Ngorongoro Insights

Ngorongoro Insights Official updates from Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA)

02/09/2026

Episode 02 of Rafiki Tembo’s SPOTTED series. 🦁
Your little virtual safari, straight from the wild to your phone. 🤎

A pride of lions relaxing right on the road inside Ngorongoro Crater, Tanzania.

Wild fact: Lions often rest on roads because the open ground can hold warmth from the sun, especially during cooler mornings and evenings. Roads also give them a clear, comfortable place to lie down while keeping an eye on what’s around them.

29/08/2026
Watumishi 41 kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiongozwa na Mkurugenzi wa idara ya ...
28/08/2026

Watumishi 41 kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiongozwa na Mkurugenzi wa idara ya utawala wa utumishi wa umma SACP Ibrahim Mahumi wametembelea vivutio vya Utalii katika hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia vivutio vya malikale na urithi wa utamaduni katika Bonde la Olduvai pamoja na Wanyamapori mbalimbali katika Kasoko ya Ngorongoro.

Ziara hiyo ni matokeo ya elimu na hamasa ya Utalii wa ndani inayotolewa kwa makundi mbalimbali kupitia ofisi kiunganishi ya Ngorongoro iliyopo Dodoma kuhusu utalii wa ndani.

CHEREKO CHEREKO BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO.Kamati tendaji ya Baraza la Wafugaji tarafa ya Ngorongoro imekutana leo ta...
18/08/2026

CHEREKO CHEREKO BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO.

Kamati tendaji ya Baraza la Wafugaji tarafa ya Ngorongoro imekutana leo tarehe 18 Agosti, 2026 ambapo pamoja na mambo mengine imechambua na kupitisha orodha ya majina ya wanafunzi wa kidato cha tano kutoka kata 11 za tarafa ya Ngorongoro wanaofadhiliwa na Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro

Majina ya wanafunzi wanaofadhiliwa na Ngorongoro yanatokana na mapendekezo ya kata zote 11 zenye Vijiji 25 ambapo kila kata inachagua wanafunzi watatu (03) ambapo wanapata fursa hiyo ikiwa ni hatua ya kuendelea kuboresha uhusiano kati ya Ngorongoro na Jamii inayoishi ndani ya hifadhi

Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa sambamba na kusaidia huduma za elimu kwa wanafunzi wa tarafa ya Ngorongoro, katika kipindi cha wiki moja ijayo itafanyika tathmini ya mahitaji ya maji na barabara zenye changamoto ambapo Ngorongoro inatarajia kuchimba visima saba (07) na kukarabati mtandao wa barabara katika maeneo ya hifadhi ili kuhudumia wananchi na watalii.

Aidha Ngorongoro kwa kushirikiana na makampuni ya simu inatarajia kuimarisha huduma ya Mawasiliano ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2026 maeneo mengi ndani ya hifadhi huduma ya mawasiliano itakuwa imeimarika.

Kamati tendaji ya Baraza la wafugaji wa Tarafa ya Ngorongoro inaundwa na waheshimiwa madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, Viongozi wa mila na wawakilishi wa wanawake, Mhifadhi NCAA,wawakilishi wa vijana.

16/08/2026

“Ngorongoro ni eneo la kipekee Duniani linalohifadhi Urithi wa Dunia ikiwemo Nyayo za Laetoli, Masalia ya Binadamu wa kale na Zana za mawe katika Bonde la Olduvai ” Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa UNESCO Mhe. Said Yakubu

NGORONGORO KIVUTIO CHA UTALII KILICHOTEMBELEWA ZAIDI MWAKA 2025.Eneo la hifadhi ya Ngorongoro limetajwa kuwa ndio kivuti...
13/08/2026

NGORONGORO KIVUTIO CHA UTALII KILICHOTEMBELEWA ZAIDI MWAKA 2025.

Eneo la hifadhi ya Ngorongoro limetajwa kuwa ndio kivutio namba moja kilichotembelewa zaidi na watalii kwa mwaka 2025 ambapo watalii 859,933 walitembelea hifadhi hiyo ambayo ni kivutio namba moja cha utalii barani afrika.

Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyofanya utafiti wa wageni wa kimataifa wakati wa kuondoka mwaka 2025 (The 2025 International visitors Exit Survey report) inaOnyesha kuwa eneo la hifadhi ya Ngorongoro limetembelewa na asilimia 14.2 ya wageni waliowasili chini kwa mwaka huo na kuwa kinara katika maeneo yote ya utalii nchini.

Ongezeko la idadi ya wageni katika hifadhi ya Ngorongoro na maeneo mengine ya nchi inatokana na jitihada za serikali na wadau wa utalii kuendelea kuitangaza Tanzania katika majukwaa na maonesho ya kimataifa huku Ngorongoro ikiboresha huduma za wageni na kuimarisha miundombinu ya utalii kwenye vivutio vilivyopo ndani ya hifadhi ili kuongeza mtawanyiko wa wageni kwenye vivutio hivyo.

Eneo la hifadhi ya Ngorongoro lina vivutio mbalimbali ikiwemo kreta tatu za Ngorongoro, Olmot na Empakai, Vivutio vingine ni pamoja na mazalia ya nyumbu ndutu, mchanga unaohama, maporomoko ya maji endoro, mapango ya tembo, mlima Lolmalasin, jabali la nasera, msitu wa nyanda za juu kaskazini, makumbusho ya olduvai na nyayo za Laetoli zenye umri wa miaka milioni 3.6 iliyopita.

