuwa lunch nje ndo wanaingia ikiwemo kina Angela na Stela na wakimsalima Boss wao.
Nickson : “Sawa boss ntahakisha kabla sijaenda ntakuwa nimeshamaliza”. Nickson alijikuta akikubali kazi ambayo ingechukua siku nzima ndani ya masaa machache ya kazi na mengine ya extra ambayo halipwi overtime lakini hana budi kwa ajili ya kuilinda ajira yake ambayo angalau inamuweka mjini.
Boss akaondoka na kunyooka moja kwa moja kwenye meza ya Stela kujua k**a kuna hili na lile ama kuna walio mulizia jumbe zilizopo maaana hiyo ndo kazi ya Stela. Alipofika kwa stela alikaaa k**a dakika 10 wakiongea na kucheka cheka . Nickson akaligundua na akakumbuka asubuhi alivyo textiwa na Stela kuhusu Angela naye akaaamua kutumia haki yake ya kulinda penzi lake aka mtext Stela akisema “Mnacheka nini hamumalizi tu!?”. Ak**alizia na kusema “Mimi nina wivu eti.”. Vile vile alivyo andikiwa na stela asubuhi k**a masaa matano yaliyo pita. Wakati bado stela anaongea na Boss alionekana kusoma ile messeji kisha akaweka simu pembeni kwa kuifunika kioo chake. Boss alipo ondoka kwenye meza yake na kuingia ofisini mwake alimjibu Nickson. “Acha utani huyu ni Boss unataka niachishwe kazi??. Tumia akili wewe mwanaume!.”.Wakati Stela ana andika hiyo Sms alionekana akisunya kabisa. Nickson akaisoma hiyo message akaona hana point ya kujitetea maana ni Boss kweli lakin aliona dalili za Stela kujigonga gonga kwa Boss wao alitamani aweze kupata ushahidi athibitishe lakini anajua lazima tu jitihada zake zigonge mwamba. Aka kumbuka ana kazi ya kuwasilisha wivu wa mapenzi usije uka mkost aka kosa namna ya kuishi mjini.
Basi Nickson aliendelea kufanya kazi huku aki pambana na muda aliendelea mpaka alipo kuja kunyanyua kichwa akaona ni saa nne usiku . Aka kumbuka hata Stela hakumuaga akahisi labda alichukia pale Angela alipo kuja kumuaga mida alipo kuwa akiondoka akajisemea nimebakisha kidogo tu ngoja nipambane nika lale alisema hapa nisipo pambana nikimuwaza Stela japo nampenda Itakua sio vyema .Lakin moyoni Nickson aliwaza na kusema hiii ndo mida Stela anayo lala labda cha kufanya ni kumuwish usiku mwema akachukua simu kwa lengo la kumuaga stela.
Nickson : “Usiku mwema mpenzi wangu. Nakupenda sana”Ali mtumia messeji ikiwa na maneno hayo Stela naye akajibu mara baada ya sekunde 30.
Stela : “Thnx”.Duh Nickson aliwaza yani huyu ni mpenzi gani jamani? . Lakin aka achana naye akacheki na sms zingine akakuta aliotumiwa na Angela “Usiku mwema jamani ufanikiwe kwenye project yako.”Angalau hayo maneno kutoka kwa rafilki yake Angela yalimfariji.
Nickson akaendelea kwenye kazi mpaka ilipo timia mida ya saa saba kasoro akai print presentation na aka copy kazi alio kuwa ana andika kwenye flash ya ofisi akasogea mpaka kwenye meza ya Stela ambaye ndiye secretary wa ofisi hiyo aka weka vitu vyote pale akazima taaa akafunga milango yote.Aka toka aka kutana na mlinzi.
Mlinzi : “Za kwanzia jana Chifu?”.Mlinzi alisema k**a utani wakacheka lakini ukiangalia ni jana asubuhi Nickson aliingia kwenye ofisi hii na anatoka saa saba usiku ambayo ni siku nyingine ambapo boss wake aliondoka mapema sana.
Nickson : “Weweee kumbe siku nyingine hiiii?. Alaaaah Sasa si bora nikakae tena naweza nkatoka mwezi ujao nkasamehewa kodi yangu ya mwezi.”Basi wote wakaangua kicheko japokua kwa mbali hayo yanampa machungu Nickson.
Nickson huyo na begi lake akapanda toyo waka kubaliana 8,000 baada ya ju bagein kwa mda apunguziwe japo kidogo maaana anujua kuna kesho.
Dreva toyo : “Man vaa helment nisije k**atwa na ma trafiki”.
