ithibatitz

Website

ithibatitz Ukurasa rasmi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Tanzania
Journalists Accreditation Board of Tanzania

07/10/2026

Mpendwa Mwandishi wa Habari, kitambulisho chako kikiwa tayari, tunakukaribisha kufika Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) jijini Dar es Salaam kukichukua.

Unatakiwa kukifuata mwenyewe. Hata hivyo, ukiwa mbali, unaweza kumwagiza mtu unayemwamini kufika ofisini kukuchukulia.

Hakikisha unayemtuma ni mtu unayemwamini, ana taarifa za kutosha kukuhusu yaani jina lako, chombo cha habari unachofanyia kazi na namba yako ya simu. Taarifa hizi zinatusaidia kuhakiki na kukabidhi kitambulisho kwa usahihi.

Tuna vitambulisho vilivyo tayari tangu mwaka jana 2025 ambavyo bado havijachukuliwa. Ikiwa umeshajulishwa kuwa chako kiko tayari, tafadhali njoo ukichukue au mtume mtu unayemwamini.

Baada ya kukipokea, kitunze kwa usalama.

Tunathamini ushirikiano wako. JAB, tuko hapa kukuhudumia!



05/10/2026



01/10/2026




Watanzania wamehamasishwa kumuunga mkono Jihan Dimack, Miss Grand Tanzania 2026, kwa kushiriki katika upigaji kura wa ki...
29/09/2026

Watanzania wamehamasishwa kumuunga mkono Jihan Dimack, Miss Grand Tanzania 2026, kwa kushiriki katika upigaji kura wa kipengele cha Country’s Power of the Year, Round 2 kupitia chapisho husika kwenye akaunti ya Instagram ya .

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa. Jihan, anayetambulishwa kwenye tovuti rasmi ya mashindano kwa jina la Jihan Mohin Dimachk, anaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Grand International 2026 yanayofanyika nchini Thailand.


Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) na Mshauri wa Rais katika Masuala ya Habari, Bw. Tido Mhando...
29/09/2026

Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) na Mshauri wa Rais katika Masuala ya Habari, Bw. Tido Mhando, amewataka Waandishi wa Habari kupanua wigo wa habari wanazoripoti kwa kuangazia masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, badala ya kujikita zaidi katika michezo na burudani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wa Clouds Media Group waliokuwa wakishiriki mafunzo kwa siku tano kuanzia tarehe 21 hadi 25 Septemba, 2026 kuhusu mchakato na taratibu za ithibati, Bw. Mhando amesema pamoja na umuhimu wa habari za michezo na burudani, vyombo vya habari vina wajibu wa kuibua na kuripoti masuala mengine yenye maslahi kwa Taifa.

“Ni sawa kuzungumzia michezo, lakini isiwe wakati wote. Lazima sisi k**a Waandishi wa Habari tuone na kuripoti mambo mengine yanayoendelea katika nchi yetu,” amesema Bw. Mhando.

Amesema Waandishi wa Habari wa ndani wana haki na wajibu wa kuripoti matukio yanayotokea nchini kwa usahihi na kwa kuzingatia maslahi ya Taifa, badala ya kuacha simulizi kuhusu Tanzania zijengwe na Waandishi wa Habari kutoka nje ya nchi kwa namna inayoweza kuathiri taswira yake.

“Waandishi wa Habari wana haki ya kuripoti mambo yanayotokea nchini mwetu bila kusubiri Waandishi wa Habari kutoka nje, ambao wanaweza kuripoti kwa namna inayoharibu taswira ya nchi. Waandishi wa Habari wa ndani wakiripoti kwa usahihi, wanaweza kulinda heshima ya nchi na kusaidia utekelezaji wa mipango yake,” amesema.

Aidha, Bw. Mhando amesisitiza umuhimu wa Waandishi wa Habari kufahamu taratibu za ithibati na kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni, ili taaluma ya uandishi wa habari itekelezwe kwa weledi na uwajibikaji.

Mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa kuhusu mchakato wa ithibati, vigezo vinavyotumika na umuhimu wa kuwa na nyaraka pamoja na taarifa zinazohitajika wakati wa kuomba ithibati.

JAB imeendelea kushirikiana na vyombo vya habari na kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kuongeza uelewa kuhusu taratibu za ithibati na wajibu wa Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa majukumu yao.



