ushirika_tcdc

ushirika_tcdc

Share

T u me ya Ushirika

Photos from ushirika_tcdc's post 14/05/2026

TCDC YATOA MAFUNZO YA KIMKAKATI KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA ZANZIBAR

Tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Ushirika Zanzibar inatoa mafunzo ya kimkakati kwa Maafisa Ushirika, wanachama, viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika Zanzibar.

Mafunzo yanayotolewa ni juu ya Uanachama wa kimkakati, Masoko ya kimkakati na endelevu na Ushirika biashara. Jumla ya maafisa Ushirika 11 upande wa Zanzibar wanachama, viongozi na watendaji 310 watanufaika na mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yameanza 11 Mei, 2026, ambapo yanaongozwa na Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo, Grace Msambaji, pamoja na Maafisa wengine kutoka Tume na Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU).

Aidha, timu hiyo ilipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ajira, Vijana na Uwezeshaji Zanzibar, Khalid Wazir, kwa uratibu wa Mrajis na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirika Zanzibar, Zainabu Hassan na Wakurugenzi mbalimbali wa wizara.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Randama ya Ushirikiano (MoU) baina ya TCDC na idara ya Màendeleo ya Ushirika Zanzibar.

Photos from ushirika_tcdc's post 13/05/2026

RC MTWARA AWASHAURI VIONGOZI DODOMA KUWAHIMIZA WAKULIMA KUTUMIA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanal Donald Msengi, amewashauri Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali kuwahimiza wakulima kutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ili kuleta mabadiliko chanya kiuchumi na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao.

Akizungumza leo Mei 13, 2026 wakati wa Mafunzo ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa Viongozi wa Chama na Serikali kutoka mkoa wa Dodoma yaliyofanyika mkoani Mtwara, Kanal Msengi amesema mfumo huo umeleta mafanikio makubwa kwa vyama vya ushirika mkoani humo kwa kuviwezesha kuwa imara kiuchumi. Ameeleza kuwa kupitia mfumo huo, vyama vimefanikiwa kufanya uwekezaji mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maghala, ununuzi wa magari, uanzishaji wa viwanda pamoja na kuchangia huduma za kijamii k**a elimu, afya na maji.

“Ni muhimu viongozi mkatumia nafasi zenu kuwahamasisha wakulima na wanaushirika kutumia mfumo huu, kwani umeleta manufaa makubwa na una uwezo wa kuleta mageuzi chanya kwa sekta ya kilimo,” amesema Kanal Msengi.

Naye Kaimu Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Mtwara, Robert Nzunza, amebainisha hatua muhimu za mchakato wa stakabadhi za ghala kuwa ni pamoja na maandalizi ya msimu wa mauzo, ukusanyaji wa mazao ghalani, usafirishaji wa mazao kwenda ghala kuu, mapokezi ya mazao, mauzo kupitia minada ya mtandao, malipo ya fedha kupitia vyama vikuu (Unions), malipo kwa wakulima na wadau, pamoja na utoaji wa mizigo ghalani.

Kwa upande wake Mkuu wa msafara huo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka mkoa wa Dodoma, Donald Mejetii, amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo viongozi hao ili waweze kuwahamasisha wakulima wa Dodoma kutumia mfumo huo kwa tija zaidi.

Viongozi wa Chama na Serikali kutoka mkoa wa Dodoma wapo mkoani Mtwara kwa ziara ya kujifunza Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika vyama vya ushirika na namna unavyoweza kuinua kipato cha mkulima. Katika ziara hiyo pia wametembelea Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU LTD pamoja na Chama cha Msingi Mayanga AMCOS.

Photos from ushirika_tcdc's post 12/05/2026

VIONGOZI DODOMA ZIARANI MTWARA KUJIFUNZA KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA

Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi Mkoa na Wilayani wakiambatana na Viongozi wa Serikali mkoa wa Dodoma wameanza safari ya Kikazi kuelekea mkoani Mtwara kwenye Vyama Vikuu na Vyama vya Ushirika vya Msingi.

