JAMII YETU

JAMII YETU

Share

Hapa tunazungumzia maisha ya Watanzania wanayo yaishi katika jamii na biashara zao kiujumla na jinsi ya kuwainua kiuchumi, mtazamo na maadili.

20/04/2018

habalini zaleo wapendwa

14/10/2016

JE???? UNA SHUGHURI YA HARUSI??, SEND OFF, KITCHEN PART, VIKAO VIKUBWA? MAKONGAMANO?, SHEREHE ZA SIASA? K**A NDIO JE?? UMEHANGAIKA KUPATA WAHUDUMU WA KUKUHUDUMIA SHEREHE YAKO NA KUIFANYA SHEREHE YAKO KUWA BORA NA YENYE KUIGWA KWA WATU WENGINE? AU YENYE MFANO KATIKA JAMII YAKO? KATIKA UPANDE WA KEKI, MAPAMBO, NA CHAKULA?????????
BASI USILIE TENA JIBU LA MATATIZO YAKO LIMEPATIKANA NI TAI CATERING PEKEE KUTOKA KAMPUNI YA TAI NDIO WENYE UWEZO WA KUKUFANYA KUWA BORA SANA. WANAO UWEZO MKUBWA SANA KATIKA KUKUHUDUMIA. TAI TUNAJARI AFYA YAKO JIVUNIE UBORA WA SHEREHE YAKO.PIA TUNAPAMBA NA KUPIKA KWENYE MISIBA MBALI MBALI.

WASILIANA NA SISI KWA 0752430751
[email protected]
Tupo Dar es salaam, Tanzania.

10/10/2016

JE???? UNA SHUGHURI YA HARUSI??, SEND OFF, KITCHEN PART, VIKAO VIKUBWA? MAKONGAMANO?, SHEREHE ZA SIASA? K**A NDIO JE?? UMEHANGAIKA KUPATA WAHUDUMU WA KUKUHUDUMIA SHEREHE YAKO NA KUIFANYA SHEREHE YAKO KUWA BORA NA YENYE KUIGWA KWA WATU WENGINE? AU YENYE MFANO KATIKA JAMII YAKO? KATIKA UPANDE WA KEKI, MAPAMBO, NA CHAKULA?????????
BASI USILIE TENA JIBU LA MATATIZO YAKO LIMEPATIKANA NI TAI CATERING PEKEE KUTOKA KAMPUNI YA TAI NDIO WENYE UWEZO WA KUKUFANYA KUWA BORA SANA. WANAO UWEZO MKUBWA SANA KATIKA KUKUHUDUMIA TAI TUNAJARI AFYA YAKO JIVUNIE UBORA WA SHEREHE YAKO.
WASILIANA NA SISI KWA 0752430751
[email protected]
Tupo Dar es salaam, Tanzania.

02/10/2016

KAMPUNI YA TAI TUNAKUPA OFA BABU KUBWA LEO HII.

Ukitutafutia tenda ya kupika chakula kwenye sherehe mbali mbali k**a vile HARUSI na SEND OFF sisi k**a kampuni ya TAI tunakupatia OFA ya sh. 100,000/= cash k**a pongezi ya kazi yako hiyo kwetu.Fanya leo zaidi uwezavyo ujinyakulie pesa nyingi mno kadri uwezavyo.

Pia kampuni yetu ya TAI tunapamba kumbi za sherehe mbalimbali kwa mitindo aina zote ambazo mteja wetu unataka,
Pia tunatoa huduma za chakula kwenye sherehe mbali mbali k**a
1. Harusi
2.Send off
3. Kitchen part
4. Vikao mbalimbali hata vya siasa
5. Semina mbalimbali.

Huduma zetu ni k**a zifuatazo.

a/ keki aina zote
b/ Chakula aina zote
c/ mapambo aina yote.

Tuna watalamu waliobobea sana na wenye uzoefu wa kazi hizi karibu sana.
Wasiliana nasi kwa
0752430751 au
[email protected]
Tupo Dar es salaam.

29/09/2016

KAMPUNI YA TAI TUNAKUPA OFA BABU KUBWA LEO HII UKITUTAFUTIA TENDA YA KUPIKA KWENYE SHEREHE KIASI CHA SH.100,000/= CASH KWAAJILI YA PONGEZI. FANYA LEO ZAIDI UWEZAVYO UJINYAKULIE KITITA CHAKO.
pia tunapamba kumbi mbali mbali kwa mitindo aina yote pia tuna tengeneza keki aina zote wasiliana nasi kwa 0752430751 tupo Dar es salaam.

