Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake Pemba

Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake Pemba

Share

Karibu katika ukurasa rasmi wa Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake.

Ukurasa huu unatoa taarifa kuhusu maendeleo ya michezo, mashindano, vipaji, matukio na shughuli mbalimbali za michezo zinazofanyika Wilayani Chake Chake

Photos from Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake Pemba's post 18/07/2026

πŸ“ MAFUNZO YA KUENDELEZA MCHEZO WA TABLE TENNIS – MITIULAYA SECONDARY SCHOOL

Kwa lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo wa Table Tennis kwa vijana, Chama cha Mchezo wa Table Tennis Zanzibar (ZTTA) kilishirikiana na Afisi ya michezo wilaya ya chake chake, leo kimeendesha mafunzo ya utangulizi katika Shule ya Sekondari Mitiulaya.

Jumla ya wanafunzi 19 walipata fursa ya kushiriki mafunzo hayo, wakiwemo wasichana 6 na wavulana 13. Washiriki walipata elimu ya msingi kuhusu mchezo wa Table Tennis pamoja na umuhimu wake katika kujenga afya, nidhamu, kujiamini na kuibua vipaji vya michezo.

Aidha, kabla ya kuanza kwa mafunzo haya, mazungumzo ya awali yalifanyika katika Shule ya Sekondari Chasasa na Shule ya Sekondari Utaani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kupeleka programu hii ya maendeleo ya mchezo wa Table Tennis katika shule hizo.

Tunatoa shukrani za dhati kwa viongozi wa shule, walimu, wanafunzi na wadau wote walioshiriki kufanikisha programu hii. Kwa pamoja tunaendelea kujenga msingi imara wa kuibua vipaji vipya na kuendeleza mchezo wa Table Tennis Zanzibar.

πŸ“ Leo tunafundisha mchezo, kesho tunazalisha mabingwa!

Photos from Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake Pemba's post 13/07/2026

MADUNGU SECONDARY SCHOOL TABLE TENNIS DEVELOPMENT PROGRAM KUZINDULIWA RASMI!

Leo Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake imezindua rasmi Programu ya Maendeleo ya Mpira wa Meza (Table Tennis Development Program) katika Skuli ya Madungu Secondary ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuendeleza michezo shuleni na kuibua vipaji vipya vya vijana.
Programu hii inalenga kuwahamasisha wanafunzi kushiriki katika mchezo wa mpira wa meza, kuwajengea nidhamu, kuimarisha afya zao, pamoja na kuwapa mafunzo ya msingi na ya kitaalamu yatakayowawezesha kufikia viwango vya juu vya ushindani.
Zaidi ya wanafunzi 40 wanatarajiwa kunufaika na awamu ya kwanza ya mafunzo haya. Aidha, programu hii itapanuliwa katika shule nyingine teule za Wilaya ya Chake Chake ili kuwafikia vijana wengi zaidi wenye vipaji na hamasa ya mchezo wa mpira wa meza.
Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake inaendelea kuamini kuwa uwekezaji katika michezo ya vijana ni uwekezaji katika afya, nidhamu na mustakabali wa jamii yetu.

Tunawashukuru uongozi wa Madungu Secondary School, walimu na wanafunzi wote kwa ushirikiano wao katika kufanikisha uzinduzi wa programu hii.
"Kujenga Vipaji vya Leo, Mabingwa wa Kesho." πŸ“πŸ’ͺ

Photos from Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake Pemba's post 12/07/2026

πŸ“ UZINDUZI RASMI WA TABLE TENNIS DEVELOPMENT PROGRAM

πŸ“ Fidel Castro Secondary School – Chake Chake, Pemba

Leo tumefanikiwa kuzindua rasmi Programu ya Maendeleo ya Mchezo wa Table Tennis katika Fidel Castro Secondary School, ambapo wanafunzi wamepatiwa mafunzo ya awali kuhusu mchezo huu ikiwa ni hatua ya kuanza rasmi safari ya kukuza vipaji vyao.

Programu hii inalenga:
βœ… Kugundua na kukuza vipaji vya wanafunzi.
βœ… Kukuza afya, nidhamu na kujiamini kupitia michezo. βœ… Kuandaa wachezaji watakaoiwakilisha shule, Wilaya ya Chake Chake, Pemba na Zanzibar katika mashindano mbalimbali.
βœ… Kupanua ushiriki wa vijana katika mchezo wa Table Tennis.

Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake inaendelea kushirikiana na shule mbalimbali kuhakikisha michezo inakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Tunatoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa Fidel Castro Secondary School, walimu, wanafunzi na wadau wote waliofanikisha uzinduzi huu.

