Kingdom Descipleship Training Center

Kingdom Descipleship Training Center

Share

We build you to become the agent of change as the Christ ambassador on this world.

02/02/2026

TABIA YA MUNGU WA BIBLIA (Sehemu ya 1)

KDTC- Sunday Evening Discipleship Classes
Bamaga- Sinza, Dar es Salaam
01/02/2026.

Utangulizi

Kwa nini somo hili ni muhimu?

Ni muhimu kwa sababu watu wengi wana picha mbili kuhusu Mungu:
- Wakati mwingine wanamwona Mungu k**a mkali, mkatili, au “muuaji,”
- Halafu wakati mwingine wanamwona Mungu k**a mwema na mwenye upendo.

Lakini tabia ya Mungu haiwezi kuwa ya namna mbili zinazopingana kana kwamba ni “chemchemi moja” inayotoa maji baridi na maji machungu kwa wakati mmoja. Tunahitaji kumjua Mungu k**a alivyojifunua katika Maandiko, si k**a anavyosimuliwa na uvumi wa watu.

Jambo la msingi: Hatupimi tabia ya Mungu kwa matukio

Ni muhimu tukumbuke hili: tabia ya Mungu haipimwi kwa matukio yanayotuchanganya.
Badala yake, tunapima matukio kwa kuyachunguza kupitia tabia ya Mungu k**a alivyojifunua mwenyewe katika Biblia.

Kwa nini? Kwa sababu ukianza na maumivu na majanga, unaweza kumtengenezea Mungu taswira isiyo sahihi na kumfanya Mungu aonekane ni Mungu wa visasi, mwenye hasira kali, na katili. Ndiyo maana tunaanza kuchunguza maandiko tukitokea “Mwanzo kabisa” ili kupata msingi wa tabia yake.

Kwa nini tunaanza Mwanzo sura ya 1–2?

Kwa sababu Mwanzo 1–2 ndicho kipindi ambacho Biblia inaonyesha ulimwengu kabla ya anguko.

Kuanzia Mwanzo sura ya 3 mpaka mwisho wa Biblia, ulimwengu unakuwa tayari umeathiriwa na dhambi na juhudi za Mungu zinafanyika kudhibiti uovu huo. Hivyo, ili kumjua Mungu alivyo kwa msingi wake (alivyojifunua), tunaanza kwenye sura mbili za kwanza.

Lengo la mfululizo wa somo hili si kuibua utata, bali ni kujibu maswali ya misingi:

1. Mungu wa Biblia ni wa namna gani kabla dhambi haijaingia?
2. Mungu anajifunua vipi katika uumbaji?
3. Agano Jipya (kupitia Yesu Kristo) linasemaje kuhusu tabia ya Mungu?
4. Kwa nini ni hatari kuchukua matukio ya hukumu/adhabu pasipo kuyapima kwa msingi wa tabia ya Mungu (kwamba ndani yake hakuna giza)?

Kwa ufupi: tunahitaji kumrudisha Mungu kwenye nafasi yake ya awali—tuache Mungu wa uvumi wa masikio ya watu, tuje kwa Mungu anayejitanabaisha mwenyewe katika Maandiko.

Tutatumia maandiko ya “angano jipya” k**a kioo cha kufasiri zaidi Mwanzo 1-2 (Agano la Kale):
• Yohana 1:1–5
• Yakobo 1:13–17
• 1 Yohana 1:5
• Warumi 5:12 (k**a rejea ya muktadha wa dhambi na athari zake)

Tabia ya Mungu inavyoanza kujifunua

1) Mwanzo 1:1— Mungu yuko kabla ya kila kitu
“Mwanzo” inaanza kwa kutuonyesha Mungu k**a aliye nje ya uumbaji:
Mungu hakuumbwa; yeye ndiye Muumba. Hii inatuwekea msingi kwamba Mungu si sehemu ya mfumo wa ulimwengu (k**a nguvu nyingine ndani ya ulimwengu), bali yuko juu ya mfumo—ndiye aliyeusababisha kuwepo.

Hii ni muhimu kwa sababu inatusaidia kuelewa: ukisema “uovu unatoka kwa Mungu,” unahitaji ushahidi mzito sana—kwa kuwa Biblia inaanza kwa kumweka Mungu k**a chanzo cha uumbaji na uzima, si chanzo cha uharibifu.

