Tanzania Kaanani ya Afrika.

Tanzania Kaanani ya Afrika.

Share

Jukwaa la kizalendo kwa ajili ya Mama Tanzania .

10/09/2025

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977.

UTANGULIZI.

MISINGI YA KATIBA.

KWA KUWA,SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru,haki,udugu na amani:_sheria ya 1984 Na.15 ib.3

KWANZA kila siku ya Jumatano.

24/08/2025
23/08/2025

Sikia Ee Tanzania, PASIPO MASHAURI TAIFA HUANGUKA;BALI KWA WINGIBWA WASHAURI HUJA WOKOVU.Mith 11:14.

KWANZA KILA SIKU YA JUMATANO.

22/08/2025

Tunapongia kuishi ndani ya Tanzania mpya, maana ya ule wimbo wa Taifa letu unakwenda kuwa halisi kwa kila mtanzania tofauti na ilivyokuwa wakati wa Tanzania ya zamani,ni kundi la watu fulani ndilo lilikuwa likibarikiwa na utajiri wa taifa letu,Wengine wao walikua ni kuimba tu

..🎼🎵🎶Mungu ibariki Tanzania...wabariki Viongozi wake.....🎼🎵🎶

21/08/2025

"Watanzania wanataka mabadiriko,wasipoyapata,wasipo yaona ndani ya CCM,watayatafuta nje ya CCM"

BABA WA TAIFA MWL.J.K.NYERERE.

21/08/2025

Yale yalio gundulika baada ya miaka 40 kule Bukina Fasso ninaona Historia inakwenda kujirudia na kwetu,TAZAMA NA UTASHUHUDIA KWA MASIKIO NA MACHO YAKO.Si muda mrefu utakiri kwa kinywa chako kwamba hakika JAMBO LOLOTE MAISHANI LIPE MUDA TU,NA UTAAMINI KWAMBA BAADA YA MUNGU, HAKIMU ANAYEFUATIA KWA UAMINIFU NI MUDA PEKEE WENGINE TUSUBIRI.

20/08/2025

SHUKRANI NA PONGEZI KWA NDG.SSH,RAIS WA SITA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Ndg.SSH,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awali ya yote napenda kumshukuru Mungu sana kwa ajili yako na Watanzania wote kwa ujumla.

Nimeandika makala hii maalum kabisa kukushukuru na kukupongeza kwa kazi nzuri uliyofanya unapoelekea kumaliza majira yako ya Uongozi (2021-2025)Ukiwa Rais wa 6 wa Taifa letu.

Ndg.Rais SSH,Wakati unaipokea nchi yetu Ili kutuongoza tulikuwa katika majonzi na msiba mzito wa kuondokewa na mpendwa wetu hayati JPM,namshukuru Mungu kwa neema ya utulivu aliyoiachilia wakati ule.

Ndg.SSH,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nini ninakupongeza na kukushukuru? Ninafanya hivyo kwa moyo wa dhati kwa sababu tu ya kukamilisha miradi ya kimkakati iliyoachwa na mtangulizi wako JPM,Haikuwa rahisi hata kidogo,na wengi wetu tulifikili isingeweza kukamilika,lakini unapoelekea kumaliza majira ya Uongozi wako,miradiya kimkakati karibia yote imekamilika.SHUKURANI NA PONGEZI NYINGI ZIKUFIKIE NDG.RAIS WETU.

Nakupongeza kwa sababu umeweza kutekeleza miradi hiyo,tazama Ukamilikaji wa ujenzi wa Nyumba ya Watanzania (Ikulu ya Chamwino),Bwawa la Kufua umeme la Mwl.Nyerere,Daraja la JPM,Ukamilikaji wa meli ya Mv.Mwanza hapa kazi tu,unamaliza muhula huu, Reli ya kisasa-SGR ikiwa imeanza kazi zake Dar-Dom na ujenzi unaendelea kuelekea mwanza na kigoma.

Siwezi kusahau kwa Habari ya barabara ya Mzunguko (Ring road) na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha msalato,miradi hii mikubwa miwili ipo jijini Dodoma Fahari ya Watanzania.

Muda hautoshi kuzungumzia miradi mingine ilokuwa ikiendelea huku na kule iloachwa na JPM katika hatua ya ujenzi,nayo haikuishia njiani imeonekana ikitekelezwa.Hongera Ndg.Rais.

Ndg.Rais SSH kwa miaka miwili nimekuwa nikiomba kupitia kurasa zangu za mitandao ya kijamii hasa hapa Facebook nikiomba kukutana na wewe,na maombi yale nilikua nikishare pia kwa wasaidizi wako k**a njia ya kuona unaweza kufikiwa na ujumbe wangu,lakini mpaka muda huu sijaweza kupokea mwaliko wako,au inawezekana nilikosea utaratibu?

Nina fahamu una majukumu mengi ya kitaifa,na siko hapa kukulaumu japo nilitamani k**a tungeonana,maana nilikuwa na ushauri wa kukueleza,na sidhani kwa muda huu ulobakia k**a ushauri huo unaweza kukusaidia.

