27/09/2022
KURA YA NDIO KWA MPAMBANAJI
AWADHI MOHAMED
We aim to improve the wellbeing of our comunity!
27/09/2022
KURA YA NDIO KWA MPAMBANAJI
AWADHI MOHAMED
05/10/2021
Mapenzi ya akina Baba hawavumi ila wamo.
21/06/2020
HERI YA SIKU YA WABABA WOTE DUNIANI.
14/06/2020
HAKI TANO MUHIMU ZA WATOTO WAKO.
Sheria ya Mtoto inamtafsiri mtoto k**a mtu mwenye umri chini ya miaka 18. Watoto ni sehemu muhimu ya jamii na ndiyo tegemeo la uendelevu wa taifa lolote, hivyo hawana budi kulelewa vizuri na kuendelezwa. Aidha, watoto wanayo mahitaji ya msingi ambayo kote Duniani yanatengeneza haki zao. Kimsingi haki za mtoto huwa ni wajibu wa mtu mzima kutimiza mahitaji ya mtoto ili awe mwenye afya, apate elimu na ashiriki katika ujenzi wa nchi yake sasa na hasa atakapokuwa mtu mzima.
Haki ya Kuishi. Hii inaanza pale mama anapopata ujauzito. Kukua vizuri kwa mimba kunategemea afya, lishe na mazingira anamoishi mama. Pia kuishi kwa mtoto baada ya kuzaliwa kunategemea upatikanaji wa mahitaji ya msingi, ambayo ni chakula cha kutosha na chenye ubora unaotakiwa, huduma bora za afya na ulinzi toka kwa wazazi, jamii na Serikali. Vifo vya watoto wadogo hutokana na ukosefu wa moja ya mahitaji tajwa hapo juu.
Haki ya Kuendelezwa. Kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Mtoto Tanzania, maendeleo ya mtoto yanahusiana na mtoto kuwa na kiwango kinachokidhi makuzi kimwili, kiakili, kiroho, kimaadili na kijamii. Ili mtoto aweze kukua vizuri anahitaji kutunzwa, kuongozwa na kulelewa katika misingi mizuri. Mathalani, kuendelezwa kwa mtoto kimwili ni kukua kimaumbile na uzito kwa uwiano wa umri. Hali hii inategemea lishe na huduma bora za afya ikiwemo kupatiwa chanjo zote muhimu na upatikanaji wa viinilishe vyote muhimu. Maendeleo ya mtoto yanahitaji jitihada toka kwa mzazi, jamii na Serikali kwa pamoja.
Haki ya Kulindwa. Inahusu kuzuia vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto katika hatua za ukuaji wao, kabla na baada ya kuzaliwa. Mathalani, mtoto anahitaji ulinzi dhidi ya kazi nzito zisizowiana na umri wake, kudhulumiwa mali hasa kwa watoto yatima, kutupwa au kutelekezwa na wazazi, utoaji mimba wa makusudi, kuonewa nk. Sera ya Maendeleo ya Mtoto Tanzania pia inasisitiza juu ya ulinzi dhidi ya unyanyasaji wa mtoto ikiwemo kukeketwa, kulazimisha kuolewa/kuoa katika umri mdogo, ubakaji, nk.
Haki ya Kushiriki. Ushiriki wa mtoto unapatikana pale mtoto anapopewa nafasi kikamilifu katika kutoa mawazo, kushiriki katika maamuzi ya masuala yanayohusu maendeleo yake, nk. katika hatua mbalimbali za ukuaji wake. Kitaalamu hatua za ushiriki wa mtoto huanza rasmi kuanzia umri wa miaka mitatu hadi anapokuwa mtu mzima. Misingi ya ushiriki wa mtoto huzingatia umri na aina ya masuala anayopaswa kushirikishwa.
Haki ya Kutobaguliwa. Ubaguzi wa mtoto umegawanyika katika makundi mbalimbali, katika yote yapo makundi makuu mawili. Ubaguzi wa kijinsia ambao mtoto wa k**e au wa kiume anaweza kubaguliwa na wazazi, walezi au jamii. Upo ubaguzi unaotokana na hali yake ya kimaisha k**a vile utajiri au umasikini, ulemavu, ugonjwa, uyatima na jinsi anavyoonekana mbele za watu. Mfano wa kuumiza ni ubaguzi wa kimfumo ambapo hapa kwetu takwimu zinaonyesha kwamba ni asilimia moja tu ya watoto wenye ulemavu wanoandikishwa kujiunga na elimu ya msingi. Hii inaathiriwa na mtazamo wa kijamii dhidi ya watoto hawa kwani wazazi huwafungia ndani kuficha aibu hivyo kuwanyima fursa ya kupata elimu.
