Quality commercial advert
All Nations Christian Center - Ancc - Arusha
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from All Nations Christian Center - Ancc - Arusha, Arusha.
15/09/2021
We wish you a wonderful and exciting new age! Have a blast💥 🎂🎉
Uzuri Bandia “
Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.” Zaburi 3:3.
Huku akikumbuka jinsi alivyovunja amri za Mungu, Daudi anaonekana kupooza kimaadili; alikuwa dhaifu na asiye na ujasiri, wakati ambapo kabla ya dhambi yake alikuwa amedhihirisha uthabiti na ujasiri.
Mvuto wake kwa watu ulikuwa umepungua sana. Na yote haya yalichangia kusaidia mipango ya mwanae asiye wa asili . . .
Wakati ambapo mfalme alipendelea zaidi maisha ya kujitenga na faragha, Absalomu alifanya bidii sana kujipendekeza ili akubalike kwa wengi …
Siku kwa siku mtu huyu aliyeonekana mwadilifu alionekana ameketi langoni mwa jiji, mahali ambapo makutano wenye shida mbalimbali walisubiri shida zao kushughulikiwa.
Absalomu alichangamana nao na kusikiliza malalamiko yao, akionesha huruma kwa shida zao na Masikitiko kwa serikali kushindwa kushughulikia kwa ufanisi.
Kwa mwonekano wake wa kupendeza, na tabia inayovutia, na huruma ya kujifanya, kwa ujanja aliteka mioyo ya watu.
Hakuwa na moyo wa ukarimu, lakini alikuwa mwenye kutaka makuu, k**a matendo yake yalivyoonesha alikuwa tayari kujenga fitina na hata kuvunja sheria ili mradi atwae ufalme.
Alikuwa radhi kulipa fadhila ya upendo na huruma ya baba yake kwa kumuua. Alitangazwa na wafuasi wake kuwa mfalme kule Hebron kisha akawaongoza kumtoa baba yake.
unyenyekevu na huzuni Daudi alipita nje ya lango la Yerusalemu, akiwa ameondolewa katika kiti chake cha ufalme, katika ikulu yake, kutoka kwa sanduku la Mungu la agano, kutokana na uasi wa mwanaye aliyempenda sana. Watu walifuata katika misafara mirefu ya huzuni k**a misafara ya maiti.
Wengi wasioona k**a aonavyo Mungu, bali wanaona mambo kwa mtazamo wa kibinadamu, wanaweza kudhani kwamba yawezekana Daudi alikuwa na sababu ya kutoridhika na kwamba kwa jinsi toba yake ilivyokuwa ya dhati miaka kabla ya wakati huu ilitosha kumwondoa katika kupata matokeo (hukumu) ya hapa duniani…
Daudi halalamiki popote. Zaburi fasaha kuliko zote alizowahi kuimba ilikuwa wakati akipanda Mlima wa Mizeituni, bila viatu na akilia, lakini roho yake ikijaa unyenyekevu, mkarimu na asiye na ubinafsi, aliyejisalimisha kwa Mungu na mwenye kuridhika. {CC 181.6}
Nikutakie jumamosi njema Mungu akubariki sana
Kazi ya Hila ya Shetani “
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Wefeso 6:12.
Biblia ina machache mno ya kusema katika kusifu wanadamu. Nafasi kidogo imetolewa katika kuelezea wema wa watu bora kabisa waliopata kuishi. Ukimya huu si bure, na haukosi la kutufundisha. Sifa njema zote walizo nazo wanadamu zinatoka kwa Mungu; Matendo yao mema yanatendwa kwa neema ya Mungu kupitia Kristo.
Kwa vile vyote wanapewa na Mungu basi utukufu wa vile walivyo au wanavyotenda ni wake Yeye peke yake; wao ni vyombo tu mikononi mwake. Zaidi ya hili—k**a masomo yote ya historia ya Biblia yanavyofundisha – ni jambo la hatari kuwasifu na kuwatukuza watu; kwani ikiwa tu mtu ataacha kumtegemea Mungu, na kutumainia nguvu zake mwenyewe, kwa hakika ataanguka. . .
Haiwezekani kwetu kwa nguvu zetu wenyewe kustahimili mapambano; chochote kinachoelekeza mawazo mbali na Mungu, chochote kinachotufanya kujitukuza au kujitegemea, kwa hakika kinatuandalia njia ya anguko.
