02/02/2026
TABIA YA MUNGU WA BIBLIA (Sehemu ya 1)
KDTC- Sunday Evening Discipleship Classes
Bamaga- Sinza, Dar es Salaam
01/02/2026.
Utangulizi
Kwa nini somo hili ni muhimu?
Ni muhimu kwa sababu watu wengi wana picha mbili kuhusu Mungu:
- Wakati mwingine wanamwona Mungu k**a mkali, mkatili, au “muuaji,”
- Halafu wakati mwingine wanamwona Mungu k**a mwema na mwenye upendo.
Lakini tabia ya Mungu haiwezi kuwa ya namna mbili zinazopingana kana kwamba ni “chemchemi moja” inayotoa maji baridi na maji machungu kwa wakati mmoja. Tunahitaji kumjua Mungu k**a alivyojifunua katika Maandiko, si k**a anavyosimuliwa na uvumi wa watu.
Jambo la msingi: Hatupimi tabia ya Mungu kwa matukio
Ni muhimu tukumbuke hili: tabia ya Mungu haipimwi kwa matukio yanayotuchanganya.
Badala yake, tunapima matukio kwa kuyachunguza kupitia tabia ya Mungu k**a alivyojifunua mwenyewe katika Biblia.
Kwa nini? Kwa sababu ukianza na maumivu na majanga, unaweza kumtengenezea Mungu taswira isiyo sahihi na kumfanya Mungu aonekane ni Mungu wa visasi, mwenye hasira kali, na katili. Ndiyo maana tunaanza kuchunguza maandiko tukitokea “Mwanzo kabisa” ili kupata msingi wa tabia yake.
Kwa nini tunaanza Mwanzo sura ya 1–2?
Kwa sababu Mwanzo 1–2 ndicho kipindi ambacho Biblia inaonyesha ulimwengu kabla ya anguko.
Kuanzia Mwanzo sura ya 3 mpaka mwisho wa Biblia, ulimwengu unakuwa tayari umeathiriwa na dhambi na juhudi za Mungu zinafanyika kudhibiti uovu huo. Hivyo, ili kumjua Mungu alivyo kwa msingi wake (alivyojifunua), tunaanza kwenye sura mbili za kwanza.
Lengo la mfululizo wa somo hili si kuibua utata, bali ni kujibu maswali ya misingi:
1. Mungu wa Biblia ni wa namna gani kabla dhambi haijaingia?
2. Mungu anajifunua vipi katika uumbaji?
3. Agano Jipya (kupitia Yesu Kristo) linasemaje kuhusu tabia ya Mungu?
4. Kwa nini ni hatari kuchukua matukio ya hukumu/adhabu pasipo kuyapima kwa msingi wa tabia ya Mungu (kwamba ndani yake hakuna giza)?
Kwa ufupi: tunahitaji kumrudisha Mungu kwenye nafasi yake ya awali—tuache Mungu wa uvumi wa masikio ya watu, tuje kwa Mungu anayejitanabaisha mwenyewe katika Maandiko.
Tutatumia maandiko ya “angano jipya” k**a kioo cha kufasiri zaidi Mwanzo 1-2 (Agano la Kale):
• Yohana 1:1–5
• Yakobo 1:13–17
• 1 Yohana 1:5
• Warumi 5:12 (k**a rejea ya muktadha wa dhambi na athari zake)
Tabia ya Mungu inavyoanza kujifunua
1) Mwanzo 1:1— Mungu yuko kabla ya kila kitu
“Mwanzo” inaanza kwa kutuonyesha Mungu k**a aliye nje ya uumbaji:
Mungu hakuumbwa; yeye ndiye Muumba. Hii inatuwekea msingi kwamba Mungu si sehemu ya mfumo wa ulimwengu (k**a nguvu nyingine ndani ya ulimwengu), bali yuko juu ya mfumo—ndiye aliyeusababisha kuwepo.
Hii ni muhimu kwa sababu inatusaidia kuelewa: ukisema “uovu unatoka kwa Mungu,” unahitaji ushahidi mzito sana—kwa kuwa Biblia inaanza kwa kumweka Mungu k**a chanzo cha uumbaji na uzima, si chanzo cha uharibifu.
