Weights and Measures Agency Tanzania - WMA

Weights and Measures Agency  Tanzania - WMA

Share

Dhima ya Wakala wa Vipimo ni kuthibiti vipimo vyote vinavyotumika na vinavyokusudiwa kutumika katika Sekta ya Biashara, Mazingira, Afya na Usalama.

Wakala wa Vipimo ni Taasisi ya Serikali iliyoko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara inayosimamia matumizi sahihi ya vipimo katika biashara, Afya, Usalama na Mazingira. Iliundwa Mwaka 2002 na Majukumu yake ni Kumlinda mlaji katika Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira kupitia matumizi ya Vipimo sahihi. Kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sek

Photos from Weights and Measures Agency  Tanzania - WMA's post 16/04/2026

KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

Na Veronica Simba - WMA

Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, imekiri kuvutiwa na utendaji kazi wa Wakala wa Vipimo (WMA) Tanzania Bara na kuahidi kuweka mikakati ya makusudi itakayoisaidia Mamlaka inayosimamia vipimo nchini humo (ZAWEMA) kutekeleza majukumu yake kwa kiwango hicho au zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Aprili 16, 2026 baada ya ziara ya mafunzo katika Kituo cha Vipimo Misugusugu, mkoani Pwani, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Mohammed Ali Suleiman, amesema Wakala wa Vipimo upande wa Tanzania Bara wamepiga hatua kubwa kiutendaji hivyo kuna kila sababu ya Zanzibar kufuata mfano huo.

“Tumeona wenzetu wamefanya kazi kubwa na wana vipimo vya kisasa ambavyo vinawawezesha kuhakiki mathalani kiwango cha maji anachotumia mteja ndicho anacholipia, halikadhalika kwenye umeme pamoja na vipimo vingine.”

Mhe. Dkt. Suleiman ameongeza kuwa, Kamati yake itaishauri Wizara ya Biashara ambayo ndiyo inayoisimamia Mamlaka ya Vipimo Zanzibar, kuweka mikakati ya makusudi ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa manufaa ya wananchi.

Amesema wataishauri Serikali kuhakikisha ZAWEMA, ambayo ndiyo Mamlaka ya Vipimo kwa upande wa Zanzibar, kwanza inakuwa Mamlaka huru lakini pia ipate mitambo ya kisasa ya uhakiki vipimo na pia ishirikiane kwa ukaribu na WMA ili iweze kutekeleza majukumu yote kwa ufanisi.

“Ukiangalia, Kituo hiki cha Misugusugu kinaipatia Serikali ya Tanzania mapato makubwa sana. Ni muhimu Serikali yetu iwezeshe ZAWEMA kufanya kazi kwa karibu na WMA ili kupata mafanikio k**a hapa,” amesisitiza Mhe. Dkt. Suleiman.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Kihulla, amesema anaamini kwamba, kupitia ziara hiyo ya mafunzo kwa Kamati kutoka Baraza la Wawakilishi, jukumu la uhakiki na ukaguzi wa vipimo linaenda kuwa bora zaidi kwa pande zote mbili; Zanzibar na Tanzania Bara.

“Niwahakikishie tu kwamba tutaendelea kushirikiana na wenzetu wa Zanzibar ili kuhakikisha Mtoa Huduma analindwa lakini pia Mpokeaji Huduma analindwa.”

Akidadavua zaidi kuhusu ushirikiano uliopo kati ya WMA na ZAWEMA, Mtendaji Mkuu amesema Taasisi hizo mbili zilikwishasaini Hati ya Ushirikiano (MoU) kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kushiriki kwenye mikutano ya kikanda na kimataifa pamoja na katika kaguzi za vipimo hususan katika bidhaa zilizofungashwa.

Amesema kuwa, WMA wakiwa ndiyo wenyeji katika ziara hiyo, wamewaonesha wageni wao utendaji kazi katika maeneo mbalimbali ikiwemo uhakiki wa tenki za kusafirishia mafuta, uhakiki wa mita za umeme pamoja na uhakiki wa dira za maji.

Wakala wa Vipimo Tanzania imekuwa ikipokea wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuja kujifunza kuhusu majukumu ya uhakiki wa vipimo.

Aidha, kwa sasa, Wakala wa Vipimo Tanzania ndiye Mwenyekiti wa Jukwaa la Kikanda linaloratibu masuala ya kivipimo (legal metrology) kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADCMEL).

