Jawabu tz

Jawabu tz

Share

Ukweli tu

Photos from Jawabu tz's post 01/06/2026

📍HISTORIA

RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan anakwenda kuandika historia kwa ziara ya kwanza ya Rais wa Tanzania Urusi baada ya miaka 57, na Rais wa Kwanza Mwanamke Barani Afrika kufanya Ziara Urusi.

01/06/2026

DKT .MWIGULU ARUDISHA TABASAMU KWA WANANCHI WALIO ZUNGUSHWA MALIPO YAO

Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba akiwa katika ziara ya Kikazi kwenye Mkutano wa hadhara uliyofanyika Katika Uwanja wa Itigi Manyoni alipokea kero za wananchi mbalimbali zikiwemo hizi za hawa wananchi ambao waliingia makubaliano ya kusambaza mbao za ujenzi wa shule lakini hawakulipwa.

Mkasa mwingine mwana mama aliyewawakilisha wenzake juu ya kuiuzia tumbaku kampuni mbili ambazo hazikuwapa malipo yao.

Tazama Kipande hiki cha Video

Photos from Jawabu tz's post 31/05/2026

DKT. MWIGULU AENDELEA KUUFYEKA MTANDAO WA WIZI WA MILIONI 500 MANYONI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza kukamatwa kwa mtumishi mwingine wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni anayedaiwa kuhusika katika mtandao wa kulinda na kutetea watumishi waliohusishwa na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwafuatilia wote waliohusika na wizi wa fedha za umma.

"Mkuu wa mkoa, mtume wa RPC, huyu naye akamatwe, aunganishwe. Nataka mtandao huu wa mchwa nitimue wote. Sina urafiki wala uungwana na wezi, walaghai, wazembe na wanyang'anyi," amesema Dkt. Mwigulu.

Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo leo Jumapili Mei 31, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Madukani, wilayani Ikungi mkoani Singida.

Amesema amepokea taarifa kuwa mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya Manyoni amekuwa akipinga hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi waliohusishwa na ubadhirifu huo, ikiwemo kutajwa kwa majina yao hadharani, jambo ambalo amesema linaashiria kuwepo kwa mtandao unaolenga kuwalinda wahusika.

"Eti analalamika kwa nini nimewataja kwa majina. Anataka tuwatunzie heshima wezi. Mwizi hatakiwi kufichwa wala kulindwa. Akamatwe na hatua zichukuliwe mara moja," amesema.

Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa Serikali haitaridhia utamaduni wa kuwahamisha watumishi wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu badala ya kuwawajibisha, akieleza kuwa hatua za kisheria, kinidhamu na urejeshaji wa fedha za wananchi lazima zitekelezwe kikamilifu.

"Hakuna kuhamisha mwizi. Akihamishwa anaenda kuiba sehemu nyingine. Wale wote waliohusika wakamatwe, warejeshe fedha za wananchi na hatua za kisheria zifuate," amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amesema ataendelea kusimamia matumizi ya fedha za umma katika halmashauri zote nchini ili kuhakikisha fedha zinazokusanywa kutoka kwa walipa kodi zinatumika kwa maendeleo yaliyokusudiwa.

"Nitashughulika na mchwa wanaokula fedha kwenye halmashauri zetu. Tunataka fedha za wananchi zitumike kujenga shule, vituo vya afya, barabara na miradi mingine ya maendeleo, si kugawanywa na wachache," amesema.

Sambamba na hilo, amekemea vitendo vya ubadhirifu katika sekta ya afya ambapo wananchi huagizwa kununua dawa katika maduka binafsi licha ya Serikali kupeleka fedha za ununuzi wa dawa katika vituo vya kutolea huduma.

"Haiwezekani Serikali ipeleke fedha za dawa halafu wananchi waambiwe wakazinue dawa mtaani. Hii ni michezo ambayo haitavumiliwa," amesema.

Waziri Mkuu pia amewahakikishia wananchi wa Ikungi kuwa atarejea wilayani humo mwezi Juni mwaka huu kwa ziara maalum ya kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

"Nitakuja mwezi huu wa sita kabla haujaisha. Tutakaa siku nzima, tusikilizane na kutatua kero za wananchi," amesema.

Photos from Jawabu tz's post 31/05/2026

DKT. MWIGULU AAGIZA WALIOIBA MILIONI 500 MANYONI KUKAMATWA

Aagiza watumishi waliohusika na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 Manyoni wakamatwe na fedha zirudishwe

Akemea rushwa, wizi wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka

Aonya viongozi wanaowaza vyeo badala ya kutatua changamoto za wananchi

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza watumishi waliohusishwa na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni watafutwe popote walipo, wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu huku fedha hizo zikirejeshwa serikalini.

"Wamechota fedha za wananchi. Watafutwe hata ambao walishahamishwa, popote walipo wakamatwe, wawekwe ndani na fedha za Serikali zirudi. Hii si fedha ya mtu binafsi, ni fedha ya wananchi," alisema Dkt. Mwigulu.

Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Jumamosi Mei 30, 2026 alipozungumza na wananchi wa Wilaya ya Manyoni katika Viwanja vya Tambukareli mkoani Singida akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.

