Sehemu ya 3.....
Ndio maana leo vijana wengi suala la kuoa limekuwa mtihani, hawajui nani wamuoe, lini na kwa nini? Ukiwauliza utasikia 'bado nipo nipo kwanza'
Pia mabinti wamekuwa na uhitaji sana wa kuolewa kwa hofu tu ya umri kuwatupa mkono na hofu ya kuonekana vibaya kwa jamii kuwa wana gundu! Hivyo wengine wanajiingiza tu popote ilimradi tu waonekane wameolewa! Yaani ni vurugu tupu!
Kwa hiyo hoja yangu leo ni kuwa, vijana wanapaswa kupunguza 'kutumia akili na utashi wa nafsi' ktk kutafuta mwenzi, bali zaidi wazingatie tija ya 'utu wa ndani wa mtu' ambao kwa lugha nyepesi tunaweza kusema wazingatie 'lengo' 'tabia' na 'mazingira' halisi ya kumtafuta huyo mwenzi!
Kwa mfano, kuna watu tumesoma shule ambazo sio sahihi kwetu kwa sababu tu ndio zilizokuwepo ktk mazingira yetu! Pia kuna aina ya maisha tuliyoishi ktk familia zetu kwa sababu tu hatukuwa na chaguo lingine!
Kuna vijana wengi kwa hakika wameshindwa kupata wenzi bora kwa sababu wamekuwa na vigezo vingi vyenye msukumo wa tamaa za nafsi zaidi! Wamewakataa tena kwa ujasiri kwa sababu tu hawana muonekano wanaoupenda, hasa mabinti!
Kwa hiyo, km vile neno tuliloanza nalo, tusizitegemee sana akili ktk kuchagua mwenzi, tumtegemee Mungu zaidi! Tusitegemee kwa kuwa tumemuomba Mungu, basi atatuletea wenzi kulingana na utashi wetu, mawazo ya Mungu sio k**a yetu, wala njia zake sio k**a zetu! Unaweza kutamani mfupi akakupa mrefu, ukitaka mweupe anakupa mweusi, n.k
Mwenzi akikujia, akakueleza haja ya moyo wake, kabla ya kumjibu 'Ndio' au 'Hapana' pata muda wa kutafakari. Muombe akupe muda wa kutafakari. Funga fikra, fungua moyo. Muulize Mungu, shirikisha Mchungaji wako ndipo utoe jibu!
Naomba kuwasilisha!
Share na vijana wengine tufanye marekebisho!
Ongeza Ufahamu
Hosea 4:6 Maarifa ni Uzima!
Sehemu ya 2..
Je! ni makosa kuzingatia vitu hivyo? La hasha! Si makosa. Sasa tatizo lipo wapi? Twende sawa!
Tatizo ni pale ambapo utashi wa akili na fahamu kwa msukumo wa tamaa ya nafsi, ndio vinakuwa vigezo pekee vya kuzingatia!
Vijana wanasahau kuwa, vigezo hivyo vyotewanavyovizingatia ni vya muda tu na vinabadilika kutokana na wakati na mazingira!
Kwa mfano, binti anaweza kuwa na muonekano wa kuvutia sana kimaumbile! Atakuwa na hips, kifuani chuchu zimesimama, makalio yamejaa vizuri, miguu ya bia n.k
Lakini atakapoingia ktk mahusiano ya kimapenzi, taratibu anaanza kubadilika, akijifungua mtoto mmoja tu anabadilika kabisa kimuonekano! Chuchu zinakuwa maziwa kwa kuwa ananyonyesha, hipsi zitapungua kutokana na kubeba jukumu zito la kubeba ujauzito kwa muda mrefu, akishajifungua tumbo linaongezeka n.k!
Sasa kuanzia hapo nafsi ya mwanaume inaanza kushauri ujinga! Inamwambia mwanaume huyu mwanamke sio type yako kabisa, laiti k**a ungempata yule mdada pale ingekuwa super sana! Cheki shape, cheki huo mguu, tazama hapo kati alivyokatika vizuri! Na mengine mengi tu ya kijinga!
