25/01/2018
Sehemu ya waumini wa masjid daarul hikma wakisali sala ya eid elfitr juu ya floo ambayo haina kuta.
Hii ni kuonyesha kwamba mssikiti huu bado haujakidhi mahitaji ya waumini wa Eneo la ndarivoi na viunga vyake
Wewe kama muislaam umechangia kwa kiasi gani ujenzi wa nyumba hii ya allah.
Ndani ya msikiti huu pia kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma madrasa ndani ya msikiti huu. Jambo ambalo ni hatari kwa ibada za wengine kulingana na age ya watoto wanosoma hapo. Wengine ni wadogo sana kwahiyo tunahitaji kuwa na mdrasa kwa ajili ya vijana wetu hawa.
Wanafunzi wako zaidi ya mia mbili na wana changamoto zao mbali mbali.......... Jipime sasa na uone bado una nafasi ya kuendeleza dini kwa kila fursa uliyopewa na الله
