Temeke Manispaa

Temeke Manispaa

Share

OFFICIAL TEMEKE MUNICIPAL COUNCIL ACC. UKURASA RASMI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE KATIKA FACEBOOK. Instagram. @temekemanispaa. YouTube. @TMC TV.

Twitter. @temekemanispaa
Facebook. @temekemanispaa

Photos from Temeke Manispaa's post 23/04/2026

FURSA YA AJIRA! πŸ“Œ

Photos from Temeke Manispaa's post 21/04/2026

CAMFED TEMEKE WAKUTANA KUPANGA MIPANGO YA YA UFUATILIAJI WA MAENDELEO YA MTOTO WA K**E.

Wajumbe wa shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kusaidia wasichana walio katika mazingira magumu kupata Elimu Afrika (CAMFED) Wilaya ya Temeke, Leo Aprili 21, 2026 wamekutana katika kikao cha Ufuatiliaji wa maendeleo na ustawi wa wanafunzi wa k**e wanaofadhiliwa na shirika hilo.

Kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbinwa Shule ya Sekondari Kibasila ulilenga kupanga mipango na kutoa semina ya jinsi ya kuwafikia watoto hao na kukusanya taarifa zao kutoka katika Shule mbalimbali Wilayani Temeke.

Kikao hicho kilimalizika kwa wajumbe kuahidi kushirikiana kwa karibu na shule zote zinazohusiana, huku wakisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kila msichana anayefadhiliwa anapata elimu bora na msaada unaohitajika kwa wakati. Wajumbe pia walisisitiza kuwa lengo la CAMFED ni kuhakikisha hakuna msichana anayeachwa nyuma, na kwamba kila jitihada itafanywa ili kuendeleza maendeleo na ustawi wa wanafunzi wa k**e wilayani Temeke.



πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ

20/04/2026

MUHIMU πŸ“ŒπŸ“Œ

Photos from Temeke Manispaa's post 18/04/2026

RC CHALAMILA AMKABIDHI RC KUNENGE MWENGE WA UHURU 2026 TAYARI KUKIMBIZWA KATIKA MKOA WA PWANI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Aprili 18, 2026 ameukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Pwani baada kukimbizwa kwa siku tano katika Mkoa huu ambapo Miradi yote ya Maendeleo katika Wilaya zote 5 za Mkoa wa Dar es Salaam imepitishwa na Mwenge wa Uhuru kwa Asilimia 100 hakuna Mradi uliokataliwa.

Mwenge wa Uhuru 2026 ulianza kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es salaam April 13, 2026 ukianza Wilaya ya Ilala, April 14, 2026 Kigamboni, April 15, 2026 Temeke, April 16, 2026 Ubungo na April 17,2026 umehitimishwa Wilaya ya Kinondoni.

Katika Mkoa wa Dar es Salaam Mbio za Mwenge wa Uhuru zikiongozwa na Ndg. Wazo Michael Mwang'onda Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ameongoza kuukimbiza Mwenge huo umbali wa Km 392.22 ukitembelea, kukagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi 35 ya maendeleo yenye thamani zaidi ya Bilioni 113.5 ambapo Miradi yote imepitishwa na Mwenge wa Uhuru kwa kishindo hakuna Mradi uliokataliwa.

Aidha Mwenge wa Uhuru ukiwa unakimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa umeendelea kuelimisha jamii na kuwahamasisha wananchi kupitia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo "Tanzani ni Yetu Sote Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo" pamoja kuhamasisha wananchi mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Rushwa na mapambano dhidi ya Madawa ya kulevya.

Kwaheri Mwenge wa Uhuru na Kila la Kheri Mkoa wa Pwani!

17/04/2026

Tazama Kiongozi wa Mbio wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 Ndg. Wazo Mwang'onda alivyopanda Jukwaani kuimba kuungana Wana Temeke katika Viwanja vya Msufini Chamazi!

Mwenge wa Uhuru 2026 kwetu ulileta tumaini, upendo na furaha kubwa! ulikuwa ni wakati mzuri sana.

Mwenge ni wetu sote tushirikiane kwa Pamoja kuleta Maendeleo.



πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ

17/04/2026

Ukisikia TEMEKE uliza kuna nini? Alafu wahi fasta, maana tunakuhakikishia hatujawahi kuwa na Shughuli iliyododa!

Mwenge wa Uhuru 2026 kwetu ulileta tumaini, upendo na furaha kubwa! ulikuwa ni wakati mzuri sana.

Mwenge ni wetu sote tushirikiane kwa Pamoja kuleta Maendeleo.

Photos from Temeke Manispaa's post 17/04/2026

"MWENGE NI WETU SOTE,TANZANIA NI YETU SOTE, TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KULETA MAENDELEO"

Photos from Temeke Manispaa's post 16/04/2026

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando ikiwa ni mwendelezo wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ndg. Wazo Mwang'onda akiwa Kiongozi wa Mbio hizo.

"Mwenge ni wetu sote, Tanzania ni yetu sote. Tushirikiane kuleta Maendeleo"



πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ

16/04/2026

KIMEWAKA HAKIJAWAKA?

Tunasepa na Kijiji leo!

Mwenge wa Uhuru Bado tunao hapa Chamazi Viwanja vya Msufini mpaka Kukuche!

"MWENGE NI WETU SOTE TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KULETA MAENDELEO"

Photos from Temeke Manispaa's post 16/04/2026

"MWENGE NI WETU SOTE, TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KULETA MAENDELEO"

Tumeupokea, Tumeukimbiza na tumekesha nao

Yaliyojiri leo Aprili 15, 2026 na huu ni mkusanyiko wa Picha mbalimbali.

Bado tunao hapa Chamazi Viwanja vya Msufini, tunapiga Ngoma juu ya Ngoma, Burudani Kibaooo!

Magodoro tumelowesha Maji hatulali leo hadi Jogoo aseme!

15/04/2026

Barobaro 'on stage' akitoa burudani kwenye Usiku wa Mwenge Temeke 2026.

Burudani mpaka majogoo!

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

46343
Dar Es Salam