21/09/2026

HAKUNA HABARI YENYE THAMANI KULIKO MAISHA YA MWANDISHI

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kujiandaa kuripoti majanga yanayoweza kujitokeza katika msimu wa mvua za Vuli, huku wakitanguliza usalama wao, kutoa taarifa sahihi na kuwaelekeza wananchi hatua za kujikinga.

Wito huo umetolewa wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ikitabiri kuwa msimu wa mvua za Vuli wa Oktoba hadi Desemba 2026 utaathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño. Kwa mujibu wa TMA, mvua za juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Septemba 21, 2026, Mjumbe wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Bw. Mgaya Kingoba, amesema wananchi hutegemea taarifa za Waandishi wa Habari kufanya maamuzi ya kujilinda wakati wa majanga hivyo, utekelezaji wa jukumu hilo haupaswi kuhatarisha maisha ya Mwandishi.

“Wakati wa majanga, Mwandishi wa Habari anatakiwa kutimiza majukumu yake huku akilinda usalama wake na kuchukua tahadhari zote muhimu. Hakuna taarifa muhimu kuliko uhai wako,” amesema Kingoba.

Amesema Waandishi wa Habari wanapaswa kuthibitisha taarifa kabla ya kuzitoa kwa umma, akieleza kuwa taarifa zisizo sahihi zinaweza kusababisha hofu na taharuki. Amewataka kufuatilia utabiri na tahadhari za hali ya hewa kutoka TMA, pamoja na kupata taarifa za uokoaji na hatua za kukabiliana na maafa kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Menejimenti ya Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Kamati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi za mikoa na halmashauri.

Kwa mujibu wa mwelekeo wa msimu uliotolewa na TMA, mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya nne ya Septemba na wiki ya kwanza ya Oktoba katika ukanda wa Ziwa Viktoria, kisha kusambaa taratibu katika maeneo mengine mwezi Oktoba na ongezeko la mvua linatarajiwa mwezi Novemba.

Kingoba amesema wajibu wa Mwandishi wa Habari hauishii kueleza madhara yaliyotokea kwani unahusisha pia kuwafahamisha wananchi tahadhari za kuchukua, maeneo salama, mahali pa kupata msaada na hatua zinazochukuliwa na mamlaka.

“Mwandishi hatakiwi kuishia kueleza tatizo pekee, bali anapaswa pia kutoa taarifa za suluhisho; kwa mfano, kuwaeleza wananchi nini kifanyike, wapi wahamie, wapi wapate msaada na hatua zinazochukuliwa na Serikali,” amesema.

TMA imeeleza kuwa unyevu mwingi kwenye udongo na mafuriko vinaweza kujitokeza katika msimu huo na kina cha maji katika mito na mabwawa kinaweza kuongezeka, huku uchafuzi wa maji ukiweza kusababisha magonjwa.

Kingoba, ambaye pia ni Kaimu Meneja wa Huduma za Kiswahili wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), amevitaka vyombo vya habari kutumia lugha inayotoa mwongozo bila kuongeza taharuki akisema Waandishi wa Habari wanapaswa kutathmini hatari za maeneo wanayokwenda, kuvaa mavazi yanayofaa, kulinda vifaa vyao vya kazi dhidi ya maji na kuepuka maeneo yenye mafuriko makubwa au uwezekano wa maporomoko.

Aidha, amesema wakati wa kuchukua picha na kufanya mahojiano, Waandishi wa Habari wanapaswa kulinda faragha, heshima na utu wa watu walioathiriwa na majanga huku pia wakiangazia mahitaji ya watoto, wanawake na watu wenye uhitaji maalum ili sauti zao ziwafikie wanaohusika na utoaji wa msaada.

Kingoba amevitaka vyombo vya habari kuanza maandalizi mapema kwa kuwapatia Waandishi wa Habari vifaa vinavyofaa na maelekezo ya usalama, ili waweze kuihudumia jamii bila kuhatarisha maisha yao.

MAFUNZO YA JAB YAWAFUNGUA WAANDISHI WASAFI MEDIAWashiriki wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kutoka Wasafi Media wameele...
18/09/2026

MAFUNZO YA JAB YAWAFUNGUA WAANDISHI WASAFI MEDIA

Washiriki wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kutoka Wasafi Media wameeleza kuwa mada zilizotolewa katika mafunzo hayo zimewasaidia kutambua makosa yaliyokuwa yakijirudia katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwapatia mwongozo wa kuboresha utendaji.

