14/05/2026
SERIKALI YATOA SIKU 3 KWA WACHIMBAJI, WANUNUZI KUWASILISHA GHARAMA ZA UZALISHAJI JASI🇹🇿
Wachimbaji wapendekeza kupandishwa bei ya madini ya jasi kutokana na gharama kuongezeka
📍 Dodoma
Wizara ya Madini imetoa siku tatu kwa wachimbaji na wanunuzi wa madini ya jasi kuwasilisha mchanganuo wa gharama za uzalishaji ili kupata suluhisho litakalowanufaisha pande zote katika biashara ya madini hayo.
Agizo hilo limetolewa leo Mei 14, 2026 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, wakati wa kikao kati ya wachimbaji wa madini ya jasi na wanunuzi zikiwemo kampuni za saruji na wazalishaji wa gypsum kilichofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Tume ya Madini.
Dkt. Kiruswa amesema Serikali inahitaji kila upande kuwasilisha kwa kina changamoto zinazoukabili ili kufanya uchambuzi utakaosaidia kufikia muafaka wenye manufaa kwa wachimbaji, wanunuzi na watumiaji wa mwisho.
“Tunataka kila upande uainishe vitu vinavyouumiza upande mmoja na vinavyoubeba upande mwingine ili baada ya uchambuzi huo tupate suluhisho la pamoja,” amesema Dkt. Kiruswa.
Aidha, ameahidi Serikali kuyafanyia kazi malalamiko kuhusu tozo mbalimbali zinazotozwa na baadhi ya halmashauri ambazo zimeelezwa kuwa zinaongeza gharama za uzalishaji na biashara ya madini ya jasi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Jasi Mkoa wa Lindi, Salum Kassim, amesema bei ya madini hayo haijawahi kuongezeka tangu mwaka 2016 licha ya kupanda kwa gharama za uzalishaji ikiwemo mafuta, vipuri vya mitambo na mishahara ya wafanyakazi.
Amesema hali hiyo imeathiri uzalishaji na kufanya wachimbaji wengi kushindwa kupata faida kutokana na biashara hiyo.
Katika mapendekezo yao, wachimbaji wamependekeza bei ya tani moja ya jasi kwa Dar es Salaam na Pwani iongezwe kutoka shilingi 110,000 hadi 150,000, Mkoa wa Mtwara kutoka shilingi 75,000 hadi 95,000, Mkuranga kutoka shilingi 95,000 hadi 130,000 huku eneo la Kiranjeranje bei ikipendekezwa kuongezeka kutoka shilingi 60,000 hadi 75,000 kwa tani.
Kwa mujibu wa Kassim, marekebisho ya bei yatasaidia kufufua uzalishaji wa madini hayo na kuboresha maisha ya wachimbaji ambao kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa za uendeshaji.
inaendelea..
14/05/2026
SERIKALI YATOA SIKU 3 KWA WACHIMBAJI, WANUNUZI KUWASILISHA GHARAMA ZA UZALISHAJI JASI
*Wachimbaji wapendekeza kupandishwa bei ya madini ya jasi kutokana na gharama kuongezeka*
📍 Dodoma
Wizara ya Madini imetoa siku tatu kwa wachimbaji na wanunuzi wa madini ya jasi kuwasilisha mchanganuo wa gharama za uzalishaji ili kupata suluhisho litakalowanufaisha pande zote katika biashara ya madini hayo.
Agizo hilo limetolewa leo Mei 14, 2026 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, wakati wa kikao kati ya wachimbaji wa madini ya jasi na wanunuzi zikiwemo kampuni za saruji na wazalishaji wa gypsum kilichofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Tume ya Madini.
Dkt. Kiruswa amesema Serikali inahitaji kila upande kuwasilisha kwa kina changamoto zinazoukabili ili kufanya uchambuzi utakaosaidia kufikia muafaka wenye manufaa kwa wachimbaji, wanunuzi na watumiaji wa mwisho.
“Tunataka kila upande uainishe vitu vinavyouumiza upande mmoja na vinavyoubeba upande mwingine ili baada ya uchambuzi huo tupate suluhisho la pamoja,” amesema Dkt. Kiruswa.
Aidha, ameahidi Serikali kuyafanyia kazi malalamiko kuhusu tozo mbalimbali zinazotozwa na baadhi ya halmashauri ambazo zimeelezwa kuwa zinaongeza gharama za uzalishaji na biashara ya madini ya jasi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Jasi Mkoa wa Lindi, Salum Kassim, amesema bei ya madini hayo haijawahi kuongezeka tangu mwaka 2016 licha ya kupanda kwa gharama za uzalishaji ikiwemo mafuta, vipuri vya mitambo na mishahara ya wafanyakazi.