Nickson : “Sorry bro siwezi hapa nasikia usingizi sana nkivaa naeza sinzia nika anguka.”Dreva toyo aka cheka akidhani ni janja janja za kukwepa kuvaa helment.
Wakaaanza safari wakaenda k**a 20 wakafika mahali ambapo barabara ina makorongo kwa dreva toyo alipitia karibu na pembezoni mwa barabara kuyakwepa makorongo na kufanya safari isiwe ngumu sana. Wakapita mahali kuna k**a kichaka pembeni ya pikipiki inapopita mara ghafla dreva alipigwa rungu la kichwa kutokea mtu aliekuwa amejificha kwenye vichaka ilio sababisha arudishe kichwa nyuma kumgonga Nickson mdomoni . Nayo piki piki ikakosa mwelekeo wote waka hangaika huku na kule waka anguka . Dreva toyo akasema “Hapa wameanza uwizi tena!”. Akanyanyuka nduki akimbilie pikipiki wakimbie kuokoa maisha yao.
Dreva toyo :”Oya mchizi shika toyo tukimbie ”. Nickson bado alikua chini akihamaki nini kimetokea akaona hi indo nafasi yake ya kukimbia aka nyanyuka akimbilie toyo hapo dreva tayari amesha anza kwenda mwendo mdogo kibishi bishi akisubiri Nickson adandie mara nickson akasikia kuna sauti za watu nyuma yake wana mkimbilia.
Itaendelea…
Link ya kupata hadithi tembelea:
My Soulmate episode 3 | Equatorstory My Soulmate episode 3 Tulipoishia Angela : “Hey mtumishi twende tukale ama ndo upo kwenye mfungo!?.”.Kabla ya Nickson haja jibu alimwangalia Stela akagundua stela alikuwa ana waaangalia tena kwa uso uliofura. Tuend
15/06/2020
MY SOULMATE EPISODE 2
PRODUCED BY : EQUATORSTORY SPECIAL
Ni alfajiri ya saa kumi na moja tuna muona Nickson akiwa kitandani kwake amekaa akiwa ana soma kwenye simu yake yeye sio mwanafunzi na isitoshe k**aliza chuo miaka kadhaa iliopita.Lakini kwa sababu Nickson hajaridhika na mahali alipofikia katika tadhnia yake mambo ya computer ama kwa kimombo tunaeza sema (IT).Nickson ameamua kutoa japo lisaaa la kuwa anasoma vitu kadhalika ili kuwa sambamba na ulimwengu huu ya maswala ya technology yanayo badilika kila siku. Mpaka ilipo fika saa kumi na moja na nusu akaaamka akabandika maji ilia pate ya kuoga kujiweka fresh kimwili na ki akili saa kumi na mbili kamili akaya bandua jikoni alipo kuwa ameyaweka kwa jiko la gas ili yasipate moto sana. Akaweka kwenye ndoo yake kijani na akiwa na taulo lake lililo chorwa picha ya Paris na limeandikwa welcome again. Sijui k**a aliwahi fika Paris but haya ni ma taulo ya wageni kwenye ma hoteli ma kubwa makubwa yamkini alilipata mtumbani?. Nickson alipo bandua maji aka anza mchakato wa kupika tambi ambazo ndo atazokula mchana ili kuoka bajet yake. Akafungua mfuko wa tambi akijaribu kuzigawa nusu kwa kutumia kipimo cha macho. Akawacha nusu kwa ajili ya siku ifuatayo akavunja vunja zile alizo chagua k**a mara 6 hivi ili kuzifanya ziwe ndogo ndogo ziweze kulika . Aka wacha maji yakiwa jikoni yapate moto ili akirudi aendeleee. Nickson akabeba ndoo na maji yake akaenda kuoga haraka akarudi ak**alizia kupika tambi na kuweka kwenye container akafunga vizuri akaweka kwenye begi lake. Akachukua nguo zake na kuvaaa akabeba na simu akaondoka kwenda kuanza shughuli yake za kila siku.
Nickson : ”Chief kwema umeamkaje bhana?”.Alikua akimsalimia mlinzi aliekuwa amekaaa maeneo ya ofisini kwenye kampuni ya Matumizi App.
Mlinzi : “Fresh Chifu naona unawahi kweli siku hizi!?”.Mlinzi alijibu.
Nickson : “Chifu si unamjua boss Sambeke alivyo mkorofi.?”.Mlinzi alidakia kwa kukubaliana naye.
Mlinzi : “Aaah Yule mzee Sambeke achana naye bhana. Yani…”Mlinzi alianza maneno yake k**a kawaida amabapo ukimpa nafasi haaachi kuzungumza.