2) Yohana 1:1–3— Uumbaji ulifanyika kwa Neno (Kristo)

- Agano Jipya linatusaidia kuelewa zaidi: uumbaji ulifanyika kwa Neno, na Neno huyo anatambulishwa baadaye kuwa Kristo. Hivyo, tunapomwona Mungu akiumba, hatumzungumzii Mungu wa mbali asiyejulikana bali tunamwona Mungu anayejifunua kikamilifu ndani ya Yesu.

3) Mwanzo 1:2–5 — Mungu huleta mpangilio, si vurugu
- Dunia inaelezewa k**a haijapangika; kisha Roho wa Mungu yupo juu yake. Hii inaonyesha kazi ya Mungu ni kuleta mpangilio, uzima, na uumbaji wenye kusudi.

Mungu anaposema, “Iwe nuru,” nuru inakuwa. Hapa tunaona tabia kuu tatu:

(i) Neno la Mungu ni lakuaminika.

Mungu anachokisema, kinatokea. Kauli yake siyakugeuka geuka; ni yenye mamlaka. Hii inatuonyesha Mungu wa kweli na wa kuaminiwa.

(ii) Mungu hutangaza mema, si uovu.

Mungu anaiona nuru kuwa njema. Hii inaweka msingi kwamba Mungu ni chanzo cha mema. Ndiyo maana Agano Jipya linasisitiza kuwa ndani yake hakuna giza.

(iii) Mungu ni muwazi: hutenganisha nuru na giza
Mungu anatenganisha nuru na giza—anaweka mipaka kwa kusudi. Hii inaonyesha Mungu si wa michanganyo, si wa udanganyifu; yeye ni muwazi na mnyoofu.

“Didactic theology” ni nini?

Didactic Theology ni theolojia ya kufundisha — inayolenga kueleza na kufundisha kwa mpangilio ukweli wa Mungu, ili waumini waelewe wanachoamini na kwa nini wanakiamini.

Kuna sehemu za Biblia zinazotoa fundisho la moja kwa moja (si simulizi tu). Mfano: 1 Yohana 1:5 inatoa msimamzo wa wazi kwamba Mungu ni nuru, wala giza hamna ndani yake kabisa.

Hilo ni fundisho la moja kwa moja (didactic)—linajenga msingi ambao tunautumia tunapokutana na simulizi ngumu baadaye.

Vivyo hivyo Yakobo 1:13–17 inasema, Mungu hashawishi mtu kutenda uovu; majaribu na kuvutwa kwenye dhambi hutokea pale mtu anapovutwa na tamaa zake mwenyewe.

Maana biblia iko wazi kuwa kila kilicho chema hutoka kwa Mungu.

4) Mwanzo 2:15–17 — Mungu ni mkarimu na mkweli
Mungu anamweka mwanadamu bustanini, anamwambia alime na kuitunza, na anampa ruhusa ya kula matunda ya miti ya bustani—isipokuwa mti mmoja.

Hapa tunaona:

1. Ukarimu wa Mungu: anampa mwanadamu mazingira, riziki, kazi, na nafasi ya kustawi.
2. Uwazi wa Mungu: onyo lake liko wazi—si la mtego.
3. Mipaka ni ulinzi: Mungu haweki mipaka kwa ubaya, bali kwa faida na uhai wa mwanadamu. Yakobo 1:13–15 inatusaidia kutuonesha: Mungu si mwenye kujaribiwa wala kujaribu kwa uovu; dhambi huanza mtu anapovutwa na tamaa zake, kisha tamaa ikikomaa huzaa dhambi na kisha dhambi huzaa mauti (matokeo ya kujitenga na uzima wa Mungu).

“Ndani yake hamna giza kwahiyo ukiona maneno k**a ‘Mungu akafanya’ yanahitaji kutafsiriwa kwa msingi wa tabia ya Mungu, si kwa matukio peke yake.”
Kanuni muhimu unayotakiwa kujua ni kwamba: “Mungu akafanya” haimaanishi “Mungu alitenda uovu”

Biblia mara nyingi hutumia lugha ya “Mungu akafanya” kuonyesha uongozi wa juu (sovereignty) wa Mungu juu ya historia—lakini kiini cha tabia yake kina baki palepale: Yeye ni nuru; ndani yake hamna giza (didactic theology). Hivyo, ili tusichafue tabia yake, tunahitaji kutambua kwamba “Mungu akafanya/amefanya” mara nyingi biblia imeandika kwa kuzingatia misingi mikuu mitatu (3):

1) Mungu anazuiya uovu (restraining evil)
- Hapa Mungu anadhibiti mipaka ya uovu ili usiende mbali kuliko kiwango anachoruhusu kwa hekima yake. Hii ni k**a “kizuizi/ukuta wa mipaka: Ni kweli Uovu upo duniani, lakini hauna uhuru wakufanya lolote; kuna “mipaka.”