Amesema hali hiyo imeathiri uzalishaji na kufanya wachimbaji wengi kushindwa kupata faida kutokana na biashara hiyo.
Katika mapendekezo yao, wachimbaji wamependekeza bei ya tani moja ya jasi kwa Dar es Salaam na Pwani iongezwe kutoka shilingi 110,000 hadi 150,000, Mkoa wa Mtwara kutoka shilingi 75,000 hadi 95,000, Mkuranga kutoka shilingi 95,000 hadi 130,000 huku eneo la Kiranjeranje bei ikipendekezwa kuongezeka kutoka shilingi 60,000 hadi 75,000 kwa tani.
Kwa mujibu wa Kassim, marekebisho ya bei yatasaidia kufufua uzalishaji wa madini hayo na kuboresha maisha ya wachimbaji ambao kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa za uendeshaji.
Hata hivyo, M
14/05/2026
SHINYANGA YAPAA KWA UCHIMBAJI WA DHAHABU NA ALMASI, YAVUTIA UWEKEZAJI WA VIWANDA
Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga umeendelea kuimarisha nafasi yake k**a kitovu muhimu cha sekta ya madini nchini, huku uchimbaji wa dhahabu na almasi ukitajwa kuwa nguzo kuu ya ukuaji wa uchumi wa mkoa huo na chanzo kipya cha fursa za uwekezaji katika viwanda vya kuongeza thamani ya madini.
Akizungumza mkoani Shinyanga, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo, Mhandisi Noel Odera, amesema mkoa umebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini zikiwemo dhahabu, almasi, madini ya ujenzi pamoja na madini ya viwandani k**a chokaa, hali inayochochea shughuli za kiuchumi, ajira kwa wananchi na ongezeko la mapato ya Serikali.
Amesema shughuli za uchimbaji zinaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali ya mkoa, zikihusisha wachimbaji wadogo, wa kati na migodi mikubwa, ikiwemo migodi ya El-Illari na Williamson Diamond iliyopo Wilaya ya Kishapu katika eneo la kimbaritiki linalozalisha sehemu kubwa ya almasi nchini.
Kwa mujibu wa Mhandisi Odera, utafiti mpya umeibua matumaini ya ongezeko la uzalishaji baada ya wachimbaji wadogo kugundua almasi katika eneo la Ng’wapangabule kwenye mwamba unaofanana na kimbaritiki, hatua inayofungua fursa mpya za uwekezaji na utafiti wa kina wa kijiolojia.
Ameeleza kuwa uzalishaji wa dhahabu unaendelea kuimarika katika maeneo ya Mwakitoryo, Nyandolwa, Mwanubi, Ishinabulandi na Mwazezema ambapo wachimbaji wadogo na wa kati wameendelea kuchangia ukuaji wa sekta hiyo kupitia ajira, kipato binafsi na mapato ya Serikali.
Mbali na uchimbaji, amesema Shinyanga ina mazingira rafiki kwa uwekezaji katika viwanda vya kisasa vya uchenjuaji wa dhahabu vinavyotumia teknolojia za Carbon in Pulp (CIP) na Carbon in Leach (CIL), vitakavyosaidia kuongeza thamani ya madini kabla ya kuuzwa na kuwapa wachimbaji huduma bora za uchenjuaji.
Aidha, amesema mkoa una fursa kubwa za uwekezaji katika viwanda vya utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na almasi ikiwemo vito vya thamani na mapambo, hatua itakayoongeza thamani ya madini ndani ya nchi na kuimarisha uchumi wa viwanda.
Mhandisi Odera ameongeza kuwa uwepo wa malighafi za kutosha k**a chokaa umeifanya Shinyanga kuwa eneo lenye uwezo mkubwa.
14/05/2026
repost from From the heart of Tanzania, we proudly celebrate one of the world’s rarest treasures, Tanzanite 🇹🇿
Today was a truly special experience at where we witnessed the beauty and value of this extraordinary gemstone and received a beautiful Tanzanite jewelry gift, a piece that carries the pride and spirit of Tanzania.
Tanzanite is not only rare, but also a symbol of the richness, elegance, and uniqueness of our nation. Even our crown carries the beauty of Tanzanite, reminding us that we are proudly representing something truly precious to the world.
We are honored to represent the beauty, culture, and rare treasures of Tanzania on this journey. Just like Tanzanite, Tanzania shines differently.
