25/06/2024
Kuna mahali umefika huoni kuendelea maana njia huoni.
Kumbuka: Bwana Yesu ndiye Njia Yoh.14:6.
Hivyo kwa lolote unalopitia mwombe Mungu Aliye hai katika Jina la Yesu Kristo huku ukimwamini amini amini nakuambia Atakuvusha salama kabisa katika hilo unalopitia.
Maana Alisema kuwa
"Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.”
— Isaya 43:2
(naongea na wale waliompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao)
17/06/2024
Swali: Je, unatamani kuwa na vya juu kiroho?
Jibu:
JITAHIDI kuwa mtu wa
1. Kupenda kujifunza Neno la Mungu na
2. Kuomba mara kwa mara
3. Kuishi Neno la Mungu
Hakika viwango vyako vya kiroho vitaongezeka.
14/06/2024
Usimzuilie Mungu Aliye hai kitu chochote ulichonacho, kwa kuwa chochote ulichonacho ni Chake Bwana Mungu hata wewe mwenyewe niwa Mungu. Yoh. 1:1-3.
KATIKA KILA ENEO MTII NA KUMHESHIMU MUNGU MWENYE UWEZA WOTE ALIYE JUU YA VYOTE.
13/06/2024
Mungu ni mfinyanzi, Anafinyanga vile Apendavyo Yeye. Utukufu kwa Mungu Aliye hai.
13/06/2024
Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka na maisha yako yatabadilika.
13/06/2024
Jesus Christ Messiah is coming be ready