30/08/2016

Ili kufikia kilele cha ndoto yako na kufanikisha malengo yako yote,ni lazima uwe mtu ambaye kila wakati uko katika hamasa ya kuchukua hatua kuelekea katika lengo kubwa ulilonalo maishani.Kati ya sababu zinazowasababisha watu wengi sana washindwe kufikia malengo yao makubwa ni ile hali ya kuwa leo wako na hamasa kubwa ya kufanya kitu kisha kesho unakuta hamasa imepungua,kesho kutwa wanaanza tena kisha siku inayofuata wamepunguza kasi tena.

K**a wewe ni mtu ambaye hamasa yako ya kufanya jambo inayumbayumba na iko k**a homa za vipindi-Leo uko juu kesho uko chini basi itakuchukua muda mrefu sana kufanikiwa.Kuna watu wengi ambao wakikutana na kitu kidogo tu basi huwa wanashindwa kabisa kuendelea kufuatilia ndoto zao.Wengine wakiambiwa neno la kukatisha tamaa na mtu,wengine wakikataliwa kitu,wengine wakiudhiwa jambo fulani n.k basi hutumia hisia zao za hasira ama kuudhika kwa kuacha kufanya jambo ambalo walishaamua tangia mwanzo kuelekea katika mafanikio yao.

Profesa Teresa Amabile wa kitivo cha biashara cha chuo kikuu cha Harvard,aliwahi kufanya utafiti juu ya mambo ambayo huwafanya wale wanaofanikiwa kuwa na uwezo wa kupiga hatua kila wakati bila kukata tamaa hata wakati wengine wote wanaonekana kuvunjika moyo kuendelea kuchukua hatua katika kuelekea kutimiza malengo yao.Utafiti huu ulifanyika kwa miaka mingi na ulipelekea kuandikwa kwa kitabu cha kanuni ya kuendelea mbele(The Progress Principle).

Katika utafiti huu aliwahusisha watu takribani 238 ambao walikuwa wamefanikiwa sana katika nyanja zao.Na akawachunguza kwa muda wa siku takribani 12,000 kwa kila siku kuwasiliana nao na kujua ni mambo gani wamefanya na pia kujua ni mambo gani waliyatumia kuwatia hamasa katika kuelekea kufanikisha malengo yao.Katika watu aliowahoji walikkuwepo mameneja takribani 26 kutoka katika makampuni makubwa sana ya kimataifa.

Utafiti huu ulikuja na matokeo kadhaa ambayo k**a na wewe utayajua basi yatakusaidia sana kuhakikisha kuwa unafanikiwa na unapiga hatua kubwa katika kutimiza malengo yako kabla mwaka huu haujaisha.

Moja,ilionyesha kuwa watu wanaofanikiwa ni wale ambao huwa wanajua bila shaka kuwa wanataka nini katika maishba yao.Ni rahisi sana kukutana na watu wanaotamani kufanikiwa ,lakini ni ngumu sana kukutana na watu ambao kwa umahsusi wanajua haswaa wanachotaka.Kuna watu wengi sana ukiwauliza watakuambia wanataka kuwa matajiri lakini kwa kiwango gani,hawajui.Wengine watakuambia wanataka kuwa wafanyabiashara wakubwa ila ukiwauliza unataka kuwa unauza nini na unataka kuwa tajiri wa kiasi gani,hawajui-Wengine watakuambia wanataka kubadilisha jamii au Taifa lao ila ukiwauliza kwa namna gani,hawajui kabisa.

Mafanikio ni matokeo ya kujua bila kuwa na shaka lile jambo ambalo unataka kufanikiwa kwalo.Leo hebu jiulize,hivi mafanikio unayoyazungumzia unayajua kwa ufasaha ama unazungumza kwa ujumla.Nimeshakutana na watu wengi sana ambao ukiwauliza kwa nini hawaishi ndoto yao watakuambia sina mtaji,ila ukijaribu kuwauliza kwa undani wanataka kufanya nini utashangaa kuwa hawako mahsusi kabisa katika kila wanachotaka kufanikiwa.Wengi wamekwama sio kwa sababu hakuna watu wanaotaka kuwasaidia ama hakuna mtaji,bali kwa sababu bado hawajajua kwa hakika wanachokitafuta katika maisha ni nini.Je,wewe unajua unachokitafuta?Tukikuamsha kutoka usingizini unaweza kutuambia kwa sentensi moja unataka mafanikio ya namna gani?K**a jibu lako ni hapana basi ujue haujajiunga katika safari ya mafanikio.Kitaalamu malengo yako yanatakiwa yawe k**a vile unatoa oda kiwandani,kiasi kwamba k**a mzalishaji wa kiwandani akiyasoma basi alete kitu sawasawa na kile ulichoagiza-Je,kwa malengo ulinayo yanakidhi kiwango hiki?K**a hapana,wala usiwe na haraka ya kukimbilia kufanya,tengeneza malengo mahsusi kuhusu mwelekeo wako.