Mfano:
• K**a moto: usipo dhibitiwa, unateketeza kila kitu. Ukiwekewa uzio, bado ni moto, lakini hauendi nje ya mipaka ulio wekewa. Hivyo ndivyo Mungu alikuwa akidhibiti uovu katika Agano la Kale.

2) Mungu anaruhusu / kuwaacha watu kwenye maamuzi yao (permission / giving over)
- Hapa Mungu haungi mkono uovu, bali anaacha mtu avune alichopanda—yaani, anaruhusu matokeo ya uchaguzi wa dhambi yatokee. Hii ndiyo maana ya “kuachwa” (God giving people over) si kwamba Mungu anafurahishwa na uovu, bali anaacha sheria ya “ulichopanda ndicho utavuna” ifanye kazi.

Kuna tofauti kati ya:
- Mungu kusababisha uovu (cause)
- Mungu kuruhusu uovu (permit)

3) Mungu anatekeleza hukumu ya haki (just judgment)
- Hapa Mungu anapinga uovu kwa hukumu, si kwa uovu. Hukumu ya Mungu ni sehemu ya haki yake—na hata hukumu hiyo, lazima ipimwe kwa msingi wa tabia yake: ni Mungu wa nuru, wa kweli, na wa haki.

Ni Muhimu kuzingatia: Hukumu si “giza ndani ya Mungu.” Hukumu ni mwanga unapolikabili giza.

*Unaweza jiuliza:* kwa nini hii ni muhimu sana kwenye Agano la Kale?

K**a nilivyo sema awali kwamba lengo si kubishana, bali kujenga msingi wa kujua tabia ya Mungu kutoka Mwanzo 1–2, halafu ndipo tuje kwenye maeneo magumu (mapigo, vita, vifo, hukumu), tukiyatafsiri kwa
“jicho la Agano Jipya.”

Kwa hiyo unapokutana na simulizi (narrative) k**a:
- “Mungu akapiga…”
- “Mungu akaua…”
- “Mungu akaleta…”
Jiulize kwanza

Haya ni maswali makuu ma tano(5) unayoweza kutumia kuchuja tafsiri (interpretation filters)

1. Je? Huu ni msimamo wa moja kwa moja (didactic) au ni simulizi (narrative)?
- Didactic: inasema wazi tabia ya Mungu (mf. “Mungu ni nuru…”).
- Simulizi(Narrative): inasimulia tukio; si kila sentensi ni “fundisho la moja kwa moja.”

2. Ni katika kundi lipi kati ya haya matatu(3) Je? Analo tenda
- Anazuiya uovu?
- Anaruhusu/kuwaacha?
- Anatekeleza hukumu ya haki?
3. Ni nini kilitangulia kabla ya tukio?
Mungu mara nyingi hutoa:
- onyo,
- muda,
- wito wa toba,
- uvumilivu,
kisha hukumu huja mwisho, si mwanzo.

Tukutane jpili ijayo kwa mwendelezo wa Somo.

K**a ungependa kujiunga na madarasa haya waweza Jisajili hapa 👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

https://forms.gle/Hgnppy3rN3JMHxkp8

21/01/2026

🔹 Uzima wa milele hauanzii mbinguni — uko ndani ya Kristo

📖 Yohana 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”
👉 Biblia haisemi: “Uzima wa milele ni kwenda mbinguni”
👉 Inasema: Uzima wa milele ni kumjua Kristo
Na Kristo anaishi ndani ya waamini.
🔹 Kristo yuko ndani yetu — na sisi ndani yake
📖 Yohana 15:4
“Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu.”
📖 Wakolosai 1:27
“Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.”
👉 K**a Kristo ndiye uzima wa milele
👉 Na Kristo yuko ndani yetu
➡️ Uzima wa milele tayari unaanza sasa
🔹 Mbinguni si eneo tu — ni hali ya uzima wa Mungu.

Watu wengi hudhani:
“Mbinguni ni mahali tunaenda baada ya kufa”
Lakini Biblia inafundisha tofauti kabisa:
- Mbinguni = ufalme wa Mungu
- Ufalme wa Mungu = utawala wa Mungu
- Utawala wa Mungu = ndani ya Kristo
📖 Luka 17:21

“Ufalme wa Mungu uko ndani yenu.”
👉 kwa sababu hiyo tukisema:
“Mbingu iko ndani ya Yesu”
ni sahihi kiroho, kwa sababu:
- Ndani yake kuna uzima
- Ndani yake kuna umilele
- Ndani yake kuna Mungu mwenyewe
🔹 Biblia inasema wazi: Uzima uko NDANI ya Yesu
📖 1 Yohana 5:11–12
“Mungu ametupa uzima wa milele; nao uzima huu umo katika Mwana. Yeye aliye na Mwana anao uzima.”
👉 Hajasema “atakayekuwa naye”
👉 Amesema “aliye naye” (sasa).

02/01/2026

🌿 Habari njema kwa wote:

Mafundisho ya Neno la Kristo na Uanafunzi

Kwa unyenyekevu na upendo wa Kristo, tunawakaribisha watu wote wanaotamani kulisikia, kulielewa na kuishi Neno la Mungu kwa usahihi.

Mafundisho haya hayana msimamo wa dini wala dhehebu, bali yanalenga kujifunza Neno la Mungu kwa uaminifu kwa kuchambua Maandiko, ili kila anayejifunza ajengwe ndani ya Kristo na akue katika uanafunzi wa kweli.

Baada ya kukamilisha mfululizo wa Safari ya Kugundua Kusudi,
sasa tunaendelea na Mafunzo ya Uanafunzi yanayoendeshwa kila Jumapili jioni.

Mafundisho haya yanawahusu waumini, na wote wenye Wito wa kutumikia kusudi la Mungu katika nafasi ya uchungaji, ualimu, Utume, uinjilisti na viongozi wa nafasi mbalimbali.

Njoo Tujifunze pamoja, tujengwe pamoja, hadi “Kristo aumbike ndani yetu” (Wagalatia 4:19).

18/12/2025

Ukoloni wa Kiroho haukufungi kwa minyororo — hukufunga kwa mafundisho.

Tatizo siyo Injili, tatizo ni Injili iliyochanganywa.
Sheria + Neema vimeunda agano bandia linalozalisha waumini waliotekwa, wanaoamini wokovu wao bado “haujakamilika”.
Lakini Yesu hakukuokoa nusu, na Mungu hakukuokoa ili uendelee kununua baraka.

Ukipandwa hofu badala ya imani, umeingia kwenye himaya ya ukoloni wa kiroho.
Unapodhibitiwa kwa laana, sadaka za kulazimishwa, na hofu ya kupoteza wokovu, huongozwi tena na Roho — unaendeshwa na mfumo.
Kanisa linaweza kujaa watu, lakini likawa tupu wa ukweli.

Neema + Ukweli humzalisha mwana aliye huru;
lakini sheria iliyochanganywa na neema humrudisha muumini utumwani.
K**a bado unaambiwa “bado hujafika”, jiulize: nani anafaidika?

Yesu alikufanya huru.
Swali ni hili: nani alikurudisha chini ya utumwa wa kiroho?

📘 Ukoloni wa Kiroho
Soma. Elewa. Uwe huru

Kupata Nakala yako WhatsApp 0743119699 au Piga 0617387825

15/12/2025

Ndani ya Ukoloni wa Kiroho utajifunza kuhusu kile tunachokiita “Agano la Tatu Feki”—mfumo wa mafundisho unaotumiwa na wakoloni wa kiroho kuiteka nafsi ya mwamini.

Mfumo huu haupo kwenye Biblia. Unachukua 50% ya Agano la Kale (sheria) na 50% ya Agano Jipya (Neema), kisha kuvichanganya na kuunda agano jipya lisilokuwepo, lenye lengo moja:
- kukunyima uhakika wa wokovu
- kukuondolea uhuru wako katika Kristo, na
- kukufanya uamini kwamba wokovu haujakamilika.

