Bodi ya Chai Tanzania

Bodi ya Chai Tanzania

Share

Ukurasa wa Bodi ya Chai Tanzania

Photos from Bodi ya Chai Tanzania's post 28/04/2026

Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2026/2027 tarehe 28 April 2026, Bungeni jijini Dodoma.

Mhe. Chongolo amesema Sekta ya kilimo imeendelea kuwa muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula, upatikanaji wa ajira, malighafi za viwandani na kuchangia katika Pato la Taifa (GDP). “Katika mwaka 2025, Sekta ya Kilimo imekua kwa asilimia 4.0. Aidha, imechangia asilimia 24.6 katika Pato la Taifa.”

Vilevile, ameeleza kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa 2024/2025 ulifikia tani milioni 23.78 ikilinganishwa na tani milioni 22.8 katika msimu wa kilimo wa 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 4.3 na kufanya utoshelevu wa chakula nchini kufikia asilimia 130.

Pia ameeleza kuwa Wizara inaendelea kukamilisha taratibu za kuanzisha Wakala ya Taifa wa Huduma za Ugani Kilimo (NAESA), ambao inatarajiwa kuanza rasmi mwaka mpya ujao wa fedha (Julai 2026). Wakala huo utawezesha kuongeza ufanisi wa huduma za ugani, kuratibu na kusimamia shughuli za ugani na kuhaulisha teknolojia kutoka kwa watafiti na wadau wengine kwenda kwa maafisa ugani na wakulima.

28/04/2026

28/04/2026
Photos from Bodi ya Chai Tanzania's post 23/04/2026

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli akiongea mbele ya mamia ya washiriki wakati wa uzinduzi wa usajili wa Jukwaa la Hotikacha la Kimataifa (HortiLogistica Africa 2026) tarehe 22 April 2026.

Uzinduzi wa usajili ulizinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Jukwaa husika linatarajiwa kufanyika tarehe 8 hadi 10 Novemba 2026, jijini Arusha.

HortiLogistica Africa 2026 itahusisha wazalishaji hapa nchini na kufungua fursa za kibiashara, uwekezaji na masoko kwa wakulima.

Photos from Bodi ya Chai Tanzania's post 23/04/2026

Akitoa hotuba yake katika uzinduzi wa HortiLogistica Africa 2026, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) amepongeza Wizara ya Kilimo pamoja na TAHA kwa ubunifu wa jukwaa hili la kimkakati, akisisitiza kuwa linaendana kikamilifu na dira ya Serikali katika kukuza uchumi kupitia sekta ya kilimo.

Ametambua mchango wa wataalam wa sekta hiyo, akimpongeza Dkt. Jacqueline Mkindi k**a hazina ya maarifa katika hotikacha, huku akibainisha kuwa jukwaa la Hortilogistica Africa lina uwezo wa kuleta mageuzi si tu Tanzania bali pia katika ukanda wa Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa ujumla.

Ameeleza kuwa Hortilogistica Africa ni daraja muhimu linalowaunganisha wakulima na wanunuzi wa ndani na kimataifa, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuliimarisha ili kuongeza tija na fursa za masoko. Aidha, amesisitiza mchango wa sekta ya hotikacha kwa zaidi ya Watanzania milioni 10, akieleza kuwa ni mhimili wa usalama wa chakula, afya na ustawi wa jamii.

Katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji, Waziri Mkuu amebainisha kuwa Tanzania ina mazingira salama na rafiki kwa biashara, akihimiza sekta binafsi kuchangamkia fursa zilizopo. Amesema Ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kuunga mkono kikamilifu juhudi za kufanikisha jukwaa hili.

Photos from Bodi ya Chai Tanzania's post 20/04/2026

Bodi ya Chai Tanzania, imeshiriki katika maonesho ya kimataifa ya chai, kahawa na kakao yanayofanyika jijini Moscow, Urusi, kufuatia mwaliko maalum ulioratibiwa na na ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi. Maonesho hayo yalianza terehe 15 hadi 18 Aprili 2026.