Mwelekeo wa Biblia ni kujenga kutotumainia nguvu za kibinadamu na kutia shime kutegemea nguvu za Mungu. Ni roho ya kujiamini na kujitukuza iliyoandaa njia kwa ajili ya anguko la Daudi.
Sifa kupita kiasi na kudanganywa na sterehe na madaraka vilikuwa na mchango wake. Kujichanganya na mataifa yaliyowazunguka pia vilimpa mvuto kwa ajili ya maovu. Kulingana na desturi za watawala wa mashariki, makosa ambayo hayawezi kuvumiliwa miongoni mwa watawaliwa hayakuhukumiwa k**a makosa k**a yakifanywa na mfalme; Watawala hawakupaswa kuwa na utii wa sheria kwa kiwango cha wananchi.
Vyote hivi vilijaribu kupunguza hisia ya Daudi juu ya ubaya wa kutisha wa dhambi. Na badala ya kumtegemea Mungu kwa unyenyekevu alianza kutumainia hekima yake na uweza. Mara tu Shetani akifanikiwa kutenganisha mtu na Mungu, aliye chanzo pekee cha nguvu, atajitahidi kuamsha shauku zisizo takatifu za asili ya mwili wa mwanadamu.
Kazi ya adui si ya ghafla; katika mwanzo wake, si ya ghafla wala ya kushtua; ni kudhoofisha nguzo za kanuni za msingi taratibu bila kutambua.
Yesu atusaidie tumtangulize mbele katika maisha yetu. Uwe na siku njema Mungu akubariki sana
Kwa wasomaji wa Biblia...
Naamini hii inafundisha: Ni kisa cha mfalme sauli na mchawi wa en-dor aliyemuita "Samwel" kutoka ktk wafu.
Pastor
"Huyo Siyo Samweli “
"Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.”
Mhubiri 9:5.
Sauli alipoomba azungumze na Samweli, Bwana hakumfanya Samweli amtokee. Hakuona chochote. Shetani hakuruhusiwa kuvuruga pumziko la Samweli kaburini, na kwa hakika kumpandisha kwa mchawi wa Endori.
Mungu hampi shetani mamlaka ya kufufua wafu. Lakini malaika wa Shetani huchukua mwonekano wa marafiki zetu waliokufa, wakizungumza na kufanya vitendo k**a wao, ili kupitia kwa hao wanaojifanya kuwa marafiki zetu waliokufa atekeleze kazi yake ya Udanganyifu.
Shetani alimjua Samweli fika, na alijua namna ya kumwigiza mbele ya mchawi wa Endori, na kutamka kwa usahihi yale yatakayompata Sauli na wanawe.
Shetani atakuja kwa namna inayokubalika sana ili apate kudanganya, na atajifanya kujali mambo yao, na kuwapotosha toka kwa Mungu bila hata wao kujua.
Anawaweka chini ya udhibiti wake, mwanzoni kwa tahadhari, mpaka pale uwezo wao wa kugundua unapoishiwa nguvu kabisa. Ndipo sasa hutoa mapendekezo kwa ujasiri, hadi pale anapoweza kuwafanya kutenda karibia kiwango chochote kile cha makosa.
Anapowafikisha kikamilifu katika mitego yake, ndipo anapenda waone mahali walipo, na kufurahia kuona kule kuchanganyikiwa kwao k**a ilivyokuwa kwa suala la Sauli. Sauli alikuwa amemruhusu Shetani kumfanya mateka wake wa hiari, na sasa Shetani anaweka bayana maelezo sahihi ya mustakabali wa Sauli. Kwa kumpa Sauli maelezo sahihi ya mwisho wake, kupitia kwa mwanamke wa Endori, Shetani anafungua njia ya Israel kuongozwa na hila zake, ili kwa kumwasi Mungu, wamjue Shetani, na hivyo akate kitu cha mwisho ambacho kinawaunganisha na Mungu. Sauli alijua kwamba katika kitendo hiki cha mwisho cha kumwendea mganga(mwaguzi), alikata kamba ya mwisho iliyomuunganisha na Mungu.
Alijua kwamba k**a awali hakujitenga na Mungu kwa kukusudia, kitendo hiki kilihitimisha utengano huo. Alikuwa amefanya mapatano na kifo, agano na kuzimu. Kikombe cha maovu yake kilikuwa kimejaa.
