02/06/2026
NJIANI KUELEKEA MOROCCO
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mhe. Ester Amos Bulaya, akiwa pamoja na Mhe.Haji Manara ndani ya ndege kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kutoa hamasa kwa timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, ambayo itashuka dimbani kesho kucheza mchezo wa fainali.
Mhe. Bulaya ni miongoni mwa wabunge waliochaguliwa kuiunga mkono na kuitia moyo timu ya Serengeti Boys katika fainali itakayozikutanisha Tanzania na Senegal, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha vijana wetu kufanya vizuri na kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa katika mashindano hayo.
Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini inawatakia kila la heri Serengeti Boys katika mchezo huo muhimu wa fainali.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Bunda Mjini
01/06/2026
HONGERA SANA MHE. ESTER AMOS BULAYA
HAKIKA WANABUNDA MJINI WANAJIVUNIA UTENDAJI KAZI WAKO
01/06/2026
Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Mhe. Ester Bulaya ametoa vifaa vya michezo kwa timu ya Bajaji FC, lakini pia ametoa vifaa vya ofisi kwaajili ya kuendeshea Umoja wa Madereva Bajaji Mji wa Bunda
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Bunda Mjini
30/05/2026
MASJIDI NURU - MIGUNGANI
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mhe. Ester Amos Bulaya, ametoa sadaka ya vitabu vya dini vya Qur'an na Juzuu katika Msikiti wa Nuru uliopo Mtaa wa Migungani, Kata ya Bunda Stoo.
Sadaka hiyo imelenga kuunga mkono shughuli za kiibada na kuwasaidia waumini wa msikiti huo katika kujifunza na kusoma Qur'an. Katibu wa Mbunge kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini alisisitiza umuhimu wa kuendelea kushikamana na maadili ya dini pamoja na kuimarisha elimu ya kiroho katika jamii.
Kiongozi wa Msikiti wa Nuru(MASJIDI NURU) alimshukuru Mbunge kwa msaada huo, alielezea kuwa vitabu hivyo vitakuwa na manufaa makubwa kwa watoto, vijana na waumini wote wanaoshiriki masomo ya dini katika msikiti huo.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Bunda Mjini