23/02/2026
MPYA‼️
TANGAZO LA. NAFASI ZA KAZI.
Ukurasa Rasmi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala
23/02/2026
MPYA‼️
TANGAZO LA. NAFASI ZA KAZI.
20/02/2026
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
19/09/2025
UPASUAJI KUONDOA DAMU ILIYOVILIA KWENYE UBONGO WAFANYIKA KWA MARA YA KWANZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MWANANYAMALA.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala imefanikiwa kwa mara ya kwanza kufanya upasuaji wa ubongo kwa mgonjwa aliyekuwa na damu iliyovilia kwenye ubongo, hatua iliyoweka historia mpya katika utoaji wa huduma za kibingwa katika hospitali hiyo.
Upasuaji huo umefanywa na timu ya madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Mwananyamala, ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali wa kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi na kubadilishana ujuzi wa kitabibu.
Akizungumza kwa niaba ya timu ya wataalamu kutoka MOI Daktari bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya fahamu Dr Brian Minja, amesema ujio wao umeleta manufaa makubwa kwa hospitali hiyo kwani wamefanikiwa kuokoa maisha ya mgonjwa aliyekuwa amepata tatizo la kuvilia damu kwenye ubongo, tatizo lililosababishwa na shinikizo la juu la damu na kupelekea mishipa kupasuka.
Ameongeza kuwa mafanikio katika oparesheni hiyo yamekuwa fursa ya kuwajengea uwezo wa vitendo madaktari wa Mwananyamala na kusaidia kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wakipelekwa rufaa kwenda hospitali za juu kwa ajili ya upasuaji k**a huo.
Kwa upande wake daktari kutoka kitengo cha magonjwa ya dharura na ajali wa hospitali ya Mwananyamala Dr. Joseph Mosha amesema ujio wa madaktari hao kumewaongezea ujuzi na ni sehemu ya matumaini kwa wagonjwa wanaofikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwani sasa baadhi yao wanaweza kufanyiwa upasuaji huo huku wenye changamoto zaidi ndiyo watapewa rufaa.
18/09/2025
WATAALAMU BOBEZI WA UBONGO, UTI WA MGONGO MOI WATIA KAMBI HOSPITALI YA MWANANYAMALA.
Wataalamu bingwa wa ubongo na uti wa mgongo kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) wamewasili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa mpango maalum wa kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa huku wakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa hospitali hiyo ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa matibabu ya wagonjwa wenye changamoto za ubongo na uti wa mgongo.
Kupitia kambi hii madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala wanashiriki kwa pamoja katika uchunguzi na upasuaji jambo linaloongeza uzoefu na kuwapa ujuzi wa kutambua na kusimamia wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka zikihusisha changomoto katika ubongo na kupunguza rufaa za wagonjwa wanaopelekwa Taasisi ya Mifupa MOI wakitokea katika Hospitali hiyo.
Timu hiyo ya wataalamu imegawanywa ili kushirikiana na wataalamu wa hospitali hiyo katika vitengo mbalimbali ikiwemo kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU), upasuaji na kitengo cha dharura hali inayowawezesha kufanya kazi bega kwa bega na watoa huduma wa Hospitali ya Mwananyamala kuanzia hatua za uchunguzi wa awali, matibabu ya kawaida, hadi upasuaji wa dharura na ufuatiliaji wa wagonjwa walioko kwenye hali hatarishi na waliopona.
Huduma zinazotolewa zinajumuisha uchunguzi wa kina wa ubongo na uti wa mgongo, upasuaji wa dharura kwa wagonjwa wa ajali, tiba za kuondoa damu iliyovuja au kuganda kwenye ubongo pamoja na huduma za ufuatiliaji na ushauri wa kitaalamu kwa wagonjwa waliopona.
Wizara ya Afya Tanzania Elimu Ya Afya Taasisi ya Tiba ya Mifupa - MOI
: DAKTARI AELEZA KUHUSU ALIYETOLEWA UVIMBE KG 6.5, ATOA TAHAEHALI HII KWA WANAWAKE.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, akifafanua kuhusu hali ya mgo ngonjwa aliyefanyiwa upasuaji na kutolewa uvimbe kilogramu 6.5, huku akitoa tahadhali kwa wanawake kuweka utaratibu wa kupima afya mara kwa mara kuepuka changamoto k**a hiyo.
