Tume ya Madini

Tume ya Madini

Share

Ukurasa Rasmi wa Tume ya Madini Tanzania | The Official Account of Tanzania Mining Commission.

Photos from Tume ya Madini's post 14/05/2026

SHINYANGA YAPAA KWA UCHIMBAJI WA DHAHABU NA ALMASI, YAVUTIA UWEKEZAJI WA VIWANDA

Shinyanga

Mkoa wa Shinyanga umeendelea kuimarisha nafasi yake k**a kitovu muhimu cha sekta ya madini nchini, huku uchimbaji wa dhahabu na almasi ukitajwa kuwa nguzo kuu ya ukuaji wa uchumi wa mkoa huo na chanzo kipya cha fursa za uwekezaji katika viwanda vya kuongeza thamani ya madini.
, amesema mkoa una fursa kubwa za uwekezaji katika viwanda vya utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na almasi ikiwemo vito vya thamani na mapambo, hatua itakayoongeza thamani ya madini ndani ya nchi na kuimarisha uchumi wa viwanda.

Mhandisi Odera ameongeza kuwa uwepo wa malighafi za kutosha k**a chokaa umeifanya Shinyanga kuwa eneo lenye uwezo mkubwa wa uwekezaji katika viwanda vya saruji, vitakavyosaidia kukuza sekta ya ujenzi, kuongeza ajira na kuimarisha maendeleo ya kijamii.

13/05/2026

*BAADA YA NUSU KARNE, LIGANGA NA MCHUCHUMA SASA KUANZA*

*Mazungumzo na Mwekezaji Yamefikia Zaidi ya Asilimia 90*

*Kuzalisha Tani Milioni 2.9 za Chuma Ghafi kwa Mwaka*

*Kuzalisha Ajira Rasmi 6,500, Zisizo Rasmi 26,000*

📍 Njombe

Serikali ya Tanzania ndani ya kipindi cha Miezi Mitatu ijayo inatarajiwa kuanza rasmi utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Liganga na Mchuchuma wenye uwekezaji wa Dola za Marekani Bilioni 2 hadi 3 baada ya mazungumzo kati ya Serikali na Mwekezaji kufikia zaidi ya asilimia 90.

Photos from Tume ya Madini's post 12/05/2026
Photos from Tume ya Madini's post 07/05/2026

NJOMBE YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

📍Njombe

Mkoa wa Njombe umetangaza rasmi fursa mpya za uwekezaji katika sekta ya madini baada ya kubainika kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali za madini ambazo bado hazijatumika ipasavyo, huku wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wakialikwa kuwekeza katika utafiti, uchimbaji na uongezaji thamani wa madini hayo.

Wito huo umetolewa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Lucas Mlekwa, wakati akizungumza katika mahojiano maalum na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma cha Tume ya Madini kinachoshiriki Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini kinachoendelea mkoani humo.

Mhandisi Mlekwa amesema tathmini za kitaalam zinaonesha kuwa wilaya za Njombe, Ludewa, Makete na Wanging’ombe zina utajiri mkubwa wa madini yenye thamani ya kiuchumi, licha ya mengi yake kutokuwa yameendelezwa kikamilifu.

Ametaja madini hayo kuwa ni pamoja na chuma, yanayotumika katika uzalishaji wa chuma cha pua na ujenzi wa miundombinu; manganese, muhimu katika utengenezaji wa chuma na teknolojia za kisasa za betri; pamoja na tantalite, madini mkakati yanayotumika katika vifaa vya kielektroniki k**a simu za mkononi, kompyuta na vifaa tiba.

Aidha, amesema mkoa huo una vito mbalimbali vinavyotumika katika mapambo ya thamani, marumaru ya bluu kwa ajili ya ujenzi na mapambo ya majengo, pamoja na jiwe la amazonite linalohitajika katika soko la kimataifa la vito.

Madini mengine yaliyopo ni mica inayotumika katika vifaa vya umeme, teknolojia na vipodozi; shaba inayotumika katika mifumo ya umeme, nishati jadidifu na mashine za viwandani; pamoja na makaa ya mawe yanayochangia uzalishaji wa nishati na shughuli za viwanda.

Mhandisi Mlekwa pia amebainisha uwepo wa dhahabu, mojawapo ya madini muhimu ya biashara na akiba ya kifedha duniani, pamoja na madini adimu (rare earth elements) yanayotumika katika teknolojia za kisasa ikiwemo magari ya umeme, mitambo ya kuzalisha umeme wa upepo, smartphones na viwanda vya teknolojia ya juu.

Photos from Tume ya Madini's post 07/05/2026

NJOMBE UNVEILS VAST UNTAPPED MINERAL WEALTH, INVITES GLOBAL INVESTORS

📍Njombe

Njombe Region has officially opened investment opportunities in its largely untapped mineral sector, with authorities inviting local and international investors to participate in exploration, mining and mineral value addition initiatives aimed at accelerating economic growth and industrial development.

The call was made by Njombe Resident Mines Officer, Engineer Lucas Mlekwa, during an exclusive interview with the Public Relations and Communication Unit of the Mining Commission participating in the 21st Working Session for Government Information, Communication, Protocol and Public Relations Officers currently taking place in Njombe.