Jambo la pili ambalo liligundulika katika utafiti huu ni kuwa watu wanaofanikiwa ni wale ambao huwa wanatiwa moyo na kila mafanikio madogo wanayoyapata huku wakiamini mafanikio makubwa yatakuja pia.Huwezi kuwa mtu ambaye huna shukrani kwa kidogo ulichonacho halafu ukategemea kupata kikubwa,hiyo haiwezekani.Utafiti uligundua kuwa watu ambao kila hatua ndogo wanayoipiga huwa wanaifurahia na kujaa na shukrani huwa wanapiga hatua kwa kasi sana.

Hii inamaanisha watu hawa kila siku wanapoamka asubuhi huangalia kile walichonacho na kuanza kushukuru kuwa wanacho na sio kuanza kuangalia wasichonacho na kuanza kunun’gunika.Wakati wewe unalalamika huna gari la kutembelea kuna mtu hana nauli ya daladala,wakati wewe unalalamika hakuna anayekujali,kuna mtu tangu azaliwe hawajui wazazi wake kwa sababu walimtupa na akaokotwa jalalani na tangia hapo anaishi kituo cha watoto yatima,wakati wewe unalalamika una viatu pea moja kuna mtu alizaliwa hana miguu kabisa,wakati wewe unalalamika mshahara mdogo kuna mtu hajui leo atakula nini na jana amekula mlo mmoja tu.

Kwa hali yoyote ile uliyonayo jifunze kuwa mtu wa shukrani,mwambie Mungu-“Nashukuru kwa hapa nilipo na hivi nilivyo,najua kuna watu wenye hali mbaya kuliko yangu.Ingawa bado sijafika ninakokwenda ila bado nina matumaini ya kufanikiwa”.Amua kuwa mtu ambaye unaona jema katika kila baya,mtu ambaye unaona tumaini katika kila kinachokatisha tamaa.Leo,anza siku yako kwa shukrani.Jikague na usiangalie usivyonavyo,hebu angalia ulivyonavyo na mshukuru Mungu kwa hali yako huku ukifanya bidii katika kufikia malengo makubwa.Leo,utashangaa jinsi ambavyo utajawa na nguvu za kuchukua hatua zaidi.Kumbuka siku zote malalmiko huwa hayawezi kubadilisha hali yako.Unapokuwa mtu wa shukrani unaruhusu ubongo wako kufanya kazi kwa kasi na kuwa na ubunifu zaidi.

Jambo la tatu waliloligundua ni kuwa watu wanaofanikiwa ni wale ambao katika kila changamoto wanayopitia huwa wanaamua kuangalia malengo makubwa na hawako tayari kukatishwa tamaa na kushindwa kudogokudogo.Utafiti uligundua kuwa hata wale waliofanikiwa sana huwa wanapitia nyakati za kukatisha tamaa na huwa wanajikuta wako chini kabisa.Tofauti yao ni kuwa kila wakati wakijikuta katika hali hiyo ya kukatisha tamaa huwa wanaweka macho yao katika ndoto yao kubwa ambayo ndiyo huwatia nguvu zaidi kusonga mbele.Je,unayo picha kubwa ya ndoto yako?K**a unayo basi kila wakati ukikutana na hali ya kukatisha tamaa,weka macho yako katika picha kubwa.Leo usikubali jambo lolote lile likukatishe tamaa ya kusonga mbele.Amua kuwa utachukua hatua kuelekea katika malengo yako.

Kumbuka kuwa ndoto yako inawezekana.

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.com/www.mentorship.co.tz ili kujifunza zaidi.

See You At The Top.

