LUGHA YA AMANI

LUGHA YA AMANI

Share

Inahusika na kuanzisha kuendeleza na kuendesha mazungumzo ya usuluhishi wa migogoro ndani ya jamii.

27/10/2024

Amani: Usighadhibike kwani ghadhabu huondoa maarifa na kuleta maamuzi butu

08/07/2024

AMANI AMANI AMANI

AFRIKA NA DUNIA KWA UJUMLA
AFRIKA MASHARIKI!
MASHARIKI YA KATI!

AMANI AMANI AMANI

ACHA VITA
ACHA MAUWAJI




28/05/2024

Hujambo!

Taja Jina la kifaa pichani hapa chini kwa kiswahili:





πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Endelea kutazama video zetu kupitia linki yetu hapa chini:

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡






πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

https://youtube.com/c/Kiswahilinaladhayake

30/11/2023

Amani inapotoweka madhara yake ni makubwa na huchukua muda mrefu hadi kurejea kwa utulivu

Hivyo ni Bora zaidi kutatua migogoro kwa njia ya amani ( diplomatic) kuliko vita (war) πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ




23/11/2023

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Khairat Ali, Abuu Sahali Abdilah Musa, Abuzulfa Abukhaydar

03/11/2023

Kwa nini huna "amani" moyoni mwako na hutafuti ufumbuzi?...

02/11/2023

Amani ikitoweka?...

06/01/2021

Dunia
Ni
Amani
Imeumbwa na Amani
Itastawi kwa Amani
Dumisha
Amani kwa akili zako zote

28/10/2020

UMUHIMU WA KUILINDA AMANI

Dunia daima iko kwenye harakati na juhudi kubwa kujiletea maendeleo mtu mmoja mmoja familia.

Vikundi jamii kitaifa na kimataifa vyote vinazungumzia maendeleo ya kiuchumi sayansi na teknolojia.

Ukweli ni kwamba fikra na mipango ya maendeleo hayawezi kufikiwa au kupatikana isipokuwa kwanza ifikiwe na ipatikane amani na amani ya kudumu.

Wapo wachache ambao mara nyingi kwa ajili ya maslahi yao machache hujaribu kuleta taharuki katika jamii ili waweze kutimiza malengo yao binafsi.

Lengo lInaweza kuwa ni kutaka mali (tamaa) uongozi wa kisiasa (umaarufu) kwa maslahi binafsi (choyo) na sio taifa au jamii kwa upana wake.

Taifa nchi au jamii yenye amani inalazimika kuilinda amani yake kwa ustawi wa maisha yao ndani na nje ya taifa nchi au jamii hiyo.

Itakuwa ajabu sana kwa taifa nchi au jamii kukaa kimya bila kuilinda amani yao kwa kujihami na hata kumkemea adui wa amani yao.

Kuilinda amani inaweza kuwa ni kwa njia ya kuchukia matendo mwenendo na vituko vya atakayejaribu kuvuruga amani, pia kwa njia ya kusema na kukemea kabisa, lakini pia kupambana naye kwa wastani wa nguvu inayoendana naye.

Naweka hapa mfano mzuri wa ndege wanaotambua umuhimu wa amani na kuilinda kwa ajili ya usalama wao mali na vizazi vyao visishambuliwe na adui yao au kuharibiwa na kusababisha uvunjifu wa amani yao.

[email protected]

23/10/2020

DUNIA INAHITAJI AMANI

Hakika dunia inahitaji amani, Afrika Ulaya Asia marekani na kwengineko wimbo ni amani lazima tuilinde amani.

Bila shaka amani ni jambo kubwa na hii inaleta tanbihi kwetu juu ya kujua umuhimu wa kujifunza jinsi ya kuijenga kuitunza na kuidumisha amani katika mataifa yetu.

Kujifunza kujua hali halisi wakati wa amani lakini pia kujua hali wakati inapokosekana amani katika jamii zetu na hata katika ngazi ya familia mpaka taifa na kimataifa.

Ziangalie familia, jamii na hata nchi na mataifa yaliyokuwa katika amani na utulivu, lakini baadae yakajisahau na kujiingiza katika machafuko hivi sasa hali za familia jamii au nchi na mataifa hayo zikoje !?

Tujifunze pia historia ya machafuko chanzo chake mara nyingi ni nini hasa, hapo utagundua kuwa ni matumizi mabaya ya uhuru wa mitandao ya kijamii.

Lakini sababu nyingine ni pamoja na tamaa ya madaraka siasa za kichochezi pengine kwa kupitia mgongo wa dini ukabila au kisingizio cha kudai haki kwa malengo tofauti.

Tunza amani kwa faida yako jiepushe na jiweke mbali kabisa na sababu zote za uvunjifu wa amani na utulivu katika ngazi zote za kijamii kitaifa na kimataifa.

Dumisha amani kwa faida yako kizazi cha sasa na cha baadae, maendeleo yoyote bila amani hayawezi kufikiwa.

Hata mataifa yanayouza silaha yenyewe hayataki machafuko katika nchi zao ili yafaidi matunda ya kazi yao kwa amani na utulivu hawataki vita katika nchi zao.

Mo Hasanaly

[email protected]

27/08/2020

UPOLE NI AMANI

Upole huleta amani na kuidumisha katika jamii,
Upole ni adabu utu heshima busara na hekma upole huonyesha utimilifu wa akili ya mtu lakini upole ni pambo la utu wa mtu mwenye akili.

Wanakosea sana wanaodhani upole ni ujinga, ubwege, uoga na udhaifu.

Upole ni maendeleo upole ni ushujaa tena ni ukomavu wa fikra lakini upole ukitafsiriwa kwa usahihi utakuta upole ni uzalendo wa kweli.

Mo Hasanaly

[email protected]
Napokea ushauri wako.

25/02/2020

Amani ni Jambo la kuliangalia Sana Katika Maisha Yetu Hapa duniani kwa kuilinda na kuilea katika misingi na taratibu za kisheria

Kwa sababu leo hii dunia nzima vijana wanahangaika na tatizo la ajira wengi wao ni kutoka mataifa yaliyopoteza amani kwa makusudi au kwa kutokujua namna ya kulinda amani ya nchi zao

Sasa wanakumbuka kuwa amani Huleta Fursa na ubunifu sahihi katika utafutaji wa riziki amani ndilo tunda tamu zaidi kwa ustawi wa jamii na dunia kwa ujumla

(Tunza Amani tengeneza fursa na Ajira)

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address

Dar Es Salaam