Haitaishia hapo tu, itamsukuma mwanaume mpaka ihakikishe anatekeleza hilo! Matokeo yake ndio kimezaliwa kitu kinachoitwa 'kuchepuka' au 'kudate'
Kwa upande wa mabinti pia, mwanaume wake pesa zitaisha, uchumi utayumba, gari litapaki au kuuzwa kabisa, kitambi kitayeyuka, hapo ndipo utasikia yaani mimi huniwezi kabisa, mwanamke matunzo, nahitaji kwenda saruni, nahitaji makeup, nguo nzuri, mafuta ya kujipaka ya bei ghali n.k! Kwa hiyo kinachofuata hapo, anaibuka mwezeshaji wa nje, anatoa huduma naye anapatiwa huduma! Mwisho wa siku 'kuchepuka' ndio agenda!
Haya yote yameletwa na nini? Uhuru wa vijana katika kuamua na kuchagua! Zamani za wazee wetu mambo haya hayakuwepo kabisa. Hata pale walipokuwa wanaamua kuoa mke wa pili, hapakuwa na migongano kwa kuwa tija ilizingatiwa na ndio maana wanawake waliweza kuishi hata nyumba moja na hapakuwa na mambo ya kuwekeana limbwata!
Itaendelea sehemu ya 3...
SOMA HII KWA MAKINI ITAKUSAIDIA!
Mithali 3:5-8 inasema:
"Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako"
Ukitafakari kwa kina maandiko haya utagundua kitu na ndicho natamani leo tushirikishane ili kuboresha fikra na fahamu zetu!
Kutokana na uzoefu na changamoto nilizopitia ktk suala zima la mahusiano ya ndoa nimejifunza mambo mengi sana!
Kwanza nimeanza kwa kujiuliza, tofauti iliyopo kati ya ndoa za wazee wetu na hizi zetu za sasa inaletwa na nini?
Majibu yakawa mengi tu! Kwanza mazingira ya utandawazi, elimu, imani za Dini, uhuru wa kuamua na kuchagua na mengine mengi!
Lakini mimi leo natamani nijikite zaidi katika hilo la "Uhuru wa kuamua na kuchagua"
Ukirudisha kumbukumbu nyuma kidogo aidha kwa maisha yako halisi au kwa kusimuliwa, utaona kuwa zamani katika suala zima la kuanzisha mahusiano ya ndoa, vijana hawakuwa na nafasi kabisa katika kuamua wala kuchagua!
Kwamba ni lini? Wapi? Yupi? au kwa nini? Nimuoe au niolewe na huyu lilikuwa ni jukumu la wazazi wenyewe!
Wakati mwingine niliwahi kuwaza, Je! ulikuwa ni udikteta wa wazee wetu!? Jibu ni hapana, ilikuwa ni busara na hekima zao! Twende taratibu utanielewa!
Zamani wazee wetu walitumia sana 'utu' wa ndani wa mtu sahihi wa kuingia nae ktk ndoa!
Hawakuendeshwa na hisia za nafsi wala utashi wa muonekano wa nje!
Ndio maana walibeba jukumu la kuwachagulia vijana wao wenzi na ndoa zao zilikuwa bora, talaka zilikuwa zenye ulazima tu, migogoro ilikuwa michache na hapakuwa na watoto wa mitaani k**a ilivyo leo!
Leo hii mwanaume ili ampate mke wa kuoa, vigezo ni k**a vile shape, makalio, sura, rangi, mavazi na mengine mengi yenye mlengo k**a huo!
Vivyo hivyo kwa mabinti, wataangalia zaidi muonekano wa huyo mwanaume, anavaaje, kimo chake, kazi yake, kipato chake na mengine mengi pia!
Itaendelea sehemu ya 2
Kupiga hatua ni shauku ya kila mwanadamu chini ya jua! Hii ni kutokana na sababu kuwa ili safari itimie, ni sharti hatua zisonge mbele! Kwa kuwa safari ni matokeo ya mwendo kutoka sehemu moja hadi nyingine na kinachoufanikisha mwendo huo ni hatua!