05/04/2026

Tunawatakia Heri ya Pasaka

03/04/2026

Wazalishaji wa bidhaa za nondo wahimizwa kuzingatia Vipimo sahihi wakati wa uzakishaji wa bidhaa hizo ili kuepuka usumbufu wa kurudia kuzalisha bidhaa hiyo kwa Vipimo sahihi k**a Sheria ya Vipimo Sura 340 inavyoelekeza.

03/04/2026

Tunawatakia Ijumaa Kuu njema

21/03/2026

Eid Mubarak

Photos from Weights and Measures Agency  Tanzania - WMA's post 20/03/2026

WAKALA WA VIPIMO WAITIKIA WITO WA RAIS SAMIA KUHUSU UPANDAJI MITI

Na WMA – Dodoma

Watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA), wameitikia wito wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaowataka watanzania kupitia makundi mbalimbali kupanda miti katika maeneo yao ili kuhifadhi mazingira.

Akiongoza zoezi la upandaji miti katika eneo ilipo Ofisi Kuu ya WMA Medeli jijini Dodoma, mapema leo Machi 20, 2026 Meneja Utawala na Rasilimali Watu, Charles Mavunde amewasisitiza watumishi wa Wakala hiyo nchi nzima kuzingatia maelekezo ya Serikali kwa kupanda miti na kuitunza ili kulinda mazingira.

Amesema kuwa, Mheshimiwa Rais Samia amekuwa akisisitiza mara kwa mara kuhusu upandaji miti katika maeneo mbalimbali na kwamba yeye mwenyewe ameonyesha mfano kwa kuwa kinara wa upandaji miti, hivyo WMA imeona ni vyema pia iitikie wito huo.

“Mtakumbuka kwamba, hata Mheshimiwa Dkt. Emmanuel Nchimbi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimwakilisha Mhe. Rais katika maadhimisho ya siku ya upandaji miti duniani na maadhimisho ya upandaji miti kitaifa, jana Machi 19, 2026 kule Lindi aliagiza kuwa makundi mbalimbali ya watanzania waendeleze utamaduni wa kupanda miti,” ameeleza Mavunde na kuhitimisha kuwa WMA imeyachukulia kwa uzito maelekezo ya viongozi hao na itayatekeleza kikamilifu.

Viongozi na watumishi mbalimbali wa WMA Makao Makuu wameshiriki zoezi hilo la upandaji miti akiwemo Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Phanuel Mtuki, Meneja Sehemu ya Fedha, CPA Ibrahim Mbinga, Meneja Mkoa wa Dodoma Said Ibrahim, Meneja Mawasiliano Veronica Simba na Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Nelson Ruturagara.

Wengine walioshiriki ni watumishi kutoka Idara mbalimbali wakiwemo maafisa, maafisa usafirishaji na wasaidizi wa ofisi.

WMA ni wakala ya serikali iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara yenye jukumu kuu la kumlinda mlaji kupitia usimamizi wa matumizi sahihi ya vipimo katika sekta mbalimbali.

08/03/2026

HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUTOKA WAKALA WA VIPIMO

Photos from Weights and Measures Agency  Tanzania - WMA's post 05/03/2026

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI MGENI RASMI, MKUU WA MKOA WA DODOMA, MHE. ROSEMARY SENYAMULE ALIPOTEMBELEA BANDA LA WAKALA WA VIPIMO (WMA) WAKATI WA UFUNGUZI RASMI WA KLINIKI YA KUPOKEA KERO ZA WANANCHI, UWANJA WA NYERERE SQUARE JIJINI DODOMA, MACHI 5, 2026.

Photos from Weights and Measures Agency  Tanzania - WMA's post 21/02/2026

Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imetoa mafunzo ya vipimo kwa wanafunzi wa Shule ya Dr. Samia Dodoma Secondary School, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa vipimo sahihi katika biashara na maisha ya kila siku.

Katika zoezi hilo, wanafunzi walipata fursa ya kujifunza kuhusu dhima na majukumu ya Wakala huo, pamoja na namna unavyolinda maslahi ya watumiaji na wafanyabiashara kwa kuhakikisha vipimo vinakuwa sahihi na vya kuaminika.

Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa WMA, Veronica Simba, amesema elimu ya vipimo itatolewa katika mikoa yote ya Tanzania Bara ili kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wanapata uelewa wa matumizi sahihi ya vipimo.

19/02/2026

Tunawatakia Ramadhan Kareem

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Dar Es Salaam
313