©JoelNanauka

Page not found – Joel Nanauka Your Dream is possible, Refuse to give up

Joel Nanauka 30/08/2016

Hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini Dangote pamoja na kuwa tajiri nambari moja Afrika bado anafanya kazi kwa masaa takribani 18 kwa siku?Umeshawahi kushangaa kwa nini Bill Gates tajiri namabri moja duniani bado yuko bize kuikuza kampuni yake na kufanya bidii ili kuongeza faida ya biashara yake kila siku?Jibu ni rahisi sana-Mafanikio katika maisha ni matokeo ya hali ya kuwa na kiu ya kuongezeka zaidi kuliko ulivyokuwa leo.Bila kujali umefika hatua gani ya maisha,bila kujali kuna watu wangapi wanakusifia kuwa umefanikiwa na umepiga hatua sana,ni lazima kiu yako ya kutaka kuendelea mbele isikauke kila siku.

Kati ya sababu imefanya watu wengi sana kuishia njiani katika kuelekea mafanikio yao ni ile hali ya kupoteza shauku ya kufanikiwa zaidi ya walivyofanikiwa leo.Mwanasayansi nguli na mvumbuzi maarufu sana,Thomas Edison aliwahi kusema “Hatutaweza kuwa na kesho iliyo bora zaidi k**a hali tuliyonayo kwa sasa tunaona imetutosheleza na hatuhitaji kuchukua hatua“.Bila shaka hili ndilo lililomfanya mwanasayansi huyu awe tayari kujaribu kutengeneza taa bila mafanikio kwa mara 999 hadi alipoweza kufanikiwa mara ya 1000.

Ila swali la muhimu sana la kujiuliza ni kuwa,hivi kwa nini watu wengi sana huwa hawako tayari kuwa na kiu na shauku ya kuboresha maisha yao ya kila siku?Je,wewe ni mmoja wa watu ambao ni k**a vile shauku yako ya kufanikiwa zaidi kwa viwango vya juu imepungua sana?Kuna sababu tatu ambazo hufanya watu wawe katika hali hii ambayo huwapelekea kushindwa kabisa kufikia malengo yao.

Moja ni kwa sababu ya kujaribu mara nyingi bila mafanikio hivyo huamua kukata tamaa.Kuna watu ukiwaona watakuambia wameridhika ama utadhani kuwa wameridhika lakini kumbe wamekata tamaa.Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuridhika na kukata tamaa;kuridhika ni uamuzi wa hiari lakini kukata tamaa ni matokeo ya kushindwa mara nyingi katika kile unachojaribu.Tukiwa shule ya msingi tuliwahi kusoma hadithi ya sungura ambaye alikuwa anajaribu kurukia ndizi mbivu,baada ya kufanya mara nyingi bila mafanikio ndipo alipoamua kusema “Sizitaki mbichi hizi”-Huku wakati anarukia anajua fika zilikuwa ni mbivu.

Ndivyo ilivyo,kuna watu wengi sana utasikia mimi sipendi biashara kabisa,ukichunguza utakuta ni kwa sababu walijaribu wakafeli hivyo wamekata tamaa,kuna wengine utawasikia hawapendi kilimo,kumbe walijaribu mazao hayakuzaa k**a walivyotegemea na mtaji ukakata kabisa,lakini wanajifanya hawapendi kilimo.

Kila kona kuna “Mr.sizitaki mbichi hizi”,kila mahali kuna akina “Mrs.Sizitaki mbichi hizi”.Hata wewe inawezekana leo unasoma hapa na kuna maeneo ya maisha yako unajifanya k**a vile hupendi kufanya kumbe ukweli ni kuwa wewe ni mmoja wa “sizitaki mbichi hizi”;kinachokufanya usifanye tena sio kwa sababu hupendi bali kwa sababu ulifeli.K**a unataka kufanikiwa katika malengo yako ni lazima uwe mtu ambaye hata baada ya kujaribu mara nyingi na kushindwa endelea kuweka kiu yako ya kufanikiwa kuwa hai na iwe juu kila wakati.

Je,kuna eneo la maisha yako ambalo umeacha kufanya na unasema kuwa hulipendi na umeridhika wakati ukweli ni kuwa umekata tamaa baada ya kujaribu?Uzuri ni kuwa kila mtu anaujua moyo wake na wakati kila mtu anaweza asijue,wewe mwenyewe ni lazima unajua.Usiogope kuanza upya na kuchukua hatua bila uoga tena.