Katika maisha yetu ya kila siku, yapo mambo mengi ambayo yanatupa kufurahi kwa kuwa tunaona tumepiga hatua. Aidha mtu alikuwa amepanga, lkn sasa amefanikiwa kujenga, kwake ni hatua. Pia katika masomo, mtu alikuwa ngazi moja ya chini aidha darasa la kwanza au kidato cha kwanza au mwaka wa kwanza n.k, kwa hiyo anapopanda ngazi inayofuata, anafurahi kwa kuwa kwake ni hatua!
Lkn kuna vitu ambavyo ndio natamani leo tuvichunguze na kuviongeza ktk fahamu zetu!
Kwa mfano kuna watu wamekuwa na desturi ya kufanya tafrija kwa ajili yao, watoto wao au hata wapendwa wao, kwa lengo la kukumbuka siku zao za kuzaliwa, ni jambo jema!
Lakini leo napenda kukukumbusha kuwa unapoona umefikia tarehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa, ujue kuwa umepiga hatua, na kwa kuwa hatua ndio hukamilisha safari, basi kimaisha kila unapoongeza mwaka mmoja wa kuishi kwako, ndipo pia umepunguza mwaka mmoja wa kuishi kwako!
Namaanisha kuwa, km ungeishi miaka 100, basi tayari umebakiza 99! Kwa hiyo nadhani jambo la msingi kuzingatia wakati ukifanya tafrija ya birthday, basi pia kumbuka kufanya na tathmini ya jinsi ulivyoishi kwa kipindi chote, na uone ni wapi pa kuboresha kwa kipindi kijacho ili kiwe bora zaidi!
Kwa mfano maeneo ya kufanyia tathmini ni pamoja na mahusiano yako!
Mahusiano ya roho yako na Mungu,
Mahusiano yako na ndugu,
Mahusiano yako na majirani,
Mahusiano yako na familia yako! N.k
Hii ndio itakuwa maana halisi ya kupiga hatua, lkn km utakuwa unaishi kana kwamba safari haina mwisho, basi safari yako ni bure kwa kuwa unaweza kusafiri kwa gharama tena umbali mrefu halafu unaenda kupata ajali stand mwisho wa safari!
Tafakari, piga hatua zenye tathmini kwa safari yenye tija!
Naomba kuwasilisha! Ubarikiwe!
Bila shaka tangu tumekuwepo katika maisha ya ulimwengu huu tumewahi aidha kusikia au kuhudhuria ktk misiba ya watu wa rika mbalimbali!
Natumaini kuwa kuna vitu vingi tunajifunza. Vipo vinavyohusu tofauti za kiimani, zipo zinazohusu tofauti za kiuchumi, tamaduni, Mila, n.k.
Lkn jambo kubwa ninalotamani tujifunze ni tofauti iliyopo kati ya hao ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki na sisi tuliosalia ktk uhai huu!
Tofauti ninayoiona ni ktk dhana ya safari. Wao wameimaliza safari yao hivyo ni rahisi kwa sisi tulio hai kuwafanyia tathmini ya namna walivyoishi na kujua hatma yao ilivyohitimishwa!
Lkn kwa sisi tulio hai, bado tuna safari ambayo ki ukweli hatujui itakoma lini, kwa namna gani na tukiwa wapi.
Tumekuwa bize kutafuta namna tutakavyoweza kuboresha maisha yetu kila uchao, lkn tukijisahau kufanya marekebisho ktk maeneo kadha wa kadha yaliyo na mchango mkubwa ktk kuamua hatma yetu baada ya kuhitimisha safari hii.
Hivyo, ninapenda kuwakumbusha kuwa, kila unapoona ajali kwa mwingine, ni ishara tosha kukukumbusha kuwa kuna sehemu umakini aidha haukuwepo au ulipungua ndio ikawa sababu ya ajali hiyo!
