Fikra Za CCM

Fikra Za CCM

Share

Hii ni Page ambayo italeta na kukufikishia habari za uhakika kutoka kwenye chama cha mapinduzi..

Photos from Fikra Za CCM's post 17/03/2022

📍Chato - Geita

Nukuu za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, alipozungumza na Umma wa Watanzania aliposhiriki katika misa ya Mwaka Mmoja wa kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) unaungana na Watanzania wote kumuombea kwa M/Mungu aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli apumzike kwa Amani na daima Watanzania tutamkumbuka.

14/02/2022

ZA UPENDO: HERI YA SIKU YA WAPENDANAO.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawatakia wanachama wa CCM na watanzania wote heri ya siku ya wapendanao. Upendo ni silaha yetu yenye nguvu, tuudumishe na kushirikiana kwa pamoja katika kulijenga taifa letu pendwa la Tanzania.



Photos from Fikra Za CCM's post 30/06/2021

*CCM YAKUTANA KIKAO KAZI NA WADAU WA SEKTA YA UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI*

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM *Ndugu Daniel Chongolo* Jumatano 30 Juni 2021 ameongoza kikao kazi cha wadau *28* kutoka katika taasisi na wadau wa sekta za uwekezaji na Uwezeshaji nchini.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Takwimu Dodoma ambacho kimeratibiwa na Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Lengo la kikao hicho ni kufatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2020-2025 ,(ibara ya 23-26) ambapo Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi limepewa jukumu la kusimamia Uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kusimamia mifuko na programm za Uwezeshaji takriban 61, wakati Chama cha Mapinduzi kikiahidi ajira million 8 katika kipindi cha miaka 5. (2020-2025)

*
*

Photos from Fikra Za CCM's post 29/06/2021

*TAARIFA KWA UMMA*

Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimefanyika Jumanne Juni 29, 2021 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa White House Dodoma.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wameazimia na kutoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Husein Ali Mwinyi kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuiongoza nchi na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.h

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamebainisha kuwa tokea nchi ilipopata msiba mkubwa wa kuondokewa na aliyekuwa Rais, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ndani ya siku mia moja za uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa na kuonyesha dira ya serikali anayoiongoza kuwah inazingatia uadilifu, Utawala wa Sheria, Haki, Usawa, kuimarisha misingi ya demokrasia, umoja na mshikamano zaidi kuendelea kutunza Amani na usalama wa nchi.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesisitiza juu ya azma ya Serikali inayoiyongoza kuhakikisha inakamilisha na kuiratibu vyema miradi yote ya kimkakatih iliyoanzishwa na inayoendelea kutekelezwa sambamba na kuhakisha uchumi wa nchi unakuwa kwa kasi.

“Miradi yote iliyopo kwenye maeneo yenu viongozi wa CCM mnaoh wajibu wa kuifatilia, kuikagua na kujua uendelevu wake bila uwoga kwani huo ni wajibu wenu wa msingi katika kutusimamia Serikali, hilo liende sambamba na kuhakikisha mnasaidia kuona mapato ya Serikali hayapotei katika vyanzo vyote vya ukusanyaji, ikumbukwe ninyi ndio kioo cha kutumurika, kwavile ilani inayotekelezwa ni ya Chama Cha Mapinduzi lazima ifanikiwe kwa kiwango kikubwa” Ndugu Samia Suluhu Hasasan Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi.
29 Juni, 2021.

Photos from Fikra Za CCM's post 29/06/2021

NUKUU: MKUTANO WA KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI CCM NA WAANDISHI WA HABARI.

Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka ameeleza maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM na hizi ni nukuu katika yale aliyoyazungumza.


Photos from Fikra Za CCM's post 29/06/2021
28/06/2021

TAARIFA KWA UMMA

*HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KUKUTANA DODOMA.*

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma kuwa Jumanne tarehe 29 Juni 2021 kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kitafanyika chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho cha kawaida kwa mujibu wa kalenda ya vikao kitafanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu, Jijini Dodoma.

Maandalizi yote ya kikao hicho yamekamilika.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi.
28 Juni, 2021.

Photos from Fikra Za CCM's post 27/06/2021

MKUTANO MKUU WA BARAZA LA WAISLAMU (BAKWATA )MKOANI TANGA.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka leo Jumapili 27 Juni 2021 amemuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Cde Daniel Chongolo katika Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu BAKWATA unaofanyika Mkoani Tanga.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Philip Isdori Mpango.

KaziIendelee

Shaka Hamdu

Photos from Fikra Za CCM's post 21/06/2021

Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndg .John Mongela amemuwapisha Mwl.Raymond Mwangwala ambaye ameteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro.

Kabla ya uteuzi huo Mwl.Raymond Mwangwala alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)

Kazi iendelee

Photos from Fikra Za CCM's post 11/06/2021

*CHAMA IMARA SERIKALI IMARA ,HODI MKOA WA TANGA*

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo leo Ijumaa tarehe 11 Juni, 2021 amewasili Mkoa wa Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kuimarisha Chama mashinani kwa siku tano kuanzia tarehe 11 mpaka 14 Juni, 2021

Katibu Mkuu ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Siasa na Uhusiano wa Kimataiga Ndg Ngemela Lubinga pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.

Katibu Mkuu katika ziara hiyo kiongozana na ujumbe wake wamepokelewa na Uongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Tanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa Ndugu Shekifu wilayani Handeni, ambapo alisimamishwa na wananchi waliojitokeza barabarani kumlaki na kupata nafasi ya kuwasalimia nao kwa ufupi.

Kesho tarehe 12 Katibu Mkuu ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Kilindi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Atakuwa Wilaya ya Pangani wakati Katibu wa Halmashauri Kuu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa atakuwa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga

Ziara hiyo ni mkakati wa Chama Cha Mapinduzi kukiimarisha mashinani na kupata nafasi ya kusimamia, kukagua na kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.

Photos from Fikra Za CCM's post 28/05/2021

DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Comrade Kheri James (MCC) akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl.Raymond Mwangwala (MNEC) wakiwa na aliyekuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndg. Leonard Singo pamoja na Katibu Mpya wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndg.Victoria Mwanziva. muda Mfupi baada ya tukio la kukabidhiana Ofisi kukamilika, tukio ambalo limefanyika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM Upanga Jijini Dar es salaam

Kazi iendelee

14/05/2021
Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam