Tume ya Umwagiliaji

Tume ya Umwagiliaji

Share

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanzishwa kwa Sheria Na.04 ya Taifa ya Umwagiliaji ya mwaka 2013.

02/05/2026

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AHIMIZA WANANCHI KULINDA MIRADI YA UMWAGILIAJI

​📍Makambako, Njombe.

​Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewataka wananchi wa Wilaya ya Makambako mkoani Njombe na Watanzania kwa ujumla kuilinda na kuithamini miradi ya Umwagiliaji inayotekelezwa na Serikali kwa kuwa ni mali yao iliyolenga kuwakwamua kiuchumi.

Akizungumza na wananchi Wilayani Makambako, Waziri Mkuu Majaliwa, amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa kwa kubadilisha mfumo wa kilimo kutoka kutegemea mvua pekee na kuelekeza nguvu kwenye sekta ya Umwagiliaji nchi nzima.

​Mhe. Waziri Mkuu ameeleza kuwa Serikali imefanya maboresho makubwa ambapo miradi ya Umwagiliaji imeongezeka kutoka miradi 13 iliyokuwepo awali hadi kufikia miradi 780 inayotekelezwa hivi sasa.

Aidha, ameongeza kuwa eneo la kilimo cha Umwagiliaji limepanuliwa kutoka hekta 560,000 hadi kufikia hekta 980,000, huku lengo likiwa ni kuvuka hekta milioni moja hivi karibuni.

Alisisitiza kuwa bajeti ya sekta ya kilimo pia imepata msukumo mkubwa ikipanda kutoka shilingi bilioni 294 hadi kufikia shilingi trilioni 1.1, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara tano.

​Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mndolwa, ameeleza kuwa katika eneo hilo la Makambako, Serikali inaenda kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 30 katika mradi mkubwa wa Umwagiliaji katika eneo la Idofi Wilayani Makambako.

Amesema, mradi huo utahusisha upanuzi wa eneo la kilimo kutoka hekta 300 zilizokuwa zikitumiwa na wananchi hadi kufikia hekta 1,300, jambo ambalo litaongeza tija na uzalishaji.

​Vilevile, Bw. Mndolwa amebainisha kuwa mradi huo utajumuisha ujenzi wa stendi ya magari, soko la kisasa, na miundombinu ya kuhifadhia mbogamboga ili kusaidia wananchi kupata soko na kuzuia upotevu wa mazao baada ya kuvuna.

Aidha Mndolwa amesema kuwa mkandarasi ameshapatikana na mkataba wa kuanza wa kazi hiyo unatarajiwa kusainiwa wiki ijayo ili utekelezaji wake uanze mara moja kwa faida ya wananchi wa Makambako.

01/05/2026

Heri ya Siku ya Wafanyakazi

#

30/04/2026

29/04/2026

29/04/2026


29/04/2026

NIRC YABAINISHA MIKAKATI YA KUIMARISHA UMWAGILIAJI BAJETI YA 2026/27

📍Dodoma

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imebainisha vipaumbele vyake kuelekea makadirio ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikilenga kuongeza tija na kuhakikisha usalama wa chakula nchini.

Akizungumza katika mahojiano maalumu mjini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Bw. Raymond Mndolwa, amesema kuwa bajeti hiyo imejikita katika kuimarisha miundombinu ya Umwagiliaji ili kumkomboa mkulima kutoka kwenye utegemezi wa mvua.

Mndolwa amefafanua kuwa mikakati hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Agenda 10/30, inayolenga kuifanya sekta ya kilimo kukua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

Alitaja maeneo ya kimkakati yatakayopewa kipaumbele kuwa ni pamoja na upanuzi wa maeneo mapya ya Umwagiliaji , ukarabati wa miundombinu ya zamani k**a mifereji na mabwawa, pamoja na kuhimiza matumizi ya teknolojia za kisasa zinazookoa maji.

"Tumejipanga kuhakikisha kuwa kila shilingi itakayotengwa inaleta tija kwa mkulima wa chini. Umwagiliaji ndiyo mhimili wa kilimo cha kisasa, na bila miundombinu imara hatuwezi kufikia malengo yetu," alisema Mndolwa.

Aidha, Mndolwa amewahakikishia wananchi kuwa Tume itakuwa makini katika kusimamia fedha hizo ili miradi yote itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati ili kuleta matokeo ya haraka katika uzalishaji.

Hatua hii imekuja wakati Wizara ya Kilimo ikiendelea na mchakato wa kuwasilisha makadirio ya bajeti yake bungeni, huku sekta ya Umwagiliaji ikionekana kuwa kipaumbele cha kwanza cha serikali katika kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia Kilimo cha Umwagiliaji.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Dodoma

Opening Hours

Monday 08:00 - 15:30
Tuesday 08:00 - 15:30
Wednesday 08:00 - 15:30
Thursday 08:00 - 15:30
Friday 08:00 - 15:30