14/05/2026
WAZIRI MAVUNDE ASIMAMISHA UCHIMBAJI WA MADINI KWENYE MTO MKOANI KATAVI
▪️Ni kutokana na mapungufu ya mpango wa usimamizi wa mazingira
▪️Aelekeza kupewa hati za makosa wamiliki wa Leseni za Utafiti mkoani Katavi
▪️Aelekeza ukaguzi wa mikataba ya msaada wa kiufundi(TSA) nchi nzima
▪️Wachimbaji wadogo wampongeza Rais Samia kwa kupatiwa Leseni tatu kubwa zilizofutwa
▪️Ziara hii ya utatuzi wa migogoro ni maelekezo ya Waziri Mkuu Mwigulu aliyotoa mkoani Katavi
▪️Wachimbaji waishukuru serikali kwa utatuzi wa changamoto zilizokuwa zinawakabili
*Katavi
Kufuatia ukaguzi uliofanywa kwa wamiliki wa leseni wanaofanya uchimbaji kwenye mto na kuathiri mazingira, Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde (Mb) atoa maelekezo ya kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji madini kwenye mto huo Mkoani Katavi.
Ametoa kauli hiyo tarehe 13 Mei, 2026 alipofanya ziara ya ukaguzi wa shughuli za uchimbaji madini katika Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi.
"Mhe. Rais ametupa maelekezo mahsusi Wizara ya Madini kuhakikisha shughuli zote za uchimbaji zinafanyika kwa mujibu wa Sheria na zisilete athari kwenye mazingira. Tumeshuhudia sote kinachofanyika hapa ni kinyume na matakwa ya Sheria yetu ya Madini Sura 123"
"Hivyo, naelekeza kuanzia leo shughuli zote za uchimbaji zisimame mpaka pale mtakapotekeleza wajibu wenu k**a mlivyoelekezwa na Afisa Madini Mkazi wa Katavi kupitia barua aliyowaandikia. Pia, wamiliki wa leseni wasilisheni mpango wa kuhifadhi mazingira kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji tena", alisisitiza Waziri Mavunde.
Vilevile, Waziri Mavunde alifanya ukaguzi wa mikataba ya msaada wa kiufundi (TSA) waliyoingia wachimbaji wadogo wa kitanzania na wawekezaji wa nje na kubaini mapungufu ambayo yalipelekea kuagiza Ofisi za Afisa Madini Wakazi wa Mikoa ya kimadini kufanya ukaguzi wa mikataba ya TSA nchi nzima ili kubaini iwapo inawanufaisha watanzania na inazingatia matakwa yaliyowekwa kisheria.
Akieleza utatuzi wa changamoto ya ukosefu wa maeneo ya uchimbaji, Mhe. Mavunde alitoa maelekezo kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini kutoa Hati ya Makosa (Default Notice) kwa wamiliki wote wa leseni za utafiti wasioendeleza na kufuata masharti ya leseni.
13/05/2026
SERIKALI YAITAKA MANTRA IANZE UZALISHAJI WA URANIUM KWA WAKATI
Ajira zaidi ya 4,000 zanukia Namtumbo, kaya 21,000 kunufaika
📍 Dodoma
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ametoa wito kwa Kampuni ya Mantra Tanzania Limited kuhakikisha inaanza uzalishaji wa madini ya uranium kwa wakati ili Watanzania waweze kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotarajiwa kutokana na mradi huo mkubwa wa kimkakati.
Dkt. Kiruswa ametoa kauli hiyo leo Mei 13, 2026 jijini Dodoma alipokutana na kufanya kikao na viongozi wa Kampuni ya Mantra Tanzania, inayotekeleza Mradi wa Mkuju River Uranium Project uliopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
Dkt. Kiruswa alikumbusha kuwa mwezi Julai mwaka 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizindua kiwanda cha majaribio cha kusindika uranium cha Mantra Tanzania, hatua iliyolenga kujaribu teknolojia ya usindikaji pamoja na kukusanya taarifa muhimu kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha uzalishaji.
Aidha, amesema Serikali haina mpango wa kufuta leseni kubwa ya uchimbaji wa uranium iliyotolewa kwa kampuni hiyo, huku akiitaka kuongeza kasi ya kutafuta mtaji ili shughuli za uzalishaji ziweze kuanza kwa wakati uliopangwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania Limited, Ilya Shchukin, amesema kampuni hiyo ipo katika hatua za mwisho za kutafuta mtaji kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mgodi na kiwanda kikubwa cha usindikaji wa uranium.