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro lililoanzishwa mwaka 1959 lenye ukubwa wa kilomita za mraba 8,292 lina hadhi tatu zinazotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), ambazo ni; Man and Biosphere Reserve (Hifadhi ya Binadamu na Baiolojia), Mixed World Heritage Site (Urithi wa dunia Mchanganyiko), Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark (Hifadhi ya Jiolojia ya Dunia), Aidha, mwaka 2023 na 2025, Hifadhi ya Ngorongoro ilichaguliwa na Mtandao wa World Travel Awards (WTA) k**a Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika (Africa’s Leading Tourist Attraction).

09/08/2026

What’s your favorite national park in Tanzania? 🇹🇿🌿

We asked an Italian traveler who has spent time exploring Tanzania to share the one park that captured their heart. In this episode, Nancy, our Sales Consultant & Travel Planner, uncovers a personal favorite and the story behind it.

Would you choose the same park?! 👇

📍cc: Ngorongoro Conservation Area Tanzania Unforgettable Ngorongoro Conservation Area Authority

LIVESTREAM  NI UNYAMA MWINGINE  KUFIKIA WATALII MILIONI 8 MWAKA 2030.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hass...
06/08/2026

LIVESTREAM NI UNYAMA MWINGINE KUFIKIA WATALII MILIONI 8 MWAKA 2030.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande katika maonesho Nanenane kitaifa jijini Dodoma ametembelea banda la Wizara ya Malisili na utalii na kushuhudia vivutio mubashara kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kusisitiza kuwa programu ya kuonesha vivutio kidijitali na kuunganisha kwenye mitandao ya kijamii ni silaha muhimu kufikia watalii milioni nane ifikapo mwaka 2030.

“Kuonesha vivutio vya utalii mubashara kutokea Ngorongoro ni silaha muhimu ya kuongeza idadi ya watalii, nimeona mna kamera za kisasa zinazoonesha uhalisia wa maajabu yaliyopo Ngorongoro, naamini wanaoshuhudia sio tu wanaotembelea maonesho ya nanenane, ila duniani kote wanaweza fuatilia kupitia Youtube na mitandao mingine ya kijamii, endeleeni kukaza buti” amefafanuo Mhe. Chande.

Mhe. Chande ameipongeza Ngorongoro kwa matumizi ya teknolojia katika utoaji huduma na kuelekeza jitihada ziendelee kwa kuwekeza nguvu kubwa katika kutumia watu mashuhuri (Influencers) mitandao ya kijamii k**a Intagram, twitter na ticktock, facebook na WhatsAp ili baadae mitandao hiyo iwe chanzo cha mapato ya Serikali kwa watu kulipia mtandaoni.

Afisa Uhusiano Mkuu wa Ngorongoro Walter Mairo amemueleza mhe. Naibu Waziri kuwa Ngorongoro inaendelea kuwekeza katika matumizi ya TEHAMA kuendelea kutangaza vivutio vyote vya utalii kwa kuwa Ngorongoro ni zaidi ya Kreta, ina maajabu mengi ikiwepo asili ya binadamu wa kale, Nyayo za Laetoli, ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus) ambapo vivutio hivi vinaifanya Ngorongoro kuendelea kuhamasisha watu kurudi Nyumbani Ngorongoro.

KISHINDO CHA NGORONGORO SCHOLARSHIP FUNDMamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na Bodi ya Miko...
05/08/2026

KISHINDO CHA NGORONGORO SCHOLARSHIP FUND

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa elimu kwa jamii ya Ngorongoro kuhusu mfuko wa Ngorongoro Scholarship Fund unaolenga kuwezesha wanafunzi wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kupata fursa ya masomo ya elimu ya juu kupitia ufadhili Ngorongoro Fund.

Elimu hiyo iliyotolewa katika ofisi za Ngorongoro ilijumuisha wadau muhimu wanaoguswa na mpango huo ambao ni viongozi wa jamii, wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali ambao wamepewa uelewa kuhusu vigezo vya mkopo, sifa za waombaji pamoja na kupitia na kujadili mwongozo wa programu ya Ngorongoro Scholarship Fund.

Katika kikao hicho, viongozi wa jamii wamepongeza hatua ya Mamlaka ya kushirikiana na HESLB katika kuandaa na kuboresha mwongozo wa mfuko huo, wakieleza kuwa utasaidia kuweka utaratibu unaozingatia usawa, uwazi na mahitaji ya wakati katika kuwawezesha wanafunzi wenyeji kupata fursa za elimu ya juu.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro, Mhe. Edward Maura, aliipongeza Mamlaka ya Ngorongoro na HESLB kwa kutoa elimu kuhusu Ngorongoro Scholarship Fund hasa jinsi wanufaika wanavyoweza kutambua fursa, kujaza fomu na kufuata taratibu za kuomba ufadhili.

“Tunawapongeza Ngorongoro na Bodi ya Mikopo kwa kutoa elimu hii kwa jamii na wanafunzi na kusaidia kuwaondolea wanafunzi changamoto na uelewa mdogo wa namna ya kuomba na kupata mikopo huu, tunaamini maamuzi haya ya Serikali yanalenga kuimarisha mahusiano kati ya jamii na Ngorongoro na tunaamini wanafunzi na jamii watatumia fursa zinazotolewa kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa” alisema Mh. Maura.

Utekelezaji wa program hii unalenga kuimarisha ushirikiano na kuboresha huduma za jamii kwa wananchi wa Ngorongoro ambapo elimu wanayopata itasaidia ushiriki wao katika program za uhifadhi endelevu na kuvutia wageni kupitia vivutio vya utalii vilivyopo.

Address

Ngorongoro Crater
Arusha
P.O.BOX1NGORONGOROCRATER

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:00
Tuesday 07:30 - 15:00
Wednesday 07:30 - 15:00
Thursday 07:30 - 15:00
Friday 07:30 - 15:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ngorongoro Insights posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share