Mungu atusaidie uwe na siku njema Mungu akutangulie .
“BWANA alitendaye jambo hili, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake; asema hivi, Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Yeremia 33:2-3. Asante Mungu kwa Neno lako asubuhi ya leo. Mpendwa umewahi kulisoma Neno la Mungu ukasikia k**a hitaji lako limeshajibiwa au ukasikia Mungu anasema nawe kwa kupitia Neno lake? K**a tumejizoeza kusoma Neno la Mungu ili mradi tu, hebu asubuhi ya leo soma Neno hili kwa kumaanisha halafu litafakari, Ikiwezekana k**a uko mahali pa peke yako jisomee kwa sauti. BWANA alitendaye, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake;. Amekuagiza umwite asubuhi ya leo, naye atakuitika, halafu atakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. NAMPENDA MUNGU KWA KUWA ANAISIKILIZA SAUTI YANGU.
Love handshake
Baba Mwoga “
Nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.” 1 Samweli 3:14.
Eli hakutawala vyema nyumba yake kulingana na maelekezo ya Mungu kuhusu serikali ya familia. Eli alifuata matashi yake. Wengi wanafanya makosa ya jinsi iyo hiyo leo. Wanafikiri wanajua mbinu bora ya kuelimisha watoto wao kuliko njia ile Mungu aliyoielekeza kwenye Neno lake. Wanawapa mielekeo potofu kwa kisingizio kuwa-- “Ni wadogo mno wasiostahili adhabu.
Subiri hadi wawe wakubwa, uweze kujadili pamoja nao.” Hivyo tabia mbaya inaachwa ikue hadi inakuwa sehemu ya maisha yao. Watoto wanakua pasipo nidhamu, wanakua na sifa za kitabia zilizo laana kwao wenyewe na zenye uwezekano wa kuambukiza sumu ya uovu kwa wengine. Kwa upambanishi na kisa cha uaminifu cha Ibrahimu, na maneno ya sifa njema yaliyoongelewa kwake; kipo kisa cha Eli, ambaye aliwabakiza watoto wake katika ofisi ya ukuhani wakati wanatenda uovu mkuu.
Hapa lipo somo kwa wazazi wote. . . Uovu, pasipo ukemeaji wo wote, uliruhusiwa na Eli. Matokeo yake ni dhambi ambayo haiwezi kupatanishwa kwa kafara au dhabihu milele zote. Wakati wengine hutenda kosa kwa ukali kupita kiasi, Eli alikuwa kinyume. Alikuwa mpole kupindukia.
Makosa ya wanawe yalipuuziwa utotoni mwao, na kutokemewa wakati wa ujana wao. Maagizo ya wazazi yalipuuziwa, na baba hakuweza kusimamia utii. Watoto waliona kuwa wanaweza kushikilia usukani wa utawala, na kila siku waliendeleza fursa hiyo. Kadri wanawe walivyoongezeka umri, walikoma kabisa kumheshimu baba yao mwoga. Waliendeleza maisha yao ya dhambi pasipo kuzuiwa.
Alijadiliana nao na kuwashauri, ila neno lake halikutiiwa. Dhambi za kutisha na uhalifu uliokithiri ulitendwa kila siku na vijana hao, hadi BWANA mwenyewe akatoa hukumu kwa hawa wahalifu wa sheria yake. Bwana mwenyewe alitangaza kuwa kwa dhambi ya wana wa Eli hakuna kafara au dhabihu ya kuleta upatanishi kwa ajili yao. Anguko lao ni kuu, na la kutisha jinsi gani—watu ambao walikabidhiwa majukumu matakatifu, kukataliwa na kuangamizwa pasipo huruma, na Mungu mwenye haki na mtakatifu!
Mungu akubariki kwa somo lilo likabadilishe maisha yetu.
Nikutakie siku njema Mungu akutangulie.
“Wala Hakuwazuia”
“Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia.”