12/09/2025
AONDOLEWA UVIMBE WA KG 6.5 ULIOSABABISHA AKOSE MTOTO ZAIDI YA MIAKA 10.
Jopo la Wataalamu na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala leo Septemba 12, 2025 wamefanikiwa kuondoa uvimbe wa kilogramu 6.5 kwa Mwanamke mmoja mkazi wa Morogoro uliopelekea akose mtoto kwa zaidi ya miaka 10.
Akizungumza mara baaada ya kuondolewa uvimbe huo Mwanamke huyo amesema baada ya kuhangaika na changamoto ya kukosa mtoto kwa zaidi ya miaka 10, takribani miezi sita iliyopita alianza kuhisi uvimbe kuongezeka ndipo aliposhauriwa kufika Hospitali ya Mwananyamala wakati alipokuwa kwa Dada yake Jijini humo.
"Kwa miaka mingi nilikuwa naishi kwa maumivu na aibu kwa sababu watu walidhani nina mimba kumbe ni uvimbe, nilipokuja Dar es Salaam kwa dada huko Kimara alinishauri nifike hapa ili kufanyiwa uchunguzi na kujua shida ni nini, hatimaye nilianza kuhudhuria na leo nafurahi kutolewa uvimbe huu kwani najihisi mwepesi" ameeleza mwanamke huyo.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa Magonjwa ya wanawake na Uzazi Hospitali ya Mwananyamala Dkt. Taiba Kassim Haidar amesema mgonjwa huyo alifanyiwa vipimo vya kina baada ya kufika hospitalini miezi sita iliyopita na kubainika kuwa na uvimbe mkubwa uliokuwa unahatarisha afya yake, na kupelekea changamoto ya kukosa mtoto.
“Tulianza kumuona kwenye kliniki zetu alipofika na tukabaini tatizo hili linahitaji kufanyiwa upasuaji na leo tumefanikiwa kuondoa uvimbe huo wenye uzito wa kilogra 6.5 kwa mafanikio, Hali yake ni nzuri na tutaendelea kumfuatilia,” amesema Dkt. Haidar na kuongeza kuwa uvimbe huo utachunguzwa kitaalamu ili kubaini k**a una hatari zaidi.
Jopo la wataalamu na madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, waliohusika katika zoezi hilo ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya wanawake Dkt. Taiba Kassim Haidar, Daktari wa Upasuaji Dkt. Hudhaima Issa na Dkt. Benjamini Uisso, Wauguzi Muuguzi Esther Munisi na Hafsa Ramadhani, Mtaalamu wa dawa za usingizi Pancrasi Haule, na Mteknolojia dawa Mustafa Juma.
Dkt. Haidar ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kufanya vipimo mara kwa mara ili kubaini iwapo wana changamoto zozote za kiafya kwa kuwakuwa kuchelewa kupata matibabu kunahatarisha afya.
09/09/2025
TUNATAFUTA NDUGU ZAKE.
: WANANCHI WATAKIWA KUEPUKA NJIA ZISIZO RASMI ZA KUTIBU MAUMIVU YA VIUNGO VYA MWILI.
Chrispina Gasaya Mfiziotherapia wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, akieleza umuhimu wa kuzingatia njia sahihi za kutibu maumivu ya viungo ili kuepuka athari mbalimbali zinazoweza kujitokeza kutokana na kutumia njia zisizo rasmi.
Wizara ya Afya Tanzania Elimu Ya Afya
ONGEZEKO LA MADAKTARI BINGWA CHACHU YA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO- DR GRACE.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dr. Grace Watts, akieleza namna ongezeko la Madaktari Bingwa lilivyochochea kupunguza vifo vya mama na mtoto.
04/09/2025
📍MUHIMU!!👇
6. DAKTARI WA KINYWA NA MENO, Nafasi 2.
Mwombaji awe na Shahada ya Udaktari wa Kinywa na Meno kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari na awe na leseni hai.