Amesema Mantra inaendelea na mazungumzo na taasisi mbalimbali za kifedha kutoka Urusi pamoja na taasisi za fedha za Tanzania ikiwemo Benki ya CRDB na Benki ya NMB ili kufanikisha upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa mradi huo.
Shchukin amesema changamoto kubwa iliyopo ni muda wa leseni ya uchimbaji unaotarajiwa kuisha muda wake Aprili mwaka 2028, hali inayosababisha ugumu kwa baadhi ya taasisi za fedha kutoa mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya mradi huo.
Akizungumzia manufaa ya mradi huo kwa wananchi, amesema zaidi ya ajira 4,000 za moja kwa moja zinatarajiwa kuundwa kwa wakazi wa Namtumbo na maeneo jirani, huku zaidi ya kaya 21,000 zikitarajiwa kunufaika kupitia mnyororo wa thamani wa shughuli za mradi huo.
13/05/2026
🌍 WEKEZA NJOMBE — KITOVU KIPYA CHA UWEKEZAJI WA MADINI TANZANIA
📍 Njombe, Tanzania
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Madini inawakaribisha wawekezaji wa ndani na kimataifa kutumia fursa adimu zilizopo katika sekta ya madini Mkoa wa Njombe — eneo lenye utajiri mkubwa wa madini ambao bado haujaendelezwa kikamilifu.
Tathmini za kijiolojia zimebainisha uwepo wa rasilimali mbalimbali za madini katika wilaya za Njombe, Ludewa, Makete na Wanging’ombe, zikiwa na uwezo mkubwa wa kibiashara na viwanda.
⛏️ Fursa za Uwekezaji Zinazopatikana
✅ Utafiti wa Madini (Exploration)
✅ Uwekezaji katika Uchimbaji Madini
✅ Uanzishaji wa Viwanda vya Uchenjuaji na Uchakataji
✅ Uongezaji Thamani wa Madini (Value Addition)
✅ Ubia na Ushirikiano wa Kimkakati
💎 Madini Yanayopatikana Njombe
• Chuma — Uzalishaji wa chuma na ujenzi wa miundombinu
• Manganese — Utengenezaji wa chuma na teknolojia za betri
• Tantalite — Simu, kompyuta na vifaa vya kisasa vya kiteknolojia
• Dhahabu — Biashara ya kimataifa na akiba ya kifedha
• Madini Adimu (Rare Earth Elements) — Magari ya umeme, nishati jadidifu na teknolojia za kisasa
• Shaba — Nishati jadidifu, nyaya za umeme na viwanda
• Makaa ya Mawe — Uzalishaji wa nishati na shughuli za viwanda
• Vito vya Thamani na Amazonite — Soko la kimataifa la mapambo
• Blue Marble — Ujenzi na mapambo ya kisasa ya majengo
• Mica — Elektroniki, insulation na vipodozi
📈 Kwa Nini Uwekeze Njombe?
✔ Utajiri mkubwa wa madini ambao bado haujaendelezwa
✔ Mazingira rafiki ya uwekezaji
✔ Sera thabiti za Serikali katika sekta ya madini
✔ Fursa kubwa za kuongeza thamani ya madini nchini
✔ Ukuaji wa viwanda na miundombinu
✔ Faida kubwa za uwekezaji wa muda mrefu
🤝 Dhamira ya Serikali
Uwekezaji katika Mkoa wa Njombe utaongeza ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda, kuongeza mapato ya Serikali na kuiweka Tanzania katika nafasi imara kwenye mnyororo wa thamani wa madini duniani.
“Tunawakaribisha wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza katika utafiti, uchimbaji na uongezaji thamani wa madini kutumia fursa zilizopo Mkoa wa Njombe.”
🌐 WEKEZA SASA TANZANIA
📩 Wasiliana na: Tume ya Madini
🌍 www.tumemadini.go.tz
13/05/2026
BAADA YA NUSU KARNE, LIGANGA NA MCHUCHUMA SASA KUANZA
Mazungumzo na Mwekezaji Yamefikia Zaidi ya Asilimia 90
Kuzalisha Tani Milioni 2.9 za Chuma Ghafi kwa Mwaka
Kuzalisha Ajira Rasmi 6,500, Zisizo Rasmi 26,000
📍 Njombe
Serikali ya Tanzania ndani ya kipindi cha Miezi Mitatu ijayo inatarajiwa kuanza rasmi utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Liganga na Mchuchuma wenye uwekezaji wa Dola za Marekani Bilioni 2 hadi 3 baada ya mazungumzo kati ya Serikali na Mwekezaji kufikia zaidi ya asilimia 90.