1 Samweli 3:13.
Eli alikuwa mtu mwema, mwadilifu; ila alikuwa mzembe katika malezi. Aliangukiwa na ghadhabu ya Mungu kwa vile hakuimarisha mambo madhaifu katika tabia yake. Hakutaka kuumiza hisia za mtu ye yote na hakuwa jasiri kukemea dhambi…
Alipenda usafi wa kitabia na haki; ila hakuwa na nguvu kimaadili kuweza kupinga uovu. Alipenda amani na umoja, hivyo akawa hamudu kukemea uovu na uhalifu. . . Eli alikuwa mpole, mwungwana, anayejali huduma takatifu na mpenzi wa mafanikio ya kazi ya Mungu. Ni mtu aliyekuwa shujaa wa maombi. Kamwe hakuinuka kupingana na Neno la Mungu. Ila alikuwa na mapungufu, hakuwa jasiri kukemea dhambi na kutekeleza hukumu; hivyo akashindwa kutimiza jukumu la kusimamia taifa la Israeli lidumishe kweli na utakatifu. Katika imani yake, alishindwa kuongezea ujasiri na uthubutu wa kusema Hapana kwa wakati sahihi na mahali sahihi.
Eli alikuwa anajua mapenzi ya Mungu. Alijua ni tabia gani inampendeza Mungu, na ipi ni chukizo kwake. Hata hivyo aliwaachia watoto wake wakue na tamaa mbaya zisizotawalika, uchu usiojua kiasi, na maadili potofu. Eli alikuwa amewafundisha watoto wake sheria ya Mungu, naye ameishi maisha yaliyo kielelezo chema; ila hapo bado alikuwa hajatimiza jukumu. Mungu alimhitaji yeye k**a baba na kuhani, awazuie kufuata mapenzi yao maovu. Hilo alishindwa kufanya. Wale wenye ujasiri kidogo mno kiasi cha kutothubutu kukemea uovu, au kwa sababu ya uzembe au kutokujali hawafanyi jitihada zo zote kuisafisha kiroho familia yao au kanisa la Mungu, watawajibika mbele za Mungu kwa uovu ulio matokeo ya upuuziaji wa majukumu yao. Tunawajibika kwa maovu ambayo yamewapata watu katika jamii k**a matokeo ya sisi k**a wazazi au wachungaji kushindwa kuyazuia yasitokee, kwa vile tulikuwa wazembe katika malezi ya watoto wetu.
Yesu tusaidie tusiwe wazembe kulea familia zetu
nikutakie siku njema Mungu akubariki katika kazi yako tukimtegemea yeye daima.
Kielelezo Hatari
“Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao.” 1 Samweli 2:25.
Eli alikuwa kuhani na mwamuzi katika Israeli. Alishikilia wadhifa wa juu uliotukuka miongoni mwa watu wa Mungu. K**a mtu aliyechaguliwa na mbingu akapewa majukumu matakatifu ya ukuhani, na kuwekwa juu ya nchi k**a mwamuzi mkuu, aliaangaliwa na kila mtu akitarajiwa kuwa kielelezo, naye alikuwa na mvuto mkuu kwa taifa la Israeli. Lakini japokuwa ameteuliwa kutawala watu, hakumudu kuweza kuitawala vyema familia yake. Akipenda amani na maisha rahisi, hakuthubutu kutumia rungu lake la mamlaka kurekebisha tabia na mwenendo mbaya wa watoto wake. Badala ya kuwakemea na kuwaadhibu, alisalimu amri kwa matashi yao akawaacha waziendee njia zao k**a wapendavyo. Badala ya kuelewa kuwa elimu ya watoto wake ni jukumu muhimu sana; yeye aliona jukumu hilo ni dogo mno, hivyo akalipuuzia. Kuhani na mwamuzi wa Israeli hakuachwa gizani kuhusiana na jukumu lake la kuwazuia na kuwatawala watoto aliopewa na Mungu wawe chini ya malezi yake. Lakini Eli alizembea jukumu hilo, kwa vile lilihusisha kupingana na mapenzi ya wanawe, na hivyo kumlazimu awaadhibu na kuwazuia….
Laana ya uasi huo ilikuwa dhahiri katika upotovu na uovu uliokuwa ukiendelea kutendwa na wanawe. Hawakuwa na kicho kuthamini tabia ya Mungu au utakatifu wa sheria yake. Huduma ya hekaluni ambayo ni takatifu mno, wao waliichukulia kwa mzaha kana kwamba ni ya kawaida kabisa. Tangu utoto wamezoea hekalu na huduma zake; ila badala ya uzoefu huo kuwafanya wawe na kicho zaidi, wamepoteza kabisa fahamu za utakatifu na umuhimu wake. Baba alishindwa kukemea ukosefu wao wa adabu mbele zake, pia alishindwa kukemea ukosefu wao wa kicho kwa huduma takatifu za hekaluni; na walipokuwa watu wazima, walishakuza tabia sugu ya uasi na kutomtambua Mungu.. . .