Jambo la pili linalowafanya watu wengi wapoteze kiu na hamasa ya kuelekea katika malengo yao ni ile hali ya kujilinganisha na watu wa chini kabisa.Kuna watu wameshindwa kuendelea mbele kwa sababu watu wote wanaowazunguka wanaonekana wako mbali sana na mafanikio na wao ndio wako juu kuliko mtu mwingine yeyote na kwa sababu hiyo wanajiona hawana sababu ya kufanikiwa zaidi.

Kuna watu wako makazini na kwa sababu wanajiona wanapokea mshahara mkubwa kuliko yoyote katika ofisi basi wanaona wameshafika,wengine marafiki zake wote wanasota na wao tu ndio wako vizuri kidogo,basi wanajiona hawana sababu ya kupiga hatua zaidi,kuna watu mtaani kwao duka lao ndio kubwa zaidi basi wanajiona wameshafika,kuna watu wao ndio wana elimu kubwa katika familia nzima basi anaona k**a vile hana haja ya kuendelea mbele zaidi n.k

Ili ufanikiwe kwa kiwango cha juu,achana na tabia ya kujilinganisha na watu walio kiwango cha chini yako ama walio sawa na wewe.Mafanikio husukumwa na shauku ya kutaka kufanana na watu walio juu yako zaidi ambao kila siku wanatakiwa wakutie hamasa ya kufanikiwa k**a wao.Hii ndio maana kila mtu anashauriwa awe na mtu ambaye katika maisha yake anatamani kufanikiwa kwa kiwango ambacho mtu huyo amefanikiwa.Acha kujifananisha na wanyonge halafu unajiona umefika.

Bado una uwezo mkubwa sana ndani yako ambao unakusubiria pale utakapoanza kutamani kiwango kikubwa cha mafanikio kuliko ulichonacho leo.Leo,tafuta mtu ambaye unatamani kufikia kiwango cha mafanikio k**a chake na zaidi,kisha jipime kile siku umepiga hatua ngapi kumsogelea.

Sababu ya tatu ni ile hali ya kujiona kuwa wewe ni bora kuliko mtu mwingine yeyote.Unapoanza kufikiria kuwa unajua kila kitu kuliko mtu yoyote yule,basi kiu yako ya kutaka kufanikiwa zaidi itapotea bila wewe mwenyewe kujua.Kuna watu wengi sana ambao wameingia katika mtego huu bila wao wenyewe kujua.Utajuaje k**a na wewe umeshanasa?K**a wewe ni mtu ambaye kila ukisikia semina ya mambo ya mafanikio ama Makala,kabla hata hujasoma ama hujahudhuria unaanza kujiona hakuna haja kwa sababu kila kitu umeshajua.

Ukizunguka sehemu mbalimbali Tanzania,utashangaa sana kukutana na watu wengi ambao wanasema wanajua sana kuhusu mambo fulani lakini utashangaa kila mwaka wako hatua ileile.Ili ufanikiwe ni lazima njaa yako ya kupata maarifa mapya iwe kubwa kuliko njaa yako ya kupiga stori na wengine,ili ufanikiwe ni lazima njaa yako ya kusikiliza wengine iwe kubwa kuliko njaa yako ya kutaka kuonyesha kuwa unajua kila kitu.Leo,amua kuwa mtu ambaye unatamani kujifunza kitu kipya kila wakati.

Kumbuka kuwa ndoto yako Inawezekana,

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com /www.mentorship.co.tz ili kujifunza zaidi.

See You At The Top

©JoelNanauka

Joel Nanauka Your Dream is possible, Refuse to give up

30/08/2016

✍🏽 *KATAA KUFA BILA KUTIMIZA NDOTO YAKO*

✋�Katika kitu kibaya sana duniani ni kitendo cha mtu kufa na ndoto ambayo haijitimizwa na huku akiwa alikuwa na kila sababu ya Kutimiza ndoto zake .

🔨Thomas Edson angekufa na ndoto yake leo hii tusingeshuhudia umeme ukiwaka na duniani pasipengukuwa sehemu nzuri ya kuishi bila kuwa na umeme.Lakini ni Jitihada za mtu mmoja ambaye inasemekana alishindwa mara 1000 lakini hakukata tamaa na mwisho ndoto yake ikatimia .Leo ndoto ya Thomas Edson imeajiri wengi sana na uzalishaji unafanyika kwa kiwango cha juu kupitia ndoto yake .