Na siko hapa kuwalaumu wasaidizi wako,japo najua fika ujumbe wangu waliupata,sasa sijajua k**a walipuuza au bado wanaufanyia kazi ili waone namna sahihi ya kuniita ili nikikutane nawe Ndg.Rais wetu.

Ndg.Rais wetu,Mimi ni mwandishi wa vitabu, hivyo katika kipindi hicho kipindi natafuta kuonana nawe,niliandika kitabu kukuhusu kiitwacho...WELEDI WA RAIS SAMIA SULUHU HASSANI KATIKA KUZIGEUZA CHANGAMOTO KUWA FURSA.Ushauri na matarajio ya Watanzania katika Uongozi wake.

Kitabu hiki kimejikita kueleza namna ulivyoingia madarakani wakati wa changamoto kubwa na namna ulivyozitumia changamoto hizo kuwa daraja la kukamilisha miradi ya kimkakati.

Ndg.Rais, mimi si tu mwandishi wa vitabu,lakini pia ni msomi wa Sayansi ya Jamii na Theologia,hivyo nina uwezo wa kuichambua jamii katika jicho la Kisoshologia na Theologia pia kwa sababu ya uwezo huo nilonao,kitabu hiki ni zao la utafiti katika jamii ya Watanzania,nilidodosa Watanzania kile ambacho wangependa kumshauri Rais wao na matarajio yao katika Uongozi wake,kazi hiyo niliifanya na kupata majibu yake.

Na ndio sababu nilitamani sana kuonana nawe ili japo niweze kutoa ushauri na matarajio walio nayo Watanzania katika Uongozi wako,najua kwa sasa huko na mambo mengi zaidi kuliko kipindi cha nyuma kwa kuzingatia tunaelekea mwishoni kabisa wa muhura wako wa Uongozi, hivyo hata huo ushauri na matarajio ya Watanzania sidhani k**a ni sahihi kuyapata kwa sasa,maana sina uhakika na utekelezaji wake kwa muda huu mchache ulobakia.NA KWA KUWA MUDA UMEISHA,MIMI NITUMIE MAKALA HII KUKUSHUKURU NA KUKUPONGEZA KWA KAZI NZURI YA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI ILIYOACHWA NA MTANGUKIZI WAKO.

Nakumbuka kuna makala yangu moja ilopita niliwaambia wasomaji wangu na Watanzania kwa ujumla kwamba ifikapo mwezi wa 7 kitabu hicho kitakua sikoni,lakini haijakuwa hivyo,naomba kutumia makala hii kuwambia wasomaji wangu waliokuwa wakikisubiri kitabu hicho kwa shauku kubwa kwamba kwa sababu ya mazingira yaliyojitokeza nje ya uwezo wangu kitabu hicho hakitoweza kuwa sokoni,mpaka pale mbingu zitakapo amua vinginevyo.Mnisamehe tu kwa sababu najua wazi mlikingoja sana.

Kwa makala hii itoshe KUTAMBUA,KUMPONGEZA NA KUMSHUKURU NDG.RAIS WETU KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI,NA MIMI NILISEMA NIKIWA RAIA WA NCHI YANGU TANZANIA NIIPENDAYO KWA MOYO WANGU WOTE,NILIAHIDI KUFANYA MAMBO 4 RAIS NA VIONGOZI WANGU.

✅Kuwashukuru na Kuwapongeza pale wanapofanya vema.

✅Kuwaonya kwa upendo pale wanapokwenda ndivyo sivyo.

✅.Kuwashauri kwa hekima kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao,na

✅.Kuwaombea kwa moyo wangu wote.

Mambo haya nimekua nikiyafanya kipindi cha Uongozi wako na maadam niko hai nitayafanya kwa Viongozi wangu wote baada yako pasipo kujipendekeza 'uchawa'

Hivyo Ndg.Rais,Makala hii imejielekeza katika eneo lile la kwanza:Pongezi na Shukrani.

Ndg.SSH,napoitimisha makala hii maalum kwako,narudia tena kukushukuru na kukupongeza kwa ukamilishaji wa miradi ya kimkakati iliyoachwa na mtangulizi wako.

KWA WATANZANIA WENZANGU,BINAFSI SIWEZI KUSEMA "OKTOBA TUNATIKI"✅ AU "OKTOBA HATUTIKI"❎ NIKIWA MHUDUMU WA INJILI NA WAKILI WA SIRI ZA MUNGU NIWEZALO KUSEMA LENYE UHAKIKA NI ILI "MAPENZI YA MUNGU YATIMIZWE JUU YA TAIFA LA TANZANIA " NA PIA NI MAOMBI YANGU MBELE ZA BWANA NIKAWE MIONGONI MWA WATAKAO YASHUHUDIA MAPENZI HAYO YA MUNGU KWETU,NA NINA AMINI KWA KUWA MUNGU ANALIPENDA TAIFA LETU,MAPENZI HAYO YATAKUWA MEMA SANA WALA SIO MABAYA.AMeN!

Mungu mbariki Rais wetu,SSH.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.

✝️Yesu Kristo,Jina lipitalo kila jina.

✍Mwl.Mazumila,E.K,Ph.D
Mtanzania na Mzalendo no.7
0768383818,
Dodoma HQ.

Wed,20 Aug 2025.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Dodoma