29/04/2026
Kwenye kikao cha WAFALME tulikubaliana jambo moja zito: _
Hakuna kutoa pesa kwa mwanamke ili akuone upo serious._ Tabia ya kupima ukweli wa mapenzi kwa noti ni matumizi mabaya ya rasilimali. Imeacha Wafalme wengi wakiwa washindi wa muda mfupi, lakini masikini wa kudumu. Wakati umefika wadada nao waache ushamba wa kudhani kwamba “akitoa pesa basi ananipenda”.
1. Pesa hainunui heshima, inakodisha umaskini.
Unapotoa pesa ili tu “akubali” au “akuone serious”, hujengi mapenzi. Unanunua attention. Shida ni kwamba attention ya kununuliwa ina tarehe ya mwisho. Noti zikiisha, na “upendo” unaisha. Matokeo yake: Wafalme wengi wamebaki na akaunti tupu, madeni, na moyo uliovunjika.
Huo si utawala, ni utumwa wa mfukoni. Rasilimali ni kwa ajili ya kujenga himaya, si kununulia validation.
2. Kulazimisha kukubalika kwa fedha ni ishara ya kutokujiamini.
Mwanaume anayejua thamani yake hajilipii kukubalika. Tabia, mipango, nidhamu, na dira ndiyo vinavutia mwanamke wa maana. Ukitoa iPhone 15, hela ya salon, na “pesa ya kutoa macho” kabla hata hajui jina la mama yako, unajishusha. Unamtuma ujumbe kwamba bila fedha wewe si kitu. Na huyo dada akija kwako, atakuja kwa ajili ya noti, si kwa ajili yako. Ukifilisika, ataondoka na noti kwenda kwa mfalme mwingine.
3. Wadada, acheni ushamba wa “Akitoa pesa ndiyo ananipenda”.
Dada, ukipima seriousness ya mwanaume kwa M-Pesa, unajitengenezea mtego. Wanaume wa kweli wana akili ya kujenga, si ya kusambaza. Atakupenda atakupa muda, ulinzi, mipango ya pamoja, atakufundisha biashara, atakuheshimu mbele za watu. Hayo hayaonekani kwenye _transaction message.
Kumbuka: mwanamke anayependa pesa kuliko mtu, atapata pesa lakini atamkosa mtu. Na pesa ya mtu mwingine haina pension. Leo yupo, kesho ameondoka na noti zake. Baki na tabia yako.
4. Mahusiano ya kifedha yanazaa aina mbili za umaskini
a) Umaskini wa Mfukoni:
Mwanaume anatoa hela kila siku ili azuie dada asiondoke. Mwisho wa mwezi anashindwa kuwekeza, anashindwa kujenga. Anabaki Mfalme wa jina tu.
b) Umaskini wa Akili:
Dada anazoea kupata bila kufanya kazi. Ubunifu unakufa. Thamani yake inabaki kwenye urembo na ushawishi. Akizeeka au urembo ukipungua, soko linamkataa. Anabaki na picha za Dubai na akaunti ya 0.
5. Wafalme hujengwa kwa nidhamu ya rasilimali, si kwa hisani za mapenzi.
Warren Buffet hajawa tajiri kwa kutuma “lunch money” kwa kila demu aliyemwambia “uko serious?”. Aliwekeza.
Wafalme wa kweli wana bajeti. Pesa ya mahusiano ni kwa ajili ya kujenga kitu: biashara ya pamoja, ardhi, elimu ya mtoto. Si kwa “ushahidi wa upendo”. Ukitaka kutoa, toa kwa sababu kuna dira, si kwa sababu unaomba ruhusa ya kupendwa.
Weka Sheria Mezani.
1. Wafalme: Usilazimishe kukubalika kwa fedha. Mwanamke wa maana atakubali kwa tabia yako, mipango yako, na heshima yako. Anayekutaka kwa pesa, mwache anunue mwanaume mwingine.
2. Wadada: Acheni ushamba. Mwanaume akitoa pesa siyo cheti cha upendo. Waulize “tunaelekea wapi?” badala ya “utanitumia ngapi?”. Pesa bila mwelekeo ni mtego.
3. Jamii: Turudishe heshima ya mahusiano. Tupendane kwa dhamira, tujenge kwa mipango, si kwa transaction.
K**a tulivyokubaliana kikao cha Wafalme: Rasilimali ni silaha ya kujenga ufalme, si tiketi ya kununulia upendo. Ukivunja sheria hii, utabaki Mfalme wa hadithi tu – mwenye kofia lakini bila kiti cha enzi.