Hakuna laana kuu katika familia k**a kuwaruhusu vijana waiendee njia waipendayo isiyompendeza Mungu. Wakati wazazi wanaafiki kila takwa la watoto wao na kuwaendekeza katika kile wanachojua kuwa hakitawafaa, muda si mrefu watoto huacha kuwaheshimu wazazi, hupuuza mamlaka ya Mungu na wanadamu, na kuwa mateka wa mapenzi ya Shetani.
Tusikilize sauti ya Yesu tusifanye yaliyo Mapenzi yetu Bali lolote tulifanyalo tulifanye kwa utukufu wa Mungu. Nikutakie siku njema Mungu akubariki sana kwa somo hilo.
Mtoto Huyu Amepewa BWANA
“Kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu.” 1 Samuel 1:28.
Akitokea hekaluni Shilo, Hana kwa ukimya alirejea nyumbani mwake Rama, akimwacha mtoto Samweli apate malezi kuhudumu nyumbani mwa BWANA, chini ya maelekezo ya Kuhani mkuu. Tangu utotoni kabisa alikuwa ameshamfundisha mwanawe kumpenda na kumcha Mungu na kujitambua mwenyewe k**a mali ya BWANA. Kwa kupitia viumbe asili karibu naye alijitahidi kumwongoza amjue Muumba. Sasa alipotengana na mwanawe, upendo wa mama haukukoma. Kila siku mtoto huyo alikuwa mlengwa wa sala zake. Kila mwaka alifuma kwa mikono yake vazi la huduma kwa ajili ya mtoto wake, na alipokuwa akisafiri na mumewe kuabudu huko Shilo, alimkabidhi mtoto vazi hilo k**a kumbukumbu ya upendo wake kwake. Kila nyuzi katika vazi hilo dogo ilishonwa kwa ombi kwamba awe safi, mwungwana, mkweli. Hakumwombea mwanawe kupata ukuu wa kidunia, ila aliomba apate ukuu ambao mbingu huuheshimu—kwamba aweze kumheshimu Mungu na kuwabariki wanadamu wenzake. Ni zawadi ya hadhi kuu jinsi gani aliyoitoa Hana! Zipo fursa za thamani kuu, mivuto yenye mustakabali mkuu, aliyokabidhiwa kila mama. Shughuli ndogo ndogo za kila siku zenye kuonekana za kuchosha zapasa kila mama azitambue kuwa ni za hadhi kuu na bora. Ni upendeleo maalumu kwa kila mama kuweza kuubariki ulimwengu kwa mivuto yao; na kwa kutenda hivyo atajiletea furaha moyoni mwake. Anaweza kuandaa njia nyofu kwa watoto wake, iwe ni jua au giza, wakue hadi vilele vya juu kiroho. Ila ni pale anaponuia kwa dhati, maishani mwake, kufuata mafundisho ya Kristo, ambapo mama anaweza kutazamia kuunda tabia ya wanawe kwa sura ya kimbingu. Ulimwengu umejawa mivuto inayoharibu tabia. Mitindo na desturi huweka mvuto mkuu kwa vijana. K**a mama anashindwa kwenye jukumu lake la kufundisha, kuelekeza, kuzuia, watoto wake kirahisi wataiga uovu, na kuigeuzia kisogo ile kweli. Hebu kila mama amwendee Mwokozi na ombi hili: “Tufundishe jinsi tutakavyomlea mtoto, na lile tutakalomtendea?” Hebu azingatie maagizo ambayo Mungu amempatia katika neno lake, naye atapewa hekima k**a lilivyo hitaji lake.
Tumuombe Baba wa Mbinguni atuwezeshe kulea watoto wetu kwa hekima ya Kimbigu. Nasisi pia tupate hekima hiyo.
Bwana atusaidie kwa masomo haya tuwe na mabadiliko ya kiroho na ya kimwili. Uwe na siku njema Mungu akubariki sana.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Website
Address
Arusha