Pamoja tunajenga vipaji, tunaimarisha afya, na tunaendeleza michezo! πŸ“πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

08/07/2026

πŸ“ AFISI YA MICHEZO WILAYA YA CHAKE CHAKE YAZINDUA PROGRAMU YA MAENDELEO YA MPIRA WA MEZA (TABLE TENNIS DEVELOPMENT PROGRAM)

Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake kwa kushirikiana na wadau wa mchezo wa mpira wa meza inawakaribisha wanafunzi na vijana wote kushiriki katika uzinduzi wa **Programu ya Maendeleo ya Mpira wa Meza**, inayolenga kuibua vipaji, kukuza uwezo wa wachezaji na kuimarisha ushiriki wa vijana katika michezo.

πŸ“… Tarehe: Jumamosi, 11 Julai 2026
πŸ•“ Muda: Saa 4:00 Asubuhi
πŸ“ Mahali: Skuli ya Sekondari Fidel Castro

Kupitia programu hii, washiriki watapata fursa ya:
πŸ“ Kujifunza mbinu na misingi ya mchezo wa mpira wa meza.
πŸ“ Kutambuliwa na kuendelezwa vipaji vyao.
πŸ“ Kuimarisha afya ya mwili, nidhamu na ushirikiano.
πŸ“ Kujiandaa kushiriki mashindano katika ngazi mbalimbali.

Tunawaalika wanafunzi, wazazi, walimu na wadau wote wa michezo kujitokeza kwa wingi kushuhudia na kushiriki katika hatua hii muhimu ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa meza katika Wilaya ya Chake Chake.

Kwa mawasiliano:
πŸ“§ Email: [email protected]
πŸ“±WhatsApp: +255 623 973 635

Tufuatilie kupitia:
πŸ“˜ Facebook: Afisi ya Michezo Chake Chake Pemba
🎡 TikTok: michezo wilaya ya chake chake

"Tukuze Vipaji, Tujenge Mabingwa wa Kesho."

Photos from Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake Pemba's post 05/07/2026

AFISI YA MICHEZO WILAYA YA CHAKE CHAKE YAPOKEA UGENI KUTOKA UINGEREZA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KUENDELEZA MCHEZO WA MPIRA WA MEZA

Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake imepata heshima ya kupokea ugeni kutoka nchini Uingereza ukiongozwa na Mr. Peter, ambaye amewasili kwa lengo la kujenga ushirikiano katika kukuza na kuendeleza mchezo wa Mpira wa Meza (Table Tennis) kisiwani Pemba, huku Wilaya ya Chake Chake ikitarajiwa kuwa eneo la majaribio (pilot district) la utekelezaji wa programu hiyo.

Katika ziara hiyo, Mr. Peter alipata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake pamoja na Afisa Mdhamini wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, kwa ajili ya kupata ridhaa, ushauri na baraka za kuanzisha ushirikiano huo muhimu unaolenga kuimarisha maendeleo ya mchezo wa mpira wa meza katika wilaya na hatimaye Zanzibar kwa ujumla.

Aidha, Afisa Michezo wa Wilaya ya Chake Chake, Ndg. Khalid Ahmed Khalid, alimpa mgeni huyo maelezo ya kina kuhusu hali halisi ya mchezo wa mpira wa meza upande wa Pemba, ikiwa ni pamoja na mafanikio yaliyopo, changamoto zinazoukabili mchezo huo na fursa zilizopo za kuukuza kupitia ushirikiano huo.

Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake inaendelea kuwa na dhamira ya dhati ya kukuza na kuendeleza michezo mbalimbali wilayani humo, kwa lengo la kuibua vipaji, kuimarisha afya na ustawi wa jamii, pamoja na kufungua fursa za kijamii, kielimu na kiuchumi kupitia sekta ya michezo.

"Pamoja tunaijenga Chake Chake yenye michezo imara na yenye kutoa fursa kwa kila mwananchi."

Photos from Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake Pemba's post 30/06/2026

VIJANA WA CHAKE CHAKE KUANDAA BONANZA KUBWA KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA DUNIANI 2026

Leo, Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake imepata fursa ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Vijana Wilaya ya Chake Chake kilichohudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Mheshimiwa Zuhura Mgeni Othman, pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya. Kikao kilichofanyika katika Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake chake, kilijadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya vijana, hususan nafasi ya michezo katika kukuza vipaji na kuimarisha mshikamano miongoni mwa vijana.

Katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Wilaya ya Chake Chake, Ndugu Fihim Abdallah Mohammed, aliwasilisha agenda mbalimbali za baraza hilo, zikiwemo maandalizi ya kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani itakayofanyika tarehe 12 Agosti 2026. Maadhimisho hayo yataambatana na bonanza kubwa litakalojumuisha michezo mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wa vijana, kuibua na kukuza vipaji, pamoja na kuongeza ari na mshikamano miongoni mwa vijana.

