Akhera YAKO

Akhera YAKO

Share

Ni page inayo husiana na kukatazana mabaya na kuhimizana ya kheri ili tuweze kuwa radhi na Allah kupitia mtume wetu rehma na amani ziwe juu yake karibuni

14/01/2026
22/11/2020

Dunia inapo elekea kwao we usisahau kuchukua zawadi zake kwa ajili ya kule tuendako

09/11/2020

Mandalizi ya Akhera ni hapa duniani ukikosea hapa hakuna sehem ya kurekebishia makosa yako

Akhera YAKO Send a message to learn more

05/06/2019

kutoka kwa Abi Umaamatu Albaahiliy amesema: “Nilimsikia Mtume Mtume (saw) yuwasema: Pindi mimi nilikuwa nimelala walinijia watu wawili ….., kisha wakaniondokea, nikawa nimefika mahali pa watu ambao wamefungwa sehemu zao za nyuma ya magoti wametanuliwa sehemu za pambizoni mwa midomo yao, sehemu zao za pambizoni mwa midomo inatona damu. Akasema: Nikauliza: Ni kina nani watu hao?. Akasema: Hao ni wale ambao kwamba wanakula kabla ya kukamilika kwa saumu zao) [Imepokewa na Ibnu Hibbaan.]
https://www.islamkingdom.com/sw

15/03/2019

NAAM

SWALA YA IJUMAA KWA MWANAMKE...

Wamekubaliana wanazuoni juu ya swala ya ijumaa sio wajibu kwa mwanamke, na kuwa yeye ataswali nyumbani kwake rakaa nne (adhuhuri) na akiwa safarini ataswali rakaa mbili.
anasema ibn mudhir katika ijmaau "na wamekubaliana kuwa hakuna ijumaa kwa wanawake"

Pia kwa hadithi ya Mtume aliposema " ijumaa ni haki ya kila muislam katika mkusanyiko isipokuwa kwa wanne, mtumwa anayemilikiwa,au mwanamke, au mtoto, au mgonjwa". kapokea Abuu Daudi, kaisahihisha Al-baniy..

Na swala iliyokuwa bora kwa mwanamke ni ile anayoswali nyumbani kwake.
Kwa hadithi aliyopokea Ibn Mas'uud, Mtume anasema "swala ya mwanamke chumbani kwake ni bora kuliko swala yake katika sebule, na swala katika chumba kilichopo ndani ya chumba anacholala ni bora kuliko swala yake katika chumba anacholala". Kaipokea Abuu Daud 570, Tirmidhy 1173.

Na swala hapa zinaingia swala zote ikiwemo Ijumaa.

Mwanamke akiswali Ijumaa msikitini swala yake hukubaliwa kutokana na ijmaa ya wanazuoni, na haitomlazimu kuswali tena adhuhuri, kutokana na kuthibiti wanawake kuswali na Mtume lakini Mtume Swalla ALLAHU alayhi wa Sallam hakuwaambia warudie swala zao. Rejea lajna ddaaim fat'wa 7/337.

Ni vizuri mwanamke anapokwenda msikitini ajistiri vizuri bila kutia manukato wala kudhihiridha mapambo yake ili kuepuka fitna ambayo kwa ajili yake hupendeza aswali nyumbani kwake...

Na ALLAH ni mjuzi zaidi...

Uislamu Dini Yangu

Want your business to be the top-listed Government Service in Bagamoyo?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Chuione16@gmail. Com
Bagamoyo
ALLAHAKBAR