Hivyo, kuliko kutumia muda mwingi kuwatakia kila la kheri huko waendako waliokwisha fariki, tutumie muda mwingi kurekebisha mienendo yetu na namna ya kuishi ili hiyo kheri iwe ni haki yetu baada ya kufariki hata k**a waliosalia wasipotutakia!
"Andaa Hatma yako Mapema"
27/12/2019
Bila shaka umewahi kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine aidha kwa miguu au kwa chombo chochote cha usafiri! Hebu jaribu kutafakari pamoja nami: kila mahali ulipofika umekuwa ukikutana na watu wengine au basi vyombo vingine vya usafiri navyo vikiwa njiani vikielekea huku na huko! Sasa jiulize, Je mlitoka sehemu moja hata mkutanie hapo? Au Je mlianza safari wakati mmoja? Mbona mmekutana kwa wakati huo?
Ninachotamani kukuongezea ktk ufahamu wako ni kuwa safari ya maisha inamuhusu mtu husika, kwenda sehemu husika, kwa wakati husika! Haijalishi nani ametangulia kuondoka, au nani katoka wapi! Cha msingi unatakiwa uwe na dira itakayokuwezesha kufika uendako, lkn pia uwe na malengo yatakayoipa safari yako tija na mantiki! Vinginevyo utajikuta unaiga safari za watu eti kwa sababu umekutana nao na ukaona safari zao ndio bora!
Unachotakiwa kukumbuka ni kuwa kwa kila hatua uliyoichukua kwa wakati ili kuianza safari yako, inatosha kabisa wala huitaji kutembea kwa kukurupuka!
Chunga sana: K**a huelewi unapoelekea, kila njia itakufikisha!
Chuki yenye upendo ndani yake!
Ndugu yangu napenda nikujulishe tu kuwa tangu umepata kufahamu maana ya maisha, bila shaka umepata uelewa wa kutosha kuhusu "CHUKI" na "UPENDO". Vitu hivi ni k**a mapacha kwa kuwa kila kimoja kinajitanabaisha kutokana na uwepo wa mwenzake, ni k**a ilivyo kwa giza na mwanga, njaa na shibe, furaha na huzuni n.k. Lakini hebu tujiulize kwa pamoja, mara ngapi umewahi kumpenda mtu au kupendwa na mtu!? Au mara ngapi umewahi kumchukia mtu au kuchukiwa na mtu!? Jibu jepesi tu ni watu wengi!
Lakini hoja yangu leo si kupendwa/kupenda wala kuchukiwa/kuchukia, bali ninataka tujifunze kuhusu sababu za hiyo chuki au huo upendo! Ni kweli kuna wakati tunawapenda/tunapendwa na watu kwa sababu tofauti tofauti k**a vile yale tuliyowatendea/waliyotutendea, muonekano, n.k, lakini pia tumekuwa tukichukia/kuchukiwa na watu kwa sababu mbalimbali!
Ninachopenda kukukumbusha leo ni kuwa, ni vema sana na haki k**a sababu yako ya kumpenda mtu itakuwa ni kuepuka kumchukia kuliko ukajikuta unamchukia kwa kuwa unaepuka kumpenda!
Chunga sana kwa kuwa "Chuki yenye msukumo wa Upendo ni nzuri kuliko Upendo wenye msukumo wa chuki"!
Wapendeni Adui zenu, waombeeni wanao waudhi"
Nafasi ya adui katika kupiga kwako hatua!
Jiulize k**a asingekuwepo Goriathi Daudi angesifiwa kwa kipi? K**a wasingekuwa wafilisti, nguvu za Samsoni zingedhihirishwaje? K**a si njaa, umuhimu wa chakula ungetoka wapi? K**a si magonjwa, umuhimu wa matabibu ungekuwa nini? Na k**a si ujinga, kusoma kungekuwa na tija ipi?
