Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa,Bukoba BRRH

Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa,Bukoba BRRH

Share

Huu ni ukurasa rasmi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba. Karibu kwa huduma bora

27/05/2026

Tunakutakia Sikukuu njema ya Eid-Al-Adha.Wizara ya Afya Tanzania

Photos from Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa,Bukoba BRRH's post 24/05/2026

MICHEZO NI CHACHU YA MSHIKAMANO NA AFYA KWA WATUMISHI BUKOBA RRH

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba wametakiwa kuendeleza utamaduni wa kushiriki michezo k**a njia ya kuimarisha afya, kuimarisha mshik**ano kazini na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Museleta Nyakiroto, wakati akifungua rasmi michezo mbalimbali iliyojulikana k**a “BUKOBA RRH GET TOGETHER BONANZA”, yenye lengo la kuwakutanisha watumishi wa kada tofauti katika mazingira ya urafiki na burudani.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Nyakiroto alisema michezo ni chachu muhimu ya mshik**ano, kwani huwapa watumishi fursa ya kujenga mahusiano mazuri nje ya majukumu ya kazi, kupunguza msongo wa mawazo na kuchochea afya njema ya mwili na akili. Aliongeza kuwa mshik**ano kazini huongeza ushirikiano, mawasiliano bora na hatimaye kuboresha huduma kwa wagonjwa.

“Mazingira ya kazi yenye afya yanahitaji watumishi wenye afya ya mwili na akili. Michezo hutuwezesha kufurahia kazi, kuimarisha umoja na kuongeza ari ya kuwahudumia wananchi,” alisema Dkt. Nyakiroto.

Michezo iliyoshirikiwa katika bonanza hilo ilijumuisha kukimbiza kuku, kuvuta kamba, utambuzi wa rangi, utambuzi wa ladha ya vinywaji pamoja na mechi ya mpira wa miguu kati ya mashabiki wa klabu za Yanga na Simba, ambapo shangwe na burudani vilitawala uwanja.

22/05/2026

UNAKOSAJEEE.Wizara ya Afya Tanzania

17/05/2026

FULL TIME

16/05/2026

TUKUTANE UWANJANI

Photos from Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa,Bukoba BRRH's post 14/05/2026

WANAMICHEZO HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, BUKOBA WAELEKEA MAWENZI RRH KWA ZIARA YA KIMICHEZO

Timu ya michezo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba imeanza safari kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ziara ya kimichezo itakayohusisha mchezo wa mpira wa miguu (football) dhidi ya timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro – Mawenzi RRH.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha mahusiano ya kitaasisi, kukuza mshik**ano baina ya watumishi wa sekta ya afya pamoja na kuendeleza afya na ustawi wa wafanyakazi kupitia michezo. Timu hiyo inajumuisha wachezaji wa kiume na wa k**e, jambo linalodhihirisha ushirikishwaji na usawa katika shughuli za michezo ndani ya hospitali.

Akizungumza kabla ya kuanza safari hiyo, Mwenyekiti wa Michezo wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, Gideon Manyaga, ameishukuru Menejimenti ya hospitali hiyo kwa kuwawezesha wachezaji kwa kuwapatia ushirikiano na ruhusa ya kushiriki mashindano hayo.

Manyaga amesema maandalizi yaliyofanywa na timu hiyo ni ya kuridhisha, akibainisha kuwa wachezaji wako katika hali nzuri ya kisaikolojia na kimwili, huku akiahidi kuwa timu hiyo itacheza kwa nidhamu na ushindani mkubwa.

“Tunashukuru Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kwa kutuunga mkono. Tumefanya maandalizi ya kutosha na tuna imani kuwa tutarejea tukiwa na matokeo mazuri,” amesema Manyaga.

Ziara hiyo ya kimichezo inatarajiwa kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya hospitali hizo mbili, sambamba na kuhamasisha wafanyakazi wa sekta ya afya kushiriki michezo k**a njia ya kuboresha afya na kuongeza ufanisi kazini.Wizara ya Afya Tanzania

14/05/2026

BUKOBA RRH FC SPORT TOUR.Wizara ya Afya

14/05/2026
12/05/2026

BUNGE LAPITISHA KWA KISHINDO BAJETI WIZARA YA AFYA MWAKA 2026/27, KULETA MAPINDUZI SEKTA YA AFYA

Na Zakayo Mosha WAF- Dodoma

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja limepitisha makadirio ya mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Afya yenye jumla ya shilingi Trilioni 1.8 kwa mwaka wa fedha 2026/27 ambayo itasaidia kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya.

Wabunge wengi waliochangia hotuba hiyo wamepongeza uamuzi mahususi wa Serikali ya awamu ya Sita kuweka msisisitizo wa Bima ya Afya kwa wote, Ujenzi wa Muhimbili mpya pamoja Uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa viwanda vya ndani vya Dawa kwa lengo la kupunguza utegemezi kutoka nje.

Hayo yamesemwa Bungeni leo Mei 12,2026 katika Bunge la 13, Mkutano wa Tatu, kikao cha 26 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waheshimiwa Wabunge wakichangia mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya Afya iliyowasilishwa Bungeni hapo tarehe 11 Mei, 2026 na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa.

"Napenda kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utashi wake wa kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya mfano katika utoaji wa huduma bora za Afya kwa Wananchi, nawashukuru Wabunge wote kwa jinsi mlivyochangia michango yenu ya mawazo na kutoa ushauri wa kina kwa Serikali kupitia Wizara ya Afya.

"Michango yote tumeichukua na kuifanyia kazi katika utekelezaji wa bajeti hii mliyopitisha kwa lengo la kuhakikisha Nchi yetu inaendelea kuwa Kitovu kikuu cha Tiba utalii kwa Nchi za Afrika Mashariki," amesema Waziri Mchengerwa

Akichangia hotuba hiyo, Mhe. Elibariki Kingu Mbunge wa Singida Magharibi (CCM) ameishauri Serikali kuongeza bajeti ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba ngazi ya msingi kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi wanaoishi vijijini, kuendelea kuweka kipaumbele katika bajeti hii kwa kutekeleza hitaji kubwa la wananchi la bima ya Afya kwa wote.Wizara ya Afya Tanzania

12/05/2026

Heri ya Siku ya Wauguzi Duniani

10/05/2026

Usikose kufuatilia.Wizara ya Afya Tanzania

Want your business to be the top-listed Government Service in Bukoba?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

P. O. BOX 265
Bukoba