Kupitia udanganyifu huu:

- Baraka zinauzwa badala ya kutolewa kwa neema

- Ufunguo wa uhuru unabadilishwa na hofu

- Na mbaya zaidi, mbingu inageuzwa bidhaa ya kununua

Hii si Injili ya Kristo—ni mfumo wa udhibiti wa kiroho.

👉 Pata nakala yako ya Ukoloni wa Kiroho ujifunze kwa kina, upate ufahamu, na urudishe uhuru wako katika Kristo.

Piga 0617387825 au WhatsApp 0743119699.

Photos from Kingdom Descipleship Training Center's post 07/12/2025

Ufafanuzi wa Dhana ya Ukoloni wa Kiroho

Ukoloni wa kiroho ni mfumo wa udhibiti uliofichika, unaoonekana k**a huduma ya kiroho, ingawa kwa hakika ni utumwa wa kiroho. Tofauti na manyanyaso ya wazi yenye ukatili au uonevu wa moja kwa moja, ukoloni wa kiroho hufanya kazi kimyakimya, kwa kutumia ushawishi wa maneno na mamlaka ya kidini, na mara nyingi, hufichwa kwa maneno ya kiimani. Viongozi wengi wa kiroho katika zama hizi wanatumia vibaya mamlaka waliyopewa, kwani hawayatumii tena mamlaka kwa lengo la kuwezesha ukuaji wa kiroho wa waumini, bali kwa ajili ya kujenga hofu, hatia, na utegemezi, ili kuhakikisha kwamba waumini wanabaki wanyenyekevu kupita kiasi na rahisi kudhibitiwa, huku yote yakifanywa chini ya kivuli cha kutunza nidhamu na “utaratibu wa kiroho.”

K**a ulivyo ukoloni wa kisiasa ambao hauishii tu kwenye majeshi na uvamizi, bali huhusisha pia lugha, elimu, tamaduni, na uchumi, vivyo hivyo ukoloni wa kiroho hauishii tu katika udanganyifu wa mtu binafsi. Ni mfumo wa kijumla unaopotosha Injili, unaoathiri mioyo, akili, na rasilimali za waumini. Wakati wakoloni wa kisiasa walichukua ardhi na utajiri, wakoloni wa kiroho hunyang’anya imani, utambulisho, na mali. Zaidi ya fedha au mamlaka, ukoloni wa kiroho hubadilisha namna mtu anavyojiona ndani ya Kristo, hadi anapoanza kuamini kuwa hajakamilika bila kupitia kwa kiongozi wa kidini.

Katika mizizi yake, ukoloni wa kiroho hubadilisha mamlaka ya Kristo na kuweka udhibiti wa kibinadamu. Badala ya kuwaongoza waumini wakikaribie kiti cha neema, ambapo Waebrania 4:16 inatuhimiza “kumkaribia Mungu kwa ujasiri”, mifumo hii hujenga fikra kwamba neema hiyo ni ya wachache tu walioteuliwa. Taratibu, ujumbe wa neema unabadilishwa kuwa mafundisho ya hofu, hatia, na wajibu mzito. Safari ya ufuasi wa Kristo unaanza kubadilika kutoka kuwa mchakato wa kubadilishwa ndani ya Kristo hadi kuwa mzunguko wa kutii kanuni na matarajio ya wanadamu.

Kufanana kwa ukoloni wa kisiasa na ule wa kiroho kuko wazi. Ukoloni wa kisiasa uliwafanya watu waumini kwamba hawawezi kujitawala bila nguvu za nje; vivyo hivyo, ukoloni wa kiroho unawafanya waumini waumini kwamba hawawezi kumsikia Mungu bila wapatanishi, hawawezi kufanikiwa bila kibali cha kiongozi, na hawawezi kuwa wauminifu bila kutii mfumo maalumu wa kidini. Katika hali zote mbili, utegemezi huo hauji kwa bahati mbaya bali unafanywa kwa makusudi kabisa. Matokeo yake, uhuru ulionunuliwa kwa damu ya Kristo unabaki wa kufikirika tu, huku waumini wakiishi kwa woga wa kukataliwa kiroho au kuadhibiwa na Mungu.

