IBADA YA JUMAPILI TAR 10/05/2025
KANISA LA PENTEKOSTE BETHEL (SEIC)
MBEZI BEACH,DAR ES SALAAM
SOMO:SUBIRI WAKATI WA BWANA NI SAHIHI
Pst ANNA KIULA
GALILAYA PRAYER MINISTRY INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM,TANZANI
Galilaya Prayer Ministry International
Preaching the word of God, healing the sick and deliverance of all people from spiritual bondages.
10/05/2026
HERI YA SIKU YA WAMAMA DUNIANI
Nami k**a Mama kwa kutambua nafasi ya kipekee ambayo wakina Mama tumepewa;
Nichukue nafasi hii kuwainua wamama wote mbele za MUNGU kwa kuwa sisi tumekua nguvu kazi ya ulimwengu.
Wewe mama unayesoma ujumbe huu MUNGU alikupa uzao kwa makusudi kabisa.
Umeshawahi kujiuliza kwanini umepewa uzao.....??
Ulishawahi kumuliza MUNGU kusudi la uzao aliokupa...??
Heri katika Utii na Imani: Wanawake k**a Sara, Hana, na wengineo walioonyesha imani walibarikiwa na Mungu katika vizazi vyao.
Wamam pamoja na mapito yote tujifunze kuwa na imani,
(Luka 1:42, 48): Elizabeti alimwambia Mariamu, "Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake," akimtambua k**a mama wa Bwana.
Sisi k**a wamama uzao wa matumbo yetu unatambulikaje mbele za MUNGU.
Biblia inawaona wamama k**a nguzo ya familia, wenye thamani kuliko marijani, na wanaostahili heshima kwa kazi yao ya malezi na uchaji.
Je, wewe k**a mama unaishi sawa na Biblia inavyokutambua;
Heri ya Mwanamke Mwema (Mithali 31:10-31): Mistari hii inamsifu mwanamke mwenye bidii, hekima, na uchaji Mungu, ikisema "watoto wake huinuka na kumwita heri, mumewe naye humsifu".
Wanawake ni jeshi kubwa;
Ufalme wa Mbinguni unatambua hilo
Usikate tamaaa,Ongeza bidii,hekima, na kumcha MUNGU
Nikutakie heri na MUNGU akukumbuke
Pst ANNA KIULA
GGalilaya Prayer Ministry InternationalDar es salaam,Tanzania
SEHEMU YA 2. SADAKA YA IMANI INAYONENA
IBADA YA JUMAMOSI
TAR 10/5/2026
GALILAYA PRAYER MINISTRY INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM,TANZANIA
08/05/2026
KARIBU KATIKA IBADA YA JUMAMOSI HII
TAR 10/5/2026 katika mwendelezo baada ya utangulizi wa somo letu 'SADAKA YA IMANI INAYONENA''
Kuna siri kubwa sana ndani ya SADAKA iliyoambatana na IMANI
Ungana nasi KESHO JUMAMOSI
IBADA ITAKUA LIVE KUPITIA
Youtube & Facebook
GALILAYA PRAYER MINISTRY INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM,TANZANIA
UTANGULIZI:SADAKA YA IMANI INANENA
IBADA YA JUMAMOSI
TAR 02/05/2026
Pst ANNA KIULA
GALILAYA PRAYER MINISTRY INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM,TANZANIA
IBADA YA JUMAMOSI
TAR 25-6-2026
SOMO: KUTABIRIA MIFUPA MIKAVU
Kwanini tunapaswa kutabiria mifupa mikavu;
Neno la MUNGU linaeleza juu ya mifupa mikavu,na je kwenye nyakati hizi tunapozungumza kwa habari ya mifupa mikavu tunalenga nini....??
KARIBU TUJIFUNZE HABARI HII
Na uhalisia katika nyakati hizi juu ya maisha yetu.