Tunza noti zako, jenga ubongo wako. Mwanamke wa maana atakupenda bure. Na Mfalme wa maana hatolipa kukubalika.
29/04/2026
MAISHA YA SINGLE MOTHER SIYO KISINGIZIO CHA KUWAJERUHI WENGINE.
Kuwa mama asiye na mume, au “single mother”, siyo kosa. Wapo wanawake waliofiwa, walioachwa, walioamua kulea watoto peke yao kwa sababu mbalimbali. Jamii inapaswa kuwasaidia, si kuwahukumu. Lakini hivi karibuni kumetokea tabia mpya mitandaoni, hasa Facebook: baadhi ya single mothers kutumia uhuru wao wa kifedha na muda wa kusafiri kueneza ujumbe kwamba ndoa ni gereza, na kwamba kila mwanamke aachike ili “aishi maisha”. Tabia ya kuwadhalilisha walio kwenye ndoa na kujivika utukufu wa kubadili wanaume kila siku ni hatari kwa jamii. Makala hii inaonya tabia hiyo kwa hoja 5 kuu.
1. Uhuru wa kifedha siyo leseni ya kuvunja misingi ya jamii.
Kupata hela na muda wa kuzunguka Tanzania nzima au nchi za nje ni baraka binafsi. Ni matokeo ya kazi, biashara, au bahati. Lakini hiyo siyo sheria kwamba kila mwanamke lazima aige njia hiyo. Ndoa ni taasisi ya kijamii na kisheria. Kuiita “gereza” hadharani ni kudharau maelfu ya familia zinazojitahidi kujenga taifa. Uhuru wako usiishie kuwa msumari wa kuwajeruhi wengine.
2. Kuhamasisha talaka kwa makusudi ni uharibifu wa kizazi.
Takwimu za Mahak**a ya Tanzania zinaonyesha talaka zinaongezeka. Mtoto anayelelewa na wazazi wote wawili ana nafasi kubwa zaidi kielimu na kihisia. Unaposhawishi mwanamke aachane na mumewe kwa sababu “wewe unaishi vizuri bila mume”, unamsukuma kuingia kwenye takwimu za watoto wanaoishi na mzazi mmoja, wenye changamoto za ada, malezi, na nidhamu. Huo ni ubinafsi, si ukombozi.
3. Kujiuza na kubadili wanaume si “soft life”, ni mteremko wa hadhi.
Kila mtu ana haki ya mahusiano. Lakini kujisifu mitandaoni kwamba unabadili mwanaume “kila uchwao” unakuwa mfano mbaya kwa mabinti wanaokutazama. UNICEF inaripoti kuwa Tanzania ina changamoto ya mimba za utotoni na UKIMWI miongoni mwa vijana. Ujumbe wa “tumia mwili upate hela” unazidisha tatizo. Maisha ya anasa ya muda mfupi huacha makovu ya magonjwa, watoto wasio na baba, na heshima iliyopotea.
4. Kuponda walioolewa ni wivu uliojificha.
Kumkashifu mwanamke aliyeamua kuvumilia ndoa yake, kumtunza mumewe na watoto, si ujasiri. Ni dalili ya kutokukubali chaguo la wengine. Ndoa ina changamoto – heshima, uvumilivu, msamaha. Siyo kila aliye kwenye ndoa “anateseka”. Wapo wanaoishi kwa amani, mapenzi na maendeleo. Kuwaita “wajinga wanaovumilia gereza” ni kuwavua utu. Kumbuka: usipotaka kitu, usikiharibie wengine.
5. Mtandao siyo mahak**a ya maisha ya watu
Facebook si ushahidi wa ukweli.
Picha za Dubai, Zanzibar, na hoteli za kifahari hazionyeshi machozi ya usiku, madeni, au upweke. Wanawake wengi waliodanganywa na “maisha ya single mother tajiri” leo wanalia kimya. Wameacha ndoa, wameingia mitaani, sasa heshima imeyeyuka na wanaume waliowahidi maisha wametoweka. Usiwe wakala wa kuwatoa wengine njia.
Kuwa single mother si dhambi. Kuwa na hela na kusafiri si kosa. Kosa ni kutumia hadhi yako kuharibu ndoa za watu, kuwatukana waliochagua familia, na kupandikiza utamaduni wa anasa za mwili k**a njia ya mafanikio.
