Ucsaf-Tanzania

Ucsaf-Tanzania

Share

UCSAF ilianzishwa na Serikali kwa lengo la kufanikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo yasio na mvuto kwa watoa huduma ya mawasiliano nchini.

13/05/2026

Mhandisi Mwalami Kapipi kutoka Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini akizungumza na wasikilizaji wa Redio Access FM jijini Mbeya, amefafanua kwa kina utekelezaji wa miradi ya mawasiliano inayosimamiwa na UCSAF nchini.

Ameeleza jinsi miradi hiyo inavyolenga kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za mawasiliano, hususan katika maeneo ya vijijini na pembezoni, na namna inavyochangia kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi kupitia kuboresha mawasiliano.

Photos from Ucsaf-Tanzania's post 13/05/2026

📍JINSI YA KUPIGA KURA

https://www.itu.int/net4/wsis/stocktaking/Prizes/2026/Vote?jts=T9UKMM

KIPENGELE CHA MRADI: AL C2. INFORMATION AND COMMUNICATION INFRASTRUCTURE

JINA LA MRADI: CONSTRUCTION OF 758 TELECOM TOWERS UNDER DIGITAL TANZANIA PROJECT.

▶️Kisha VOTE FOR THIS PROJECT.

MWISHO WA KUPIGA KURA NI LEO TAREHE 13 MEI, 2026

Piga kura sasa tuwakilishe Tanzania kimataifa!

11/05/2026

📍TUTAKUWA MBASHARA
Kupitia Shalom FM Redio 97.3 kesho tarehe 12 Mei, 2026.

📍Mada: Uboreshaji wa huduma za mawasiliano unaofanywa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ( UCSAF). Tukiangazia zaidi Mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

05/05/2026

📍TUTAKUWA MBASHARA
Kupitia Access FM Mbeya, leo tarehe 5 Mei, 2026 kuanzia saa 11 ( saa kumi na moja) hadi saa 12 (saa kumi na mbili) jioni.

📍Mada: Uboreshaji wa huduma za mawasiliano unaofanywa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ( UCSAF) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Mhandisi Mwalami Kapipi atakuwa studio muda huo, USIKOSE.

04/05/2026

📌MRADI WA UJENZI WA MINARA 758 KUSHINDANIA TUZO ZA WSIS 2026.

📍JINSI YA KUPIGA KURA, FUATA MAELEKEZO HAYA

➡️Tumia kiunganishi (link) hii kujisajili.

https://www.itu.int/net4/wsis/stocktaking/Prizes/2026/Vote?jts=T9UKMM

Fuata maelekezo ya kujaza taarifa zako na mwisho unabonyeza sehemu iliyoandikwa REGISTER. Baada ya hapo utapokea barua pepe ( email) ili kuthibitisha akaunti yako.

➡️ Ingia kwenye tovuti ya WSIS ambapo utajaza taarifa zako.

➡️Fungua fomu ya kupigia kura.

KIPENGELE CHA MRADI: AL C2. INFORMATION AND COMMUNICATION INFRASTRUCTURE

JINA LA MRADI: CONSTRUCTION OF 758 TELECOM TOWERS UNDER DIGITAL TANZANIA PROJECT.

➡️Kisha bonyeza VOTE FOR THIS PROJECT.

04/05/2026

.

03/05/2026

Je, unajua unaweza kusaidia Tanzania kushinda tuzo za kimataifa?

Ni rahisi sana 👇

1️⃣ Jisajili WSIS (thibitisha email)
2️⃣ Ingia kwenye akaunti yako
3️⃣ Nenda: WSIS Prizes > Vote > Voting Form

Kisha piga kura kwa miradi yetu 👇
✅ Jamii Stack (AL C1)
✅ Minara 758 ya Mawasiliano (AL C2)
✅ Cyber Champions (AL C5)

👉 Bonyeza Vote For This Project kwa kila mmoja

Asante kwa kura yako! 🙌Shirikisha na wengine tushinde pamoja.


Reposted from

Photos from Ucsaf-Tanzania's post 01/05/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe, ambapo amewataka wafanyakazi kuendelea kuwa chachu ya uzalishaji, kuongeza ufanisi na kuzingatia nidhamu katika maeneo yao ya kazi ili kuchochea maendeleo endelevu ya Taifa.

Watumishi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wameshiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo ya kitaifa, wakionesha mshik**ano na wafanyakazi wengine kutoka sekta mbalimbali nchini.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo: “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”

.

Photos from Ucsaf-Tanzania's post 01/05/2026

Wafanyakazi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), wameungana na wafanyakazi wengine wa Mkoa wa Dodoma kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi 2026’, yaliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Dodoma.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. RoseMary Senyamule, ambaye alisisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uzalendo ili kuchochea maendeleo endelevu ya nchi. Aidha, alitambua mchango wa wafanyakazi katika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu yameongozwa na kaulimbiu isemayo: “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050,”

.

01/05/2026

Kupitia upatikanaji wa huduma za mawasiliano, wakazi wa kijiji cha Msolokelo wilayani Mvomero katika mkoa wa Morogoro sasa wanaweza kuwasiliana kwa urahisi zaidi, kupata taarifa muhimu kwa wakati, na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Aidha, mawasiliano yamechochea ukuaji wa biashara ndogo ndogo, ambapo wafanyabiashara wanatumia mitandao ya simu kuagiza na kutangaza bidhaa zao, kupokea malipo kwa njia za kidijitali, na kupanua wigo wa wateja wao hata nje ya kijiji.

Huduma hizi pia zimeboresha upatikanaji wa huduma za kijamii k**a vile afya na elimu, ambapo wananchi wanaweza kupata ushauri wa kitaalamu kwa njia ya simu au mtandao bila kulazimika kusafiri umbali mrefu.

Kwa ujumla, kukamilika kwa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini imekuwa chachu ya maendeleo katika Kijiji cha Msolokelo, yakichangia kuinua uchumi wa wananchi na kuboresha ustawi wa maisha yao kwa kiasi kikubwa.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Jengo La UCSAF, S. L. P 1957, 10 Barabara Ya UCSAF, Makulu
Dodoma
41107

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00