Alisema taarifa alizopokea zinaonesha kuwa jumla ya zaidi ya shilingi milioni 501 zilichotwa kutoka akaunti mbalimbali za halmashauri ikiwemo Akaunti ya Maendeleo (zaidi ya shilingi milioni 213), Akaunti ya Amana (zaidi ya shilingi milioni 259) na Akaunti ya Mapato ya Ndani (zaidi ya shilingi milioni 42), jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa na Serikali.

Waziri Mkuu aliwataja watumishi wanaodaiwa kuhusika katika ubadhirifu huo kuwa ni aliyekuwa Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Mwakapala, ambaye kwa sasa amehamishiwa mkoani Songwe, Mhasibu wa Mapato Edward Kilungu na Eliamini Maliki.

Aidha, alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (RPC) kuhakikisha watumishi hao wanatafutwa, wanakamatwa na kuwekwa mahabusu hadi fedha za Serikali zitakapopatikana.

"Mweka Hazina Mwakapala arudishwe, Edward Kilungu na Eliamini Maliki watafutwe. Wakamatwe, wawekwe ndani na wasitoke mpaka fedha ya Serikali irudi," alisema Dkt. Mwigulu.

Aidha, Waziri Mkuu alimuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kuhakikisha watumishi wote waliohusika wanasimamishwa kazi mara moja huku taratibu za kinidhamu na kisheria zikiendelea.

"Barua za kuwasimamisha kazi zitoke leo leo na hatua zinazostahili za kiutumishi zifanyike haraka. Wasitoke mpaka fedha za wananchi zirudi," alisema.

Sambamba na hilo, Dkt. Mwigulu alikemea vitendo vya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka, akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita haitamvumilia mtu yeyote atakayehujumu rasilimali za wananchi.

"Ninachukia uvivu, uzembe, wizi na kuonewa kwa wanyonge. Nitawashikisha adabu wezi, walaghai na wote wanaotumia nafasi zao kuwaumiza wananchi," alisema.

Aidha, alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja na vyombo vya Serikali kwa kugundua na kuanza kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu huo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alikemea tabia ya baadhi ya viongozi kutumia muda mwingi kufikiria uchaguzi na vyeo badala ya kutatua changamoto za wananchi, akisisitiza kuwa Watanzania wanahitaji maendeleo na huduma bora zaidi kuliko siasa za makundi.

"Watanzania wana kiu ya maendeleo. Kiu waliyonayo si ya kugawana madaraka, bali ni maendeleo na kuondoka kwa kero zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku," alisema.

Aliongeza kuwa viongozi wanapaswa kutumia nafasi walizopewa kutatua matatizo ya wananchi badala ya kutumia muda mwingi kufuatilia nafasi nyingine za uongozi.

"Kila mmoja afanye kazi katika nafasi aliyopewa. Watanzania wana shida nyingi zinazohitaji ufumbuzi na si siasa za makundi au mbio za madaraka," alisema.

Pia, Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kusimamia haki za wananchi, kuimarisha uwajibikaji katika utumishi wa umma na kuhakikisha fedha za maendeleo zinafika na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza hatua mbalimbali za kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa elimu bila ada kwa Kidato cha Tano na Sita, Programu ya Samia Scholarship na kuondoa riba kwa mikopo ya elimu ya juu kwa wahitimu ambao hawajapata ajira.

Aidha, alieleza kuwa Serikali imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, Reli ya Kisasa (SGR), miradi ya maji, afya, barabara na usambazaji wa umeme vijijini ili kuharakisha maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.

Waziri Mkuu aliwahakikishia wananchi wa Manyoni na Watanzania kwa ujumla kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha matunda ya maendeleo yanawafikia wananchi wote.

"Niwahakikishie Watanzania kwamba yote yaliyomo kwenye Ilani na ahadi za Mheshimiwa Rais yataendelea kutekelezwa kwa manufaa ya wananchi," alisema.

Photos from Jawabu tz's post 31/05/2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Profesa Kitila Alexander Mkumbo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kuanza Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA2050), tarehe 31 Mei, 2026 Ikulu, Dar es Salaam.

Photos from Jawabu tz's post 31/05/2026

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Ndugu Gilead Teri akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mikakati ya kuvutia uwekezaji wakati wa mkutano wa taarifa ya Tume ya Taifa ya Mipango kuanza Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA2050) tarehe 31 Mei, 2026 Ikulu, Dar es Salaam.

Photos from Jawabu tz's post 31/05/2026

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Ndugu Bakari S. Machumu akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kuanza Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA2050) tarehe 31 Mei, 2026 Ikulu, Dar es Salaam.

31/05/2026

IKULU WIKI HII



31/05/2026

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel:
Ikulu Tanzania na Tovuti: www.ikulu.go.tz


30/05/2026

Madai ya kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inadharau Mahakama ni upotoshaji wa dhahiri. Msajili Msaidizi Sisty Nyahoza, anaeleza ukweli kuhusu zuio hilo la Mahakama.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Dar Es Salaam