TPDC 2026 || Pongezi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi), Mhe. Deus Clement Sangu, amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kazi kubwa na yenye tija inayofanya katika kukuza uchumi wa taifa, hususan kupitia sekta ya gesi asilia.
Akizungumza baada ya kutembelea banda la GASCO ambayo ni kampuni tanzu ya TPDC katika maonesho ya OSHA yanayoendelea kitaifa mkoani Njombe, Waziri Sangu alieleza kuridhishwa na namna shirika hilo linavyozingatia kwa vitendo masuala ya afya na usalama mahali pa kazi.
Alitoa ushuhuda wake binafsi akisema:
“Nimejionea mwenyewe viwango vya hali ya juu vya usalama vinavyozingatiwa na GASCO, hasa nilipotembelea mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Madimba. Hili ni jambo la kuigwa na taasisi nyingine nchini.”
Mbali na hilo, Waziri Sangu alisifu mchango wa miradi ya gesi asilia katika kukuza ajira kwa Watanzania, akitolea mfano wa mradi wa bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
“Miradi ya gesi asilia imekuwa chachu kubwa ya ajira nchini. Tunaona wazi namna bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam lilivyofungua fursa nyingi za ajira, na kinachofurahisha zaidi ni kuona wazawa wakishiriki kikamilifu kuendesha mitambo ya kuchakata na kusafirisha gesi hiyo,” alisisitiza.
Aidha, alimpongeza TPDC kwa kuendelea kuleta maendeleo kwa jamii zinazozunguka miradi yake kupitia programu za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Alibainisha kuwa miradi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia ujenzi wa vituo vya afya, miradi ya maji safi na salama, pamoja na ujenzi wa shule.
Kwa ujumla, Waziri Sangu alisisitiza kuwa juhudi za TPDC ni mfano bora wa namna rasilimali za taifa zinavyoweza kutumika kuleta maendeleo jumuishi—kuanzia kukuza ajira, kulinda afya na usalama kazini, hadi kuinua ustawi wa jamii zinazozunguka miradi hiyo.
TPDC Tanzania
natural gas,tpdc,Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,wizara ya nishati na madini,gas,oil,mafuta,gesi,Tanzania Petroleum Development
Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) is the National Oil Company of Tanzania through which the Ministry of Energy and Minerals implements its petroleum exploration and development policies. TPDC has a manpower strength of about 400 and is organized into seven directorates and three Units, namely: Directorate of Upstream, Directorate of Downstream, Directorate of Finance, Directorate o
TPDC 2026 ||
28/02/2026
TPDC 2026 || Mnazi bay
TPDC kwa kushirikiana na M&P wameanza rasmi uchorongaji wa visima vitatu vipya vya uzalishaji gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay, mradi unaotarajiwa kuongeza uzalishaji wa gesi kwa futi za ujazo milioni 45 na kugharimu takribani TZS bilioni 234.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi ameipongeza TPDC kwa hatua hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea na maandalizi ya uchorongaji wa visima zaidi, akibainisha kuwa mahitaji ya gesi asilia yanaongezeka kwa kasi katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, uzalishaji wa umeme, usafiri, taasisi na matumizi ya majumbani.
Aidha, alieleza kuwa mradi huu ni sehemu ya juhudi za makusudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini. Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Mafuta na Gesi), Dkt. James Mataragio, amesema Wizara kupitia TPDC imewekeza takribani TZS trilioni 1 katika miradi ya kuongeza upatikanaji wa gesi asilia.
27/02/2026
TPDC 2026 || Gesi ya Ntorya
Waziri wa Nishati, Deogratius John Ndejembi, ameitaka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhakikisha Mradi wa Ntorya unakamilika kwa wakati ili ifikapo Septemba 2026 visima hivyo vianze rasmi kuzalisha gesi.
Waziri Ndejembi ametoa msisitizo huo leo, Februari 27, 2026, akiwa mkoani Mtwara katika ziara ya kikazi ya siku moja, ambapo aliweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka visima vya Ntorya kwenda Madimba, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Amesema Watanzania wanatarajia kuona matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa katika sekta ya gesi, hivyo ifikapo mwezi wa tisa mwaka 2026 kusiwepo visingizio vya kuchelewesha uzalishaji.
“Watanzania wanahitaji matokeo. Mradi huu lazima ukamilike kwa wakati k**a tulivyojipangia,” amesisitiza Waziri Ndejembi.
Aidha, amehimiza ushirikiano wa karibu kati ya watekelezaji wa mradi na viongozi wa maeneo husika — wakiwemo wenyeviti wa vijiji, madiwani, wabunge na halmashauri — ili miradi ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) itekelezwe kwa ufanisi, uwazi na kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha.
Katika mkakati wa kuimarisha sekta ya nishati, Waziri Ndejembi amesema Tanzania inalenga kufikia uzalishaji wa megawati 8,000 za umeme ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni karibu mara mbili ya kiwango cha sasa, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya viwanda.
26/02/2026
TPDC 2026 || Upandaji wa miti
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na wabia wa mradi wa LNG, kampuni za Shell na Equinor, wametekeleza agizo la Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, la kupanda miti ya matunda na vivuli katika Shule ya Msingi Likong’o Mkoani Lindi. Shule hiyo ni mradi mpya wa kimkakati unaojengwa kwa udhamini wa mashirika hayo ili kuboresha miundombinu ya elimu katika eneo la mradi wa kusindika gesi asilia (LNG). Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, ambaye ameshuhudia hatua hiyo muhimu ya utunzaji wa mazingira na maendeleo ya jamii.