Mlinzi : “Mi nakuambia huyu jamaa hana mtu anao ishi nae sio mke wala ndugu wala mtoto.”. Nickson akadakia kwa mshangao.
Nickson : “Weweee usiniambie… Man!?” Nickson alionekana kuhitaji taaarifa zingine japo kuwa haaamini amini.
Mlinzi : “Ndio Chifu mi nakumbuka nlishawahi kulinda kwake miaka kadhaa iliopita pako kimya jumba kubwa lakini ndani inawaka taaa moja tu!.” Maongezi yao yalianza kunoga wakiwa wanasubiria mlango wa ofisi ufunguliwe ili Nickson aweze kuingia.
Nickson: “Au ulishuhudia yote wakati watu wote wamelela? .”.Nickson alimuuliza mlinzi bila kua amini amini.
Mlinzi : “Hapana man nimekaaa pale mwezi nikilinda na sijaona watu wengine zaidi ya wafanyakazi tu. Boss wetu Sambeke alitumia mda mrefu sana ili kupata mafinikio mpaka mke wake Wanjiku alimuacha maaana alikua anakaaaa mwezi hapigi kitu yake .”Nickson akadakia tena.
Nickson : “Mwezi hapigi kitu anaumwa ama? “Mlinzi alimdakia na kwa kuashiria yupo serious kwamba ni kweli.
Mlinzi : “Hapana chifu alikuwa anajifanya bize sana kazi tu kumpa vitu vya thamani mke wake mambo mengine k**a baba wa familia alikuwa hagusi saivi mke wake kaolewa na kadogo ambako hana hela lakini anamjali sana.”Mara wakakatishwa na sauti ya stela.
Stela : “Habari za asubuhi jamani”. Stela aliuliza huku akiwa anatafuta simu kwenye pochi yake alio kua amebeba . Nickson alichukua nafasi hiyo kumwangalia Stela vizuri ambaye ndiye mpenzi wake na secretary wa boss Sambeke. Nickson na mlinzi wakaitikia kwa pamoja.
Mlinzi & Nickson : “Kwema tu hatujui wewe.”
Stela : “Aah salama tu”. Stela alifanikiwa kutoa funguo alizokuwa akipekuwa huku Nickson hajabandua macho yake kuangalia alichokua amevaaa. Stela alikuwa amavaa Blauzi ya Blue na Sketi fupi nyekundu ambayo ilikuwa imembamba kweli na kuchora ka figure yake kidogo.
Nickson : “Mambo mengine lakini?”. Nickson aliuliza hivyo utasema sio mpenzi wa Stela maaana bado hawaja report mahusiano yao kwa Manager wao ili wajulikane ni wapenzi na sheria za kazi haziruhusu vitu k**a hivyo . Kwayo wameamua kuya ficha kwa muda mpaka mapenzi yao yatakapo kolea.
Stela : “Kwema tu” Stela aligeuka na kumuangalia Nickson . Ambaye alikua amevaaa k**a anaenda kanisani nguo zote alio vaaa ni za kitambaa na sio nyembamba k**a za wakaka wengine lakin angalau yupo smart.
Nao wakaingia ndani Nickson akageuka kumu ashiria mlinzi kwamba maongezi yao yanaeza endelea. Nickson akatoa bahasha ya kaki aliekuwa amambea mpenzi wake vitumbua ili anywee chai hii ni kuonesha kujali tu.
Stela : “Vitumbua umenunua jana nini?”.Stela aliuliza akiwa amepindisha mdomo kidogo na ka kushangaaa kiasi .
Nickson : “Leo asubuhi jamani Mpenz…. I mean stela.” Aliogopa kutamka neno mpenzi aki hofia anaeza sikika akafukuzwa kazi mara moja.
Stela : “Akasema mbona vya baridi jamani sasa mimi nakulaje!?. Bhana mi nipe buku nikanywe supu.”.Stela alisema huku akiwa ametoa mkono nje katika namna ya kupokea .
Nickson : “Acha ushamba wewe kuna Microwave tuvipashe bhana.”Nickson alipotezea hyo bajet nyingine ya supu isiyo na mpango. Nickson akachukua akaweka kwenye microwave akaweka na mda na kiasi cha joto cha kupashia. Akaenda kukaaa na kuwasha computer aliopewa ili aanze shughuli zake na wafanyakazi wengine wakaaanza kuingia katika kampuni hiyo ya Matumizi App.
Angela : “We muinjilisti wa tabora mjini umeamkaje!?”.Hiyo ni sauti ya Angela mmoja wapo wa wafanyakazi katika kampuni hiyo . Nickson alipogundua ni Angela anamtania k**a kawaida yake alianza kutabasamu na kujibu.