Udanganyifu huu mara nyingi hujificha katika dhana za kiroho k**a “ulinzi wa kiroho,” “utii kwa viongozi,” au “kupanda mbegu ya imani.” Ingawa maneno haya yanaonekana kuwa ya Kibiblia na yenye uhalali wa kiimani, mara nyingi hufasiriwa upya ili kuhalalisha udhibiti, kunyamazisha wapinzani, na kulinda mamlaka ya viongozi wanaotaka kutawala mioyo ya watu. Chini ya lugha ya imani, hujificha mfumo unaolenga si kulea makuzi ya kiroho, bali kudhibiti; si kuendeleza ukomavu wa kiimani, bali kuimarisha utegemezi wa kudumu.
Jambo la kusikitisha ni kwamba waumini wengi huchanganya mifumo hii ya udanganyifu na ufuasi wa kweli wa Kristo. Wakiwa na nia njema ya kutii, wanajikuta wametoa uhuru wao wa kiroho na kuingia taratibu katika minyororo ya utumwa wa kidini.

Mtume Paulo aliona hatari hii mapema na akalionya kanisa la Korintho kwa kusema:
“Lakini nina hofu kuwa, k**a vile Hawa alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Kristo...” (2 Wakorintho 11:3 NENO)
Wasiwasi wa Paulo haukuwa juu ya uasi wa moja kwa moja, bali juu ya udanganyifu usio wa moja kwa moja—kupoteza umakini kwa Kristo huku mtu akidhani bado anamfuata kwa uaminifu. Hatari hiyohiyo ipo hata kwa waumini wa leo, wanapochanganya udhibiti wa kibinadamu na uongozi waki Mungu.

Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Basi, simameni imara wala msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa..” (Wagalatia 5:1 BHN)
Kujisalimisha kwa ukoloni wa kiroho maana yake nikubadilisha kazi halisi na kamili ya Kristo na kujiweka chini ya aina nyingine ya utumwa wa kidini—utumwa unaoonekana kuwa mtakatifu, lakini unaopunguza nguvu na maana ya msalaba. Kinachoanza k**a utiifu kwa viongozi kinageuka kuwa minyororo ya kiroho; kinachoanza k**a heshima kinageuka kuwa woga; na kinachoanza k**a imani kinabadilishwa kuwa chombo cha udanganyifu.

Mpaka kufika mwisho wa sura hii, utaona jinsi mfumo wa ukoloni wa kiroho unavyotoa mtazamo mpana wa kufichua aina za udhibiti unaoendelea kanisani leo. Utajifunza kutambua mbinu zinazotumiwa na wakoloni wa kiroho—k**a vile kudhoofisha utambulisho wa waumini, kuunda utegemezi kwa viongozi, na kutumia rasilimali za watu kwa manufaa binafsi. Zaidi ya yote, utagundua namna ya kurejesha uhuru wako halisi ndani ya Kristo.

Zaidi ya hayo, Injili inatupatia njia mbadala wenye uzima: uhuru, heshima, na ukomavu ndani ya Kristo. Ufuasi wa kweli hauwezi kumfanya mtu kuwa mtumwa, bali humfanya awe huru na mwenye nguvu. Unahamisha utegemezi kutoka kwa wanadamu kwenda kwa Kristo pekee. Lengo langu si kufichua uovu, bali kufunua ukweli unaoweka huru—kwa maana Kristo yule anayetuokoa ndiye huyo huyo anakualika uishi katika uhuru, ukamilifu, na ukomavu wa kweli ndani Yake.

Kutoka Ukoloni wa Kisiasa hadi Ukoloni wa Kiroho
Unaposikia neno ukoloni, pengine akili yako inakwenda moja kwa moja kwenye picha za mataifa ya kigeni yakivamia nchi nyingine, yakinyakua ardhi, kuandika upya sheria, na kubadilisha mifumo ya kijamii. Lakini kwa undani, ukoloni haukuhusu tu majeshi au vita – ulikuwa ni udhibiti wa kimfumo. Wakoloni walitumia lugha, elimu, dini, na utamaduni wao k**a silaha za utawala, huku wakinyonya maliasilia na nguvukazi za watawaliwa. Walijenga kwa makusudi hali ya kujiona kutofaa kwa wenyeji, wakishawishi mataifa waumini kwamba hawawezi kujitawala. Utegemezi haukujitokeza kwa bahati mbaya – uliundwa kikamilifu. Uhuru ulifanywa uonekane ni mgumu na jambo lisilofikirika.