Hayo yalibainishwa Mei 9, 2026 na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Shamba la Parachichi la Havira Farm Mkoani Njombe, pembeni mwa Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini, kinachotumika k**a sehemu ya tathmini na kujipanga.
Alisema hatua hiyo inaashiria mwanzo wa utekelezaji wa mradi huo uliosubiriwa kwa miaka mingi ukitarajiwa kuongeza mapato ya Seikali, ajira kwa wananchi, kukuza sekta ya viwanda vya chuma na ustawi wa jamii inayozunguka mradi na taifa.
Aliongeza kwamba, mradi huo unatarajiwa kuzalisha tani milioni 2.9 za chuma ghafi kwa mwaka pamoja na tani milioni 1.1 za bidhaa za chuma kwa mwaka, huku ukitarajiwa kutoa zaidi ya ajira rasmi 6,500 na ajira zisizo rasmi zipatazo 26,000
‘’ Katika kipindi cha miaka 25 ya kwanza ya mradi, jumla ya mapato ya dola za Marekani 1,990,489,585,000 zinatarajiwa kupatikana ambapo kwenye miradi ya makaa ya mawe kiasi cha dola za Marekani 92,593,820; uchimbaji chuma kiasi cha dola za Marekani 910,781,519 na kiwanda cha chuma kiasi cha dola za Marekani 987,114,246,’’ alisema Msigwa.
Pia, aliongeza kwamba utekelezaji wa mradi huo utahusisha ujenzi wa msongo wa umeme wa Kilovoti 220 kati ya mchuchuma na na liganga na barabara kutoka Mchuchuma na Liganga ukiwemo mgodi wa makaa ya mawe mchuchuma wenye uwezo wa kuzalisha tani milioni 3 kwa mwaka na Kituo cha kufua umeme kwa megawati 600.
Msigwa alisema tayari Serikali imelipa zaidi ya shilingi bilioni 15 za fidia kwa wananchi ili kupisha utekelezaji wa mradi huo, hatua inayoonesha dhamira ya Serikali
12/05/2026
WAKURUGENZI WAPYA BODI YA STAMICO WAANZA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MADINI KANDA YA ZIWA
📍 Geita
Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imeanza ziara ya kukagua miradi ya Shirika hilo katika Kanda ya Ziwa kwa lengo la kujionea maendeleo ya utekelezaji wa shughuli za uchimbaji pamoja na uendeshaji wa miradi hiyo.
Ziara hiyo inalenga kuwapa wajumbe wa bodi nafasi ya kuifahamu kwa undani miradi inayosimamiwa na STAMICO, namna inavyoendeshwa pamoja na kufuatilia utekelezaji wa maazimio yaliiyoachwa na bodi iliyopita
Wajumbe hao walianzia ziara yao katika Kituo cha Mfano cha Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Dhahabu cha Lwamgasa, ambacho hutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mjumbe wa Bodi ya STAMICO, Bw. Leonard Chacha, alisema kituo hicho kimekuwa na mchango mkubwa katika kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo kupitia elimu ya uchimbaji wa kisasa unaozingatia afya, usalama kazini na utunzaji wa mazingira.
Alisema mbali na mafunzo ya uchimbaji, wachimbaji hao pia huwezeshwa kutumia mashine na teknolojia za kisasa katika uchenjuaji wa dhahabu ili kuongeza tija na kupunguza upotevu wa madini pamoja na athari kwa mazingira.
Baadaye wajumbe hao walitembelea Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef unaoendeshwa kwa ubia kati ya STAMICO na kampuni ya TRX Gold Corporation, ambako walipata taarifa ya utekelezaji wa mradi huo pamoja na kukagua shughuli mbalimbali za uzalishaji ku kuanzia uchimbaji hadi uchenjuaji wa madini.
Bodi hiyo pia ilieleza kuridhishwa na kiwango cha utunzaji wa mazingira katika mgodi huo na kupongeza uongozi wa Buckreef kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha shughuli za uchimbaji haziathiri mazingira yanayouzunguka eneo la mradi.
Kwa niaba ya wajumbe wengine wa bodi, Bw. Wilson Mutagwaba alisema ameridhishwa na hatua zinazochukuliwa katika mgodi huo, hususan katika eneo la usalama kazini.
“Tumefurahishwa kuona suala la usalama limepewa kipaumbele kikubwa na wafanyakazi wote wanaafuata taratibu za usalama kwa umakini,” alisema Mutagwaba.
Bodi ya Wakurugenzi ya STAMICO imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kuhakikisha miradi ya shirika hilo inaleta tija.