Pst Eliah Z Kiula
GALILAYA PRAYER MINISTRY INTERNATIONAL
25/04/2026
Join us for this SERVICE
Facebook & YouTube
GALILAYA PRAYER MINISTRY INT
Don't forget to SUBSCRIBE,LIKE & COMMENT
It's today 25 th APRIL 2026
At 03:00Pm
You are all welcome
*SOMO: JE, UMEJIANDAA KWA MUUJIZA WAKO?*
Andiko kuu: Mathayo 24:44
"Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja."
*UTANGULIZI*
Wakati Yesu akiwa na wanafunzi wake, alitumia mifano mingi ili kuleta uelewa zaidi kwa wanafunzi wake. Moja ya mifano tunayoenda kujifunza leo ni ya wanawali kumi waliogawanyika katika makundi mawili; watano wakiwa wenye busara na watano wakiwa wapumbavu. Lengo kuu la mfano huu lilikuwa ni kufundisha kuhusu kujiandaa au kuwa tayari kwa ujio wa Yesu Kristo kwa mara ya pili.
๐Mfano wa Yesu kuhusiana na wanawali
Mathayo 25:1โ13
1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.
2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.
3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;
4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.
6 Lakini usiku wa manane pakawa na kelele, โHaya, bwana arusi yuaja; tokeni mwende kumlaki.โ
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, โTupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.โ
9 Lakini wale wenye busara wakawajibu wakisema, โSivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali nendeni kwa wauzao mkajinunulie.โ
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja; nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine wakasema, โBwana, Bwana, utufungulie.โ
12 Akajibu akasema, โAmin, nawaambia, siwajui ninyi.โ
13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
*MHUTASARI KWA UJUMLA*
Kwanini kuwa wanawali wenye busara na wapumbavu?
Wanawali wanawakilisha sisi sote, ambapo ni kundi moja kwa mwonekano, lakini utofauti wake utakuja baada ya kuja kwa Yesu Kristo.
Wanawali wenye busara ni lile kundi litakalokuwa limejiandaa vyema, kwa kuwa na imani ya kutosha pamoja na Roho Mtakatifu, ili kuhakikisha wanaendelea kuvumilia mpaka kustahimili ujio wa Yesu Kristo, ambaye anatajwa k**a Bwana arusi.
Lakini wanawali wapumbavu ni wale watakaoonekana hawana imani ya kutosha wala Roho Mtakatifu wa kuwasaidia kustahimili mpaka kuja kwa Yesu Kristo.
๐ Taa ni imani ambayo haitakiwi kuzimika. K**a isemwavyo katika Biblia kuwa:
"Ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."
Hivyo kila mmoja wetu anahitaji kuwa na imani thabiti (kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo) na kuamini kwamba yapo.
๐ Lakini mafuta ni Roho Mtakatifu, ambaye hatakiwi kabisa kupungua au kukosekana, maana hutenda kazi ya kutuongoza, kututia nguvu, kututakasa na kutusaidia kudumu katika imani hadi mwisho.
*HITIMISHO*
Tunatakiwa kuwa tayari kwa ajili ya ujio wa Yesu Kristo. Maana k**a tukimkosa Roho Mtakatifu, hatutakuwa na imani imara, au imani zetu hazitafanya kazi na hazitakuwa na msaada kwetu.
Tufanye hima tusije tukakataliwa k**a wale wanawali wapumbavu, ambao hawakufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kuja kwa Bwana arusi, k**a fungu la 12 linavyosema:
"Amin, nawaambia, siwajui ninyi."
Na mtumwa wa Yesu Kristo
Pastor Eliah Z. Kiula
Galilaya Prayer Ministry International
+255 755 239 238 | Dar Es salaam | Tanzania | East Africa
SOMO: OMBEA ARDHI ILI KUKWAMUA HATIMA YAKO
Utangulizi
Kumbuka ardhi ni Kila kitu. Mtu ni ardhi na yote aliyo nayo yametokea ardhini na maisha ya mtu yeyote yanapatikana na yapo juu ya ardhi.