Nickson : “Bwana Yessssssu asifiwe…?”. Nickson aliangualia ka kicheko huku Angela akimwangalia kwa tabasamu bashasha.
Angela : “Ah we acha kunihubiria saivi umetumwa nini!?” Angela alijibu huku akiwa anaanza kucheka .
Nickson : “Kwema lakini!? Jamani!?”. Saivi Nickson alijibu huku akiwa ana angalia simu yake ilio toa mlio wa kua ashiria messeji mpya.
Angela : “Kwema vipi ile kipande cha presentation ulicho nipangia si umekipata?”.Alimuuliza Nickson aliokuwa ana soma text mpya aliokuwa ameipokea kwenye simu yake.
Nickson : “Ya niliipata kwenye email asubuhi nimeisoma nikiwa njiani nikawa najiuliza uliandika wewe au aliandika mtoto wako? Sio kwa huo mwandiko mbaya”.Wakaaanza kucheka tena.
Angela : “Acha kunichora mwandiko wa mtoto kwenye computer bhana!?. Haahahah”. Nickson akawa bize anasoma text alietumiwa kumbe ni text kutoka kwa stela aliemtumia akiwa hapo ofisini “Acha kucheka na huyo kigagulo mi nina wivu eti. Ntakuja nimlabue hapo hapo!!!!!. Mwambie aondoke kabla sijapandisha mapepo yangu.”.Nickson aliposoma hivyo akamkatisha Angela kia akili.
Nickson : “Haya bhana usiwaze nimeipata ntashughulikia wala usiwe na shaka!”. Angela alipoona maongezi k**a yamefifia akanza kuondoka na kuelekea kwenye kiti chake.
Basi siku ikaendelea huku kila mmoja akiwa bize na kazi zake lakin macho ya Stela yalikua k**a radar inayomfatilia Nickson kila hatua hata akienda chooni haaachi kupashangaaa hapo mpaka atoke.Ilipofika mda wa kula Stela akamwambia Nickson kwa sms “Twende tukale” lakini Nickson aligoma kwa kusema “Wewe ni vipi huoni watu watatu shtukia kwamba tupo pamoja sana!?”. Stela nayo aliona ni point.
Angela : “Hey mtumishi twende tukale ama ndo upo kwenye mfungo!?.”.Kabla ya Nickson haja jibu alimwangalia stela akagundua stela alikuwa ana waaangalia tena kwa uso uliofura.
Itaendelea…..
hadithi hii unaeza kuipata kamili ndani ya
My Soulmate by Equatorstory Specials | Equatorstory Huwezi kumjua Soulmate wako mpaka pale mtapo pitia majaribu kadhaaa
13/06/2020
My Soulmate Episode 1
Produced by EquatorStory Specials
Stela :”Nickson uko wapi jamani ?? Mpaka sasa umechelewa sana.”. Ilikuwa ni sauti ya stela akimngojea mpenzi wake Nickson alie kuwa njiani akitokea kazini .
Nickson:”Nimekuona mpenzi hapo ulipo nakuja jamani.”. Nickson alisogea taratibu kumfikia mpenzi wake aliekuwa akimngojea na jazba taratibu ilianza kupanda kisa mpenzi wake amechelewa.
Nickson:”Mambo mpenzi?”.
Stela :”Mxxheeewww ”.
Nickson: “Jamani mpenzi nisamehe bure tu jamani ni kazi.”
Stela:”Aaah kazi gani bhana..???.” Stela aliuliza kwa hasira akianza kuhisi mpenziwe hamchukuliii serious.
Stela:”Haiwezekani tuuupange huu mtoko karibu mwezi mzima alafu uchelewe!. Baby kweli unanipenda???.” Stela alitamani kuondoka akasimama kwa hasira.
Stela:”Nenda kalale na hiyo kazi yako k**a unaipenda hivyo. Maaana wewe unatumia matope ama ubongo?. Mimi si nimeondoka kazini mapema sana yani we bado hata ndo unatoka sasa. So hujapitia nyumbani kuoga ushaaanza kunukia jasho.”Nickson akamshika mkono kwa nguvu na Stela akaaanza kumpiga vikofi kwenye mkono aliemshikia Nickson ili asiondoke .
Nickson: “Baby am sorry nakupenda wewe lakini bila hiii kazi sidhani k**a tungekua hapa. Baby ni dakika 20 tu jamani. Tafadhali nisamehe sitorudia mpenzi.”Stela akaaanza akakumbuka aliwahi kumwambia Nickson kipindi hicho “Mapenzi hayaliki”.
