Nuru ya Ulimwengu

Nuru ya Ulimwengu

Share

Yohana 12:46
Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.

19/09/2024

Watu wa mko tayari?


29/08/2024

Watu wengi wanafikiri wanaweza kupoteza uzima wa milele kwa sababu wanadhani ni _k**a BOX_ wanakabidhiwa walibebe na wawe makini wasidondoshe. šŸ˜€

Ndugu, uzima wa milele siyo BOX.. ni Roho wa Mungu anaungana na roho yako kuwa kitu kimoja kwa nguvu ya ufufuo wa Yesu Kristo.
Hakuna FORCE ulimwenguni humu au ule ujao unaoweza kuuvunja huo muunganiko.

Wewe tulia katika pendo la Baba. Fanya mambo mengine. Focus kwenye ukuaji wa kiroho. Kazi ya kulinda wokovu mwachie aliyekuokoa.

—Global Family Gatherings
"God's Standards"

17/08/2024

Chukua hii!!

Unaweza ukawa unafanya kazi zote kanisani—tena kwa bidii, ukajitahidi kuwa na tabia njema sana... na ukawa mwombaji wa kimataifa, mtoaji mkubwa, unaenda uinjilisti wa nyumba kwa nyumba, masokoni na barabarani, misheni porini, vijijini ukawa hukosi, NA BADO UKAWA HUJAOKOKA.

šŸ¤”Mambo hayo yote ni ya MUHIMU SANA lakini IKIWA HUNA UHAKIKA KUWA UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO KWA KUFA NA KUFUFUKA KWAKE YESU KRISTO ndugu yangu hayo YATAKUWA BURE KABISA.

✊Kama kila siku unajitakasa asubuhi, mchana unajiona haufai mbele za Mungu, unaogopa kwenda Jehanamu, unajitahidi usikose mbingu..WEWE HUJAOKOKA.

Unaidharau kazi ya YESU MCHANA KWEUPE.
"God's Standards"

14/08/2024

Sikia hii!!!

Msamaha wa dhambi ndiyo kiini cha Wokovu. Unapatikana mara moja kwa kuamini dhabihu bora ya Yesu Kristo yaani kufa na kufufuka kwake.

Hakuna namna ya bora ya kuhubiri wokovu bila kuweka sawa hilo.šŸ‘‡šŸ‘‡

ā€œā€¦.maana ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zaoā€¦ā€

ā˜ļøā˜ļøhilo ndilo jambo maalumu lililomleta Yesu Kristo.

Na YEYE PEKE YAKE NDIYE ANAYEWEZA KUKUPA ONDOLEO LA DHAMBI.

ā€œGod’s Standardsā€

07/08/2024

Kujitahidi kuacha dhambi ili UOKOKE ni kujidanganya. Yesu katika huduma yake duniani alifuatwa na makahaba, walevi, watoza ushuru, kwa sababu walikubali Mafundisho yake.. waliona kabisa kwa Yesu kuna dawa ya yale yanayowasumbua.

walisikia mara nyingi akisema "UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO" Dawa ya dhambi haianzi na kuacha, inaanza na KUSAMEHEWA kwanza kisha ndipo unapewa stamina ya kuziacha.

Kuacha dhambi zako uende kwa Yesu ni sawa na kupona kwanza kisha uende kwa daktari.

COME AS YOU ARE. NJOO KWA MWOKOZI


"God's Standards"

30/07/2024

Jiandikishe kwa namba hizi +255 683 507 807


20/07/2024

Dalili ya kwanza kuwa umejipanga kwenda kudanganywa kanisani ni KWENDA bila BIBLIA au kwenda na Biblia ambayo huwa unafungua pale mhubiri anaposema "TUFUNGUE KITABU FULANI"

Biblia inayokaa kabatini na kufunguliwa Siku ya Makusanyiko tu haitakusaidia.

Ni vyema kujiwekea utaratibu wa kujifunza Biblia mwenyewe au kupitia mambo uliyofundishwa kwenye kusanyiko k**a ndivyo yalivyoandikwa.