Engineer Mlekwa said recent assessments indicate that the region is richly endowed with diverse mineral resources located in Njombe, Ludewa, Makete and Wanging’ombe districts, many of which remain underdeveloped despite their strong commercial potential.

He identified iron ore, used in steel production and infrastructure development; manganese, vital for steel manufacturing and modern battery technologies; and tantalite, a strategic mineral used in electronic devices including mobile phones, computers and medical equipment.

The region also hosts valuable gemstones for jewellery markets, blue marble used in construction and architectural finishing, and amazonite, an ornamental gemstone attracting international demand.

Other minerals include mica, widely applied in electrical insulation, electronics and cosmetic industries; copper, essential for electrical wiring, renewable energy systems and industrial machinery and coal, which supports energy generation and industrial processing.

Engineer Mlekwa further revealed the presence of gold, a key export mineral used in jewellery and financial reserves, alongside rare earth elements, which are increasingly critical for advanced technologies such as electric vehicles, wind turbines, smartphones and high-tech manufacturing.

“We invite investors interested in exploration programmes, mining operations, value addition and partnerships to take advantage of the available opportunities in Njombe Region,” he said.

05/05/2026

*Tanzanite ya Tanzania Yang’ara kwenye Jukwaa la Met Gala 2026 Jijini New York*✨

📍 New York, Marekani

Mwonekano wa kipekee wa bilionea kutoka India, Sudha Reddy, katika Met Gala 2026 umeiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa ya vito vya thamani. Akiwa amevalia mkufu wa tanzanite wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 15 (sawa na zaidi ya TSh bilioni 39), uliobeba jiwe adimu la karati 550 lijulikanalo k**a “Queen of Mererani” kutoka Mererani Hills, dunia imeshuhudia uzuri na thamani ya rasilimali za Tanzania katika kiwango cha juu kabisa.

Katika tukio hilo lililofanyika Jumatatu, Mei 4, Metropolitan Museum of Art jijini New York, mfanyabiashara huyo mwenye makazi yake Hyderabad, India na umri wa miaka 47 alijitokeza kwenye jukwaa kubwa zaidi la mitindo duniani.

Hata hivyo, kivutio kikuu cha mwonekano wake kilibaki kuwa mkufu huo wa kihistoria wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 15.

đź’Ž Kito hiki kinabeba ujumbe mkubwa kutoka Tanzania: madini si rasilimali tu, bali ni simulizi, urithi na fursa ya kimataifa.

🔹 Tanzanite inaendelea kuthibitisha nafasi yake k**a jiwe la kipekee duniani
🔹 Tanzania ina nafasi ya kimkakati katika soko la vito vya thamani duniani

Huu ni ushahidi kuwa Sekta ya Madini inaweza kuwa chachu ya uchumi, ubunifu na utambulisho wa taifa kimataifa.

,The Home of Tanzanite
Luxury Investment ValueAddition

Photos from Tume ya Madini's post 03/05/2026

TANZANIA YAANZA ENZI MPYA UZALISHAJI WA HELIUM DUNIANI*

*Yajipanga Kubeba Suluhu ya Uhaba wa Gesi hiyo Duniani*

*Helium One Global Yasema Akiba ya Songwe ina Thamani Kubwa Kijiolojia*

*Mradi Kuanza Kutekelezwa baada ya Miezi 18, Zaidi ya Dola Milioni 60 tayari Zimewekezwa*

*Serikali Kumiliki Asilimia 17 ya Hisa kupitia Kampuni ya Ubia ya Songwe Helium Limited*

📍*Songwe*

Tanzania imeanza rasmi Safari Mpya ya Kihistoria ikiingia kwenye ramani ya dunia k**a Mzalishaji na Msambazaji wa kimkakati wa Gesi ya Helium. Hatua hiyo inafuatia baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Uchimbaji wa gesi hiyo baina ya Serikali na kampuni ya Helium One Global Limited kupitia Kampuni ya Ubia ya Songwe Helium Limited, katika hafla iliyofanyika Mei 2, 2026 Mkoani Songwe.

Photos from Tume ya Madini's post 01/05/2026

WATUMISHI WA TUME YA MADINI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI KITAIFA NJOMBE

📍Njombe

Watumishi wa Tume ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe wameshiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa Mei 1, 2026 katika Viwanja vya Lunyanywi, Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Maadhimisho hayo yanayofunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanahusisha wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali nchini waliokusanyika kuenzi mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya taifa pamoja na kujadili ustawi wao na kuboresha mazingira ya kazi.

Watumishi wa Tume ya Madini wameshiriki katika maandamano rasmi pamoja na taasisi nyingine za umma na binafsi, wakionesha mshik**ano wa wafanyakazi wa Sekta ya Madini katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza uchumi kupitia rasilimali madini.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu isemayo, “Kazi zenye staha ni nguzo imara kwa maendeleo endelevu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050,” imelenga kuhamasisha ajira zenye heshima, kulinda haki za wafanyakazi na kuimarisha mchango wao katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya muda mrefu ya nchi.

Maadhimisho ya Mei Mosi hufanyika kila mwaka duniani kote k**a jukwaa la kutambua mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kuhimiza mazingira bora na salama ya kazi.

29/04/2026
Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Mining Commission HQ
Dodoma

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 07:30 - 17:00
Thursday 08:00 - 15:30
Friday 08:00 - 15:30