Kuna wakati nyani wanashangilia sana wanaposikia aliyekuwa akiwafukuza kila siku wasile mahindi shambani kwake! Baada ya muda kupita msimu wa kulima ulifika shamba lile halikulimwa nyani wakaanza kufa kwa kukosa chakula, ndipo waligundua kuwa kumbe waliyekuwa wanamuona adui yao ndiye aliyekuwa anawalimia mahindi!
Nasi katika maisha haya tunao watu ambao kimtazamo ni maadui zetu kwa kuwa tu wamekuwa kinyume na utashi, fikra, mitazamo na malengo yetu, lakini tukumbuke kuwa uwepo wao ndio unatufanya kuziboresha hatua zetu kuelekea mafanikio k**a wakiondolewa huenda tusipige hatua kwa kuwa tutalala tukiamini mambo ni rahisi!
Pia zimekuwepo nyakati tofauti tofauti katika maisha za furaha, huzuni, amani, vita, shibe, njaa n.k, yote haya yameruhusiwa ili kuleta maana halisi ya maisha!
Chunga sana usije ukaomba adui yako aondolewe utaharibu maisha yako kwa kuwa analo jukumu kamili la kuyafanya maisha yako yawe bora kila siku!
"Wapendeni Adui zenu, waombeeni wanao waudhi"
Mungu aliumba vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana!
Leo natamani tujifunze kitu katika hivyo vinavyodhaniwa kuwa havionekani. Hapo ulipo jaribu kuandika herufi au namba yoyote kisha itazame kwa makini! Ukiwa makini utagundua kuwa kwa kila herufi au namba uliyoandika inaonekana ilivyo kwa sababu kuna sehemu zimebaki wazi bila kupitiwa wala kuguswa na maandishi yako!
Sasa tunajifunza nini hapo? Kumbe yasiyoonekana ndio yanayafanya yanayoonekana kuonekana! Hebu jiulize k**a hicho ulichokiandika kisingeacha hizo nafasi zilizowazi, bila shaka hiyo isingesomeka k**a ulivyoiandika!
Ngoja nikupe story fulani fupi! Siku moja Mwalimu mmoja alitaka kuwafundisha wanafunzi wake kuondoa mazoea na kuishia kuamini katika vinavyoonekana tu. Basi alichukua karatasi nyeupe isiyo na doa wala alama yoyote, kisha akaweka alama ya doti ndogo nyeusi katikati ya ile karatasi, alivyomaliza akainua ile karatasi juu akiwaonyesha wale wanafunzi akawauliza jamani mnaona nini kwenye hii karatasi? Wote kwa ujasiri tena kwa sauti kubwa wakajibu "Doti Nyeusi" kisha akauliza kweli mna uhakika? Wakajibu Ndioooooooooo! Baadae awauliza mmewezaje kuona doti ndogo nyeusi lakini msiweze kuona rangi nyeupe ambayo ndio imechukua sehemu kubwa ya hii karatasi!? Mwisho wakagundua kuwa ni mazoea tu yaliwagharimu wakaamini kuwa doti ilionekana kwa kuwa iliandikwa lakini kumbe ili ionekane ilihitaji sehemu nyeupe iliyoachwa wazi bila kuandikwa kitu!
Nasi katika maisha tujifunze kuwa wakati unapokuwa na kitu unaweza kujisahau na kudhani umekamilika, kumbe ili ujue umuhimu wa kuwa na kitu, ni sharti ukose kitu ili ukipata kitu utambue thamani ya hicho kitu!
Vivo hivyo kwetu binadamu kila mtu ana maana sana katika maisha yetu hata k**a hawajawahi kutupatia kitu, uwepo wao tu unatosha maana unatusaidia kujitathimini! Tajiri anajijua alivyo kwa kuwa yupo mwingine maskini, mrefu amejijua kutokana na uwepo wa mfupi, mnene kwa sababu ya mwembamba, n.k!
Hivyo yasiyoonekana ndio yanayoyafanya yanayoonekana yaonekane
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Telephone
Website
Address
Elijah5emmanuel@gmail. Com
Arusha
MAJIYACHAI