K**a una ushahidi Facebook, ni vema kuutumia kwa busara: toa elimu, si kejeli. Kumbusha mabinti kwamba thamani ya mwanamke haipimwi kwa nchi alizotembelea wala wanaume aliobadili, bali kwa tabia, akili na mchango wake kwa jamii.
Tuchague maneno yetu. Tusijenge taifa la watu waliovunjika kwa sababu ya post za kuhamasisha ubinafsi.
Andiko hili ni kwa ajili ya kuonya tabia, si kushambulia single mothers wote.
Wapo wengi wenye heshima, wanalea watoto kwa taabu na unyenyekevu. Hao tunawaheshimu na kuwapa mkono.
29/04/2026
MAISHA YA MITANDAONI NA MITEGO YA "SINGLE MOTHERHOOD" K**A FASHENI.
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la ajabu kwenye mitandao yetu. Kuna kampeni ya chini kwa chini inayojaribu kuaminisha jamii kuwa kuwa "Single Mother" ni sifa, ni ujanja, na ndiyo njia pekee ya mwanamke kupata uhuru na maendeleo.
Lakini tuseme ukweli Kuwa Single Mother siyo uzoefu wa kutamaniwa, na wala siyo SHERIA kwamba kila mwanamke lazima aishi hivyo ili afanikiwe.
Kuna mambo machache ya kutafakari:
✅ MAFANIKIO HAYANA HALI YA NDOA: Kupata hela, kumiliki gari, au kuzunguka nchi za nje siyo matokeo ya kuachika. Kuna wanawake wengi wako kwenye ndoa na wanafanya makubwa kuliko unavyoona kwenye picha za Facebook. Usidanganyike na picha za "vacation" ukadhani ndoa ndiyo inakuzuia kupata hela.
✅ UHURU AU UPOTEVU? Kuna tofauti kati ya mwanamke huru na mwanamke anayetangatanga. Kutumia kisingizio cha "uhuru"
Inasikitisha kuona Facebook imekuwa dampo la akili mbovu.
Kuna kundi la wanawake wamejawa na kiburi cha ajabu, wanatumia picha za matembezi, safari za nje, na mapozi ya bandia kuaminisha watu kuwa "Single Motherhood" ni mafanikio. Huu ni upotoshaji wa kiwango cha lami na ni lazima usemwe!
Kupata hela na kuzunguka nchi siyo kigezo cha kuwa single. K**a unadhani lazima uachike au uishi bila mume ndipo ufanikiwe, basi una matatizo ya akili. Kuna wanawake wana heshima zao ndani ya ndoa na wanazunguka dunia nzima kuliko ninyi mnaojiuza kwa vipande vya fedha na safari za kupewa.
Kuwa "Single Mother" kwa hiyari na kuponda walioolewa ni LAANA.
Unajisifia uhuru, lakini uhuru wako ni wa kubadilisha wanaume k**a nguo? Huo siyo uhuru, huo ni "ukahaba uliopambwa." Kutwa kucha unashinda Facebook kuponda walioolewa ili kuficha maumivu ya upweke yanayokutafuna moyoni. Unajiona mjanja, kumbe ni gunia la misiba!
Acheni kuwahadaa mabinti wadogo.
Unawafundisha watoto wa watu kuwa ndoa ni utumwa wakati wewe unatumika k**a chombo cha starehe na wanaume tofauti kila wiki. Unajenga sifa kwenye mchanga huku ukiharibu msingi wa familia. Maisha ya "kujiuza" na kutanga na njia siyo ya kuonewa gere, ni ya kuhurumiwa.
Watoto wanahitaji baba, siyo picha za "vacation." Wakati unajisifia kuwa "strong single mother," kumbuka unawanyima watoto wako haki ya msingi ya kuwa na baba. Unatengeneza kizazi chenye makovu kwa sababu ya ubinafsi wako na tamaa za mwili.
Maisha ya anasa unayoyaonyesha Facebook huku ukiwatukana walioolewa ni kichekesho.
Pesa za "kuhongwa" na safari za "kubet" hazitakaa zilingane na heshima ya mwanamke anayetambua thamani ya familia na utu wake.
K**a umeachwa au maisha yamekupiga, tulia ulee watoto wako kwa adabu. Lakini usituletee kampeni za kijinga za kutaka wanawake wenzako waachike ili wawe wahuni k**a wewe.
Heshima ni bure, lakini kuipoteza ni gharama!.
04/04/2026
We met on Facebook and talked for over a month before planning to meet. He lives in Tema, and I’m in Adenta. He wanted me to visit him in Tema, but I wanted our first meeting to be on neutral grounds. Eventually, we agreed to meet at the mall.