🔨Huna sababu ya Kufa na ndoto yako kwa sababu ulishawahi sikia historia ya Yusufu nanmna ambavyo alikuwa na ndoto kubwa lakini ndoto yake ikiwa na vipangamizi vingi sana kuanzia kwenye familia yake.Haikuwa rahisi kwake lakini hakukubali mazingira yaue ndoto zake .Tunashuhudia Yusufu anawaokoa ndugu zake ambao walitaka kuua ndoto yake.

🔨Ukifa na ndoto yako maana yake kuna watu utasababisha wawe na maisha magumu maana walitegemea wewe utimize ndoto yako waweze kuwa na unafuu wa maisha.Ni watu ambao wameandaliwa kufanya kazi chini yako ,utengeneza Maisha hatma ya maisha yao.

🔨Nyuma yako liko kundi kubwa ambalo lina maisha magumu sana .Wanasubiri uanzishe ile kampuni uliyosema unaanzisha lakini hujaanzisha ,wanasubiri ile shule uliyosema unaanzisha lakini mpaka sasa hujaanzisha wanasubiri uanzishe ile supermarket ambayo iko kwenye mpango mkakati wako tokea mwaka juzi lakini bado hujaanzisha.

🔨Nasikitika kukwambia kuwa umekuwa chanzo cha ukosefu wa ajira nchini kwa sababu hujatimiza ndoto yako .Angalia ndugu yule anvyohangaika pengine wewe ndiwe mwajiri wake .Machozi yake yako juu yako .Angalia anataka kujiua na achome vyeti vyake kwa sababu yako inauma sana .

🔨Rafiki yangu Michael Mathias Uhahula Mkurugenzi wa Asasi Foundation yenye makao makuu kule mkoani njombe alitambua siri ya kutokufa na Ndoto yake na kupitia ndoto yake ya kuwasaidia watu kuwekeza katika Mashamba na Misitu ameweza kuajiri vijana miambili(200) wa Kitanzania .Kijana huyu mwenye umri mdogo wa miaka 27 sasa amefanya mambo makubwa sana na ameokoa maisha ya watanzania wengi sana kupitia wazo alilokuwa nalo .

🔨Sielewi kwanini hujatimiza ndoto zako wakati hata wewe hapo ulipo unafanyia kazi ndoto ya mtu .Beba mzigo wako ,Jifungue ndoto yako maana iko tayari.Unataka watu wakukumbuke kwa jambo gani uliloliacha Duniani k**a hutaki kutimiza ndoto yako ???

30/08/2016

👂🏾 *KUMBE TATIZO UNALOTAKA KULITATUA NALO LIMEJIPANGA😳*

Hebu k**a wewe ulisoma shule ya msingi enzi zile za Nyerere, Mwinyi au Mkapa tujikumbushe hadithi hii ambayo ina funzo kubwa sina uhakika wa enzi za Kikwete na sasa Maghufuli k**a hadithi hii inasomwa .Hadithi hii ni ile ya *Nani atamfunga Paka Kengele???* .Twende wote hapa chini na ujifunze kitu .

"Kulikuwa na duka Kubwa la Vyakula na Vinywaji katika mji. Panya Wengi waliishi katika duka hilo la vyakula na vinywaji. Chakula kilikuwa ni kingi sana kwa ajili yao. Walikula kila kitu na kuharibu mifuko yote ya vyakula. Waliharibu pia mikate, biskuti na matunda ya duka.

Mwenye duka alishikwa na wasiwasi kweli. Hivyo, yeye alipata wazo "mimi lazima ninunue paka na atakaa humu ndani ya hili duka. Kufanya hivo naweza kuokoa mambo yangu."

Alimnunua Paka mmoja mzuri, mkubwa na kisha kumwacha pale. Paka alikuwa na wakati mzuri wa kuwinda panya na kuwaua. Panya hawakuweza kuzunguka kwa uhuru sasa. Waliogopa kwamba wakati wowote paka ange wak**ata na kuwala.

Panya walitaka kufanya kitu fulani. Wakaitisha mkutano na wote wakasema "Ni lazima kujikwamua na paka. Je, kuna mtu ana maoni?"

Panya wote wameketi na kuogopa. panya mmoja mwelevu alisimama na akasema, "paka hutembea kwa upole. Hilo ni tatizo. K**a tunaweza kumfunga kengele kwenye shingo yake, basi mambo yatakuwa mazuri. Tunaweza kujua harakati zake zote ".

