11/04/2026
MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA NA KATIBU WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA PROF. ElISANTE OLE GABRIEL ALIPOFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYA KAZI KILICHOFANYIKA TAREHE 10 APRILI, 2026 KATIKA UKUMBI WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA JIJINI DODOMA.
13/03/2026
JAJI MKUU AWAAPISHA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMANa
Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa Mahakama
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. George Masaju leo tarehe 13 Machi, 2026 amewaapisha wajumbe wanne wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Katika hafla iliyofanyika leo kwenye ofisi za Tume ya Utumishi wa Mahakama jijini Dodoma, Jaji Mkuu amemuapisha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Gerson Mdemu kuwa Mjumbe wa Tume kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Aidha, Jaji Mkuu pia amemuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kufuatia kuteuliwa kwa mara ya pili na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 29, 2025.
Jaji Mkuu pia amewaapisha kwa mara ya pili Mawakili Bahame Tom Nyanduga na Dosca Kemilembe Mutabuzi kuwa Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama baada ya kumaliza kipindi chao cha miaka mitatu cha kuwa Wajumbe wa Tume na kuteuliwa tena na Rais kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 112 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tume ya Utumishi wa Mahakama inaundwa na wajumbe wafuatao; Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ambaye ni Mwenyekiti, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani anayeteuliwa na Rais, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Wajumbe wawili wanaoteuliwa na Rais.
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Ibara ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Sura ya 237. Chombo hiki kimeundwa kwa lengo la kusimamia utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kusimamia Ajira na Nidhamu za Watumishi wa Mahakama.
08/03/2026
ANAWAKE TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Watumishi Wanawake wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wameungana na wanawake wengine Duniani kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.
Siku hii ni Maalumu ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii, uchumi na uongozi.
Katika maadhimisho hayo, watumishi hao walipata fursa ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uwezeshaji wa wanawake mahali pa kazi, usawa wa kijinsia, pamoja na umuhimu wa kuendelea kujenga uwezo wa wanawake ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu yao.
Aidha, maadhimisho hayo yalisisitiza umuhimu wa mshikamano miongoni mwa wanawake, kuhamasishana katika kujitambua na kutumia ipasavyo fursa za Watumishi zilizopo ili kuleta maendeleo binafsi na ya Taasisi kwa ujumla.
Tume ya Utumishi wa Mahakama imeendelea kuthamini mchango wa wanawake katika utumishi wa umma kwa kuhamasisha mazingira ya kazi yenye usawa, kuheshimu haki na kutoa fursa sawa za maendeleo kwa watumishi wote.
Kaulimbiu ya mwaku huu ni “ Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana. Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050.” Hii ni kaulimbiu inayosisitiza umuhimu wa kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata haki na fursa sawa katika nyanja zote za maendeleo.
19/02/2026
WEKEZENI KWENYE WATAALAMU NA MIUNDOMBINU YA TEHAMA: PROF. OLE GABRIEL
Na Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa Mahakama, Arusha
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel amewashauri wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Mashirika ya Umma kuwekeza kwenye Wataalamu na Miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi.
Akiwasilisha Mada kuhusu Mifumo ya Kielekitroniki ya Ubadilishanaji wa Taarifa kwa kutumia Akili Unde kwenye Mkutano wa Sita wa Mwaka wa Serikali Mtandao leo tarehe 18 Februari, 2026 jijini Arusha, Prof. Ole Gabriel alisema kuwekeza kwenye Utaalam na miundombinu ya TEHAMA kutazisaidia Taasisi na Mashirika ya Umma kuongeza tija na ufanisi.
Prof. Ole Gabriel alisema kuwa Mahakama ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika matumizi ya mifumo mbalimbali ya Kielekitroniki ambayo imerahisisha kwa kiasi kikubwa shughuli za utoaji haki nchini na kutoa muda kwa wananchi kushiriki katika shughuli za kujiongezea kipato.
”Taasisi inapojikita kwenye matumizi ya mifumo ya Kielekitroniki husaidia kuokoa muda kwa kuwa wananchi watapatiwa huduma kwa haraka na kwenda kufanya shughuli za uzalishaji”, alisisitiza Mtendaji Mkuu.
Mkutano wa Sita wa mwaka wa Serikali Mtandao unafanyika jijini Arusha ambapo umewakutanisha Wataalam wa masuala ya TEHAMA na wataalamu wengine zaidi ya 1,000 kutoka Taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma ili unajadili jitihada za Serikali Mtandao, mafanikio pamoja na changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa jitihada hizo na namna ya kukabiliana nazo.
Aidha. Mkutano huo wa siku tatu unatarajiwa kumalizika kesho tarehe 19 Februari, 2026.
19/02/2026
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Utumishi wa Mahakama wakishiriki kikao kilichofanyika leo tarehe 13 Februari, 2026, kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ustawi wa watumishi, kuongeza ufanisi wa kazi na kuimarisha utendaji wa taasisi. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel.
07/01/2026
Usaili wa awamu ya pili wa waombaji kazi kada ya Hakimu Mkazi II umeendelea kufanyika leo tarehe 07 Januari, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (Ndoa na Mirathi)Temeke, Dar es salaam.
07/01/2026
Zoezi la usaili awamu ya pili limeendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Jumuishi cha Mahakama (Mirathi na Ndoa) Temeke, Dar es Salaam ambapo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika, ( katikati) akiwaelekeza waombaji wa kazi kada ya Hakimu Mkazi II taratibu za usaili leo tarehe 06 Januari, 2026.
17/12/2025
Sehemu ya Wasailiwa Kada ya Afisa Ununuzi, Afisa Ugavi, na Afisa ugavi msaidizi wakiwa kwenye Usaili kwa njia ya Kielekitroniki uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo tarehe 17 Disemba, 2025. Usaili wa aina hii unaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini mpaka Tarehe 23/12/2025
16/12/2025
Waombaji wa nafasi za kazi zilizotangazwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama hivi karibuni wakiwa kwenye Usaili wa awamu ya kwanza kwa njia ya Kielekitroniki uliofanyika Chuo cha Uhasibu Dar es salaam. Usaili wa aina hii unafanyika katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia leo mpaka Tarehe 23/12/2025
25/11/2025
fisa wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Bw. Stephen Sumari akitoa elimu kwa Watumishi wa Mahakama kuhusu Tume pamoja na Majukumu yake.”