TMDA

Website

TMDA Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from TMDA, Government Organization, Dodoma.

TMDA wahimiza wataalam wa afya Kibaha kuzingatia maadili ktk kusimamia dawa tiba zenye asili ya kulevya ili dawa hizo zi...
21/09/2026

TMDA wahimiza wataalam wa afya Kibaha kuzingatia maadili ktk kusimamia dawa tiba zenye asili ya kulevya ili dawa hizo zisiingie mtaani kinyume na sheria, hayo yamejiri wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa wataalam wa afya wanaosimamia mnyororo wa dawa tarehe 18/09/2026.

Mnamo tarehe 19 Septemba 2026, TMDA ilitembelea Kiwanda cha MSD cha Uzalishaji wa Glovu, Idofi, Njombe, kutoa mwongozo w...
20/09/2026

Mnamo tarehe 19 Septemba 2026, TMDA ilitembelea Kiwanda cha MSD cha Uzalishaji wa Glovu, Idofi, Njombe, kutoa mwongozo wa kiudhibiti ili kuhakikisha uzalishaji wa glovu salama na zenye ubora, kwa ajili ya kulinda afya na usalama wa jamii.

Baraza la Saba la Wafanyakazi wa TMDA lapatiwa mafunzo ya kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika kutekeleza majukumu y...
20/09/2026

Baraza la Saba la Wafanyakazi wa TMDA lapatiwa mafunzo ya kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya udhibiti na kulinda afya ya jamii. Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 16 Septemba 2026, Iringa.

19/09/2026
Wakurugenzi na Mameneja wapatiwa mafunzo ya GIAMIS tarehe 15 Septemba 2026, Iringa, kwa lengo la kuimarisha uwajibikaji ...
16/09/2026

Wakurugenzi na Mameneja wapatiwa mafunzo ya GIAMIS tarehe 15 Septemba 2026, Iringa, kwa lengo la kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika udhibiti wa mifumo na utekelezaji wa majukumu ya kulinda afya ya jamii.

16/09/2026
  HABARILEO with .repost・・・DAR ES SALAAM; MAMLAKA ya Dawa na Vifaatiba (TMDA) imesema itateketeza dawa na vifaatiba vyen...
10/09/2026

HABARILEO with .repost
・・・
DAR ES SALAAM; MAMLAKA ya Dawa na Vifaatiba (TMDA) imesema itateketeza dawa na vifaatiba vyenye thamani ya Sh milioni 300 vilivyokamatwa Septemba 7 na 9, mwaka huu mkoani Dar es Salaam.
-
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dk Adam Fimbo alisema kushirikiana na Jeshi la Polisi ilibaini uingizaji haramu wa shehena ya dawa kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) zilitoka nchini India na zikiwa zimehifadhiwa katika masanduku 20.
-
““Dawa hizo hazijasajiliwa nchini hivyo ubora, usalama na ufanisi wake haukuwa umethibitishwa na TMDA.
-
“Hatua ya kuteketeza inalenga kulinda afya za wananchi dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo ubora, usalama na ufanisi wake haujathibitishwa na mamlaka,” amesema.
-
Amesema Septemba 9, 2026, TMDA ilibaini shehena nyingine iliyokuwa na dawa za sindano, zikiwemo lignokeni, bupivakeni, adrenalini na vitamini.
-
“Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa shehena hiyo ilikuwa na viambata hai vinavyotumika katika dawa za kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani, kifafa, shinikizo la juu la damu na kisukari, pamoja na dawa zinazotumika katika kupunguza unene. Pia kulikuwa na vifaatiba vya meno bandia,” alisema Dk Fimbo.
-
Alisema TMDA itaendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kubaini na kuwachukulia hatua wahusika wa uingizaji na biashara ya bidhaa tiba kinyume cha sheria.
-
Dk Fimbo alisema TMDA imeimarisha mifumo ya ukaguzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuongeza ukaguzi wa kushtukiza katika mipaka, viwanja vya ndege na bandarini, pamoja na kutumia vifaa vya kisasa kupima ubora wa bidhaa tiba.
-
Zaidi tembelea //www.habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Aveline Kitomary

Address

Dodoma
1253

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TMDA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share