Stela:”Sawa nimekusamehe lakini usirudie tena. Lakini baby….”Stela aliamua kumsamehe na wakaaanza maongezi yao .
Nickson: “Stela sema mama!..”.
Stela:”Baby kweli wewe tunapanga mtoko unanpangia na kitu cha kula mimi si mpenzi wako natakiwa nile kitu nachotaka bhana.”Stela alisema huku akiwa na ka uchungu.
Nickson :”Baby..”.Stela akamkatisha.
Stela:”Subiri sijamaliza kuongea ”. Nickson alikaa kimya akimsikilizia mpenzi wake .
Nickson :”Sawa mama zungumza ”.Nickson aliamua kuwa mpole na kuwa msikivu kwa sababu ana amini kwamba katika mahusiano lazima kuwe na usikivu pale mmoja wapo anapotaka kuzungumza .Nickson alikaaa na kuweka mkono wake wa kuume kidevuni huku akikuna taratibu ndevu zake mbili tatu.
Stela : “Huwezi ukaniambia ety pamoja na kusubiri huu mtoko mweeeezi mzima unaniambia bajeti yako ni 10,000 tu?”.
Nickson : “Mama ..”. Stela alimsimamisha hapo kabla hajafika mbali .
Stela:”Eeeeeh nishakwambia uache kuniiita Mama unanizeeesha bhana.”
Nickson:”Am sorry baby. Unajua nataka uwe mama watoto wangu tena nataka motto wa kwanza aitwe Rose k**a ni wa kiume ataitwa Samuell”.
Stela:”Nickson am serious na swali langu.”Stela alioneka akianza kunyanyua nyusi ya kulia na kupindisha shingo kidogo k**a anavyofanyaga akiwa na hasira au akiwa serious na jambo.
Nickson :”Sawa Ma… I mean sawa Baby stela…. Nakujibu “.
Stela : “Enheee…..”. Stela alikaaa chonjo kusikilizia jibu huku akisogeza nywele zake za rasta zijulikanazo k**a yeboyebo na kucha zake alizongezea za bandia za rangi ya nyekundu ili zisi mghasi .
Nickson:”Baby unajua mimi nina majukumu na laki na nusu nimetoka kwa ajili ya project.”.Stela akamkatisha hapo hapo .
Stela :”Tena ishia hapo hapo.” Mara wakasikia sauti ya mtu mwingine kutazama ni waiter wa pale hoteli waliopo ijulikana nayo k**a “Mwambao hotel” iliopo upande wa pili kutazamana na Stand ya ma bus “Dar express”.
Waiter:”Jamani za jioni Kwema hapa!?”.Waiter aliuliza kwa sauti ya upole na kwa sauti ya ukarimu.
Nickson & Stela: ”Salama tu.” Wote waliiitikia kwa pamoja k**a waliambizana kujibu hivyo.
Waiter:”Niwahudumie nini joini ya leo?”.
Nickson : “Kuku nusu kiasi gani?”. Nickson aliuliza akimwangalia waiter kwa makini asikie bei chapu apige hesabu ya fasta .
Waiter:”Ni 6000”. Waiter alijibu lakini akaongezea . “Kwa sasa kuku zimeisha ndugu labda k**a hamtojali mchukue nyama choma nusu 5,000”.Nickson moyoni akajisemea kumbee bora hata bajeti itaaenda sawa sawia.
Nickson:”Sawa naomba hiyo hiyo”. Akamgeukia Stela na kumuambia. “Baby utakula na nini? “
Stela : “Na chipsi tu”. Stela alisema hivyo akizungusha macho maaana anajua ingekua mtu mwingine angeagiza nyama kilo na ndizi k**a tano. Ili apate na ya kumbebea mdogo wake aliemwacha (Yunis) nyumbani.
Nickson:”Na mimi naomba na chipsi .” Alisema huku ana piga mahesabu yake “chipsi 2x2000 =4000 na nyama choma 5000 so inakuwa 9000 na soda moja 10,000 yake imeisha.”.Nickson akamgeukia mpenzi wake .
Nickson:”Baby unakunywa na soda gani?”.Alimuliza mpenzi wake kwa upendo na ujasiri kuwa bado yupo ndani ya bajet ya 10,000.
Stela : “Na grand malta.” Stela alijibu akiangalia upande mwingine wa hoteli ile ilokuwa bize kweli na ma bus yakishusha watu kutoka sehemu mbali mbali.Nickson moyoni alistuka kidogo akajisemea “Kiiiiibo na grand tena?”. Nickson akamwai waiter wakati stela akiangalia ma Bus “Mwambie haipo..” alisema kwa mdomo bila kutoa sauti.
