Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Website Contact the organization

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE

*RC MTANDA: " UCHAGUZI UMEKWISHA, SASA TUIJENGE BARIADI"* Bariadi,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Said Mtanda, amewataka ma...
13/10/2026

*RC MTANDA: " UCHAGUZI UMEKWISHA, SASA TUIJENGE BARIADI"*

Bariadi,

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Said Mtanda, amewataka madiwani na wananchi wa Wilaya ya Bariadi kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa na badala yake kushirikiana kwa pamoja katika kuharakisha maendeleo ya wilaya hiyo.

Mhe. Mtanda ametoa wito huo alipozungumza na madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji Bariadi, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea halmashauri za Mkoa wa Simiyu kwa lengo la kufuatilia shughuli za maendeleo na kuimarisha utendaji kazi katika maeneo mbalimbali.

Amesisitiza umuhimu wa viongozi na wananchi kushirikiana, kuzingatia maslahi ya umma na kuelekeza nguvu zao katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi badala ya kutumia muda mwingi katika tofauti za kisiasa.

Aidha, amewahimiza madiwani na watumishi wa halmashauri kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwajibikaji na kuzingatia misingi ya utumishi wa umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo yanayokusudiwa.

Mhe. Mtanda amebainisha kuwa ushirikiano miongoni mwa viongozi na wananchi ni nguzo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wa Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla.

Simiyu RS,
13 Oktoba 2026.

RC MTANDA ATETA NA  MADIWANI, WATUMISHI  WA UMMA BUSEGA,ASISITIZA MAADILI, NIDHAMU NA USHIRIKIANO KATIKA UTUMISHI WA UMM...
12/10/2026

RC MTANDA ATETA NA MADIWANI, WATUMISHI WA UMMA BUSEGA,

ASISITIZA MAADILI, NIDHAMU NA USHIRIKIANO KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

Busega,

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Said Mtanda amewataka madiwani na Watumishi wa Umma Wilayani Busega kuzingatia maadili, nidhamu, upendo na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya kuwahudumia Wananchi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi hao katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, katika ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu ya kutembelea halmashauri.

RC Mtanda ameeleza kuwa maadili na nidhamu ni misingi muhimu inayopaswa kuzingatiwa na kila mtumishi wa umma ili kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa uadilifu, uwajibikaji na kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa.

Amesisitiza kuwa watumishi wanapaswa kutambua dhamana waliyopewa na Serikali na kuitumia kwa manufaa ya wananchi, huku wakiepuka vitendo vinavyoweza kuathiri ufanisi wa utendaji kazi na imani ya wananchi kwa viongozi wao.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa upendo na kuheshimiana baina ya madiwani, watumishi wa umma na viongozi wengine katika maeneo yao ya kazi.

Ameeleza kuwa mazingira bora ya kazi hujengwa kwa kuzingatia mawasiliano mazuri, kusikilizana na kutatua changamoto kwa njia ya maelewano, jambo litakalosaidia kuimarisha mahusiano kazini na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Katika hatua nyingine, RC Mtanda amehimiza ushirikiano wa karibu kati ya madiwani na watumishi wa umma, akieleza kuwa makundi hayo yana majukumu yanayokamilishana katika kusimamia na kutekeleza mipango ya maendeleo.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kufanya kazi kwa pamoja, kubadilishana mawazo na kuweka mbele maslahi ya wananchi badala ya tofauti binafsi, ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati na huduma za kijamii zinatolewa kwa ufanisi.

Simiyu RS,
12 Oktoba 2026.

12/10/2026
09/10/2026

*BODABODA MWANZA WAMFWATA RC MTANDA SIMIYU, WAMPA TUZO YA SHUKRANI, WASEMA NI KIONGOZI WA MFANO.*

Bariadi,

Umoja wa waendesha pikipiki almaarufu Bodaboda kutoka Mkoani Mwanza wamempa tuzo k**a shukrani Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Said Mtanda kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa kwa umoja huo alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Bodaboda hao walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyoko Nyaumata Wilayani Bariadi na kumkabidhi tuzo hiyo kutokana na namna alivyojitoa kwa hali na mali kusaidia chama chao.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mhe.Mtanda amewashukuru Bodaboda hao kwa kutambua na kuthamini mchango wake kwao alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

"Ni nadra sana watu kuheshimu na kuthamini mchango wa watu wengine,kitendo cha nyinyi kufunga safari ndefu na kuja maana yake mmeniheshimisha sana kwa hiyo na mimi ninawashukuru na kuwatakia kila.la.kheri" Alisema Mkuu wa Mkoa Mhe.Mtanda.