Mbinu hizohizo ziko ndani ya makanisa leo. Ukoloni wa kiroho unaakisi ukoloni wa kisiasa, isipokuwa uwanja wa vita ni nafsi yako. Badala ya kutumia jeshi, viongozi hutumia hofu, hatia, unyanyasaji wa kiimani, na tafsiri potofu za maandiko k**a silaha za kiroho. Badala ya kuandika upya sheria za kiraia, viongozi huandika upya matarajio ya kiroho – wakifundisha kwamba huwezi kumfikia Mungu bila baraka, kibali, au “ulinzi wa kiroho” kutoka kwao. Utegemezi huo si wa bahati mbaya; unapandikizwa makusudi ili waumini wabaki watiifu, wanyonge, na rahisi kudhibitiwa.

K**a vile wakoloni wa kisiasa walivyopora heshima na haki ya kujitawala kwa mataifa, vivyo hivyo wakoloni wa kiroho wanalenga kupora ujasiri na uhuru wako ndani ya Kristo. Hata hivyo, Biblia inasema: “Tukikaribie kiti cha enzi cha neema kwa ujasiri” (Waebrania 4:16). Lakini, chini ya utawala wa kiroho, ukweli huu unafichwa. Unaaminishwa kwamba wewe ni dhaifu, mwenye dhambi sana, na huna ukomavu wa kutosha wa kumkaribia Mungu wewe mwenyewe. Badala ya kusaidia watu wakue kiimani, mifumo hiyo hujenga utegemezi wa kudumu – ambapo kila sala, kila baraka, na kila uamuzi lazima upitie kwa kiongozi.

Ufanano wa ukoloni wa kisiasa na huu wa kiroho hauishii tu hapo. Mathalani, ukoloni wa kisiasa uliwatajirisha wachache na kuwaacha wengi katika umasikini na mateso. Vivyo hivyo, ukoloni wa kiroho unawafanya viongozi wachache waishi kwa anasa – wanaishi katika majumba makubwa, magari ya kifahari, na fahari za kidunia – huku washirika wakihangaika kuwalipia kodi, kuwanunulia chakula, au kusomesha watoto wao. Wakoloni wa kisiasa walihalalisha unyonyaji kwa kisingizio cha “kuleta ustaarabu”; wakoloni wa kiroho wanahalalisha unyonyaji kwa kisingizio cha “kupanda mbegu ya imani” au “kuheshimu upako.”
Kilicho hatari zaidi ni kujificha kwao katika kivuli cha kiroho. Wakoloni wa kisiasa walidai wanasaidia mataifa wakati kwa kweli walikuwa wanawapora uhuru wao. Vivyo hivyo, wakoloni wa kiroho wanadai kwamba wanakuchunga na kukulinda, ilihali wanakufunga kwenye kifungo cha woga, hatia, na utegemezi. Ndiyo maana onyo la Paulo kwa Wagalatia linaendelea kuwa la msingi kwa kizazi chetu:

Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Basi, simameni imara wala msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa...” (Wagalatia 5:1 BHN)
Ukoloni wa kiroho hauko tu katika dosari za uongozi au matumizi mabaya ya mamlaka—ni Injili bandia. Inakufunga badala ya kukuweka huru, inakunyonya badala ya kukuwezesha, na inainua mamlaka ya kibinadamu huku ikididimiza utawala wa Kristo.

Ni mfumo wa uonevu uliojificha katika lugha ya kiroho. K**a vile ukoloni wa kisiasa ulivyopingwa, vivyo hivyo lazima ujifunze kuutambua ukoloni wa kiroho jinsi ulivyo kwamba ni wa kinyanyasaji uliofungwa katika lugha ya kidini. Hadi hapo ndipo utaweza kuukataa ukoloni wa kiroho kwa kweli ya Injili. Jinsi neno “Ukoloni” Linavyoeleza Vyema Matumizi Mabaya ya Imani
Huenda ukajiuliza, “Kwa nini nimetumia neno ukoloni? Je, hili si tatizo la matumizi mabaya ya imani tu?” Jibu ni dhahiri: ukoloni si tendo la unyanyasaji au matumizi mabaya pekee, bali ni mfumo uliobuniwa kwa makusudi—mfumo wenye mikakati, unaotegemea miundombinu mahsusi inayolenga kukuweka kifungoni bila wewe kujua. Nimetumia neno hili kwa sababu linafafanua vyema jinsi ambavyo baadhi ya mazingira ya makanisa yameundwa si kwa kusudi la kulea na kukuza, bali la kutawala, kuteka na kutiisha; ili uongozeke kirahisi na kutekeleza kila agizo bila kuhoji uhalali wake kibiblia.

Ukoloni siku zote unaanza na udanganyifu. “Huwezi kuishi bila sisi.” Katika historia ya siasa, mataifa yaliambiwa kwamba hayawezi kustawi bila “ustaarabu” wa wakoloni wao. Vivyo hivyo, ndani ya kanisa unaambiwa kwamba huwezi kumfikia Mungu bila maombi, ruhusa, au baraka ya kiongozi wa kiroho. Matokeo yake ni sawa tu na ule ukoloni wa kisiasa—heshima, uwezo wa kuamua, na uhuru wa kiroho unaporwa kabisa.

Neno “ukoloni” linafichua namna rasilimali zako zinavyotumiwa vibaya. K**a vile wakoloni wa kisiasa walivyopora ardhi, madini, na nguvukazi kwa manufaa yao, vivyo hivyo wakoloni wa kiroho wanavuna zaka, sadaka, na “malimbuko” yako kwa manufaa yao binafsi. Kadiri unavyotoa, ndivyo mfumo unavyodai zaidi. Utajiri unatiririka kutoka chini kwenda juu siku zote, huku wewe ukibaki katika mzunguko wa hatia na upungufu kifedha.
Lakini sasa nisikilize: hili si fundisho la kibiblia. Kristo aliondoa kiambaza kwa damu yake ili uweze kupata nafasi ya moja kwa moja ya kumfikia Mungu (Waebrania 10:19–22). Roho Mtakatifu alimiminwa juu ya wote, si wachache walioteuliwa (Matendo 2:17). Hakuna mchungaji au nabii anayesimama k**a mpatanishi wa kudumu kati yako na Mungu, kwa maana biblia inasema:-

“Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu,” (1 Timotheo 2:5 NENO).
Kwa hiyo, mtu akikuambia, “Huwezi kubarikiwa hadi unitumikie mimi au upande mbegu kwenye huduma yangu au utalaaniwa na hutakwenda mbinguni usipotoa zaka/fungu la kumi,” unapaswa utambue mara moja ukweli uliofichika nyuma ya kauli hiyo ni kutaka kupata fedha ya aibu: hiyo si injili ya Kristo—huo ni ukoloni wa kiroho.

Vifuatavyo ni viashiria vya kukusaidia kutambua kwamba huenda uko chini ya ukoloni wa kiroho: -
.


Pata nakala yako kuzipata dalili hizi sita. Ili kupima k**a uko kwenye mazingira ya Ukoloni wa Kiroho.

Photos from Kingdom Descipleship Training Center's post 17/10/2025

Kimekamilika. Mwezi huu English Version na mwezi ujao Swahili version.

Hiki siyo cha kukosa, walengwa ni:-
1. Muumini
2. Viongozi wa kidini
3. Walimu wa neno la Mungu
4. Wainjilistti
5. Jamii kwa ujumla

16/09/2025

Safari ya Kugundua Kusudi: Kutoka Edeni Hadi Umilele

Karibu kwenye darasa la kipekee la wiki 12 lililo andaliwa na Kingdom Discipleship Training Centre (KDTC). Lengo kuu ni kukusaidia kugundua na kuishi kusudi la Mungu katika maisha yako kuanzia asili ya mwanadamu pale Edeni hadi umilele.

📖 Mada Kuu: Kutoka Edeni Hadi Umilele – Kugundua na Kuishi Kusudi la Mungu
🗓️ Kila Jumamosi kwa muda wa wiki 12 kuanzia tarehe 04/10/2025
⏰ Saa 4:00 Asubuhi – Saa 7:00 Mchana
📍 Bamaga – Karibu na Chuo cha Ustawi wa Jamii
👤 Mwalimu: Kabenda Balete

👉 Hii ni nafasi ya kujifunza Neno la Mungu kwa undani, kujitambua, na kutembea katika mpango alioukusudia Mungu kwa maisha yako.

🔗 Jisajili hapa: https://forms.gle/uQtULaYuiSJWwTdC6

📞 Kwa mawasiliano zaidi: +255 742 411 411

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Kitunda
Dar Es Salaam