Wakizungumza wakati wa tathmini ya mafunzo hayo yaliyofanyika Septemba 17 na 18, 2026, katika Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) jijini Dar es Salaam, Gerald Hando, Aggai Kifumu na David Rwenyagira wameeleza kuwa mafunzo yamewaongezea uelewa kuhusu sheria, maadili na uzalendo katika uandishi wa habari.

Wamebainisha kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili Waandishi wa Habari na wazalishaji wa maudhui ni shinikizo la kuongeza idadi ya wafuasi katika majukwaa ya kidijitali, kukidhi matakwa ya hadhira pana na kasi ya mabadiliko katika mazingira ya kidijitali kuwa kubwa kuliko maboresho ya baadhi ya sheria zinazoongoza shughuli zao.

Kwa mujibu wa washiriki hao, mazingira hayo yanaweza kusababisha baadhi ya Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa mazoea au kujikuta wakifanya makosa ya kisheria na kimaadili bila kuwa na uelewa wa kutosha.

Wamesema mafunzo hayo yamewajenga kitaaluma, yamewafungua kutoka katika utendaji wa mazoea na kuwapatia mwongozo wa kufanya maamuzi sahihi katika majukumu yao ya kila siku.

Aidha, wameiomba JAB kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa Waandishi wa Habari kutoka vyombo vingine, huku kipaumbele kikitolewa kwa wanaofanya kazi na kuzalisha maudhui kupitia majukwaa ya kidijitali, ambako changamoto za uzingatiaji wa sheria na maadili zimeendelea kujitokeza.

Wamesema kasi ya uzalishaji na usambazaji wa maudhui katika majukwaa hayo imeongeza uwezekano wa kutokea kwa makosa ya kisheria na kimaadili, hivyo elimu endelevu inahitajika ili kuimarisha weledi na uwajibikaji.

Mafunzo hayo yalihusu Sheria ya Huduma za Habari, maadili ya uandishi wa habari na uzalendo, yakilenga kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari na watangazaji wa Wasafi Media kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, viwango vya taaluma na maslahi ya jamii.



17/09/2026

Mbali na kuhimizwa kuisoma na kuielewa vema Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na kanuni zake, Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuzifahamu na kuzisoma mara kwa mara sheria nyingine nne zinazohusu na kuongoza utekelezaji wa majukumu yao, ili wafanye kazi kwa weledi na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Wito huo umetolewa leo, Septemba 17, 2026, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, wakati akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Huduma za Habari na historia yake katika siku ya kwanza ya mafunzo kwa Waandishi wa Habari wa Wasafi Media.

Mafunzo hayo, yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa JAB jijini Dar es Salaam, yanalenga kuwaongezea Waandishi wa Habari uelewa kuhusu sheria na maadili, pamoja na uzalendo katika uandishi wa habari, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uwajibikaji.

Wakili Kipangula amesema kuzijua sheria si jambo la hiari kwa Mwandishi wa Habari, bali ni msingi wa kufanya kazi kwa kujiamini, weledi na uwajibikaji.




#𝐰𝐚𝐬𝐚𝐟𝐢𝐦𝐞𝐝𝐢𝐚

Je, unakubaliana na kauli hii?Mavazi unayo aa ukiwa eneo lako la kazi yanachangia kwa kiasi kikubwa jinsi jamii inavyoku...
16/09/2026

Je, unakubaliana na kauli hii?

Mavazi unayo aa ukiwa eneo lako la kazi yanachangia kwa kiasi kikubwa jinsi jamii inavyokuchukulia na kukuheshimu k**a Mwandishi wa Habari. Heshima taaluma kwa kuvaa vizuri na kwa staha ukiwa kazini.

Kumbuka: Unapokuwa kazini, huwakilishi nafsi yako pekee bali unawakilisha taaluma nzima na taasisi unayoifanya kazi. Mavazi yasiyo ya kiofisj au yasiyo na staha yanashusha thamani ya taaluma husika.




Ithibati Tz
15/09/2026

Ithibati Tz

Address

14 Jamhuri
Dar Es Salaam
11470

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ithibatitz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share