Aidha Mhe.Mtanda ameahidi kuwachangia boda boda hao viti kwa ajili ya Ofisi yao ambapo pia amekubali kuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa ofisi zao.

Kwa upande wao viongozi wa chama cha waendesha bodaboda kwa niaba ya bodaboda wa Mkoa wa Mwanza wamemuelezea Mhe.Mtanda k**a mtu mwenye mchango mkubwa katika kuwaunganisha na kuwainua bodaboda hao kiuchumi.

Wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumteua Mhe.Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Simiyu RS
9 Oktoba, 2026.

KADOGOSA: TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUINUA SEKTA YA UJENZIWaziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kadogosa, amesema atashirikiana k...
02/10/2026

KADOGOSA: TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUINUA SEKTA YA UJENZI

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kadogosa, amesema atashirikiana kwa karibu na viongozi pamoja na watumishi wa Wizara hiyo ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa katika Sekta ya Ujenzi inatekelezwa kwa weledi na ufanisi, kwa lengo la kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika kuendeleza miundombinu nchini.

Mhe. Kadogosa ameyasema hayo leo, Oktoba 2, 2026, katika Ofisi za Wizara ya Ujenzi, Mtumba jijini Dodoma, mara baada ya kuwasili na kukabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Septemba 27, 2026.

Amesema yupo tayari kujifunza, kupokea maoni na ushauri kutoka kwa viongozi, watumishi na wadau mbalimbali kuhusu namna bora ya kuendeleza na kukuza Sekta ya Ujenzi nchini, akisisitiza kuwa sekta hiyo ina mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya taifa.

“Niwaeleze kuwa Ofisi yangu ipo wazi kwa yeyote mwenye maoni na ushauri wa kuboresha Sekta yetu. Mlango upo wazi, tushirikiane kwa pamoja kuinua Sekta hii,” amesema Mhe. Kadogosa.

Aidha, Mhe. Kadogosa amepongeza namna Wizara, kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), ilivyojipanga kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua zinazotarajiwa kunyesha nchini, huku akisisitiza umuhimu wa Wakala huo kuendelea kuchukua tahadhari na hatua stahiki za kuimarisha usalama na uendelevu wa miundombinu ya barabara na madaraja.

Kwa upande wake, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na sasa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Ulega, amewataka watumishi wa Wizara ya Ujenzi kumpa ushirikiano wa kutosha Waziri mpya ili Wizara hiyo iendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kusonga mbele katika ujenzi wa taifa.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo, Oktoba 2, 2026, katika Ofisi za Wizara ya Ujenzi, Mtumba jijini Dodoma, yakishuhudiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu, Balozi, Mhandisi Aisha Amour, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Charles Msonde, Menejimenti ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara.

WADAU WA MAAFA SIMIYU WAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI  KUKABILIANA NA EL NINO.Bariadi.Wadau wa usimamizi wa maafa mkoani Si...
01/10/2026

WADAU WA MAAFA SIMIYU WAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI KUKABILIANA NA EL NINO.

Bariadi.

Wadau wa usimamizi wa maafa mkoani Simiyu wamekutana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Nyaumata, Bariadi, kujadili maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño.

Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Pendo Sospeter Kulen'gwa amefungua kikao hicho kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa usimamizi wa maafa wamekutana kwa lengo la kuimarisha utayari, uratibu na ushirikiano katika kuchukua hatua kabla, wakati na baada ya kutokea kwa majanga yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa.

Timu ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge uratibu na wenye ulemavu pia wameungana na wadau hao wa Maafa Mkoani Simiyu katika kikao hicho kujadili umuhimu wa kubaini maeneo yaliyo katika hatari ya mafuriko, kuimarisha mifumo ya utoaji wa tahadhari kwa wananchi pamoja na kuweka mikakati ya uokoaji na utoaji wa huduma za dharura endapo maafa yatatokea.