Hivyo kusema baraka za mtu zinatokana na ardhi ni sahihi. Pia k**a baraka zimegeuzwa kuwa laana uwe na uhakika laana ya mtu inakaa katika ardhi ili kuzuia au kuigandamiza hatima Yako njema.
KABLA ya dhambi baraka zilikuwepo katika ardhi na baada ya dhambi laana ilikaa mahali pa baraka zako.
Kibiblia neno "nchi" kwenye baadhi ya maandiko lina maana ya "ardhi" na Maeneo mengine k**a mavumbi au udongo.
Mwanzo 1:10" MUNGU akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; MUNGU akaona ya kuwa ni vyema."
โโKwa kifupi tunaweza kusema kwamba ardhi ni sehemu ya dunia tunayoikanyaga,tunayojenga juu yake, tunayoilima, tunayofanya biashara juu yake n.k
Kuna mambo mengi sana kuhusu ardhi kiroho, leo tujifunze tu kwa sehemu ili tukaombe na kupata ushindi.
Kwa sababu somo letu leo ni la maombi basi ngoja nianze hivi;
Kwanini ufanye maombi juu ya ardhi?
1. Ni kwa sababu ardhi inaweza kutunza kumbukumbu za kifungo cha kiroho kwa mtu husika.
*Yeremia 22:29-30 "* Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la BWANA. BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda."
โโArdhi inaambiwa kwamba iandike juu ya mtu Fulani kwamba hatafanikiwa, ardhi kumbe inaweza kuandika taarifa za Mtu fulani.
โโKwa hiyo ardhi inaweza ikasemeshwa na kutunza kifungo k**a Yule aliyeisemesha hiyo ardhi alivyotamka.
Katika somo la leo, ninapozungumzia ardhi iliyobeba vifungo sina maana ya kwamba kila ardhi popote imebeba kifungo kwa ajili yako, nazungumzia ardhi inayokuhusu k**a imebeba kifungo kwa ajili yako.
Kuna ardhi moja pia inaweza kubeba kifungo kwa ajili ya mtu mmoja anayeishi hapo lakini kifungo hicho kisimpate mtu mwingine anayeishi katika ardhi hiyo hiyo maana yeye hayuko kwenye maelekezo ya mtoa kifungo hicho.
Je k**a ardhi ya kwenu ilisemeshwa na mchawi juu ya kifungo itakuwaje?, usipoomba unaweza kuzaliwa kifungoni, ukaishi kifungoni, ukakulia kifungoni na kuzeekea kifungoni, ndio maana leo tunaomba juu ya ardhi.
2. Ardhi inaweza kupokea laana kwa ajili ya mtu atakayeitumia.
Yoshua 6:26 "Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za BWANA mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo."
Vipi k**a ni wewe ndio unaishi katika ardhi ya namna hiyo?
Yaani ukiishi katika ardhi hiyo ujue mtoto wako wa kwanza lazima afe mapema kisha mtoto wa mwisho akiwa ni mwanaume naye afe mapema, lakini hapo hatuoni mtu akitamkiwa mabaya hayo ila imetamkiwa ardhi ya eneo fulani, lakini madhara yakawapata watu.
Ardhi ya Yeriko ilitamkiwa na Mtumishi wa MUNGU na ikawa vile vile kwa sababu ya makosa ya watu.
Vipi kwa habari za wakuu wa giza, unadhani hawajui kwamba ardhi ikisemeshwa inasikia na kutunza kumbukumbu au kusimamia kifungo?
Ukweli wanajua na wameshawafunga watu wengi, leo tunapoomba kuhusu ardhi ujue unaenda kujitoa katika mitego ya siri sana ya mawakala wa shetani, unaenda kujitoa katika kifungo cha siri sana cha wakuu wa giza.
