Ubungo Manispaa Page

Ubungo Manispaa Page

Share

Ukurasa rasmi wa Manispaa ya Ubungo (Page)

Photos from Ubungo Manispaa Page's post 19/03/2023

๐Œ๐ˆ๐€๐Š๐€ ๐Œ๐ˆ๐–๐ˆ๐‹๐ˆ ๐˜๐€ ๐”๐Ž๐๐†๐Ž๐™๐ˆ ๐“๐‡๐€๐๐ˆ๐“๐ˆ ๐–๐€ ๐ƒ๐Š๐“. ๐’๐€๐Œ๐ˆ๐€ ๐’๐”๐‹๐”๐‡๐” ๐‡๐€๐’๐’๐€๐
๐‘๐š๐ข๐ฌ ๐–๐š ๐‰๐š๐ฆ๐ก๐ฎ๐ซ๐ข ๐ฒ๐š ๐Œ๐ฎ๐ฎ๐ง๐ ๐š๐ง๐จ ๐–๐š ๐“๐š๐ง๐ณ๐š๐ง๐ข๐š

๐”๐๐”๐๐†๐Ž ๐“๐”๐๐€๐’๐„๐Œ๐€ ๐€๐’๐€๐๐“๐„ ๐’๐€๐๐€ ๐Œ๐€๐Œ๐€ ๐Ÿ™

๐Œ๐š๐œ๐ก๐ข ๐Ÿ๐Ÿ—, ๐Ÿ๐ŸŽ๐Ÿ๐Ÿ - ๐Œ๐š๐œ๐ก๐ข ๐Ÿ๐Ÿ—, ๐Ÿ๐ŸŽ๐Ÿ๐Ÿ‘ ๐Ÿ’ช








Photos from Ubungo Manispaa Page's post 18/03/2023

MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA, UBUNGO TUPO VIZURI

ASANTE SANA MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ๐Ÿ™








Photos from Ubungo Manispaa Page's post 17/03/2023

LAAC YAFURAHISHWA NA MIPANGO ZA MANISPAA YA UBUNGO JUU YA SOKO LA MABIBO.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali za mitaa (LAAC) imeipongeza Manispaa ya Ubungo kwa juhudi za kuhakikisha soko la Mabibo kuwa ni soko lenye kuwanufaisha wananchi wote wa Manispaa hiyo.

Pongezi hizo amezitoa leo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Halima Mdee Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa ziara waliyoifanya ndani ya Manispaa hiyo.

Hayo yamejiri kufuatia suala la eneo la soko hilo ambalo hapo awali lilikabidhiwa kwa viongozi wa soko hilo na baadae kupelekea kutoweza kusimamia vyema soko hilo kwa maana ya kutokutoa taarifa za mapato na matumizi, na kutosimamia vyema usafi na utunzaji wa mazingira ya soko hilo na kupelekea mazingira hatarishi kwa wananchi na wajasiriamali kwa ujumla ndani ya soko hilo

Akifafanua suala hilo Mkurugenzi wa Manispaa amesema soko hilo kwa sasa lipo chini ya eneo la kiwanda cha nguo Urafiki na tayari pande zote kwa maana ya Manispaa na Kiwanda hicho wamekubaliana soko hilo lisimamiwe na Manispaa hiyo na kwa sasa taratibu zingine zinaendelea kufuatwa ikiwemo ya kupata umiliki halali wa soko.

Kamati hiyo imeitaka wizara ya TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha kuwa suala la umiliki wa ardhi ya soko hilo linafanyiwa kazi haraka ili kuondoa mvutano uliopo na mchakato wa kuliendeleza soko hilo uendelee kwa maslahi ya watanzania.

โ€œNimefurahishwa na hatua ya halmashauri ya Ubungo kushirikisha wadau wote wa soko wanashirikishwa juu ya uendeshwaji wa soko hilo na wote kwa pamoja kuona ni vyema soko hilo lisimamiwe na Manispaa kwa maslahi ya wananchi woteโ€ alisema Mdee.

Kwa upande wake Mhe. Jesca Msambatavangu Mbunge wa Iringa Mjini amesema Serikali lazima ione umuhimu wa haraka wakuhakikisha suala hili linaisha kwa kuhakikisha Manispaa inapata hati na kulisimamia vyema soko hilo kwa maslahi ya wananchi wetu.

โ€œEneo hilo tayari kwa sasa lina wajasiriamali wengi na bado mara kadhaa Manispaa imekuwa ikihakikisha soko hilo linakuwa na mazingira salama kwa maana ya usafi wa soko hilo kwani wajibu wa Serikali ni kuwahudumia wananchiโ€ alisema

tanzania



Photos from Ubungo Manispaa Page's post 16/03/2023

KIKAO KAZI CHA TATHIMINI YA UTENDAJI KAZI KWA IDARA YA AFYA NUSU MWAKA 2022/2023

Idara ya afya Manispaa ya ubungo imefanya kikao kazi cha tathmini ya utendaji kazi kwa nusu mwaka julai- disemba 2022 ambapo taarifa kutoka vitengo mbalimbali vya idara ya afya, hospitali za umma na binafsi pamoja na zahanati ziliweza kutoa tathmini ya shughuli zilizotekelezwa

Aidha Katika kikao hicho Kuna vituo vya Afya, hospitali na zahanati ambazo zilionekana kufanya vizuri kwa utoaji mzuri wa huduma kwa wananchi na kufanikiwa kupewa vyeti vya pongezi kwa utendaji bora

Akiongea katika kikao hicho Mganga Mkuu Dkt.Tulitweni Mwinuka amesisitiza watumishi wote wa Afya kufanya kazi kwa weledi na kila mmoja katika kituo chake afanye kazi kwa uzalendo ili kuhakikisha Ubungo inaendelea kusimama imara katika utoaji wa huduma za afya

Aidha, Dkt. Tulitweni aliwapongeza wale wote ambao wamepata vyeti vya pongezi kwa kuonyesha utendaji kazi mzuri na kuwaasa waendelee kuwajibika vyema katika kuhakikisha huduma nzuri za afya zinatolewa kwa wananchi

Zoezi la ugawaji wa vyeti vya pongezi kwa hospitali, zahanati na vituo vya Afya pamoja na hospital binafsi zilizofanya vizuri ulifanyika ikiwemo Hositali ya Wilaya ya Ubungo, Sinza, kituo cha Afya Kimara, zahanati ya Kibwegere, zahanati ya Msumi, zahanati ya Mburahati, zahanati ya Kiluvya, zahanati ya Mabibo na zahanati ya Kwembe



Photos from Ubungo Manispaa Page's post 16/03/2023

HABARI PICHA

Mapema leo Machi 16, 2023 waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) amezindua mradi wa ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji kutoka Makongo hadi Bagamoyo uliotekelezwa na DAWASA.

Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tegeta A ambapo Majaliwa alibonyeza kitufe maalumu cha kuruhusu maji k**a ishara ya uzinduzi wa mradi huo ambao umegharimu shilingi Bilioni 65.4 kwa kushirikiana na Benki ya dunia

Mradi huo utanufaisha wakazi 450,000 kutoka Makongo Hadi Bagamoyo






Photos from Ubungo Manispaa Page's post 15/03/2023

๐“๐€๐๐†๐€๐™๐Ž ๐‹๐€ ๐Š๐€๐™๐ˆ

Photos from Ubungo Manispaa Page's post 14/03/2023

HABARI PICHA

Timu ya Menejimenti ya Manispaa ya Ubungo ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. Beatrice Dominic ikiwa kwenye ukaguzi wa kituo cha Mabasi cha Magufuli kwa lengo la kuhakikisha hakuna mapato yanayopotea kwenye kituo hicho na kuimarisha mikakati ya ukusanyaji wa mapato ya kituo hicho.

13/03/2023

MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA, UBUNGO TUPO VIZURI

Huduma ya Afya inazidi kuboreshwa kwenye mitaa na kata mbalimbali za Manispaa ya Ubungo

Hichi ni kituo cha Afya Amani, ambapo majengo mawili yameongezwa ili kupanua zaidi uwezo wa kuhudumia wananchi wa kata ya Kwembe na maeneo jirani









Photos from Ubungo Manispaa Page's post 10/03/2023

TAARIFA KWA UMMA

Photos from Ubungo Manispaa Page's post 10/03/2023

KONGAMANO LA MAFANIKIO YA MIAKA MIWILI YA UONGOZI WA MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN LAFANYIKA KWA KISHINDO

Katika kuelekea kutimiza kwa miaka miwili ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu Machi 19, 2021 alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo machi 10, 2023 ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam imeandaa kongamano maalumu la kusheherekea mafanikio mbalimbali yaliyopatikana ndani ya miaka hii miwili ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan

Kongamano hilo limefanyika mapema leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo Upanga Manispaa ya Ilala ambapo pia umehudhuriwa na viongozi mbalimbali ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam

Akiongea katika kongamano hilo mgeni rasmi Mhe. Amos Makalla amesema kwa kipindi cha Miaka miwili mkoa wa Dar es Salaam umepiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali.
- Katika sekta ya maji kumekua na miradi mikubwa ya maji ikiwemo ujenzi wa tenki kubwa la maji la Mshik**ano pamoja na Tegeta A,
Pia ametoa fedha Bilion 65 kwaajili ya usambazaji wa maji maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam pamoja na kutoa Bilioni 350 kwaajili ya ujenzi wa mifumo ya maji taka
- Upanuzi wa barabara kubwa kutoka Kimara mpaka Kibaha umefikia asilimia 97 na fedha zilizoletwa ni zaidi ya Bilioni 218
- Uboreshaji wa masoko umeshatumia zaidi ya shilingi Bilioni 24.5 kwa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam
- Katika Sekta ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, Bilioni 18 zimetolewa kwa vikundi mbalimbali ndani ya mkoa wa Dar es Salaam
- Uendelezaji wa miradi ya usafiri wa kwenda kwa haraka ambapo sasa ipo awamu ya pili kati ya awamu sita zinazotakiwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali

Hakika katika miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan, hatua kubwa ya maendeleo imefikiwa katika mkoa wa Dar es Salaam

Makalla ameendelea kusema kuwa bado mipango mikubwa ya maendeleo katika mkoa huu inaendelea kuwekwa ikiwemo mpango wa kujenga daraja kubwa la juu kutoka Magomeni mpaka Fire na hiyo itaondoa kero ya mafuriko katika eneo la mto Msimbazi








07/03/2023

- Kuelekea Miaka Miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan Madarakani, Ubungo tunashukuru kwa Uongozi wake ambao unaacha Alama ya Ushindi katika Sekta ya Elimu

- Shule maalumu ya Mkoa ya Wasichana inajengwa katika mtaa wa Njeteni kata ya Kwembe Manispaa ya Ubungo kwa Gharama ya Shilingi Bilioni tatu za Kitanzania

- Sisi Ubungo Tunasema ASANTE SANA MAMA, UBUNGO TUPO VIZURI










Photos from Ubungo Manispaa Page's post 06/03/2023
Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


55068
Dar Es Salaam
LUGURUNI