Babati Town Council

Babati Town Council

Share

P. O BOX 383 BABATI

Photos from Babati Town Council's post 02/06/2026

Millioni 57 za wawezesha kikundi cha Vijana Sokoni kujiajiri.

Halmashauri ya Mji Babati kupitia mikopo ya 10% isiyo na riba ya Vijana, Wanawake na wenye Ulemavu inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri imewezesha kikundi cha Vijana sokoni kununua pikipiki za magurudumu matatu (Bajaji) tano na kujiajiri kupitia shughuli za usafirishaji.

Naye Bw.Samweli Paulo Mwenyekiti wa kikundi hicho ameeleza kuwa wamenufaika k**a kikundi lakini pia mtu mmoja mmoja kwa kujipatia kipato na kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Aidha ameongeza kuwa hali ya maisha imekuwa bora ukilinganisha na kipindi cha awali.

Halmashauri ya Mji Babati imeendelea kutenga 10% ya mapato yake ya ndani ili kuwezesha makundi hayo kiuchumi na kufikia adhma ya Serikali ya kuwezesha Vijana kujiajiri.

01/06/2026

"Dira 2050,Tuwajibike Kukijanisha Tanzania".

@owm_tz

29/05/2026

"Tunza Mazingira yakutunze"

29/05/2026

LIPA MAPEMA ILI KUEPUKA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

Photos from Babati Town Council's post 27/05/2026

Lango la Mamire, Fursa ya Uwekezaji Babati.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Remidius Mwema amesema lazima kuandaa mkakati maalum wa kutumia fursa ya kufunguliwa kwa geti la Mamire ikiwemo uwekezaji wa hoteli na Biashara ili kusadifu hali halisi ya kuwa karibu na hifadhi ya Tarangire.

Mhe.Mwema amezitaka Halmashauri za Babati kuhakikisha wanahamasisha vikundi vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani za Halmashauri kuwekeza kwenye utalii wa utamaduni na mambo mengine muhimu.

Hata hivyo amebainisha kwamba Serikali ina mpango wa haraka wa ujenzi wa kituo cha Polisi kwenye eneo la Wang'waray ili kuhakikisha usalama muda wote kwa wawekezaji watakaojitokeza kuwekeza.

Naye Afisa hifadhi Tarangire Bw. Deogratius Mwageni amekiri kuwa tayari lango hilo limeanza kufanya kazi na kwamba ndiyo litakuwa lango litakalotumiwa na Watalii wanaotembelea hifadhi hiyo ya Taifa Tarangire kutokea Mikoa ya kusini pamoja na kanda ya kati.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi.Monica Mbogwe ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Biashara na Viwanda amesema kufuatia ufunguzi wa geti la Mamire kunatoa fursa ufunguzi wa soko la nyama choma ambapo tayari Elimu imekwisha tolewa kwa wafugaji ili waboreshe ufugaji na kukidhi mahitaji ya soko la nyama.

Fursa ambazo zinatarajiwa kuongeza na kukuza uchumi wa Halmashauri ni pamoja na matarajio ya uwepo wa shughuli za utalii kwenye Ziwa Babati ambapo Watalii watakaotembelea watakutana na mandhari nzuri ya ziwa Babati na kufanya utalii wa ndani ya ziwa.

Sambamba na hilo Halmashauri ya Mji Babati imetenga eneo maalum la uwekezaji lenye ukubwa wa hekari 9 kwaajili ya hotel za five stars katika eneo la Miomboni.

27/05/2026

Kheri ya Sikukuu ya Eid - Al- Adha.

Tusherehekee kwa Amani na Upendo.🙏

26/05/2026

Halmashauri ya Mji Babati tupo tayari kukuhudumia wasiliana nasi kwa Kufuata Maelekezo hapo juu.👆👆

Karibu Tukuhudumie.

Photos from Babati Town Council's post 25/05/2026

Manyara Tanzanite Marathon 2026 kuwezesha uboreshaji wa huduma za Watoto wachanga na njiti.

Hayo yameelezwa na Mhe. Queen Cuthbert Sendiga Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika mkutano na Waandishi wa Habari Ofisini kwake.

Maandalizi ya mbio maalum za Hisani (Marathon)yameanza na yanatarajiwa kufanyika 22 Agosti 2026 katika Mkoa wa Manyara kwa Lengo la kuboresha huduma za Watoto wachanga na njiti ikiwemo kununua vifaa tiba,kujenga jengo la Watoto wachanga na njiti katika Hospitali ya Wilaya Hanang,kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuutangaza Mkoa kwa utalii,Ameeleza

Amesema kuwa"Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa akipambana na kupunguza vifo vya mama Wajawazito na Watoto, sisi k**a Mkoa tunaunga juhudi hizi muhimu katika jamii ili kuwasaidia akina mama wanaopata ujauzito isiwe sababu ya kifo lakini pia watoto wachanga na njiti waishi".

Aidha ameongeza kuwa Jumla ya Shilingi milioni 886.6 zinatarajiwa kukusanywa na zitaelekezwa katika vituo mbalimbali vya Afya ili kuboresha utoaji wa Huduma.

Aidha Dkt. Andrew Method Mganga Mkuu Mkoa wa Manyara ameeleza katika mkutano huo wastani wa Watoto njiti 3000 huzaliwa kwa mwaka.

Sambamba na hilo Mhe. Sendiga amewaomba Wadau wote makampuni binafsi,Serikali,Wafanyabiashara na Wanamichezo kujitokeza kwa Wingi kushiriki mbio hizo za hisani.

"Hatua Moja,Okoa Maisha ya Mtoto"

@manyara_rs

22/05/2026

PONGEZI NI CHACHU YA KUENDELEA KUFANYA VIZURI ZAIDI TUKUTANE VIWANJA VYA HALMASHAURI YA MJI BABATI

Photos from Babati Town Council's post 21/05/2026

NEEC yaendesha Mafunzo ya Biashara endelevu kwa Maafisa Biashara na Watoa Huduma za Biashara Halmashauri ya Mji Babati.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeendesha mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wakufunzi (Training of Trainers - TOT) kuanzia tarehe 19 hadi 21 Mei 2026.

Aidha Bw. Macdonald Lulanzi Afisa wa NEEC ameeleza kuwa Mafunzo hayo yamelenga kufundisha mbinu za kufanya biashara endelevu, ikiwa ni pamoja na taratibu za kuanzisha na kurasimisha biashara.

Pia Kuwajengea uwezo washiriki hao ili wakawafundishe na kuwasaidia Wananchi wengi zaidi kiuchumi kwa kuwapa mbinu bora na endelevu za kibiashara.

Want your business to be the top-listed Government Service in Babati?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Town Director's Office, Babati Town Council, 1 Council Street, Bagara Manyara
Babati
27103

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30