Bodi ya chai ilipata fursa ya kutembelea ofisi za ubalozi na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Fredrick Kibuta, alieleza kuwa ubalozi umeendelea kuwa kiungo muhimu katika kukuza diplomasia ya uchumi kwa kuwaunganisha wafanyabiashara wa Urusi na wafanyabiashara kutoka Tanzania, katika sekta za chai na kahawa. Lengo kuu ni kujifunza soko la Urusi lilivyo, kufungua na kupanua fursa za biashara na masoko ya mazao hayo nchini Urusi pamoja na kujenga mahusiano kwa kuwashawishi wafanya biashara wa Tanzania kutumia majukwaa haya kuonesha bidhaa wanzazozalisha na kuwa na mahusino endelevu ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili.

Aidha, Mheshimiwa Balozi ameeleza kuwa kuna mipango inayoendelea ya kuanzishwa kwa Baraza la Wafanyabiashara wa Tanzania na Urusi, ambalo litasaidia kurahisisha utambuzi, ushirikiano na uwekezaji kati ya wadau kutoka nchi zote mbili na kuwa na data base ya wafanya biashara na mazao yaayozalishwa Tanzania kwa ajil ya kurahusixha upatikanai wa taarifa.

Katika hatua nyingine muhimu, Balozi alieleza kuwa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara kutoka Urusi na Tanzania unatarajiwa kufanyika mwezi Mei nchini Tanzania. Mkutano huo unalenga kuwakutanisha wadau mbalimbali, kwa ajii ya kubadilishana uzoefu na kujadili fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo chai na kahawa, usafirishaji wa bidhaa, njia zinazotumika za malipo.

05/04/2026

Pasaka Njema

Photos from Bodi ya Chai Tanzania's post 27/03/2026

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Bi. Beatrice Banzi, amekutana na muhamasishaji wa Kampuni ya HongDingXin inayojishughulisha na uzalishaji wa chai maalum ya orthodox katika Wilaya ya Kilolo, kwa lengo la kujadili maendeleo ya uzalishaji wa chai na mikakati ya kupanua masoko ya kimataifa.

Katika kikao hicho, pande zote mbili zilijadiliana kuhusu namna bora ya kuimarisha na kuongeza wigo wa masoko ya chai hiyo hususan katika nchi ya China ambako tayari kampuni hiyo imeanza kuuza bidhaa zake.

Aidha, juhudi zinaendelea kufanyika ili kufungua masoko mapya katika nchi za Urusi, Uholanzi na Qatar, hatua inayotarajiwa kuongeza thamani ya chai ya Tanzania katika soko la dunia.

Vilevile, mazungumzo hayo yaligusia mpango wa kuanzisha tea bar kubwa itakayotoa fursa kwa watumiaji kufurahia aina mbalimbali za chai hatua itakayochochea matumizi ya chai ndani ya nchi na kuongeza uelewa kuhusu ubora wake.

Kwa upande mwingine, Kampuni ya HongDingXin imeonesha dhamira ya kununua chai nyeusi aina ya CTC (loose tea na blended) kwa ajili ya kuipeleka katika soko la China, jambo litakalowanufaisha wakulima na wadau wa zao la chai nchini kwa kuongeza fursa za soko na kipato.

Hatua hizi zinaakisi jitihada za dhati zinazofanywa na sekta binafsi kwa kushirikiana na Bodi ya Chai katika kuitangaza na kuendeleza chai ya Tanzania, hususan ile inayozalishwa Kilolo, pamoja na kuongeza ushindani wake katika masoko ya kimataifa.

21/03/2026

Eid ni furaha, na furaha ina ladha ya chai ☕✨

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

P. O. Box 2663, Tetex Building Pamba Road
Dar Es Salaam
00000