21/12/2024
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa, ameipongeza Bandari ya Tanga kwa kuandika historia kwa kuwezesha kukusanya takribani bilioni 100 ndani ya miezi mitano. Hayo ni matokeo ya uboreshaji wa miundombinu ya bandari hiyo uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliogharimu bilioni 429.1
Katika ukusanyaji wa mapato hayo, bilioni 38.53 zilikusanywa na Bandari ya Tanga na bilioni 57 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga.
Prof. Mbarawa ametoa Pongezi hizo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tanga ili kukagua maboresho makubwa yaliofanyika katika bandari ya hiyo.
Katika kipindi hicho cha miezi mitano pia Bandari ya Tanga imefanikiwa kuhudumia meli 172 ikiwa ni zaidi ya lengo la kuhudimia meli 90 kwa miezi mitano.
Mhe. Waziri huyo, aliendelea kwa kusema kuwa, mafanikio hayo ni matokeo ya uwekezaji wa sh. bilioni 429.1 uliofanywa katika kuboresha magati mawili yenye urefu wa mita 450 pamoja na ununuzi wa vifaa vya kuhudumia mizigo ya wateja.
“Matokeo yameonekana, ni wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo gharama za uwekezaji zitakuwa zimesharudi. Ajira zimeongezeka kwa sababu watu wanafanyakazi muda wote,” alibainisha.
Aidha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Juma Kijavara amesema, Serikali imetoa kibali cha kujenga gati maalum kwa ajili ya meli za makasha. Ujenzi wa gati hiyo ambayo itakuwa na urefu wa mita 300 mchakato wa kumpata mkandarasi karibu unakamilika. Pia itajengwa gati ya mita 50 kwa ajili ya meli za abiria.
Kwa upande wa Bandari ya Pangani Mhe. Waziri Mbarawa amesema anatambua umuhimu wa bandari hiyo kwa usafirishaji wa Bidhaa za Mazao hivyo Serikali ina mpango wa Kuiboresha kwa kuchimba mchanga uliopo katika lango la kuingilia meli pamoja na kuweka maboya ya kuongozea meli.
20/12/2024
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari unaofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) Jengo la One Stop Centre, Ukumbi wa Mikutano Ghorofa ya nne, Jijini Dar es Salaam, tarehe 19 Desemba,2024.
17/12/2024
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT) Ndg. Mary Chatanda ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kupitia Bandari ya Tanga kwa ufanisi mkubwa wa kuhudumia Meli kutoka 18 kwa mwezi hadi kuhudumia Meli 32 kwa mwezi.
Ndg. Chatanda ametoa pongezi hizo wakati Wajumbe wa Jumuiya hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini walipofanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tanga, ili kuona Maboresho Makubwa yaliyofanywa na Serikali katika Bandari hiyo.
Ndg. Chatanda amesema, ufanisi wa Bandari ya Tanga umetokana na juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya maboresho makubwa katika Bandari ya Tanga, yaliyogharimu Shilingi Bilioni 429.1.
Pia amesema kuwa, TPA imeonesha uaminifu mkubwa kwa kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa kupanua Bandari ya Tanga zinatumika kikamilifu ili kuleta matokeo chanya.
Aidha Ndg.Chatanda amewataka Wajumbe wa Jumuiya hiyo kuwa Mabalozi wazuri wa kusemea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali, ikiwemo mradi wa maboresho ya Bandari ya Tanga.
17/12/2024
Wateja na Wadau wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) Nchini Uganda, wameipongeza TPA kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika Bandari zake na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
Pongezi hizo wamezitoa mwishoni mwa juma lililopita Jijiji Kampala, katika tukio lililoandaliwa na Ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa lengo la kuwashukuru kwa kuendelea kuiamini TPA na kuendelea kuchagua kusafirisha shehena kupitia Bandari zake.
Wateja na Wadau hao pia wametoa maoni yenye lengo la kuboresha zaidi huduma za TPA, kuimarisha ushirikiano na Wateja pamoja na Wadau wake huku wakionesha kufurahishwa na mipango mipya ya kujenga uwezo kwa Mashirika ya Grindrod Logistics Africa na Shirika la Reli la Uganda (URC), Mashirika yanatoa huduma za usafiri kwa njia ya Reli na Maji hususani Ziwa Victoria.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uganda Mhe. Meje Jenerali Paul Kisesa Simuli, ameendelea kuwahakikishia mazingira Rafiki ya kuendelea kufanya Biashara kati ya Nchi hizi mbili hasa kutokana na kuendelea kuongezeka kwa ufanisi katika utoaji huduma katika Bandari zote za TPA.