โโNdugu, ardhi ya sehemu fulani inaweza kuwa chanzo cha tatizo lako ndio maana kila muda unaota ndoto za ardhi hiyo na kumbe unajulishwa ni wapi umeshikiliwa kipepo, ni wapi uchumi wako umeshikiliwa, ni wapi uzao wako umeshikiliwa, ni wapi afya yako imeshikiliwa, ni wapi kibali chako kimeshikiliwa n.k
Mimi Mtumishi wako na mtumishi wa Mungu Eliah Z Kiula mwenyewe niliwahi kuona ndotoni zamani kule nilikowahi kuishi nikapata Ufunuo namna ya kushughulikia kiroho juu ya ardhi hiyo na kilichokuwa kimesemeshwa juu yangu kwenye ardhi hiyo, namshukuru MUNGU wa Mbinguni maana kwa Nguvu zake nilishinda.
3. Ardhi inaweza kubeba ukiwa hivyo mtu anayekaa katika ardhi ya eneo hilo anakuwa mtu wa ukiwa.
Isaya 62:4 "Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa BWANA anakufurahia ,na nchi yako itaolewa."
Ukiwa maana yake kukaukiwa,kuishiwa.
Ukiwa ni upekwe unaotokana na kuondokewa.
โโUkiishi kwenye ardhi yenye ukiwa unaweza kuwa mtu wa kuondokewa na watu muhimu kwako, kuondokewa na baraka zako n.k
Yako mambo mengi sana kuhusu ardhi, siku moja nitafafanua katika somo kamili na katika kitabu.
Nini ufanye katika maombi kuhusu ardhi?
1. Tubu kwa ajili ya ardhi unayokaa ili hiyo ardhi ipone, ikipona hiyo ardhi ni uponyaji na baraka na kwako pia.
2 Nyakati 7:14 "ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao."
MUNGU anaahidi kusamehe na kuiponya ardhi.
2. Haribu kwa njia ya maombi madhabahu za giza, futa kafara za kipepo na futa maagano ya kipepo kwa sababu hayo mambo matatu yote hufanyika katika ardhi.
Kumbu 12:2-3 "Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo."
3. Futa vifungo vya giza vikivyokupata kutokana na kifungo kilichofanyika ardhini.
Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."
4. Haribu kumbukumbu zote mbaya kukuhusu wewe au unaowaambea zilizotunzwa ardhini na wapige kimaombi watunza kumbukumbu wa kipepo kukuhusu wewe.
๏ปฟMathayo 7:8 "kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
5. Kwa sababu ardhi ikisemeshwa inazingatia ilichoambiwa(Yeremia 22:29-30) wewe kwenye maombi leo fanya haya.
A. Futa kwa damu ya YESU KRISTO kila kitu ulichofungwa ardhini.
B. Isemeshe wewe ardhi ili iwakatae wachawi, waganga wa kienyeji na iwakate kila wanadamu walio mawakala wa shetani.
C. Iambie ardhi itoe baraka zako ili uzipate.
Kumbu 28:4 "Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako."
Katika maombi ya ardhi unaweza hata ukauchukua udongo wa ardhi husika na kuutakasa kwa damu ya YESU KRISTO na kuuombea kisha unauunganisha na ardhi husika.
Inawezekana ulinunua kiwanja lakini jirani yako na hicho kiwanja chako alisema "atakayejenga hapa nyumba yake haitakamilika kamwe"
Inawezekana mlizaliwa katika ardhi iliyokuwa na Madhabahu za giza zilizofunga eneo hiyo na watakaozaliwa hapo.
Angalizo na hitimisho
Kufanya KAZI ili upate chakula na nahitaji Yako mengine ni wajibu na KAZI Yako muhimu sana Kwa maisha yako.
Kuamua juu ya jambo Fulani kazi. Kuamua kufuatilia na kujifunza juu ya ARDHI na maisha Yako ni KAZI na wajibu wako.
Mimi niliye mtumwa wa Yesu Kristo kwako nimetimiza wajibu wangu Kwa sehemu Moja na sehemu ya pili nimeiacha kwako msomaji wangu.
Ona jinsi ulivyo na wajibu na KAZI kubwa ya kukomboa ARDHI katika kukomboa na kuiponya hatima Yako njema.
