TAWIRI YAINGIA UWANDANI KUDHIBITI KERO YA MAMBA WILAYANI KOROGWE
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea na kazi ya kubaini maeneo ya kujenga vizimba vya kuzuia Mashambulizi ya Mamba kwa Wananch katika kijiji cha Kwaisewa ambapo ni miongoni mwa maeneo yenye changamoto ya hofu ya wananchi kushambuliwa na Mamba.
Timu ya wataalamu ikiongozwa na Dkt. Janemary Ntalwila, Mkuu wa Kitengo cha habari na Elimu na Mtaalamu wa kudhibiti migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori akiambatana na Revocatus Meney, Mtafiti na mtaalamu wa kudhibiti migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori inashirikiana na viongozi wa Wilaya na Kijiji cha Kwaisewa katika upimaji na uhakiki wa eneo la ujenzi wa Kizimba cha Mamba katika mto Pangani kijijini hapo.
Akizungumza na Viongozi wa Kijiji na wananchi wanaoathirika,
Dkt. Janemary ametoa wito kwa wanakijiji cha Kwaisewa kushirikiana na timu sambamba na kuzingatia maelekezo ya matumizi ya Kizimba kitakapokamilika ili kuwa na tija kwa kupunguza athari za mamba.
Naye mtafiti Revocatus Meney ametoa rai kwa wananchi kushiriki kwa dhati ili mafundi wabobezi kukamilisha ujenzi wa vizimba ndani ya muda mfupi.
Mwisho, ujenzi wa vizimba vya kuzuia mamba katika kijji cha Kwaisewa upo hatua ya pili ya upimaji wa eneo hatarishi na uwekaji alama za eneo Kizimba kitakapojengwa.
Tanzania Wildlife Research Institute-TAWIRI
TAWIRI is a parastatal organization responsible for conducting and coordinating wildlife research
Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI) was established by Act of the Parliament of the United Republic of Tanzania No. 4 of 1980, under the name “Serengeti Wildlife Research Institute”, with the aim of conducting and overseeing wildlife research (including beekeeping research) in the country. The original name of the Institute was changed in 1999, under the Act of Parliament No. 10, to give
31/01/2025
31.01.2025
30/01/2025
16/01/2025
WATAALAM WA MALIASILI WAKUTANA JIJINI ARUSHA
Wataalam sekta za Wanyamapori na Misitu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakutana Jijini Arusha, kujadili utekelezaji wa mashirikiano baina ya pande mbili kwa ustawi wa uhifadhi na kukuza utalii nchini.
Wakizungumza wakati wa kikao hicho viongozi wa pande zote mbili, Bi. Kay Kagaruki, Mkurugenzi Msaidizi Matumizi Endelevu ya Wanyamapori , Kutoka Wizara ya Malisili na Utalii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Bw. Said Juma Ali Mkurugenzi wa Misitu, Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamesema mashirikiano hayo yameleta tija katika sekta ya uhifadhi wa wanyamapori, Misitu na Utalii.
Aidha, Miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika kikao kazi hicho ambacho kimefanyika makao Makuu ya TAWIRI, ni pamoja na utekelezaji wa Mikataba ya Kikanda na Kimataifa, udhibiti wa ujangili, utoroshwaji wa nyara, usimamizi wa rasilimali za misitu, nyuki na wanyamapori, utafiti na biashara katika sekta za misitu, nyuki na wanyamapori na uendelezaji Utalii.
🇹🇿Tanzania Unforgettable
08/11/2024
*BENKI YA SAMPULI ZA WANYAMAPORI KATIKA UHIFADHI ENDELEVU*
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia Sehemu ya Sayansi ya Tiba na Maabara ya Wanyamapori imebainisha benki za sampuli za kibaolojia katika maabara, zinasaidia kupata taarifa za uchunguzi wa kisayansi zinazotumika katika uhifadhi endelevu wa wanyamapori hapa nchini .
Akizungumza wakati wa zoezi la kuchakata na kuhifadhi sampuli hizo na taarifa zake, mtaalamu wa maabara kutoka TAWIRI Anselmi Munga amesema, TAWIRI inajivunia kuwa na maabara za wanyamapori katika vituo vya Utafiti wa Wanyamapori Serengeti, Nyanda za juu Kusini na Makao Makuu ya Taasisi ambapo ndani yake kuna sampuli za kibaolojia za aina mbalimbali za wanyamapori zenye zaidi ya miaka 30
“Benki hizi ni muhimu kwani hutunza sampuli za Kigenetiki, seli za kisomatiki, tishu, damu, na kuwa na datakanzu ya kisayansi ya wanayamapori wakiwemo waliokatika hatari ya kutoweka” amebainisha Munga
Aidha, Munga ameeleza TAWIRI imeweka mkakati katika uhifadhi na utunzaji wa sampuli na taarifa zake kwa kuwezesha maabara kuwa na mfumo mzuri wa nishati ya umeme ambapo kuna majokofu yanayotumia umeme wa jua naumeme wa dharura (generator).Pia sampuli zinahifadhiwa kwa kutumia mitungi ya kimiminika cha Naitrojeni na kemikali
Munga Ameeleza, sampuli za wanyamapori zinatumika kusaidia katika mashtaka ya kijangili (forensic), kuandaa msingi wa utambuzi wa vinasaba (DNA) pamoja na kutoa taarifa za mabadiliko ya wanyamapori (evolution)
“kwa kutumia sampuli hizi tunaweza kubaini changamoto zinazokabili aina fulani ya wanyamapori k**a vile magonjwa hivyo kuongeza jitihada za kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo ” ameeleza Munga
06/11/2024
WAFUGAJI ARUSHA WAPEWA ELIMU YA UFUGAJI NYUKI
Zaidi ya wafugaji 100 wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamenufaika na mafunzo ya ufugaji bora wanyuki, uongezaji thamani mazao ya nyuki, uchakataji wa sumu ya nyuki na uandaaji wa maziwa ya nyuki (Royal Jelly) .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya Mafunzo hayo yaliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) wafugaji hao wameshukuru kujengewa uwezo wa ufugaji nyuki kisasa
"tumejifunza namna sekta hii ya nyuki ilivyo na faida kubwa endapo tutafuga kisasa ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani mazao ya nyuki" ameeleza Bw. Meneja Memuruti Menye.