Waiter:”Samahani Grand malta zimeisha”. Nickson akadakia fasta .
Nickson:”Leta na supa leta tu si ndio beby?. “alimuliza stela akiwa na confidence hawezi kataaa ndo soda aliokunywa walipo enda uzunguni park mara ya mwisho .
Stela :”Ndio na supa-leta ya moto tafadhali”.Stela alijibu akiwa hajui kuwa hana namna .
Waiter:”Sawa chipsi mbili na nyama choma na supa leta. Kaka utakunywa nini?”. Waiter alitaka kujua Nickson atakunywa nini.
Nickson:”Ah mi nina hii tayari”. Aliwahi kumwonesha soda ya takeaway alie kuja nayo .Sawa waiter akaondoka na kuwaacha wakiendelea mazungumzo yao.Nickson alitumia hizi sekunde kadhaaa akimwangalia mpenzi wake alivyo. Stela hyo siku alikua amevaaa suruali ya jeans inayombana nakuonesha umbo lake kiasi flani cha kuvutia . Alikua kavaa t-shirt ambayo Nickson alimpa k**a zawadi imeandika na maaandishi kwa nyuma ikisema “ExonGraphics” ambalo ndo jina la kampuni ambalo Nickson anatarajia kufungua hivi punde.
Nickson:”Enhee mpenzi ulikua unasemaje?”. Stela alimgeukia taratibu akiwa anaonekana kuwa alizama kwenye kukuru-kakara za pale stand inayo tazamana na hotel waliiopo.
Stela:”Nataka ugali maharage”. Alijibu hapo wakaaanza kucheka yeye pamoja na Nickson wakikumbuka kipindi kile ambacho Stela alimjibu Nickson wakati huo bado mahusiano yao hayaja anza alikua akimtesa tu na vituko vya stela vya hapa na pale.
Stela:”Baby lakini kweli mi nakushauri uachane na hiyo project bora ufanye biashara nyingine k**a kuchukua nguo kwenye soko la maimoria uje uuuze nipe hata mimi nitakuuzia. Pia ntakusaidia kuchagua.”
Nickson:”Lakini baby mimi nikipata Camera moja tu inanitosha kutoka katika maisha haya ”.Nickson alisema akiwa na matumaini.
Stela :”Kwani Camera kiasi gani?”. Aliuliza akitaka kujua yamkini ata weza kumpa ushauri.
Nickson : “Camera nzuri laki saba na lenzi laki tatu. “. Stela alianza tena kupandisha nyusi ya kulia akaweka nywele tena vizuri akanyoosha mkono kumuashiria Nickson aaache kuongea.
Stela : ”Sawa na umechanga sh ngapi mpaka sasa!? ”. Stela aliuliza huku amesogeza kichwa mbele na sikio linamtazamia Nickson asikie jibu kwa makini.
Nickson:”Ndo nimetoa laki na nusu sai….”. Stela akamkatisha.
Stela:”Baby iyo hela nyingine utapata wapi?”.
Nickson : “Ntajichanga tu Baby namwamini Mungu ”.Stela akawa ana guna mhhh mhhhh.
Stela: ”Sawa iyo hela yote uka nunue Camera uanze kutafuta wa kuwapiga picha na Studio huna na Laptop yako yenyewe ndo hyo……. ”. Stela ali kuwa kimya kidogo
Stela :” Baby kuwa mjanja umesoma mpaka umemaliza chuo umemaliza huezi kufanya vitu vya kijinga hivyo”.
Nickson : “Hayaaa sasa ushaaanza..”Nickson alijua tu wataaanza kugombana kisa mipango yake.
Stela : “Nishaanza nini? Afu nishakuambia usinikatishe nikiongea.”Stela aliendelea tu kuongea k**a ana rap nyimbo anayoipenda.
Nickson: “Sasa mpenzi sikia nikuambie kitu mimi ntakupa hela uongeze na yako tuanze biashara”.
Stela : “Nickson mimi nitawezaje kutoa hela hapo na unajua dhahiri ya mimi ni secretary wa pale Matumizi Company ya Yule Mmasai Vicent Mbekure ”Stela alikua anaongea kudhibitisha hela ndogo alionayo .
Nickson:”Sawa Baby mimi nitafanya kukupa ”.Nickson sio wa maneno mengi sana na alijua mpenzi wake anataka kumwambia kitu gani.
