UVCCM BUZA

UVCCM  BUZA

Share

UMOJA WETU NDIO MSINGI WA UKOMBOZI WETU KISIASA,KIUCHUMI NA KIJAMII. �

27/02/2025

*BALOZI NCHIMBI AWASILI NAMIBIA MSIBA WA SAM NUJOMA*

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), *Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,* amewasili nchini Namibia, akiongoza ujumbe wa CCM kwenye mazishi ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa hilo, *Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma,* yatakayofanyika tarehe 1 Machi, 2025.

Balozi Dkt. Nchimbi pamoja na msafara wake aliongozana nao, ambao pia yumo Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, aliwasili Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Hosea Kutako, jijini Windhoek, na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Mhe. Caesar Waitara, tarehe 26 Februari 2025.

Balozi Nchimbi atashiriki ratiba mbalimbali za utoaji wa heshima za mwisho na kumuaga Dkt. Sam Nujoma, kuanzia tarehe 27 Februari 2025, ambapo Chama Tawala cha Namibia, SWAPO, ambacho ni rafiki wa kihistoria wa CCM, kimeandaa shughuli kwa ajili ya heshima ya mwasisi wake huyo.

Baada ya hapo, Balozi Nchimbi atashiriki ibada ya kitaifa ya kumuaga Hayati Dkt. Nujoma iliyopangwa kufanyika tarehe 28 Februari 2025, kabla ya shughuli ya mazishi ya kitaifa itakayofanyika tarehe 1 Machi 2025, katika eneo la makaburi ya mashujaa, yaliyoko makao makuu ya nchi hiyo, jijini Windhoek.

Uhusiano kati ya Namibia na Tanzania, halikadhalika CCM na SWAPO na watu wa nchi hizo mbili, ni wa kihistoria, ukiwa umejengwa katika misingi imara tangu wakati wa harakati za kupigania uhuru dhidi ya wakoloni na makaburu.

Itakumbukwa kuwa Hayati Dkt. Nujoma na viongozi na wanachama wengi wa SWAPO na Namibia waliishi maeneo mbalimbali uhamishoni nchini Tanzania, tangu miaka ya 1960, wakishiriki mapambano ya kupigania uhuru wa nchi yao, ambako pia ndipo walipoanzisha Chama cha SWAPO ili kuendesha shughuli za kuikomboa nchi yao kisiasa, hadi walipopata uhuru mwaka 1990.

29/03/2022

Jipime, Ukiona unatosha Nenda ukachukue Fomu.

Photos from UVCCM  BUZA's post 08/02/2022

Ahsant Mh Dorothy kilave mbunge jimbo la temeke kwa kuupiga mwingi

08/02/2022
Photos from UVCCM  BUZA's post 08/02/2022

Ccm imara inaanza na Mimi shiriki uchaguzi kwa uwadirifu.

04/02/2022

Shamra shamra za sherehe za kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi

05/01/2022

Tunaungana na Mh Rais Samia Suluhu Hassain # alipo mama vijana Tupo

15/06/2021

Ziara ya kamati ya siasa wilaya ya Temeke pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakiambatana na Diwani wa kata ya Buza wakikagua maendeleo ya kituo cha Afya kilichopo Buza.

08/02/2021

Vijana Taifa la leo na kesho

08/02/2021
Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Dar Es Salaam