2) Yohana 1:1–3— Uumbaji ulifanyika kwa Neno (Kristo)
- Agano Jipya linatusaidia kuelewa zaidi: uumbaji ulifanyika kwa Neno, na Neno huyo anatambulishwa baadaye kuwa Kristo. Hivyo, tunapomwona Mungu akiumba, hatumzungumzii Mungu wa mbali asiyejulikana bali tunamwona Mungu anayejifunua kikamilifu ndani ya Yesu.
3) Mwanzo 1:2–5 — Mungu huleta mpangilio, si vurugu
- Dunia inaelezewa k**a haijapangika; kisha Roho wa Mungu yupo juu yake. Hii inaonyesha kazi ya Mungu ni kuleta mpangilio, uzima, na uumbaji wenye kusudi.
Mungu anaposema, “Iwe nuru,” nuru inakuwa. Hapa tunaona tabia kuu tatu:
(i) Neno la Mungu ni lakuaminika.
Mungu anachokisema, kinatokea. Kauli yake siyakugeuka geuka; ni yenye mamlaka. Hii inatuonyesha Mungu wa kweli na wa kuaminiwa.
(ii) Mungu hutangaza mema, si uovu.
Mungu anaiona nuru kuwa njema. Hii inaweka msingi kwamba Mungu ni chanzo cha mema. Ndiyo maana Agano Jipya linasisitiza kuwa ndani yake hakuna giza.
(iii) Mungu ni muwazi: hutenganisha nuru na giza
Mungu anatenganisha nuru na giza—anaweka mipaka kwa kusudi. Hii inaonyesha Mungu si wa michanganyo, si wa udanganyifu; yeye ni muwazi na mnyoofu.
“Didactic theology” ni nini?
Didactic Theology ni theolojia ya kufundisha — inayolenga kueleza na kufundisha kwa mpangilio ukweli wa Mungu, ili waumini waelewe wanachoamini na kwa nini wanakiamini.
Kuna sehemu za Biblia zinazotoa fundisho la moja kwa moja (si simulizi tu). Mfano: 1 Yohana 1:5 inatoa msimamzo wa wazi kwamba Mungu ni nuru, wala giza hamna ndani yake kabisa.
Hilo ni fundisho la moja kwa moja (didactic)—linajenga msingi ambao tunautumia tunapokutana na simulizi ngumu baadaye.
Vivyo hivyo Yakobo 1:13–17 inasema, Mungu hashawishi mtu kutenda uovu; majaribu na kuvutwa kwenye dhambi hutokea pale mtu anapovutwa na tamaa zake mwenyewe.
Maana biblia iko wazi kuwa kila kilicho chema hutoka kwa Mungu.
4) Mwanzo 2:15–17 — Mungu ni mkarimu na mkweli
Mungu anamweka mwanadamu bustanini, anamwambia alime na kuitunza, na anampa ruhusa ya kula matunda ya miti ya bustani—isipokuwa mti mmoja.
Hapa tunaona:
1. Ukarimu wa Mungu: anampa mwanadamu mazingira, riziki, kazi, na nafasi ya kustawi.
2. Uwazi wa Mungu: onyo lake liko wazi—si la mtego.
3. Mipaka ni ulinzi: Mungu haweki mipaka kwa ubaya, bali kwa faida na uhai wa mwanadamu. Yakobo 1:13–15 inatusaidia kutuonesha: Mungu si mwenye kujaribiwa wala kujaribu kwa uovu; dhambi huanza mtu anapovutwa na tamaa zake, kisha tamaa ikikomaa huzaa dhambi na kisha dhambi huzaa mauti (matokeo ya kujitenga na uzima wa Mungu).
“Ndani yake hamna giza kwahiyo ukiona maneno k**a ‘Mungu akafanya’ yanahitaji kutafsiriwa kwa msingi wa tabia ya Mungu, si kwa matukio peke yake.”