Kwamba zile tunazodhani ni haki za watoto kumbe ni fursa za kulea kwetu wazazi. Uporomokaji wa maadili kote Duniani kumefanya mataifa kutiana vitanzi kuhakikisha watoto wanastawi kupitia mikataba na matamko mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na kwingineko. Yaani hata pamoja na kuwepo haki hizi bado wapo baadhi ya wazazi wanaodhani ni uzungu kumpatia mtoto mahitaji yake ili akue vizuri.
11/06/2020
JUMAMOSI HII FAHAMU ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA SHINIKIZO LA DAMU BP.
08/06/2020
TANGAZO
12/04/2020
SALAM ZA PASAKA.
Corona...
Taarifa Muhimu:
Namba za kupiga simu bure endapo utaona una dalili au utaona mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Korona
0800110124
0800110125
Namba hizi kupiga Ni bure hata k**a hauna salio kwenye simu yako.
DALILI ZA UGONJWA WA CORONA
Dalili zionekanazo mara kwa Mara:
• Homa
• Kikohozi kibichi
• Uhemaji wa tabu
• Maumivu ya mwili
• Kuuma kwa koo mfano wa
matonses (tonsillitis)
• Kukosa hamu ya kula
Dalili za mara chache:
• Kuhara
• Kutapika
• Kichwa kuuma
• Kukohoa damu
• Maumivu ya kifua
Nani hupatwa na korona?
• Watu wote (wak**e kwa kiume) waweza
kudhurika na korona
• Wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa Zaidi.
• Wazee pia wapo katika hatari kubwa kupatakorona kwani wana kingamwili hafifu.
KINGA:
• Kuosha mikono vizuri kwa maji safi na sabuni
• Tumia vikinga pua na mdomo (masks) ikiwa unahudumia washukiwa wa korona.
• Epuka kugusa na kurekebisha kikinga mdomo na pua (mask) na uso.
• Zingatia walau umbali wa futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona
• Hakuna chanjo mpaka sasa
Kirusi cha korona katika mwili wa
binadamu:
• Huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona (incubation perion)
• Huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au kugusana moja kwa moja.
• Epuka kusalimiana kwa mikono
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
23/03/2020
Zingatia.
21/03/2020
Corona
Kwengineko Duniani:
Hali Ni Mbaya Sana Italia..
- Idadi ya vifo imezidi ya China kwa watu 150
- Wachina sasa wameitwa kwenda kuwasaidia Waitalia
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, https://sverigesradio.se/sida/artikel.aspx?programid=83&artikel=7433896 hadi kufikia jana, ndani ya saa 24, watu 475 wamekufa kwa Corona Italia. Mji wa Lombadiet Kaskazini mwa Italia ndio ulioathirika zaidi.
Italia ndio nchi pekee ya dunia inayoongoza kwa sasa kwa idadi ya walioambukizwa na vifo. Hadi kufikia Machi 19 watu 3405 wamekufa. Ni sawa na watu 150 zaidi kwa idadi ya waliokufa China ambayo kwa sasa haina tena maambukizi mapya ya ndani ya nchi.
Asilimia 87 ya waliokufa Italia ni wazee wa zaidi ya miaka 70.
Shirika la Msalaba Mwekundu la China limeshatuma ndege Italia yenye vifaa tiba na madaktari mabingwa waliobobea kwenye janga la Corona.
Inasemwa Waitalia wamekuwa wakipuuzia maelekezo ya watalaam.
Nini tafsiri ya kinachotokea Italia kwa Afrika?
Tofauti na Italia, ambayo idadi ya wazee wake wote inatosha ukitawanya kwa nchi zote za Afrika Kusini ya Jangwa la Sahara, Afrika Kusini ya Sahara ikiwamo Tanzania, idadi kubwa ya watu wake ni vijana.
K**a Corona itasambaa zaidi Afrika Kusini ya Sahara ikiwamo Tanzania, basi, mbali ya wazee wetu wachache na watoto, tujihadhari zaidi na raia wetu wenye pia kuwa na maradhi mengine k**a vile Ukimwi, Kifua Kikuu na mengineyo yenye kupunguza kinga za mwilini. Hata k**a, Corona inaweza pia kuwa na madhara ya kusababisha vifo kwa vijana.
Maggid
23/01/2020
LEO DODOMA.
Mwenye kujua hii kesi ilifanyika wapi na k**a anawajua baba na mama wa huyu mtoto namba taarifa zao kwenye 0755 484866.