Ukiona kuna kitu hukielewei muulize aliyekufundisha au uliza kwenye Makusanyiko madogo na waamini wengine..

Faida ya kuwa serious na mafundisho ni nyingi...

Kwanza itakusaidia wewe mwenyewe lakini pia itamsaidia Mwalimu wako ajue kwamba WANAOKUJA KUMSIKILIZA SIYO MAZEZETA.. Yeye pia ataongeza bidii katika kujifunza na kujiandaa kufundisha.

Lakini ukija bila Biblia, umejiandaa kuja kushangilia unabii wa nabii na swaga za mtume au suti ya Mchungaji..utashangaa utakapoambiwa "MAANDIKO YANASEMA KWENYE KITABU CHA ELIYA 2:5 UKITOA SADAKA INAYOUMA MUNGU ANAJIBU KWA MOTO" Na utasema "AMEEEEN"

19/07/2024

"Hata asingenisaidia Mungu angemwinua mtu mwingine anisaidie"

.. hii sentensi ni mbaya, ni kukosa kuwa na shukrani... katika maisha yako yote hata siku moja usichukulie poa muda, rasilimali na msaada ambao mtu amekupa.

usisahau haraka ulivyoshikwa mikono. Usiwatumie watu k**a makopo na kusema...
"Mungu alitaka akutumie wewe kwa yale majira"...baada ya hapo unamwona k**a takataka.

tambua nafasi ya watu kwenye maisha yako. Linda sana hiyo.

Be very grateful.
GRATITUDE IS SPIRITUALITY.

"God's Standards"

16/07/2024

Mtu yeyote akiamua kuwa na matokeo katika kanisa la mahali anakuwa na matokeo.

Kila mmoja amewezeshwa katika ufufuo wa Yesu Kristo kuwa makao ya Mungu na Mungu kufanya kazi ndani yake.

Cha muhimu ni kuwa tayari kufundishwa na kufundishika.

Unaweza kuwa na mchango katika hilo kusanyiko.

Unaweza pia kuwa kikwazo. Inategemea umeamua kuelemea wapi!

Chagua sawa. Kuwa chombo cha huduma ya Roho.

Fanya Uinjilisti na Uanafunzi; ukiwa na changamoto ongea na kiongozi wako.


ā€œGod’s Standardsā€

13/07/2024

Kumwamini Yesu Kristo ni jambo bora kabisa kuwahi kufanywa na mwanadamu. Ila k**a hujui maana yake au kumwamini Yesu kumekufanyia nini na kutakufanyia nini, unaweza kujikuta unatukuza KUJIAMINI au KUAMINI JITIHADA ZAKO.

šŸ‘‰Only look unto him.
šŸ‘‰It's not a STUPID MOVE to believe Jesus.
šŸŽˆNimemwamini Yesu Kristo.

"God's Standards"

Photos from Nuru ya Ulimwengu 's post 20/06/2024

Hello!!
Ni furaha yangu kukaribisha jumamosi hii katika kongamano hili kubwa la Vijana.

22.06.2024
03:00 Asu - 10:30Jioni

Ni Kibaga - Kinyerezi.

01/06/2024

Yesu anasema "Nawapa uzima wa MILELE, wala hawatapotea KAMWE" akaongezea "wala HAKUNA mtu atakayewapokonya katika mkono wangu"

Mwandishi wa Waebrania anasema Mungu amesema "Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena KABISA"; anasema "Kwa dhabihu moja idumuyo hata MILELE amewakamilisha hata MILELE hao wanaotakaswa"

Yesu aliingia patakatifu kwa damu yake akapata Ukombozi wa MILELE.. anaongezea Yesu amekamilishwa akawa sababu ya wokovu wa MILELE"

Wokovu mpotevu (usio wa milele); siyo wa Yesu Kristo.

Cc.
—Ap. Shemeji Melayeki
"God's Standards"

Want your business to be the top-listed Government Service in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Arusha