Stela : “Sawa mimi ntaenda maimoria mwenyewe ukinipa ”. Mara waiter akaja
Waiter: ”Jamani chakula chenu kiko tayari. Munaweza kwenda kunawa pale mkihitaji waiter alisema hivyo akinyoshea mkono bomba la kunawia. “Jamani karibuni na mu enjoy.”
Nickson wakasimama wakaenda kunawa k**a walivyoshauriwa wakala kwa kucheka kulishana hapa na pale. Mara wachokozane. Walipo maliza Nickson alilipa bill iliyo kuja k**a alivyotegemea na kupigia mahesabu . Nickson akampa mpenzi wake nauli na pia akaanza kutembea kwa miguu kuelekea ghetto kwake.
Stela : “Baby kwaheri! Nimeshiba” . Alimwita Nickson aliokuwa ameanza kutafuta njia ya kwenda nyumbani kwake . Nickson akageuka aka mpulizia busu la hewani mpenziwe.
Itaendelea….
Kujipatia story hii kamili tembelea
My Soulmate by Equatorstory Specials | Equatorstory Huwezi kumjua Soulmate wako mpaka pale mtapo pitia majaribu kadhaaa
04/05/2020
Hadithi mpya by Chrix L Kessy. Tembelea https://equatorstory.com/story/30/desire-shauku. Uwe mmoja wapo wa wasomaji wa hadithi hiii kali!
DESIRE- SHAUKU by Chrix L kessy | Equatorstory Siku zote mtaka yote kwa pupa ukosa yote, Tamaa mbele mauti nyuma, hii ni misemo ambayo baadhi yetu tunaifahamu kiundani. Basi naomba fuatailia simulizi hii fupi yenye kukujenga na kukuelimisha. kwa ushauri na maoni wasiliana nami kwa nambari 0673025050. barua pepe (email) [email protected]...
30/04/2020
Hakika utajifunza mengi katika kisa hiki, ambacho ni chakweli chenye kuelezea maisha halisia ya mtunzi na mwandishi wako. Danny Msimulizi Njombe. Tembelea sasa www.equatorstory.com
MAISHA YA MTUNZI by Danifordy ben | Equatorstory Hakika utajifunza mengi katika kisa hiki, ambacho ni chakweli chenye kuelezea maisha halisia ya mtunzi na mwandishi wako. DANIFORDY BEN
29/04/2020
17/04/2020
Tembelea www.equatorstory.com kupata account yako bure.
Like page kupata zaidi.
10/04/2020
Mtunzi : Chris L Kessy
Jina langu naitwa Daudi nina mke ambaye kwa sasa ni mjamzito, Mimba yake ina nipa mashaka sana kwani toka kipindi cha nyuma sikuwa na maelewano mazuri na yeye.
"hivi mke wangu huyo anaye kutumia text kila siku ni nani" Kulikuwa kuna ujumbe umeingia pindi nilipo kuwa nimeketi chumbani na mke wangu majira ya usiku.
'Jamani mume wangu mimi simjui kila siku nakwambia namba hiyo ni ngeni."
"sasa namba ngeni ndiyo kila siku iwe inakutumia ujumbe tu.."
Nilichukua ile simu ya mke wangu kwa lengo la kupiga sema kwa bahati mbaya haikuwa na salio na pia chaji ilikuwa imeisha ikazima ghafla. Nikaamua kulala zangu usingizi.
Siku iliyo fuata sikuweza kukumbuka kupiga hiyo namba kutokana na kuwa busy na mambo yangu.
Nilidamka asubuhi na kisha nikaelekea zangu kazini.
BAADA YA MIEZI 9 MKE WANGU ALIFANIKIWA KUJI FUNGUA SALAMA.
"Hongera sana mkeo amejifungua mtoto wa kiume."
alisema daktari.
"Asante sana" nilimjibu.
Tulitoka pale hospitali nikiwa na mke wangu pamoja na mama yake.
"Mwanangu Daudi mi nafikilia Lilian akakaae kwanza nyumbani na mtoto mpaka itakapo timu 40 ndiyo atarejea kwako ili na wewe upate muda mzuri wa kufanya mambo yako." Aliniambia mama mkwe.
"sawa" nilimkubalia.
Basi mke wangu ilibidi aondoke na mwanangu kwenda kukaa kwa mama yake.
Nilikuwa napeleka pesa za matumizi, pamoja na matunda, kuku wa nyama kwa ajili ya supu ili tu mke wangu arejeshe mwili wake. Nilifurahi sana kupata mtoto wa kiume kwani ndiyo ombi langu la kwanza kwa Mungu.
Kipindi chote icho nilikuwa na amani na mke wangu kwani sikuwa na mikwaruzo yoyote pia ata ile namba ya simu iliyo kuwa inakosea kutuma ujumbe hakuwa ikisumbua tena.
BAADA YA SIKU 40 KUFIKA NILIANDAA SHUGHULI KWA AJILI YA KUTOKA MWANANGU.
Shughuli hiyo ilifanyikia nyumbani kwa mama mkwe wangu, watu walikuwa wengi sana, walikula na kunywa mpaka kusaza.
Ilipo fika usiku nilimchukua mke wangu na kurudi nyumbani.
Nilipo fika nyumbani tuliingia ndani na kuketi sebuleni.
Wakati tulipo keti sebuleni tukipiga stori mbili tatu na mke wangu ghafla ujumbe ukaingia kwenye simu ya mke wangu.
Simu yake ilikuwa ipo mezani nilikuwa wa kwanza kuichukua na kuisoma wakati mke wangu aliniaga mara moja na kwenda chooni. Ujumbe ulikuwa unasema hivi.....
"Hongera sana kwa kuniletea mtoto wa kiume mke wangu.."
Nilishtuka, nilipoitazama ile namba kwa umakini nikaja kukumbuka ni namba ambayo ilikuwa inamsumbua sana mke wangu kipindi cha nyuma. Na ndiyo namba ambayo ilikuwa inafanya nisiwe na maelewano mazuri na mke wangu.
Nikawa najiambia mwenyewe "huyu mtu atakuwa ana mahusiano na mke wangu kwanini ampe hongera ya kujifungua.."
Nilipatwa na hasira nilijikuta na mtazama mwanangu akiwa amelala kwenye sofa, nilimchukua na kisha machozi yakawa yana nitoka... ile mke wangu anarejea kutoka chooni anafika na kunikuta nimembeba mtoto uku nikilia.
"vipi mume wangu una tatizo gani, na mbona unalia..? aliniuliza swali mke wangu.
"Nilicho kifanya nilinyanyua kidole na kumuonyesha mke wangu simu yake, alisogea na kuichua. Baada ya kuchukua kitu cha kwanza kukutana nacho ni ule ujumbe, aliusoma
. ile alipo maliza kuusoma akasema...
"Ukweli mume wangu mimi hii namba siijui... Naapa kwa Mungu wangu tena anihadhibu mimi siijui hii namba kweli tena.." kabla hajamaliza kuongea maneno yake nilijikuta nimechukua maamuzi ya kinyama sana kwani nilimnyanyua mtoto wangu juu na kisha nikampigiza chini... kwa kuwa alikuwa bado ni kichanga hivyo ilipelekea kichwa kupasuka, na damu ilitapaka pale sebuleni.. Nilimuua mwanangu..!!
"Mamaaaaa mwananguuuuu...!! mke wangu alipiga mayoe alilia sana alitoka pale na kuukimbilia mwlili wake pale chini.
Mimi nilibaki nimesimama uku mwili ukinitetemeka na jasho jingi likinitoka.
Wakati mke wangu akiwa analia ghafla ile simu yake ikaanza kuita tena... nilitoka na kisha nikaichukua, nilipoitazama ilikuwa ni ile namba ikipiga... Taratibu nikaipokea uku machozi yakinitoka na mafua kwa mbali...
"Unataka nini.." nilimuuliza
"Aisee kaka
Ngoja kwanza nikuambie kitu ambacho kitakusaidia wewe mkuu ambaye unasoma hii.
Hadithi hii inapatikana ndani ya equatorstory.com mwendelezo na hadithi k**a hizi utaipata ndani humo.
Basi twendelee
"Aisee kaka samahani sana unajua hii namba siku zote nilikuwa natuma jumbe nilikuwa najua ni ya mke wangu kumbe sio nilikuwa nakosea namba ya mwisho..." Nisamehe sana bwana... leo ndiyo nimegundua maana amenitafuta baada ya kutoka kujifungua .
"Nini....? nilijikuta nimetoa sauti kubwa ya mshangao...
JE MKE WANGU NITAMWAMBIA NINI MPAKA ANIELEWE..? NA JE UMEJIFUNZA NINI KUHUSIANA NA HII SIMULIZI...?
Kuendelea na hadithi hii tembelea
https://equatorstory.com/story/16/ep/2.
Asante
WRONG NUMBER (Namba ngeni) episode 1 | Equatorstory WRONG NUMBER (Namba ngeni) episode 1 Jina langu naitwa Daudi nina mke ambaye kwa sasa ni mjamzito, Mimba yake ina nipa mashaka sana kwani toka kipindi cha nyuma sikuwa na maelewano mazuri na yeye. "hivi mke wangu huyo anaye kutumia te