Naye, Mfugaji Bi. Naatosim Parmandi amesema mafunzo ya vitendo yamekua na tija sana, wameweza kutembelea na kushuhudia zoezi la upandishaji na ukaguzi wa mizinga pamoja na uchakataji wa asali unavyofanyika maabara
"kabla ya mafunzo nilikuwa natumia njia za kiasili kuvuna asali ambapo zilikua zikiwaathiri nyuki". amesema Parmandi
Mtafiti kutoka TAWIRI Bw. Kipemba Ntiniwa ameeleza kuwa, nyuki ni fusra katika kujikomboa kiuchumi ambapo ametoa wito kwa wafugaji waliopata mafunzo kuwa walimu kwa wengine
"Ili kufuga nyuki kibiashara ni muhimu kujua aina ya nyuki ili kuwa na makundi imara, nitoe wito mkawe walimu wa wengine". amesema Ntiniwa
Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya TAWIRI Njiro-Arusha ambapo watafiti wa nyuki wametoa elimu ya ufugaji bora wa nyuki wakubwa (wadungao) na nyuki wadogo (wasiodunga), uongezaji thamani mazao yanyuki, utalii wa nyuki, zana za ufugaji nyuki kwa wafugaji.
24/10/2024
TAWIRI YAHIMIZA TAFITI ZA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI KWA WANYAMAPORI
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Eblate Mjingo amepongeza mradi wa utafiti wa Uandaaji Ramani za kubainisha makimbilio ya wanyamapori (Refugia) kwa miaka ijayo kwa kuzingatia athari za mabadiliko ya tabia ya nchi uliofanywa na watafiti kutoka chuo cha Massachusetts -Marekani kwa kushirikiana na watafiti wa TAWIRI
"Ramani hii itasaidia mamlaka husika kuhifadhi maeneo hayo yaliyobainishwa, hivyo kuhakikisha ustawi wa wanyamapori wakati wote" amefafanua Dkt. Mjingo
Dkt.Mjingo ametoa wito kufanyika tafiti zaidi za mabadiliko ya tabia ya nchi zilizojikita katika uhifadhi wa wanyamapori kwani bado kuna ombwe " Mabadiliko ya tabia ya nchi hayawaathiri binadamu pekee na mimea, hivyo kuna uhitaji mkubwa wa watafiti kuangazia mabadiliko ya tabia ya nchi kwa wanyamapori ili kushauri nini kifanyike kuhifadhi rasilimali hii " amehimiza Dkt.Mjingo
Aidha. Dkt.Mjingo amesema Tanzania imeendelea kuwa makazi pendwa ya spishi mbalimbali za Wanyamapori kutokana na uhifadhi mzuri sambamba na hali ya hewa " kutokana na hali nzuri ya uhifadhi, wanyamapori wahamao mfano nyumbu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wamekuwa wakibaki ndani ya maeneo yao kwa muda mrefu na pale wanapohama hurejea mapema sana '' ameainisha Dkt.Mjingo
Naye Dkt. Toni Lyn Morelli, mtafiti kutoka Chuo cha Massachusetts - Marekani akiwasilisha matokeo ya utafiti ya mradi huo wa ''Climate Adaptation for Biodiversity Conservation in the Face of Climate Change in Tanzania'' amesema kwa kuzingatia nchi ya Tanzania ni makazi ya bioanuwai kubwa, Utafiti huu ni kwanza kufanyika barani Afrika hivyo kuifanya Tanzania kuwa ya kwanza kuwa na ramani inayoainisha maeneo ya makimbilio ya wanyamapori miaka ijayo kwa kuzingatia athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wasilisho hili limefanyika katika ukumbi wa makao makuu ya TAWIRI na kuhudhuriwa na watafiti wabobezi katika njanja mbalimbali wa TAWIRI wakiwemo Wakurugenzi wa Vituo vya Utafiti .
Ikiwa ni Kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) yabainisha mambo matatu (03) aliyohimiza Hayati Mwl.Nyerere kuhusu uhifadhi wa wanyamapori.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Arusha
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 16:00 |
| Tuesday | 08:00 - 16:00 |
| Wednesday | 08:00 - 16:00 |
| Thursday | 08:00 - 16:00 |
| Friday | 08:00 - 17:00 |