Kanuni muhimu unayotakiwa kujua ni kwamba: “Mungu akafanya” haimaanishi “Mungu alitenda uovu”
Biblia mara nyingi hutumia lugha ya “Mungu akafanya” kuonyesha uongozi wa juu (sovereignty) wa Mungu juu ya historia—lakini kiini cha tabia yake kina baki palepale: Yeye ni nuru; ndani yake hamna giza (didactic theology). Hivyo, ili tusichafue tabia yake, tunahitaji kutambua kwamba “Mungu akafanya/amefanya” mara nyingi biblia imeandika kwa kuzingatia misingi mikuu mitatu (3):
1) Mungu anazuiya uovu (restraining evil)
- Hapa Mungu anadhibiti mipaka ya uovu ili usiende mbali kuliko kiwango anachoruhusu kwa hekima yake. Hii ni k**a “kizuizi/ukuta wa mipaka: Ni kweli Uovu upo duniani, lakini hauna uhuru wakufanya lolote; kuna “mipaka.”
Mfano:
• K**a moto: usipo dhibitiwa, unateketeza kila kitu. Ukiwekewa uzio, bado ni moto, lakini hauendi nje ya mipaka ulio wekewa. Hivyo ndivyo Mungu alikuwa akidhibiti uovu katika Agano la Kale.
2) Mungu anaruhusu / kuwaacha watu kwenye maamuzi yao (permission / giving over)
- Hapa Mungu haungi mkono uovu, bali anaacha mtu avune alichopanda—yaani, anaruhusu matokeo ya uchaguzi wa dhambi yatokee. Hii ndiyo maana ya “kuachwa” (God giving people over) si kwamba Mungu anafurahishwa na uovu, bali anaacha sheria ya “ulichopanda ndicho utavuna” ifanye kazi.
Kuna tofauti kati ya:
- Mungu kusababisha uovu (cause)
- Mungu kuruhusu uovu (permit)
3) Mungu anatekeleza hukumu ya haki (just judgment)
- Hapa Mungu anapinga uovu kwa hukumu, si kwa uovu. Hukumu ya Mungu ni sehemu ya haki yake—na hata hukumu hiyo, lazima ipimwe kwa msingi wa tabia yake: ni Mungu wa nuru, wa kweli, na wa haki.
Ni Muhimu kuzingatia: Hukumu si “giza ndani ya Mungu.” Hukumu ni mwanga unapolikabili giza.
*Unaweza jiuliza:* kwa nini hii ni muhimu sana kwenye Agano la Kale?
K**a nilivyo sema awali kwamba lengo si kubishana, bali kujenga msingi wa kujua tabia ya Mungu kutoka Mwanzo 1–2, halafu ndipo tuje kwenye maeneo magumu (mapigo, vita, vifo, hukumu), tukiyatafsiri kwa
“jicho la Agano Jipya.”
Kwa hiyo unapokutana na simulizi (narrative) k**a:
- “Mungu akapiga…”
- “Mungu akaua…”
- “Mungu akaleta…”
Jiulize kwanza
Haya ni maswali makuu ma tano(5) unayoweza kutumia kuchuja tafsiri (interpretation filters)
1. Je? Huu ni msimamo wa moja kwa moja (didactic) au ni simulizi (narrative)?
- Didactic: inasema wazi tabia ya Mungu (mf. “Mungu ni nuru…”).
- Simulizi(Narrative): inasimulia tukio; si kila sentensi ni “fundisho la moja kwa moja.”
2. Ni katika kundi lipi kati ya haya matatu(3) Je? Analo tenda
- Anazuiya uovu?
- Anaruhusu/kuwaacha?
- Anatekeleza hukumu ya haki?
3. Ni nini kilitangulia kabla ya tukio?
Mungu mara nyingi hutoa:
- onyo,
- muda,
- wito wa toba,
- uvumilivu,
kisha hukumu huja mwisho, si mwanzo.
Tukutane jpili ijayo kwa mwendelezo wa Somo.
K**a ungependa kujiunga na madarasa haya waweza Jisajili hapa 👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
https://forms.gle/Hgnppy3rN3JMHxkp8

21/01/2026
02/01/2026
18/12/2025
15/12/2025
07/12/2025
17/10/2025