Mkuu wa Wilaya Longido

Mkuu wa Wilaya Longido

Share

Ukurasa rasmi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Longido, Karibu tukuhudumie.

15/07/2024

Mwenge wa Uhuru 2024 Mkoa wa Arusha

08/07/2024
17/03/2024

Mikutano ya Hadhara...

28/01/2024

Wananchi wote wa maeneo husika mnakaribishwa.

Photos from Mkuu wa Wilaya Longido's post 14/10/2023

Misa Maalum ya Kumbukizi ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu, Babati Mkoani Manyara leo tarehe 14 Oktoba, 2023.




Photos from Mkuu wa Wilaya Longido's post 01/09/2023

UTAMBULISHO WA MRADI WA MAJI KWA KAYA ZISIZO NA UWEZO

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Marco H. Ng'umbi ameshiriki hafla ya kuutambulisha Mradi wa kupeleka huduma ya maji kwa kaya zisizo na uwezo kwa gharama nafuu. Katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya aliwaeleza Washiriki kuwa Serikali ya Wilaya pamoja na Mamlaka za Maji AUWSA na RUWASA tayari wameshaweka mikakati ya kufufua Visima vyote ambavyo havitumiki ili vianze kutumika na kuongeza nguvu kwenye mkondo mkubwa wa maji unaotoka Mto Simba pamoja na kulinda vyanzo vyote vya maji Wilayani. Hata hivyo ameipongeza Mamlaka ya Maji AUWSA kwa kazi wanayofanya usiku na mchana ya kutengeneza miundombinu ya maji ambayo inaharibiwa na watu wasio na nia njema na kupeleka huduma ya maji kwa wananchi pamoja na changamoto za hapa na pale. Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Wilaya ametoa Agizo kwa Wenyeviti na Vitongoji na Vijiji na Watendaji wao kuwa kuanzia sasa hatosita kuwak**ata na kuwapeleka Mahak**ani kwa uharibifu wa Miundombinu ya maji utakaofanywa kwenye maeneo yao bila kuchukua hatua kwani ugharimu maisha ya Watu wengine wasiohusika na uharibifu huo. Aidha, amewasihi Wadau hao wakati wa utekelezaji wa Mradi huo kuweka kwenye mpango na kujenga Mbauti kwa ajili ya kunyweshea Maji Mifugo. Alimalizia kwa kutoa Rai ya kwenda kuwashirikisha Wananchi kikamilifu kwani wao ndio wanawatambua Wananchi wasio na uwezo, na kuwashukuru Mamlaka ya Maji AUWSA na Shirika la VEI kwa kuleta Mradi huo wa kuwezesha kaya zisizo na uwezo kupata huduma ya Maji Wilayani Longido na kuwahakikishia kuwa Serikali imeupokea na itatoa ushirikiano wa kutosha.

Akizungumza katika utangulizi wake, naye Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Longido Bw. William Shayo alisema "Mradi huu utakwenda kugusa zile Kaya Maskini kabisa ambazo kipato chake ni cha chini wakati wa utekelezaji wake".

Kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Longido naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mhe. Saimon Oitesoi amewashukuru Wadau hao wa maendeleo wakishirikiana na Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha kwa kuwajali Wananchi wa Longido kwa kuleta Mradi huo kwani hutaenda kugusa hasa zile kaya zisizo na uwezo wa kufanya maunganisho ya Maji kwa sababu ya ukubwa wa gharama.

Photos from Mkuu wa Wilaya Longido's post 31/08/2023

HAFLA YA KUFUNGA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KETUMBEINE.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Marco Ng'umbi amelishukuru Shirika la World Vision Tanzania kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo k**a ya Afya, Elimu, Maji na kupeleka vyakula mashuleni kwa muda wa miaka 15 na kuisimamia vizuri kwa mda wote huo, kwa niaba ya Wananchi wa Longido amewasihi Wadau hao kwenda kuangalia maeneo mengine ya Wilaya ili kwenda kutekeleza miradi k**a hiyo baada ya kufunga mradi wao kwenye Tarafa ya Ketumbeine.

"Tunawashukuru sana kwa kazi kubwa mliyoifanya kwenye Wilaya ya Longido kwani hii ni Sadaka kubwa sana mmefanya kwa kuwajali wahitaji. Hakika Watoto na wanufaika wengi wemenufaika sana. Hata hali ya usomaji na kujiunga na shule imefanikiwa kwa asilimia 100%," alimaliza kwa kusema.

Naye Mkurugenzi wa World Vision Tanzania ameshukuru Mungu na Wananchi wanufaika na miradi hiyo kwa kuifikia siku ya leo na kumaliza mradi uliokuwa ukitekelezwa kwa kipindi cha miaka 15 kwenye Tarafa ya Ketumbeine , pi amemshukuru Mgeni rasmi kwa kuweza kutenga muda na kushiriki shghuli hiyo, aidha ameipongeza timu nzima iliyotekeleza na kusimamia mradi wa Ketumbeine AP pamoja na kutoa shukrani za kipekee kwa Wafadhili wote wa ndani na nje wa miradi iliyotekelezwa kwenye Tarafa ya Ketumbeine.
"Hakika namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa mema na baraka hizi zote" alisema.

Want your business to be the top-listed Government Service in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Longido
Arusha