"Ndiyo, hilo ni jibu sahihi," walisema panya wote. panya wa miaka mingi alisimama polepole na akauliza, "Ni Nani atakaye Mfunga paka kengele? " Baada ya muda mchache hakukuwa na yeyote wa kujibu swali hili.:"

✍🏽Angalia wakati huyu Mwenye duka akiwa na mawazo ya kutatua tatizo ili aendelee na biashara yake kumbe adui yake mkubwa naye amejipanga asikamilishe azima yake .

✍🏽 *FUNZO*

*Wakati unapoingiwa na wazo la kufanya jambo fulani mazingira yanayokuzunguka huja na vipangamizi vya kutofanikisha mambo yako .Mazingira hayo yanaweza kuwa ni watu wasiotaka uendelee na kukurudisha nyuma*

*Wakati unatafuta kukamilisha ndoto zako na malengo yako wapo watu watakaa kikao kwa pamoja na kukufanya usifanikishe ndoto yako .Watatafuta mbinu za kukufunga kengele .Kengele ni maneno utakayoambiwa kuhusu kile unachowaza kukifanya na ukiyasikiliza utavunjika moyo sana na hutasonga mbele.*

*Wakati naendelea kuandika ghafla hapa nakumbuka hadithi ya Yusufu kwa wale Wakristo akitajwa kuwa moja ya watu na ndoto kubwa za kufanikiwa lakini ndugu zake nao wakaa kikao k**a walivyokaa panya ili Wamwangamize Yusufu .Nadhani Unakumbuka ilifika hatua akauzwa na hapa ni baada ya pona pona ya Kuchinjwa na ndugu zake wa Damu.Usingekuwa moyo dhabiti wa Yusufu asingeweza kufanikisha ndoto zake.*

*Daima siyo kitu rahisi kufanikisha kile unachowaza .Unapaswa kujua hata mazingira yamejipanga vizuri kabisa kuhakikisha kwamba hufanikishi kile ambacho umekipanga .Hivyo ili kukifikia lengo inahitaji ujenge uwezo mkubwa wa kuzalisha njia mbadala wa kulikabili Tatizo au Changamoto unayopitia*

12/07/2016

FAIDA YA KUWA NA THAMANI ENEO ULIPO

🌷Utapendwa na watu wengi utachukiwa na wachache maana kuna watu kazi yao ni kuwachukia wengine
🌷Utakuwa jasiri kuwashauri na kuwafundisha wengine
🌷Hutanyanyaswa kazini kwako na sehemu yoyote
🌷Utaheshimika na watu haijalishi una kipato gani au ukoje
🌷Uzao wako utaheshimika

11/07/2016

MASOMO MATATU

SOMO LA KWANZA.

Nilikuwa kanisani nikimsikiliza muhubiri mmoja maarufu, muhubiri alitoa mfukoni noti za shilingi elfu kumi kumi zilizokuwa na jumla ya Tsh laki moja, akauliza, "ni nani miongoni mwenu anataka nimpe hii laki moja?"

Watu wengi waliokuwa mle kanisani walinyosha mikono, kila mmoja alikuwa akishauti mimi! Mimi!. Nikaanza kushangaa ni nani atakuwa na bahati ya kupewa ile pesa kati ya mamia ya watu waliohudhuria ile ibada.

Pia nikajiuliza kwa nini (ambapo bila shaka na baadhi ya wahudhuriaji wengine nao walijiuliza) atoe kitita cha shilingi laki moja kirahisi rahisi hivyo.

Wakati watu wakiendelea kupiga kelele kusema nipe mimi, nipe mimi huku wamenyosha vidole vyao, kutokea nyuma akaibuka msichana mdogo mwenye umri k**a miaka 18 hivi, akaenda mbele kule aliko yule muhubiri akafika mbele na kuchukua ile laki moja kutoka mkononi mwa yule muhubiri.

"Safi sana, msichana! Umefanya vema," alisema yule muhubiri.
"Wengi wetu tunapenda kukaa tu na kusubiri mambo mazuri yaje yenyewe. Hii haitaweza kuwasaidia hata kidogo, unatakiwa kuinuka na kutafuta mafanikio. Mafanikio hayawezi kuja k**a umekaa tu.

