Nabii Bashando
Support this ministry by sending your offering through Mpesa +255757964805 Name: Martin Shaboka.
Issue siyo urembo, pesa, shepu, elimu au umaarufu, kinachotazamwa ni maadili ya mwanamke sawasawa na maandiko na pia asili ya mwanamke katika kuuk**ata moyo wa mumewe. Biblia inaagiza wanawake wawe watii (Efeso 5:22), na pia kichwani waonyeshe dalili ya kumilikiwa (1 Wakorintho 11:10). Ambapo zamani dalili hiyo ilikuwa ni kilemba, baadaye ikaja kuwa pete ya ndoa, ila kwa sasa inapaswa kuwa akili pevu (A mature mind) ya kumstahi mume k**a mamlaka inayokumiliki. Zile mambo za haki sawa au hamsini kwa hamsini huwa zinaishia kwenye mgawanyo wa majukumu huko ofisini kwenu, ndani ya vyama, au kwenye makampuni na kadhalika, ila ukivileta ndani ya nyumba huwa vinavunja ndoa, maana kwenye ndoa wewe mwanamke unatambuliwa k**a kitu kinachotakiwa kumilikiwa, kupendwa na kutunzwa kwa heshima. Kwenye Mithali 18:22 imeandikwa, "Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA." Pigia mstari hapo kwenye "KITU CHEMA" kwa kiingereza ni good thing.... Mwanamke wewe ni kitu yaani propert ya mumeo k**a vile nyumba yake, gari yake, simu yake, tv yake, nakadhalika, ila tofauti yako na hivyo vitu vingine ni kwamba una uwezo wa kujua jema na baya na pia umeunganishwa na roho yake,tendo linalokufanya uwe sehemu ya mwili wake.
Kwenye amri za Mungu sheria ya mke imeenda sambamba na sheria ya vitu na watumwa, ukisoma kitabu cha Kutoka 20:17 imeaandikwa, "Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako."
Nahitimisha kwa kukuambia mwanamke kuwa mwanaume ni mamlaka kubwa sana juu yako ambayo ili ikupe unachotaka ki hisia inabidi ujitengeneze kisaikolojia kuwa kitu chema kinachomilikika, ukija na Yes no nyiiingi utaishia kuwa super woman, mara mwanamke wa mithali na vile vimisemo vya what man can do even woman can do lakini ndoa itaota mbawa na kukukimbia you know....
God of miracles and wonders is still alive 🙏
Tunamshukuru Mungu kwa kumnusuru binti yetu na ajali ya kuangukia mlango wa kioo na kioo hicho kumchana usoni. K**a siye BWANA aliyekuwa pamoja nasi Bashando na aseme sasa...
Nimeonana na ndugu yangu aliyekuwa mchumba wa muimbaji Irene Robert ikiwa ni wiki saba baada ya kuzuiwa katika kituo cha polisi mabatini kwa ajili ya uchunguzi wa shauri la kifo cha utata cha Marehemu Irene Robert. Ndugu yetu yuko salama na bado ana matumaini makubwa katika Kristo aliyemtetea na kumtoa kwenye msala mkubwa huu aliyoangushiwa.
Kitu ambacho wengi hawajui ni kwamba Brian ni muumini mwaminifu wa kipawa na huduma yangu na amekuwa akisapoti huduma yangu kimya kimya kwa muda wa miaka mingi...
For many months I have been inviting my neighbors to church but they have been reluctant to come to church. The other day while I was preparing to go preach at a stand, the Holy Spirit led me to go outside my house and preach. When I asked my first neighbor to use his yard to preach, he welcomed me without resentment, and when I started preaching some neighbors came out and joined us.
The good news is that in that day's preaching we had ten people while others were peeping from a distance to see what was going on, and with God's help we led ten people in a prayer of repentance....
Jesus is good....
The Gospel must be preached everywhere so that the end may come....
21/05/2026
ITAMBUE NEEMA ULIYOPEWA NA UISIMAMIE KWA UAMINIFU
Na. Mchungaji Bashando
Katika 1 Wakorintho 12:8-11 imeandikwa:
"Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa... mwingine imani... mwingine karama za kuponya... mwingine unabii... lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake k**a apendavyo yeye."
Mungu kupitia Roho Mtakatifu huwapa wote katika mwili wa Kristo neema tofauti kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa. Hakuna neema ndogo wala kubwa mbele yake, kwa sababu zote zinalenga lengo moja: kumtukuza Kristo na kujenga waamini.
Changamoto inatokea pale mtu anapodharau neema aliyopewa na kuanza kutamani ile ya mwingine. Hapo ndipo wivu, udanganyifu, na utafutaji wa sifa za kibinadamu huanza kuingia. Hii ndiyo husababisha baadhi kutoa shuhuda za uongo, kuigiza miujiza, na kujishindia majina makubwa ambayo Mungu hajawapa.
Kutambua neema yako haimaanishi ukae kimya. Bali uifanyie kazi kwa bidii, uvumilivu, unyenyekevu, na uaminifu katika kidogo ulichopewa. Na wakati wa Mungu ukifika utakua tu.
Mtume Paulo alisema: "Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari" [2 Tim 2:15].
Kumbuka kuwa hata ukiwa mwaminifu, njia ya wito si ya ushindi wa kila wakati. Yeremia, Paulo, na Yesu wenyewe walipitia kukataliwa na mateso wakiwa waaminifu. Mafanikio ya Kikristo hayapimwi kwa ukubwa wa jukwaa, bali kwa uaminifu wako mbele ya Mungu [Luka 16:10].
Pia ujue kuwa wewe ni kiungo cha mwili mmoja. Neema yako haikutolewa ili ujitenge, bali ili uihudumie sehemu nyingine za mwili. Uhalisi katika wito wako ndio unaokuleta utulivu na maana ya kweli.
Itambue. Ikuze. Iitumie. Na uache Mungu ndiye atoaye matokeo.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Contact the business
Telephone
Website
Address
Shaban Robert Street
Dar Es Salaam
