26/11/2024
Ni Rahisi Sana!! Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Jitokeze Kupiga kura
🗓️ Jumatano, Novemba 27, 2024
🕗 Saa 2 Asubuhi mpaka Saa 10 jioni.
"Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”
31/10/2024
Mechi ya watani wa jadi kutoka Soko la Kimataifa la Samaki ( Feri ) imelizika kwa Umoja Fc kuifunga timu ya Kijiwe Sugu Fc bao Moja kwa bila na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya mchezo wa beach soka katika Mashindano ya kombe la Mama Samia Ferry Fish Market.
Mashindano haya yaliyoandaliwa na Uongozi wa Soko Chini ya Meneja wa soko Ndg. Suleman Mfinanga na Mwenyekiti wa wadau Ndg. Mbaraka Kilima.
Akizungumza kocha wa timu ya Umoja Bw. Ronaldo mara baada ya kumalizika mechi amesema , "ushindi huu tuliutegemea kwasababu tulijiandaa vya kutosha kwenye uwanja wa mazoezi na wachezaji wangu wamefanya vizuri licha kupata kadi nyekundu moja ."
Naye Kapteni wa timu ya Umoja Fc Mohamed Hafidh amesema , "tumepata ushindi kwasababu tumefuata maelekezo ya kocha wetu japo kuwa watani wetu walikuwa wagumu lakini tunashukuru tumefanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua inayofuata . "
Mdau wa michezo kutoka Feri Bw. Athumani sanga amesema kuwa wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika mashindano haya kwasababu licha ya zawadi mbali mbali zinazoshindaniwa lakini pia michezo inaleta watu pamoja na kudumisha tamaduni ya kufanya mazoezi.
Mashindano haya bado yapo katika hatua ya makundi huku baadhi ya timu zikiwa zimefuzu hatua ya robo fainali.
05/09/2024
**NEW RELEASE**
Usiache kuitazama ngoma kali ya
Frida Amani - DUDE (visualizer)
Produced by Slimsal
mixed & mastered BY
WANENE studios
Kindly help to share and don't forget to comment
Frida Amani - Dude (Visualizer)
Frida Amani drops a powerful new anthem, channeling the legendary spirit of Tanzania’s Bikidude. This track is all about girl-boss energy and celebrates the ...
06/10/2023
Unlock the potential of tourism investments at 's Investment Forum. Dive deep into details that matter!
Tap into Opportunities
05/10/2023
Mhe. Dorothy George Kilave Mbunge wa Jimbo la Temeke amekabidhi Viti na Meza zaidi ya 130 Kwa Walimu wa Shule ya Msingi Taifa, Likwati na Barracks.
Hafla ya Makabidhiano imehudhuriwa na Viongozi wa CCM ngazi ya Kata ya Miburani, Mhe Mkenga Diwani wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa ya Miburani, Mratibu Elimu Kata na Mratibu Wa Jimbo la Temeke kutoka Ofisi ya Mchumi Manispaa ya Temeke.
Katika Hafla hii ya Mabidhiano, Mhe Dorothy Kilave Mbunge Temeke Ameishukuru Sana Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan* Kwa kujibu Kero za Wananchi Kwa kuidhinisha Fedha za Maendeleo Jimboni, Hususani Fedha za Mfuko wa Jimbo ambazo ndizo zimetumika kununua Samani za Walimu ili kutatua Kero ya upungufu wa Meza na Viti katika Ofisi za Walimu Kata ya Miburani.
Utekelezaji wa ILANI ya CCM Jimbo la Temeke...
04/10/2023
OPERESHENI TATUA KERO UKEREWE
📍UWANJA WA GETRUDE MONGELA
💡04/10/2023
Mkuu wa wilaya ya ukerewe Mhe. HASSAN BOMBOKO Ameongoza Operesheni Tatua Kero Ukerewe Kwa Kutatua Changamoto, Migogoro na Kero Mbalimbali za Wananchi Wilayani Ukerewe.
Aidha Mkuu wa Wilaya Amewaonya Watendaji Wote Wa Kata na Vijiji Kutokuwa Chanzo cha Migogoro na kero Mbalimbali za Wananchi, na wawe Sehemu Katika kutatua Changamoto na migororo yao.
SAMIA NA UKEREWE SULUHU NA MAENDELEO -SUK25
IENDELEE
14/09/2023
✍️Nukuu
Jukwaa la mjadala la wataalamu wa teknolojia ya kidijiti (ITU-T SG20) wanaokutana Arusha, Tanzania kujadili maendeleo ya miji maridadi / miji ya kidijiti (citiverse) Arusha, Tanzania.
08/08/2023
Nanenane📌
♦️DKT. SAMIA AFUNGA SHEREHE ZA MAONESHO YA WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI (NANENANE)♦️
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 08 Agosti, 2023 amefunga rasmi maonesho ya wakulima (nanenane) yaliyofanyika Kitaifa jijini Mbeya.
Maadhimisho hayo ya siku nane yaliyofanyika katika viwanja vya
John Mwakangale, jijini Mbeya yamefikia kilele chake leo huku yakiwa na kauli mbiu isemayo "vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula".
Wakati akifunga maashimisho hayo, Mheshimiwa Dkt Samia alihitimisha kwa kutoa wito kwa wakulima wa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha kwa mwaka mzima ili kuendana na hali ya hewa ya Tanzania.
Shirika la Posta Tanzania ambalo ni mdau mkubwa wa usafirishaji nchini, limepata nafasi ya kushiriki maadhimisho hayo kwa kufanya maonesho ya siku nane ya kutoa huduma na elimu ya huduma kwa wananchi namna shirika hilo linavyoenda sambamba na kusafirisha mizigo ya wakulima na wadau wengine.
Aidha Shirika la Posta Tanzania linajivunia huduma yake ya Post Cargo ambayo ni miongoni mwa huduma zinazolenga kundi la wakulima, wafugaji na wavuvi kwa namna ya kisafirisha mazao yao na kufikia Masoko mbali mbali ya ndani na nje ya nchi.
Shirika limewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Bw. Amos Millinga kwa niaba ya Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania aliyeambatana na Meneja wa Posta Mkoa wa Mbeya Bw. Michael Mwanachuo, pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoani humo.