Na maisha yetu ndivyo yalivyo, tunaziona fursa nyingi sana zikiwa zimetuzunguka, kila mtu anahitaji mambo mazuri. Ila tatizo hatutaki kusimama na kuzifuata hzo fursa. Simama sasa na ufanye kitu, usisubiri mafanikio huku umekaa, kamwe hayatakuja. Usijali kuhusu watu watasema nini. Chukua hatua.

SOMO LA PILI.

Baadae yule muhubiri akatoa tena noti ya shilingi 10000 na akainyanyua ili wote tuione. Nikafikiri anarudia k**a mwanzo tena. Lakini akauliza swali jepesi. "Noti hii inathamani gani?" Waumini wakajibu "shilingi elfu kumi". "Mko sahihi" akawajibu.

Akaichukua ile noti akaifinyanga finyanga na kuwauliza tena noti ile inathamani ya shilingi ngapi!? "shilingi elfu kumi" wakajibu wale wauminii!

Akaitupa chini ipe noti, akaikanyaga kanyaga sana, akaichukua na kuuluza tena noti hii ina thamani ya kiasi gani? "Shilingi elfu kumi" waumini walijibu vilevile.

Muhubiri akawaambia nataka muweka katika akili yenu hili, "mtu hata aichakaze, aikunje kunje na kuikanyaga noti ya fedha, thamani ya noti itabaki pale pale."

"Maisha yetu ndivyo yalivyo, tunatakiwa tuwe k**a noti ya shilingi elfu kumi. Ktk maisha kuna kipindi tutasalitiwa, tutakanyagwa, tutaonewa na kupigwa. Ila usiache thamani yako ipotee, kwa sababu mtu amekuumiza tu, hiyo haimaanishi ndio thamani yako imepotea. Wewe ni wa thamani mno jinsi ulivyo. Usiache thamani yako ipotee kwa sababu ya wachache!

SOMO LA MWISHO.

Njia tofauti, jibu moja.
2+5=7
6+1=7
3+4=7
7-0=7
7+0=7
9-2=7
8-1=7

Pointi yangu iko wapi?

Pointi yangu ni kwamba kuna njia nyingi za kufikia mafanikio yako. Mungu hawezi kukufikisha katika mafanikio yako labda k**a mama yako, baba yako, marafiki au ndugu walivyofanikiwa, kila mmoja hua na njia ya mafanikio tofauti Mungu aliyompangia.

Unaweza fikia mafanikio yako aitha kwa kuongeza watu katika maisha yako au kupunguza watu. "kujumlisha na kutoa" marafiki na baadhi ya vitu katika maisha yako kunaweza kusiwe kwa furaha kwa upande wako, ila Mungu ana makusudi yake.

Katika safari yako unaweza ukakumbana na kusalitiwa, kuumizwa kihisia, kuchekwa na kusimangwa! Acha kulia na futa machozi yako kila hali unayopitia ina makusudi yake. Mungu anakutengeneza uwe bora zaidi ya hivyo ulivyo.

Jibu langu ni jepesi tu

TUTAKUA K**A VILE MUNGU ALIVYOTUPANGIA TUWE!
Mwenyezi Mungu awabariki.

11/07/2016

Je unafanya nini pale ambapo hakuna mtu anaamini katika ndoto yako,malengo yako ama uwezo wako?

Sehemu muhimu itakayojulisha k**a utafanikiwa ama la ni jinsi utakavyokabiliana na wakati wa kukataliwa(How you handle rejection).Pengine ni kukataliwa kwenye kazi uliyoomba, tenda uliyoomba,mteja unayetaka kumuuzia kitu,mkopo,mahusiano,kukataliwa wazo lako n.k

Kila wakati kumbuka kuwa UNACHOFANYA baada ya Kukataliwa ni muhimu zaidi kuliko hata kukataliwa kwenyewe.Mambo ya Kuzingatia:

1)Usitafsiri kukataliwa kwako kumaanisha kuwa wewe ni mtu usiyeweza kufanikiwa tena,bado unayo nafasi ya kufanikiwa.

2)Tafuta jambo la Kujifunza katika kukataliwa kwako na uwe tayari kujaribu tena kwa mbinu mpya.

3)Usijenge chuki na Aliyekukatalia-amini kuwa kuna siku anaweza kutumika kuwa msaada kwa namna nyingine ama Mungu anataka kumtumia mwingine na sio lazima yeye.

See You At The Top.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

0752430851, 0657062046, E-mail Bensonseth30@gmail. Com
Dar Es Salaam