Aidha, zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia ushirikiano na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), ambao wamewezesha upatikanaji wa miche 2,000 itakayopandwa katika viwanja vya shule hiyo. Upandaji wa miti hii haulengi tu kurejesha uasilia wa mazingira, bali pia kutengeneza mazingira rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi kupitia vivuli na lishe ya matunda. Hatua hii inadhihirisha dhamira ya TPDC na wabia wake katika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi wa LNG unaenda sambamba na uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye.
26/02/2026
TPDC 2026 || Upandaji wa miti
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na wabia wa mradi wa LNG, kampuni za Shell na Equinor, wametekeleza agizo la Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, la kupanda miti ya matunda na vivuli katika Shule ya Msingi Likong’o Mkoani Lindi. Shule hiyo ni mradi mpya wa kimkakati unaojengwa kwa udhamini wa mashirika hayo ili kuboresha miundombinu ya elimu katika eneo la mradi wa kusindika gesi asilia (LNG). Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, ambaye ameshuhudia hatua hiyo muhimu ya utunzaji wa mazingira na maendeleo ya jamii.
Aidha, zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia ushirikiano na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), ambao wamewezesha upatikanaji wa miche 2,000 itakayopandwa katika viwanja vya shule hiyo. Upandaji wa miti hii haulengi tu kurejesha uasilia wa mazingira, bali pia kutengeneza mazingira rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi kupitia vivuli na lishe ya matunda. Hatua hii inadhihirisha dhamira ya TPDC na wabia wake katika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi wa LNG unaenda sambamba na uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye.
21/02/2026
TPDC 2026 || Pongezi kwa TPDC
Katika kuhitimisha kikao kazi na mafunzo kwa Menejimenti ya TPDC, Mhe. Salome Makamba, Naibu Waziri wa Nishati, ameipongeza Menejimenti ya Shirika kwa kuandaa mafunzo hayo pamoja na kikao cha tathmini ya utendaji, akibainisha kuwa hatua hiyo itaongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi.
Aidha, ameitaka TPDC kuendelea kufanyia kazi maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi, hususan yale yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa uzinduzi wa Bunge mwezi Novemba 2025, ambapo Wizara ya Nishati na taasisi zake zilielekezwa kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 angalau asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.
Vilevile, amepongeza jitihada za TPDC katika kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya majumbani, pamoja na ujenzi wa vituo vya kujaza gesi asilia na utoaji wa vibali kwa sekta binafsi kujenga vituo hivyo, hatua inayochangia kupunguza msongamano wa magari katika vituo vilivyopo na kuimarisha upatikanaji wa huduma.
TPDC 2026 || Ziara ya k**ati ya bunge
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Salome Makamba, amesema wamepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa Kamati na kuahidi kuyafanyia kazi huku akiongeza kuwa TPDC kupitia Wizara ya Nishati inaendelea kutoa huduma ya gesi ya CNG katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa gesi asilia unaimarika zaidi, hatua itakayosaidia kupunguza gharama za usafiri, kuongeza matumizi ya nishati safi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.
TPDC 2026 || Ziara ya Kamati ya Bunge
TPDC 2026 || Ziara ya k**ati ya Bunge
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imetembelea kituo mama cha kushindilia gesi asilia cha Mlimani-CNG jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza namna kituo hicho kinavyoendesha shughuli zake na kutoa huduma kwa wananchi, huku ikiishauri Serikali kuongeza juhudi katika kuimarisha matumizi ya gesi asilia nchini.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho kilichopo chini ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Subira Mgalu, amesema gesi asilia ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi kupitia upatikanaji wa nishati nafuu na rafiki kwa mazingira.
Mbali na hayo ameiomba Serikali kuhakikisha inaongeza matumizi ya gesi asilia kwenye magari na majumbani ili kupunguza utegemezi wa mafuta ya petroli na dizeli huku akiwataka wawekezaji kuwekeza zaidi katika miundombinu ya CNG ili wananchi wengi waweze kufikiwa na kunufaike na huduma hiyo.
Aidha, ameishauri Serikali kuangalia utaratibu wa kuhakikisha magari ya taasisi za umma yanatumia CNG kwa lengo la kupunguza gharama za mafuta na kuongeza ufanisi wa matumizi ya fedha za umma, na kuitaka TPDC kuongeza vituo vya kujaza gesi asilia nchini ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka.
19/02/2026
TPDC 2026 || Ramadhani Mubarak
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linawatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani jamii yote ya Waislamu Tanzania.
18/02/2026
TPDC 2026 || Mafunzo ya Uongozi
Leo tarehe 18/02/2026 Menejimenti ya TPDC imejikita katika mafunzo ya “Leadership and Leadership Roles”—hatua muhimu ya kukuza uongozi wenye dira, maadili, na uwajibikaji thabiti ndani ya Shirika. Mafunzo haya yamelenga kuimarisha uwezo wa viongozi wakuu wa Shirika katika kufanya maamuzi sahihi, kusimamia rasilimali kwa ufanisi, na kuongoza timu kuelekea malengo ya kimkakati ya TPDC.
Katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi, uongozi si cheo bali ni wajibu unaohitaji hekima, uthubutu, na maono mapana. Kupitia mafunzo haya, TPDC imelenga kuimarisha uwezo wa viongozi wake ili kuwa na viongozi wanaoongoza kwa mfano, wanaochochea ubunifu, na wanaojenga mshik**ano unaoleta matokeo chanya kwa Shirika na Taifa kwa ujumla.
“TPDC tunaendelea kujenga msingi imara wa uongozi bora—kwa sababu kesho ya nishati yetu inaanzia kwenye uongozi wa leo”.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Contact the business
Telephone
Website
Address
Azikiwe/Jamhuri Street
Dar Es Salaam