Viongozi hao wakingozana na Mrajis Msaidizi wa mkoa wa Dodoma, Joseph Chitinka na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Dodoma, Theresia Nyoka wameanza ziara hiyo leo Mei 12, 2026 kutokea mkoani Dodoma kuelekea mkoani humo.

Mrajis Msaidizi wa mkoa wa Dodoma ameeleza lengo la ziara hiyo ni kuwajengea uwezo, kujifunza utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye Vyama Vikuu na Vyama vya Msingi vya Ushirika mkoani Mtwara na hivyo kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kiushirika ndani ya Mkoa wa Dodoma.

Ziara hiyo inafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Mei 13 hadi 14, 2026 na kuwahusisha Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa, Wenyeviti wa CCM Wilaya Mkoani Dodoma, Sekretariti ya Mkoa CCM, baadhi ya Makatibu wa Chama wilaya na Wenezi, Makatibu, Makatibu Tawala Uchumi na Uzalishaji Viwanda na Biashara na Kilimo.

Photos from ushirika_tcdc's post 11/05/2026

Karibu Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoa wa Kilimanjaro

11/05/2026

Manda wa Kakao Leo Mei 11, 2026 CHAMA Kikuu cha Ushirika KYECU LTD

Photos from ushirika_tcdc's post 11/05/2026

MAKARANI NA MAMENEJA AMCOS LINDI WAJENGEWA UWEZO WA MIFUMO YA TEHAMA

Chama kikuu cha Ushirika cha mkoa wa Lindi, Lindi Mwambao LTD kwa kushirikiana na Kampuni ya Rotai pamoja  na Maafisa Ushirika wa Halmashauri ya Mtama na Lindi Manispaa wametoa Mafunzo ya maboresho ya mfumo wa makusanyo ya mazao ya wakulima kupitia mizani za kidigitali (Kilimo Ujazo) kwa Makarani wa Vituo.

Mafunzo hayo yametolewa na Kampuni ya Rotai Mei 9, 2026 kwa lengo la kuandaa taarifa za masagirisho (PND) kutoka katika matawi ya Chama cha Msingi kwenda ghala Kuu kupitia Mfumo huo.

‎Afisa TEHAMA wa kampuni ya Rotai, Tumaini Lupaso amesema amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia Vyama  kupima mazao yao kwa uhakika na kuandaa taarifa za masafirisho (PDN) kutoka katika matawi ya chama cha msingi kwenda Ghala kuu kupitia mfumo  wa KILIMO UJAZO tofauti na njia ya awali ambapo taarifa hizo zikiandaliwa kwenye makaratasi, lakini pia   kuwawezesha Mameneja kupitia Mfumo wa KILIMO HUB  kuona taarifa mbalimbali za makusanyo ya Matawi yake pamoja na makusanyo ya mazao ya wakulima katika ngazi ya AMCOS.

‎Kwa upande wake, Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Mtama, Emanuel Yohana amesema maboresho hayo yanaenda kuongeza uwazi wa Taarifa na uwajibikaji katika AMCOS ambapo kupitia mfumo wa KILIMO HUB unawawezesha wadau mbalimbali(maafisa ushirika na wataalamu wa chama kikuu)  kuingia na kuangalia moja kwa moja  taarifa za makusanyo ya AMCOS katika ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa kwa ujumla.

‎Mafunzo hayo ya siku moja yameambatana na Mafunzo ya Mfumo wa Kilimo Hub kwa mameneja wa AMCOS wa Halmashauri ya Mtama na Lindi Manispaa.

Photos from ushirika_tcdc's post 09/05/2026

Matumizi ya MIZANI ya Kidigitali kupima Mazao ya Wakulima kuondoa Dhuluma. Morogoro yazindua utekelezaji wake.