Aidha, alieleza umuhimu wa kupata baraka na ushirikiano wa uongozi wa wilaya ili kuhakikisha bonanza hilo linafanikiwa kwa kiwango cha juu na kuwa chachu ya maendeleo kwa vijana wa Chake Chake.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Mheshimiwa Zuhura Mgeni Othman, aliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Baraza la Vijana, Afisi ya Michezo na wadau wote husika ili kuhakikisha maandalizi na utekelezaji wa bonanza hilo unakuwa wa mafanikio na mfano wa kuigwa katika wilaya.

Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake inaendelea kushirikiana kwa karibu na Baraza la Vijana pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha michezo inabaki kuwa chombo muhimu cha kuibua vipaji, kuimarisha afya na kuchochea maendeleo ya vijana.

28/06/2026

πŸ“ CHAKE CHAKE TABLE TENNIS TRAINING PROGRAM – COMING SOON!

Je, una ndoto ya kuwa mchezaji bora wa Table Tennis? Hii ndiyo fursa yako!
Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake inawatangazia watoto, vijana na watu wazima kujiandikisha katika programu maalum ya mafunzo ya mchezo wa Table Tennis, yenye lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo.
πŸ“Œ Makundi ya Umri:
πŸ”Ή 7 – 10 miaka
πŸ”Ή 11 – 14 miaka
πŸ”Ή 15 – 17 miaka
πŸ”Ή 18+ miaka
πŸ“ Jisajili mapema upate nafasi yako!
πŸ“ž Usajili: 0623 973 635
Karibu ujifunze, ujenge uwezo wako na uwe sehemu ya kizazi kipya cha wachezaji wa Table Tennis kutoka Wilaya ya Chake Chake.
Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake – Kuibua Vipaji, Kukuza Vipaji, Kuendeleza Vipaji. πŸ’šπŸ“

Photos from Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake Pemba's post 23/06/2026

Baraza la Vijana na Afisi ya Michezo Chake Chake Waungana Kuandaa Maadhimisho Maalum ya Siku ya Vijana Duniani kwa Msimu wa Michezo

Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake imekutana na uongozi wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Chake Chake katika kikao maalum kilichohudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa baraza hilo pamoja na Idara ya Maendeleo ya Michezo. Lengo kuu la kikao hicho lilikuwa ni kuratibu maandalizi ya shughuli za kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani.

Kikao hicho kilijadili na kupanga mambo mbalimbali muhimu yanayohusiana na maandalizi ya maadhimisho hayo, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa vikao vingine vya baadas vitakavyoendelea kuratibu kwa pamoja shughuli hiyo muhimu kwa vijana wa wilaya.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, ndugu Fihim Abdallah Mohammed, alitoa hamasa kwa viongozi wenzake wa baraza hilo na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya Baraza la Vijana na Idara ya Maendeleo ya Michezo ili kufanikisha kwa ufanisi maandalizi ya maadhimisho hayo.

Kwa upande wake, Afisa Michezo wa Wilaya ya Chake Chake, ndugu Khalid Ahmed Khalid, aliunga mkono juhudi hizo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuratibu, kukuza na kuendeleza michezo wilayani humo, ikiwa ni njia ya kuwapa vijana fursa ya kuibua na kuendeleza vipaji vyao.

Baraza la Vijana la Wilaya ya Chake Chake kwa awamu hii limejipanga kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani kwa namna ya kipekee, ambapo michezo mbalimbali ya vijana itajumuishwa katika shughuli hiyo ili kuhakikisha maadhimisho hayo yanakuwa ya mafanikio na yenye mvuto mkubwa kwa jamii.

23/06/2026

πŸ€ CHAKE CHAKE TOTO BASKETBALL LEAGUE 2026 πŸ€

Afisi ya Michezo Wilaya ya Chake Chake inawakaribisha vijana wote kushiriki katika mashindano makubwa ya mpira wa kikapu kwa watoto – Chake Chake Toto Basketball League 2026.

Huu ni muda wa kuonesha vipaji, kujenga nidhamu na kukuza ndoto za michezo kwa kizazi kipya.

πŸ“ Jiandae kushuhudia vipaji vipya vikizaliwa
πŸ“… Muda si mrefu kuanza
πŸ”₯ Usikose kuwa sehemu ya historia

Want your business to be the top-listed Government Service in Chake Chake?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

MKUU WA WILAYA OFFICE
Chake Chake
7100

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30