Amesema Ufanisi wa Bandari uliopo sasa unaotokana na Maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali katika Bandari kupitia TPA, ni faida kubwa katika ukuaji wa Uchumi na Biashara kati ya Nchi hizi mbili pamoja na Uchumi wa kikanda.
Naye Mwakilishi wa TPA Nchini Uganda Bi. Lona Stafford, amewashukuru Wateja na Wadau hao kwa kuendelea kuiamini Mamlaka na kutumia Bandari zake na kusisitiza kuwa TPA itaendelea kuongeza ufanisi zaidi katika utoaji wa huduma zake.
12/12/2024
Maofisa wanafunzi na Wakufunzi (48) kutoka Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Jamuhuri ya watu wa China (National Defence University of China ) leo tarehe 12 Disemba 2024 wamefanya ziara ya kimafunzo katika Bandari ya Dar es Salamaam kujifunza shughuli za Bandari pamoja na masuala ya siasa, ulinzi na maendeleo ya nchi.
Ujumbe huo umepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
12/12/2024
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Disemba 11,2024 zimeonyesha utayari wa ushirikiano katika uboreshaji wa biashara ya Uchukuzi kwenye Bandari ya Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya TPA.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw.Plasduce Mbossa amesema tukio hilo ni kielelezo cha kuonyesha utayari wa pande hizo mbili kuelekea makubaliano ya kushirikiana katika kutekeleza mpango kazi wa TPA Katika kuboresha Bandari zake.
Naye Mkurugenzi wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya barani Afrika,Bw.Hans Stausboll amesema Kamisheni ya Umoja wa Ulaya inaamini maboresho yatakayofanyika kupitia ushirikiano huu, yataongeza ufanisi wa uhudumiaji wa shehena katika Bandari ya Dar es Salaam.
12/12/2024
Ujumbe wa Wakufunzi na Wanafunzi (19) kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ukamanda (Commandant National Defence College cha nchini Kenya wakiongozwa Luteni Jenerali Juma Mwinyikai wamefanya ziara ya kimafunzo katika Bandari ya Dar es Salamaam (TPA) kujifunza shughuli za Bandari pamoja na masuala ya kiuchumi, siasa na kiutamaduni pamoja na mchango wa TPA katika kuimarisha ulinzi na usalama wa Bandari na nchi kwa Ujumla.
Ujumbe huo ulipokelewa na Meneja zimamoto na Usalama Bw. M***a Biboze kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed Gallus Abed
12/12/2024
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA ) imeshiriki Tamasha la Utalii la kisiwa cha Mafia “Mafia Island Festival 2024” lililofanyika wilayani Mafia Mkoa wa Pwani hivi karibuni.
Mgeni rasmi katika Tamasha hilo la siku tatu, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Aboubakar Kunenge.
10/12/2024
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile (Mb) leo Desemba 10,2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw.Abed Gallus Abed kuhusu Shughuli mbalimbali za utekelezaji katika Bandari ya Dar es Salaam.
Wengine waliokuwepo katika mazungumzo hayo ni wawakilishi kutoka DP World na Afisa Masoko Mkuu Bw.Emmanuel Mrutu.
10/12/2024
Bendera ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) ikiwa Uhuru Peak katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kwenye tamati ya Kampeni ya Twenzetu Kileleni, wakati wa maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, tarehe 9 Desemba,2024.
Kampeni hii ya Twenzetu Kileleni, huu ukiwa ni msimu wake wa nne, iliratibiwa na kampuni ya Utalii ya Zara Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) kupitia njia ya Marangu ambapo Watumishi wawili wa TPA, Bw. Edmund Kazingoma (kushoto) kutoka Bandari ya Mtwara na Bi. Rose Kileo (kulia) kutoka Kurugenzi ya Masoko na Uhusiano, ndio walioifikisha Bendera hiyo Kileleni