09/05/2026

Karibu Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Tanga, 2026

Photos from ushirika_tcdc's post 09/05/2026

Benki ya Ushirika yazindua Tawi Mtwara

Benki ya Ushirika (Coop Bank) inaendelea kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wanachama wake na Watanzania kwa ujumla Kwa kuzindua rasmi tawi lake jipya mkoani Mtwara, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha Uchumi Jumuishi nchini.

Tawi hilo limezinduliwa na Mhe. Kanali Donald Msengi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, 8 Mei, 2026 huku akipongeza Benki ya Ushirika kwa kuendelea kuwekeza mkoani humo na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji.

Photos from ushirika_tcdc's post 08/05/2026

VIJANA WA USAFIRISHAJI DODOMA WAHAMASISHWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA USHIRIKA KUPITIA SGR

​Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania imefanya zoezi la uhamasishaji kwa vijana 57 kujiunga na Ushirika wanaojishughulisha na usafirishaji wa bodaboda, bajaji, na taxi katika stesheni ya SGR - Samia Suluhu Hassan, mkoani Dodoma.

Uhamasishaji huo umefanyika Mei 7, 2026, uliokuwa na lengo la kuwaelimisha vijana hao namna ya kuungana na kuanzisha vyama vya ushirika ili kunufaika na fursa pana za kiuchumi zinazochipuka kutokana na mradi huo mkubwa wa reli ya kisasa.

​Wakizungumza na vijana hao, Mrajis msaidizi - Uhamasishaji, Ibrahim Kadudu na Ndimolwo Laizer, Afisa Ushirika Mwandamizi walibainisha kuwa eneo la SGR limegeuka kuwa kitovu cha uchumi mdogo (micro-economy) kinachounganisha biashara na huduma mbalimbali.

Aidha, Vijana hao walihimizwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wajipange kwa kuanzisha mifumo ya kidigitali, kuboresha huduma za usafirishaji wa mizigo na vifurushi, pamoja na kujenga chapa (brand) yenye uaminifu na usalama ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wanaotumia reli hiyo.

Pia Uhamasishaji ulihusisha ​Wadau wengine wakiwemo jeshi la Polisi na shirika la DSIK, ambao walisisitiza umuhimu wa ushirika k**a njia bora ya kuwafikia vijana kwa urahisi na kuwapatia elimu ya usimamizi wa fedha.

​Zoezi hilo limepokelewa kwa mwitikio mkubwa ambapo vijana hao wameonyesha utayari wa kuanzisha vyama vya ushirika wa usafirishaji na SACCOS ili kujiimarisha kiuchumi.

Photos from ushirika_tcdc's post 05/05/2026

UHAMASISHAJI WA MFUMO WA STAKABADHI YA MAZAO GHALANI KATIKA MAZAO YA VIUNGO – MUHEZA, TANGA

Wilaya ya Muheza mkoani Tanga imeanza kuhamasisha matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Mazao ghalani hususan katika mazao ya viungo. Uhamasishaji huo umefanyika kwa lengo la kuwawezesha wakulima kuelewa namna mfumo huo unavyofanya kazi na manufaa yake katika kuongeza tija na kipato.

Mazao makuu ya viungo yanayolimwa katika eneo hilo ni pamoja na karafuu, pilipili manga, iliki na mdalasini. Uhamasishaji huo umefanyika katika chama cha ushirika cha ZIMISA AMCOS, chenye jumla ya wanachama 364. Wakulima wamepatiwa uelewa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazao yao kwenye maghala yaliyoidhinishwa, kutumia mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani k**a njia ya kuboresha masoko na kuongeza thamani ya mazao yao.

Kwa ujumla, uhamasishaji huu unatarajiwa kuongeza ufanisi katika mnyororo wa thamani wa mazao ya viungo, kuimarisha ushirika, na kuinua kipato cha wakulima katika Mkoa wa Tanga.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Kuu Street
Dodoma