Baraza la Michezo la Taifa

Baraza la Michezo la Taifa

Share

Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
"Michezo ni Afya, Michezo ni Ajira"

Photos from Baraza la Michezo la Taifa's post 13/05/2026

VIONGOZI WA WIZARA, TAMISEMI NA BMT WAKUTANA NA KATIBU TAWALA MKOA WA MANYARA

Viongozi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), leo Mei 13, 2026 wamekutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Mhaji kwa lengo la kujitambulisha rasmi ofisini hapo.

Katika kikao hicho, Bi. Mhaji ameushukuru uongozi wa wizara pamoja na BMT kwa kuupa Mkoa wa Manyara kipaumbele katika maendeleo ya michezo, hususan kupitia mafunzo ya walimu wa michezo yanayoendelea mkoani humo.

Amesema mafunzo hayo yanayowakutanisha walimu wa michezo kutoka mikoa ya Manyara na Arusha yataongeza ujuzi na uwezo wa walimu katika kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi mashuleni.

Aidha, ameeleza kuwa Mkoa wa Manyara utaendelea kushirikiana na wadau wa michezo kuhakikisha michezo inakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla.

13/05/2026

KAIMU MKURUGENZI WA MICHEZO, UTAMADUNI NA SANAA TAMISEMI AIPONGEZA BMT KWA MAFUNZO YA WALIMU WA MICHEZO MANYARA

Kamimu Mkurugenzi wa Michezo, Utamaduni na Sanaa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ameipongeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kuratibu mafunzo ya walimu wa michezo yanayoendelea mkoani Manyara, akieleza kuwa mafunzo hayo yataongeza uwezo wa walimu katika kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa wanafunzi.

Amesema mafunzo hayo ni hatua muhimu katika kuimarisha maendeleo ya michezo shuleni pamoja na kusaidia kukuza ushindani wa michezo katika mikoa ya Arusha na Manyara.

Aidha, amebainisha kuwa walimu watakaopata mafunzo hayo watakuwa chachu ya kuendeleza gurudumu la michezo mashuleni kwa kutumia maarifa na mbinu mpya za kufundisha michezo kwa wanafunzi.

Mafunzo hayo yanaendelea kwa siku kadhaa yakihusisha walimu wa michezo kutoka maeneo mbalimbali, huku yakilenga kuongeza ufanisi wa ufundishaji wa michezo na kukuza vipaji vya wanafunzi nchini.

12/05/2026

MAFUNZO YA WALIMU WA MICHEZO KUTOKA MIKOA YA ARUSHA NA MANYARA

12/05/2026

MAFUNZO YA WALIMU WA MICHEZO KWA WATU WENYE ULEMAVU ( IRINGA)

12/05/2026

HONGERA TANZANITE QUEENS

Photos from Baraza la Michezo la Taifa's post 12/05/2026

MAKONDA ASAINI HATI YA MAKUBALIANO UENDESHAJI AFCON 2027 – MOTSEPE ASHUHUDIA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (Mb), leo amesaini hati ya makubaliano ya uendeshaji wa mashindano ya AFCON 2027, inayojulikana k**a CAF Joint Resolution Total Energies.

Tukio hilo la kihistoria limeshuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, jijini Nairobi, nchini Kenya.

Hatua hiyo inalenga kuimarisha uratibu na ushirikiano katika maandalizi ya mashindano makubwa ya soka barani Afrika.

Aidha, katika mazungumzo hayo, wamejadili hatua muhimu kuelekea mashindano ya AFCON 2027, ikiwamo tathmini ya hatua iliyofikiwa na nchi katika maandalizi, utayari wa kitaifa, pamoja na maendeleo ya miundombinu inayohitajika.

Vilevile, Serikali imewasilisha ombi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kutumia lugha ya Kiswahili k**a lugha rasmi katika mashindano hayo ya mwaka 2027.

Mkutano huo ulijumuisha mawaziri kutoka nchi tatu wenyeji wa AFCON 2027, Kenya, Uganda na Tanzania, pamoja na wenyeviti wa k**ati za maandalizi za AFCON (LOC), Marais wa mashirikisho ya mpira wa miguu ya nchi hizo, pamoja na wataalamu wengine kutoka wizara za michezo katika nchi waandaaji.

Photos from Baraza la Michezo la Taifa's post 09/05/2026

Maandalizi yamepamba moto ndani ya Ukumbi wa The Super Dome Masaki tayari kwa usiku mkubwa wa Tuzo za BMT leo Mei 09, 2026
Mandhari, mwanga na mpangilio vinaonyesha wazi kuwa usiku wa leo utakuwa wa kipekee kwa wanamichezo na wageni wote watakaohudhuria.

07/05/2026

WANAOWANIA TUZO KIPENGELE CHA WANAHABARI BORA WA KIUME WA MWAKA 2025

07/05/2026

WANAOWANIA TUZO KIPENGELE CHA MWANAHABARI BORA WA K**E WA MWAKA 2025

07/05/2026

MAANDALIZI YA USIKU WA TUZO ZA BMT KWA WANAMICHEZO BORA MSIMU WA 4 2025 YAFIKIA 90%

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

MKAPA STADIUM, 2nd Floor
Dar Es Salaam