Aidha, wadau hao wameelekezwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa, ikiwemo kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kuepuka maeneo hatarishi wakati wa mvua kubwa.

Kikao hicho kimeweka msisitizo katika kuimarisha maandalizi ya Mkoa wa Simiyu ili kuhakikisha hatua za haraka na madhubuti zinachukuliwa kukabiliana na athari za El Niño, huku usalama wa wananchi, mali na miundombinu ukizingatiwa.

Simiyu RS,
1 Oktoba, 2026.

REDIO KWIZERA FM SASA RASMI MKOANI SIMIYU,KUSIKIKA KUPITIA MASAFA YA 91.1 Katika jitihada za kupanua wigo wa usikivu Nch...
01/10/2026

REDIO KWIZERA FM SASA RASMI MKOANI SIMIYU,KUSIKIKA KUPITIA MASAFA YA 91.1

Katika jitihada za kupanua wigo wa usikivu Nchini Redio kwizera FM imebisha hodi Mkoani Simiyu ikipatikana kupitia masafa ya 91.1

Mhariri wa Redio Kwizera FM.Bi Zawadi Bashemela akiambatana na timu ya wataalamu wa Habari na masoko wa Redio hiyo wamefika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuitambulisha Redio hiyo.

Akizungumza na katibu Tawala msaidizi sehemu ya usimamizi wa rasilimali watu Bi.Pendo Sospeter kwa niaba ya katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo , Bi.Bashemela amesema Kwizera FM imeimarisha usikivu wake Mkoani Simiyu na kwamba hatua hiyo ni jitihada za Redio hiyo kupanua wigo wa usikivu katika maeneo mbalimbali Nchini ili kukidhi mahitaji ya wasikilizaji wake.

Amesema Kwizera FM iko tayari kushirikiana vyema na Serikali pamoja na wadau mbalimbali Mkoani Simiyu katika kuhabarisha na kuelimisha Jamii.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya usimamizi wa rasilimali watu Mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa huo Bi.Prisca Kayombo amewahakikishia Kwizera FM ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa jukumu la uhabarishaji jamii.

Amesema Serikali Mkoani Simiyu imekuwa ikishirikiana vyema na vyombo mbalimbali vya habari katika kuhakikisha Wananchi wanapata haki ya msingi ya kikatiba ya kupata taarifa.

Simiyu RS
1 Oktoba 2026.

28/06/2026

..

MAADHIMISHO MIAKA 30 YA TRA SIMIYU,RC SIMIYU AZINDUA GARI LA OFISI INAYOTEMBEA, AAGIZA HUDUMA ZIWAFIKIE WANANCHI PEMBEZO...
27/06/2026

MAADHIMISHO MIAKA 30 YA TRA SIMIYU,RC SIMIYU AZINDUA GARI LA OFISI INAYOTEMBEA, AAGIZA HUDUMA ZIWAFIKIE WANANCHI PEMBEZONI.

Bariadi,

Simiyu: Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anamringi Macha, amezindua gari maalumu la utoaji huduma za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) maarufu k**a Ofisi Inayotembea, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya TRA.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Macha ameipongeza TRA kwa kuendelea kuboresha huduma zake kwa kutumia mifumo na teknolojia inayowarahisishia wananchi kupata huduma za kodi kwa urahisi zaidi.

Amesema kuanzishwa kwa gari hilo ni hatua muhimu ya kusogeza huduma karibu na wananchi, hususan wale wanaoishi katika maeneo ya pembezoni ambayo ni vigumu kufikiwa na ofisi za kudumu za TRA.

Mhe. Macha ameiagiza TRA kuhakikisha gari hilo linatumika kufikisha huduma katika maeneo ya vijijini na pembezoni ili kupanua wigo wa walipakodi na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutoa taarifa mapema kwa wananchi kabla ya gari hilo kufika katika eneo husika, ili waweze kufahamu ratiba ya huduma na kujitokeza kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na TRA.

Kwa upande wake meneja wa TRA Mkoa wa Simiyu Bw.Omar Kirobo, amesema uzinduzi wa Ofisi Inayotembea ni sehemu ya jitihada za taasisi hiyo za kuendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma za kodi, sambamba na kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Simiyu RS
27 Juni,2026.

Address

P O BOX 4
Bariadi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu:

Shortcuts

Share