1. Ni KAZI Yako na wajibu wako kusoma ili kuelewa uhusiano uliopo kati ya ARDHI na hatima Yako Kisha uombe
2. Lakini pia Mungu amekutumia Msaada wake katika jambo kwamba amewaweka tayari watumishi wake kusimama nawe pale unaposhindwa Kisha kuhitaji Msaada zaidi. Nakukaribisha Kwa utumishi na Msaada zaidi toka Kwa Mungu
Mtumwa wa Yesu Kristo
Pastor Eliah Z Kiula
Galilaya Prayer Ministry International
+255 755 239 238 | Dar Es salaam | Tanzania | East Africa.
๐๐จ๐๐๐จ๐ก๐๐๐ก๐๐ฆ๐๐ ๐ก๐ ๐ ๐๐๐๐๐ก๐ข
๐๐๐๐๐ ๐ฌ๐ ๐๐จ๐ ๐๐ ๐ข๐ฆ๐ ๐ง๐๐ฅ ๐ญ๐ด-๐ฐ-๐ฎ๐ฌ๐ฎ๐ฒ
๐๐๐๐๐๐๐ฌ๐ ๐ฃ๐ฅ๐๐ฌ๐๐ฅ ๐ ๐๐ก๐๐ฆ๐ง๐ฅ๐ฌ ๐๐ก๐ง๐๐ฅ๐ก๐๐ง๐๐ข๐ก๐๐
Agano ni tendo la hiari na sio lazima;
Uko huru kuchagua ni upande gani unataka kufanya agano nako kwa ajili ya kile unachokitamani.
Maagano mengi watu huingia bila kujua wameingia kwenye agano;
Kutokuwa na agano sahihi kwa MUNGU kunakufanya kuwa na milango ya wazi kwa ajili ya maagano mengine ya uharibifu.
Mfano mdogo huu utakusaidia;
Fikiria ikiwa utaingia agano la kusimama mbele za MUNGU kila siku kwa ajili ya ''KUMTUMIKIA MUNGU'' kwenye eneo ambalo MUNGU amekupa kipawa au karama.
Kwa jinsi hiyo utaepukana na mambo mengine mengi ambayo pengine yangeweza kukuingia kwenye maagano yasiyo sahihi.
Pst Anna Z.Kiula
GALILAYA PRAYER MINISTRY INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM,TANZANIA
๐๐จ๐๐๐จ๐ก๐๐๐ก๐๐ฆ๐๐ ๐ก๐ ๐ ๐๐๐๐๐ก๐ข
๐๐๐๐๐ ๐ฌ๐ ๐๐จ๐ ๐๐ ๐ข๐ฆ๐ ๐ง๐๐ฅ ๐ญ๐ด-๐ฐ-๐ฎ๐ฌ๐ฎ๐ฒ
๐๐๐๐๐๐๐ฌ๐ ๐ฃ๐ฅ๐๐ฌ๐๐ฅ ๐ ๐๐ก๐๐ฆ๐ง๐ฅ๐ฌ ๐๐ก๐ง๐๐ฅ๐ก๐๐ง๐๐ข๐ก๐๐
Agano ni tendo la hiari na sio lazima;
Uko huru kuchagua ni upande gani unataka kufanya agano nako kwa ajili ya kile unachokitamani.
Maagano mengi watu huingia bila kujua wameingia kwenye agano;
Kutokuwa na agano sahihi kwa MUNGU kunakufanya kuwa na milango ya wazi kwa ajili ya maagano mengine ya uharibifu.
Mfano mdogo huu utakusaidia;
Fikiria ikiwa utaingia agano la kusimama mbele za MUNGU kila siku kwa ajili ya ''KUMTUMIKIA MUNGU'' kwenye eneo ambalo MUNGU amekupa kipawa au karama.
Kwa jinsi hiyo utaepukana na mambo mengine mengi ambayo pengine yangeweza kukuingia kwenye maagano yasiyo sahihi.
Pst Anna Z.Kiula
GALILAYA PRAYER MINISTRY INTERNATIONAL
DAR ES SALAAM,TANZANIA
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Contact the business
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam
