Randilen Wildlife Management Area

Randilen Wildlife  Management Area

Share

We are a community run Wildlife Management Area in Northern Tanzania, lying on the North East boarder of Tarangire National Park. #visitRandilenWMA

DC MONDULI AFANYA KIKAO CHA MAJUMUISHO, ASISITIZA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA WMA RANDLENI

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Gloriana Kimath, leo Mei 7, 2026, amefanya kikao cha majumuisho katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kufuatia ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha za hifadhi ya jamii ya wanyamapori katika Randleni WMA.

Katika ziara hiyo, jumla ya miradi 28 imekaguliwa ndani ya vijiji 8 vinavyounda hifadhi ya Randleni, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha rasilimali za uhifadhi zinawanufaisha wananchi moja kwa moja.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Kimath ametoa maelekezo mbalimbali kwa watendaji na wadau ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Miongoni mwa maelekezo hayo ni kuhakikisha miradi yote iliyobaki (viporo) inakamilika ndani ya mwaka 2026, pamoja na kusisitiza ushirikishwaji wa wananchi tangu hatua za awali kabla ya kuanza kwa mradi wowote.

Aidha, amewataka wataalam wa Halmashauri kuwa karibu na watendaji wa vijiji ili kutoa ushauri wa kitaalam utakaosaidia utekelezaji bora wa miradi hiyo.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kimath amemuelekeza Afisa Mipango kuhakikisha anawajengea uwezo watendaji wa vijiji ili waweze kutumia mfumo wa kielektroniki wa manunuzi serikalini (NEST), kwa lengo la kuongeza uwazi na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma.

Vilevile, amewasisitiza viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na wananchi kuendelea kulinda na kutunza hifadhi ya Randleni, akieleza kuwa ni chanzo kikuu cha mapato na maendeleo kwa jamii inayozunguka eneo hilo.

@glorianakimath 
@muhsinkassim2001 
@rs_mkoa_arusha 
@maelezonews 
@ikulu_mawasiliano 
@owm_tz 22/05/2026

DC MONDULI AFANYA KIKAO CHA MAJUMUISHO, ASISITIZA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA WMA RANDLENI Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Gloriana Kimath, leo Mei 7, 2026, amefanya kikao cha majumuisho katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kufuatia ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha za hifadhi ya jamii ya wanyamapori katika Randleni WMA. Katika ziara hiyo, jumla ya miradi 28 imekaguliwa ndani ya vijiji 8 vinavyounda hifadhi ya Randleni, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha rasilimali za uhifadhi zinawanufaisha wananchi moja kwa moja. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Kimath ametoa maelekezo mbalimbali kwa watendaji na wadau ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi hiyo. Miongoni mwa maelekezo hayo ni kuhakikisha miradi yote iliyobaki (viporo) inakamilika ndani ya mwaka 2026, pamoja na kusisitiza ushirikishwaji wa wananchi tangu hatua za awali kabla ya kuanza kwa mradi wowote. Aidha, amewataka wataalam wa Halmashauri kuwa karibu na watendaji wa vijiji ili kutoa ushauri wa kitaalam utakaosaidia utekelezaji bora wa miradi hiyo. Katika hatua nyingine, Mhe. Kimath amemuelekeza Afisa Mipango kuhakikisha anawajengea uwezo watendaji wa vijiji ili waweze kutumia mfumo wa kielektroniki wa manunuzi serikalini (NEST), kwa lengo la kuongeza uwazi na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma. Vilevile, amewasisitiza viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na wananchi kuendelea kulinda na kutunza hifadhi ya Randleni, akieleza kuwa ni chanzo kikuu cha mapato na maendeleo kwa jamii inayozunguka eneo hilo. @glorianakimath @muhsinkassim2001 @rs_mkoa_arusha @maelezonews @ikulu_mawasiliano @owm_tz

05/04/2026

Heri ya Sikukuu ya Pasaka!

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Randilen, tunawatakia Pasaka njema iliyojaa upendo, amani na matumaini mapya.

🌳

21/03/2026

Eid Mubarak! 🌙✨️

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Randilen (Randilen WMA) inawatakia Waislamu wote Sikukuu njema ya Eid al-Fitr, baada ya kukamilisha ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Siku hii ikawe chanzo cha furaha, amani na mshik**ano miongoni mwetu, huku ikiimarisha moyo wa kujali na kuhifadhi rasilimali za asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

✨️

16/03/2026

🌿Kupitia Mkutano wa Business of Conservation conference Bcc 2026 iliyofanyika Nairobi Kenya , Mafunzo muhimu kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Randilen WMA ni;

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Randilen (Randilen Wildlife Management Area) imekuwa mfano mzuri wa uhifadhi unaoongozwa na jamii.

Kupitia mpango wa nyanda za malisho (grass banks), takribani 95% ya wafugaji kutoka vijiji wanachama wananufaika kwa kupata maeneo ya malisho. Aidha, mapato yatokanayo na utalii yanaelekezwa katika maendeleo ya vijiji na shughuli za uhifadhi wa eneo, jambo linaloonyesha jinsi uhifadhi unavyoweza kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa jamii.

Randilen pia imechangia kuimarisha usalama wa ardhi kwa kusaidia kurejesha ardhi iliyokuwa imechukuliwa na watu binafsi na kuirudisha kwa manufaa ya jamii nzima, pamoja na kusaidia kutatua migogoro ya ardhi na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambapo takribani ekari 11,160 zilirejeshwa baada mipaka kubainishwa.

Vilevile, juhudi za kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori zimeimarishwa kupitia hatua mbalimbali za kukabiliana na tembo wanaoharibu mazao ya wakulima.

Kwa upande wa maendeleo ya jamii, fursa za ajira na kujiajiri zimeongezeka kupitia miradi k**a Kituo cha Utamaduni cha Wanawake cha Enaboishu.

Wakati huo huo, kikao kilisisitiza umuhimu wa utawala bora kwa kuimarisha mifumo ya usimamizi katika maeneo ya ulinzi wa maliasili, utalii na mapato, usimamizi shirikishi wa malisho, pamoja na kuboresha mawasiliano kati ya uongozi, watendaji na jamii kwa ujumla

Kwa ujumla, ujumbe mkubwa uliotolewa ni kwamba uhifadhi unaoongozwa na jamii unaweza kufanikiwa pale ambapo jamii zinamiliki kikamilifu maliasili zao za asili, zinazisimamia kwa uwajibikaji, na kunufaika moja kwa moja na matunda ya uhifadhi huo.

Photos from Randilen Wildlife  Management Area's post 05/03/2026

Katika mkutano wa Business of Conservation Conference unaofanyika Nairobi, Meneja wetu Meshurie Melembuki aliiwakilisha Jumuya ya Hifadhi ya Wanyamapori Randilen (Randilen WMA) na kuwasilisha uzoefu wa jamii yetu katika mjadala wa kimataifa kuhusu uhifadhi wa mazingira.

Kaulimbiu ikiwa “Kubadilisha Simulizi ya Uhifadhi: Ni Jukumu la Kila Mtu Afrika na Zaidi,” mkutano huo ulijikita katika kuhamisha mazungumzo ya uhifadhi kutoka kwenye nadharia kwenda kwenye vitendo.

Kupitia kipindi cha "fireside chat" kilichoongozwa na mada isemayo “Kutoka Ngazi ya Jamii: Mifumo ya Kibiashara katika Uhifadhi unaoongozwa na Jamii,” wazungumzaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika walijadili nini kinafanya uhifadhi unaoongozwa na jamii kufanikiwa na changamoto zinazobaki. Ujumbe mmoja uliibuka wazi: jamii lazima ziwe na mamlaka ya kweli katika kufanya maamuzi, umiliki halisi wa juhudi za uhifadhi, na manufaa yanayoonekana kutoka katika uchumi wa wanyamapori.

Akishiriki uzoefu wa Randilen WMA, Meshurie alisisitiza kuwa mafanikio yetu yanatokana na ushiriki wa jamii na mifumo imara ya uongozi na usimamizi. Pale jamii zinapopewa nafasi ya kweli katika kufanya maamuzi, imani huongezeka na uhifadhi unakuwa jambo ambalo watu wanalilinda na kuliongoza wenyewe.

Ni ukumbusho muhimu kwamba mustakabali wa uhifadhi hautajengwa kwa kuitenga jamii, bali utajengwa kutoka ngazi ya jamii, kwa jamii kuwa katikati ya kila hatua.

ALU | International Institute for Environment and Development (IIED) | ALU School of Wildlife Conservation

Photos from Randilen Wildlife  Management Area's post 24/02/2026

Hongera kwa Olais Melakiti, mshindi wetu katika Chemsha Bongo ya (Facebook).

11/02/2026
Photos from Randilen Wildlife  Management Area's post 09/02/2026
Want your business to be the top-listed Government Service in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address

Arusha