Taficotz

Taficotz

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Taficotz, Government Organization, P. O. Box 2336, Dar es Salaam.

Ukurasa Rasmi wa Shirika la Uvuvi Tanzania
Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ni Shirika lenye dhamana ya kukuza sekta ya uvuvi nchini kupitia Uvuvi wa Bahari Kuu

14/05/2026

SERIKALI KUNUNUA MELI MBILI ZA UVUVI WA BAHARI KUU 2026/2027
katika Mwaka 2026/2027, miradi na kazi zitakazotekelezwa kwa kuzingatia vipaumbele vya Wizara ni pamoja na Kukamilisha ununuzi wa meli mbili (2) za Uvuvi wa Bahari

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, wakati
akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, Bungeni jijini Dodoma leo mei 14, 2026.

14/05/2026

BIASHARA YA MAZAO YA UVUVI SOKO LA NDANI YAPAA

Katika Mwaka 2025/2026, biashara ya mazao ya uvuvi katika soko la ndani imeendelea kuimarika ambapo hadi mwezi Aprili, 2026 jumla ya tani 439,673.63 zenye thamani ya shilingi bilioni 4.20 ziliuzwa katika soko la ndani ikilinganishwa na tani 422,639.10 zenye thamani ya shilingi bilioni 2.83 zilizouzwa mwaka 2024/2025. Kuimarika kwa biashara ya samaki katika soko la ndani kumetokana na kuimarika kwa miundombinu ya ubaridi ya kuhifadhi mazao ya uvuvi na miundombinu ya usafirishaji wa mazao ya uvuvi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, wakati
akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, Bungeni jijini Dodoma leo mei 14, 2026.

14/05/2026

SERIKALI KUANZA UJENZI WA BANDARI YA UVUVI YA BAGAMOYO

katika Mwaka 2026/2027, miradi na kazi zitakazotekelezwa kwa kuzingatia vipaumbele vya Wizara ni pamoja na kukamilisha usanifu wa kina na kuanza Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Bagamoyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, wakati
akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, Bungeni jijini Dodoma leo mei 14, 2026.

13/05/2026

Usikose kufuatilia Fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi.


🐟
/2027

11/05/2026
09/05/2026

Usikose kufuatilia Uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Bajeti hiyo itawasilishwa na Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi, tarehe 14 Mei 2026, Bungeni jijini Dodoma.

01/05/2026



Photos from Taficotz's post 01/05/2026

Watumishi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) wameungana na wafanyakazi wote duniani kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani, katika maadhimisho yaliyofanyika leo 01 Mei 2026 kimkoa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo kwa mwaka 2026 yamebeba kaulimbiu isemayo: “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”

26/04/2026

Photos from Taficotz's post 25/04/2026

HISTORIA YAANDIKWA RAIS SAMIA AKIZINDUA MELI YA UVUVI WA BAHARI KUU YA TAFICO

◼️Ni ya kwanza tangu nchi ilipopata uhuru mwaka 1961
◼️Ina uwezo wa kubeba hadi tani 48 kwa wakati mmoja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua meli ya kwanza ya Uvuvi wa bahari kuu ambayo itaiwezesha nchi kuvua samaki waliopo kwenye ukanda wa maalum wa uchumi wa bahari (EEZ) ambao awali haukuweza kufikiwa kutokana na kukosekana kwa meli ya aina hiyo.

Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika Aprili 25,2026 kwenye ufukwe wa Makao makuu ya Shirika la Uvuvi nchini (TAFICO) Kigamboni mkoani Dar-es-salaam ambapo Mhe. Rais Samia amesema kuwa hatua hiyo inalenga kukuza fursa za ajira, kuongeza mapato ya Serikali na kuboresha lishe.

“Niipongeze Serikali ya Japan kwa kushirikiana nasi katika kutengeneza meli hii na kupitia wao kwa kushirikiana na UNDP tutapata boti mbili za kasi ambazo zitasimamia doria ya uvuvi wa bahari kuu” Ameongeza Mhe. Rais Samia.

Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuboresha sekta ya Uvuvi kupitia ujenzi wa bandari za uvuvi ikiwemo ya kilwa ambayo imefikia asilimia 97 na Bagamayo ambazo zote kwa pamoja zinalenga kuimarisha uchumi, ajira na usalama wa chakula.

“Sambamba na hilo tutaimarisha mafunzo na tafiti za kitaalam ili kuhakikisha rasilimali za bahari zinasimamiwa kwa ufanisi na misingi endelevu kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo” Amesema Mhe. Rais Samia

Aidha Mhe. Rais Samia ametoa maelekezo mbalimbali kwa Wizara ikiwa ni pamoja na kutunza Meli hiyo, kutatua changamoto za wavuvi wadogo zinazohusu mitaji na mazingira ya kufanya shughuli zao, kutoa elimu ya usimamizi wa fedha kwa wavuvi ili fedha wanazopata ziwanufaishe na kutumia sheria na taratibu kwenye usimamizi wa uvuvi endelevu na badala ya nguvu na mabavu.

Akizungumza awali, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amemshukuru Rais Samia kwa jitihada za kuendeleza sekta ya Uvuvi nchini ambapo ameeleza kuwa Meli hiyo ni sehemu ya Meli nyingine 4 zinazotarajiwa kununuliwa na Serikali ili ziimarishe uvuvi wa bahari kuu.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

P. O. Box 2336
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 09:30 - 15:30
Friday 09:30 - 15:30