I got there first and ordered something to eat while waiting for him. He was an hour late. When he finally arrived and saw me eating, he said, “Why did you order when I’m not here? What if I’m not able to pay?”
I smiled and welcomed him. I told him not to worry because I could pay. He ordered a bottle of water, and we sat talking. Throughout the conversation, I could see his eyes were fixed on my food. He wasn’t even concentrating and was also sweating. I said, “Why don’t you order food? If you’ll allow me, I’ll pay.”
He called the waitress and asked to be served the same food I was eating. While he ate, he became calmer and more focused. His sense of humor came back—the one thing I loved about him. We spent hours together, but it felt like minutes. When we were leaving and I tipped the waitress, he asked why I was giving her money when she was only doing her job.
When we were parting, he walked me to the car park, and I opened my car door. He asked, apparently surprised, “Is that your car? You didn’t tell me you were a rich girl. Or it belongs to your dad? Who got it for you?”
He asked a hundred questions within a minute. I told him that was the car I drove to the venue. I didn’t answer any of his other questions because I didn’t see the need to. I drove away while he stood akimbo, watching me leave the park.
When he got home, he texted, “I’m sorry if I made you feel some type of way. I know I’m not your type, but we can be friends if you don’t mind.”
Two days later, he was asking me for a favor because life was hard. This is the same person who told me he was an engineer at the port. When I didn’t respond to his messages, he blocked me, and that was it.
I’m like, what did I do? I thought we were getting to know each other, so why the haste in blocking me? I liked him. I was getting to love him until he messed it all up.
28/03/2026
Ulimwengu wa Malezi na Ucheshi wa Maisha ya Uzazi.
Malezi ya mtoto ni safari ya kipekee ambayo huja na changamoto zake, mafunzo mapya, na wakati mwingine matukio ya kushangaza yanayoweza kumfanya mzazi acheke au hata asijue la kufanya. Hadithi ya mama mmoja anayeshuhudia mtoto wake akicheza “mkutano wa kifamilia” na wanasesere wake, inaakisi ukweli mmoja muhimu: watoto wana uwezo mkubwa wa kufikiria, kuiga, na kujifunza kupitia ulimwengu wa ndoto na michezo.
Katika tukio hili, mtoto Vivian anaonekana kuchukua nafasi ya “mama” kwa wanasesere wake. Anawapanga, anawahoji, na hata kuwapa “nidhamu” kana kwamba ni kikao rasmi cha watu wazima. Hii si ajabu kwa mtazamo wa maendeleo ya mtoto. Watoto mara nyingi huiga yale wanayoyaona kutoka kwa wazazi na jamii yao. Michezo ya kuigiza (role play) huwasaidia kuelewa majukumu, hisia, na mahusiano ya kijamii.
Kwa mzazi, tukio k**a hili linaweza kuleta hisia mchanganyiko—kati ya kushangaa, kucheka, na hata kuhisi kupoteza udhibiti wa hali ya nyumbani. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, michezo hii ni ishara ya ukuaji wa akili na ubunifu wa mtoto. Ni njia ya kujifunza uwajibikaji, uongozi, na hata mawasiliano.
Ni muhimu kwa wazazi kuchukua nafasi ya kutazama na kuelewa zaidi kuliko kukosoa mara moja. Badala ya kuona k**a “tatizo,” hali k**a hii inaweza kuwa fursa ya kumfundisha mtoto maadili, huruma, na usawa katika uhusiano.
Kwa mfano, mzazi anaweza kujiunga na mchezo kwa njia ya kujenga, na hivyo kusaidia mtoto kuelewa tofauti kati ya mchezo na uhalisia.
Kwa upande mwingine, tukio hili linaonesha pia jinsi watoto wanavyoona dunia ya watu wazima. Kauli k**a “mummy, raising children is not easy” zinadhihirisha jinsi mtoto anavyochukua na kurudia maneno ya wazazi wake. Hili linaweka wazi jukumu kubwa la wazazi kuwa mfano bora kwa watoto wao katika mazungumzo na matendo.
Kwa ujumla, malezi si tu juu ya kutoa mahitaji ya msingi k**a chakula na malazi, bali pia ni safari ya kujifunza pamoja na mtoto. Ni safari inayohitaji uvumilivu, uelewa, na wakati mwingine—uwezo wa kucheka hali zinazoonekana kuwa za kushangaza.
Katika nyumba nyingi, k**a ilivyo katika hadithi hii, mtoto anaweza kuwa chanzo cha furaha na mshangao usioisha. Na kwa wazazi, kukubali ukweli huu ni hatua muhimu ya kuelewa kwamba kila siku katika malezi huleta hadithi mpya.
Hatimaye, maisha ya uzazi yanabaki kuwa mchanganyiko wa upendo, mafunzo, na ucheshi—na wakati mwingine, watoto wetu hutufundisha zaidi kuliko tunavyowafundisha sisi.
28/03/2026
Jana tulishiriki kisa cha msichana mmoja aliyekuwa akimtafuta baba wa mtoto wake.
Alieleza kuwa alipokuwa Kidato cha Nne, mwanaume mmoja alimpeleka kwenye nyumba ya kulala wageni huko Bijilo ambako walifanya mambo mengi ikiwemo kushiriki ngono zembe.
Muda mfupi baadaye, aligundua kuwa alikuwa mjamzito.
Ndani ya chini ya saa mbili tangu tulipochapisha kisa hicho, mmoja wa wafuasi wetu alimsaidia kupata namba mpya ya simu ya mwanaume huyo.
Alipowasiliana naye, mwanaume huyo alikiri kuwa aliwahi kulala naye, lakini akasema anahitaji kipimo cha vinasaba (DNA) kuthibitisha k**a kweli yeye ndiye baba wa mtoto.
Pia aliomba msichana huyo atake kisa hicho kifutwe, lakini tulikataa. Kitendo alichomfanyia ni kosa kubwa la jinai, kwa sababu msichana huyo alikuwa bado mdogo (chini ya umri wa kisheria).
Nchini Gambia, umri wa kuruhusiwa kushiriki tendo la ndoa ni miaka 18. K**a msichana ana chini ya miaka 18, hata k**a atakubali,
hairuhusiwi;
👉Kufanya naye tendo la ndoa
👉Kumgusa kingono au kumfanya akuguse kingono
Ikiwa atajaribu kumtafuta tena basi atakuwa kwenye hatari ya kifungo.
Itaendelea...........
28/03/2026
CHANGAMOTO YA MAHUSIANO YA FACEBOOK..
Nilikutana na msichana kupitia Facebook, tukazungumza kwa siku kadhaa mpaka tukakubaliana kukutana. Kwa kuwa alikuwa anaishi mbali, nikaamua kumtumia pesa ya usafiri. Hakuomba, nilifanya tu kwa nia njema.
Dakika chache kabla hajaondoka, nikamtumia pesa. Baada ya muda mfupi akanipigia simu na kuniuliza kwa nini sikumuuliza kabla ya kutuma pesa. Nikamuuliza k**a kuna tatizo, akasema MTN imekata pesa yote.
Sikujua kwamba alikuwa anadaiwa na Kwikloan, hivyo pesa niliyomtumia ilikatwa moja kwa moja. Alikasirika sana, akaanza kulalamika na hata kunionyesha hasira.
Nikamwambia samahani, nilikuwa sijui, nilikuwa tu nataka kumsaidia. Lakini yeye akasema hata k**a ni msaada au surprise, bado nilipaswa kumuuliza kwanza.
Mwisho wa siku, hakutokea kwenye miadi. Hakuniambia mapema—niligundua baada ya kumpigia simu nikiwa tayari nimefika. Akaniambia hawezi kuja kwa sababu ya hali ya hasira niliyomsababishia.
Ukweli ni kwamba nilikuwa tayari hata kumrudishia ile pesa k**a angekuja, lakini hakufika. Kilichoniumiza zaidi ni kuona jambo dogo k**a hilo limekuwa sababu ya yeye kutoheshimu miadi.
Siku nzima na hata kesho yake hakunipigia simu. Nilitarajia angepiga na kuomba radhi, lakini hakufanya hivyo. Kwa kuwa nina heshima yangu, sikuona sababu ya kumpigia.
Baada ya siku moja, yeye ndiye alipiga. Badala ya kuomba radhi, aliniambia nimemkasirisha sana hadi akashindwa kujizuia. Bado alikuwa ananilaumu. Kisha akasema tupange tena miadi, lakini safari hii nitume pesa kupitia VODACOM.
Hapo ndipo nilipoamua kumzuia.
Kwangu mimi, haikuwa suala la pesa, bali namna alivyoshindwa kuwajibika na jinsi alivyohandle hali nzima. Hilo ndilo lililonikera zaidi.
Mitandaoni tunakutana na WATU wenye hulka na tabia mbalimbali Lakini huyu alikuwa mwendawazimu kabisa.