03/10/2025
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania- ALAT
Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) ilianzishwa rasmi tarehe 13 Disemba 1984 kufuatia kuanzishwa upya kwa mfumo wa Serikali za Mitaa mwaka 1982.
03/10/2025
28/04/2024
Mchengerwa ahimiza ALAT kutatua migongano Serikali za Mitaa
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wamehimizwa kuitumia Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kutatua mivutano na migongano inayojitokeza baina ya Wakurugenzi wa halmashauri na Wenyeviti na Mameya wa halmashauri ili mivutano hiyo isije kuathiri ustawi wa halmashauri hizo.
Wito huo umetolewa tarehe 23 Aprili, 2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 38 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar.
Amesema kwa kuwa ALAT ni chombo muhimu na pekee kinachowakutanisha watendaji wa halmashauri na waheshimiwa Madiwani, hivyo k**a kuna matatizo madogo madogo yanayojitokeza amewataka Viongozi hao kukitumia chombo hicho ili kuondoa migongano inayoweza kuathiri ustawi wa halmashauri.
“Kumekuwepo na mivutano na migongano kati ya wakurugenzi na madiwani, sote tunajenga nyumba moja tunavutana nini huko?” amehoji Mhe. Mchengerwa na kuongeza:
“kila mara mnawaazimia wakurugenzi, k**a kuna matatizo madogo madogo, tumieni chombo chetu cha ALAT ili kuweza kuleta suluhu na kuwasaidia watanzania katika maeneo yetu.”
Amesisitiza: “pale ambapo mnaona pana hitilafu tumieni ALAT, fikisheni malalamiko yenu kule, pelekeni maoni na mimi na Mwenyekiti wa ALAT tunazungumza mara kwa mara, na mara ya mwisho tulipokutana na k**ati tendaji tumezungumza kwa kina na baadhi ya mambo tumeanza kuyafanyia kazi.”
Kuhusu ukusanyaji mapato Waziri Mchengerwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha risiti zinatolewa kwa kila muamala ili kuzuia upotevu wa mapato.
Aidha Waziri Mchengerwa amesema kuanzia mwaka ujao wa fedha kigezo cha ziada cha kuzipima Halmashauri zote nchini ni kwa kila Halmashauri inapaswa kubuni vyanzo vipya vya mapato kuanzia viwili na kuendelea kwa kila mwaka wa fedha.
Mambo mengine aliyosisitiza Mhe. Waziri kuwa ni pamoja na Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa wanasikiliza kwa makini kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, na wasisubiri viongozi wa ngazi ya kitaifa watembelee halmashauri hizo ndipo wazipatie ufumbuzi kero zao.
Mapema Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Sima Constantine Sima amemweleza Mhe Mchengerwa changamoto mbalimbali zinazozikabili Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo changamoto ya umbali kutoka baadhi ya halmashauri kwenda katika bohari za serikali kwa ajili ya kuweka mafuta jambo linalosababisha magari ya serikali kutembea umbali mrefu kufuata mafuta katika bohari hizo.
Mkutano huo unaotarajiwa kukamilika tarehe 25 Aprili, 2024 unawakutanisha washiriki 600, wakiwemo Wastahiki Mameya wa Majiji na Manispaa, Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri, na Wakurugenzi wa Halmashauri zote 184 za Tanzania Bara na Viongozi wengine wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Jambo Letu; Shiriki kwa Maendeleo ya Taifa”
Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt Hussein Mwinyi anatarajia kufunga Mkutano huo tarehe 25 Aprili, 2024.
28/04/2024
Matukio mbalimbali wakati wa Mkutano Mkuu wa 38 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ALAT uliofanyika katika ukumbiwa Golden Tulip mjini Zanzibar kuanzia tarehe 23 aprili hadi 25 april 2024
02/05/2023
02/05/2023
Viongozi ALAT wapongeza utekelezaji Miradi Manispaa Iringa
Na Peter Joseph, Iringa
Uongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) umepongeza ubora wa miradi ya kijamii ambayo imetekelezwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Salim Abri Asas katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi na watendaji wa ALAT kabla ya kumtunukia tuzo ya cheti MNEC huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe.Sima Constantine Sima amesema ALAT imempatia tuzo hiyo kutokana na kuthamini kazi kubwa ya kujitolea aliyoifanya ya kufadhili miradi mbalimbali katika halmashauri za mkoa wa Iringa.
Miongoni mwa miradi iliyofadhiliwa na ASAS ni pamoja na ile ya elimu, afya na ujenzi wa soko la wafanyabiashara wadogo wadogo katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa,
Mbali na kutoa fedha za ufadhili wa miradi Makamu Mwenyekiti huyo amesema wao k**a wasimamizi wa halmashauri zote 184 nchini kuna kitu wamejifunza baada ya kuitembelea miradi hiyo na kujionea ubora wa miradi hiyo.
Amesema utekelezwaji mzuri wa miradi hiyo uliofanywa na ASAS umewapa somo Viongozi wa ALAT kuhusu usimamizi wa fedha za miradi ya halmashauri wanazoziongoza.
“Mbali na msaada unaotolewa lakini ‘standard’ ya miradi inayotekelezwa, kuna kitu kikubwa cha kujifunza sisi k**a wasimamizi wa halmashauri,” amesisitiza Mhe. Sima na kuongeza:
“Mradi unatekelezwa lakini katika kiwango chenye ‘standard’ kubwa ambacho hata sisi (wasimamizi wa halmashauri) tungepewa ufanywe chini ya usimamizi wetu wenyewe tusingeweza kufanya kitu k**a kile,” amesema.
Makamu Mwenyekiti huyo wa ALAT Taifa ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza amesema kuwa anapoona miradi ikitekelezwa na mdau k**a ASAS katika utimilifu kuliko k**a ingesimamiwa na halmashauri, anaamini kuwa ipo haja kwa viongozi wa halmashauri kuongeza uwajibikaji ili kuleta ufanisi katika miradi inayosimamiwa.
Mojawapo ya mradi uliomvutia Makamu Mwenyekiti huyo wa ALAT ni mradi wa ujenzi wa soko la wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu k**a ‘wamachinga’ ambapo amekiri kuwa kukosekana kwa miundombinu muhimu inayotumiwa na wafanyabiashara hao k**a kuwepo kwa vibanda kwa ajili ya vivuli na vyoo ni changamoto kubwa kwa majiji sita nchini.
“Agizo la Mhe Rais (Samia Suluhu) lilikuwa twende tukawapange lakini swali muhimu tunapaswa kujiuliza sisi viongozi wa halmashauri ni wapi tukawapange wamachinga,” amesema Mstahiki Sima na kuongeza:
“Sisi pale Mwanza kuna sehemu tulikuwa na dampo pale tuliwapeleka wafanyabiashara hao kule lakini kesho yake walirudi mjini, kwa sababu tulikosa mtu wa kutusaidia kufanya reconciliation (upatanisho) k**a alivyofanya ASAS hapa Iringa.”
Amesema kuwapatia miundombinu wanayoyahitaji wamachinga ndiyo jambo kuu la msingi kabla ya kuwapeleka wafanyabiashara wadogo wadogo kwenye maeneo yaliyotengwa na halmashauri.
Amesema haina maana kwa viongozi wa halmashauri kupanga kutumia mathalani shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuweka mafuta kwenye magari na kuwatumia Mgambo na Maaskari ili kuwatoa wamachinga katikati ya miji wakati halmashauri zinashindwa kutumia walau shilingi laki tano kujenga vibanda na vyoo kwa ajili ya kuwawezesha Wamachinga hao kuendesha shughuli zao katika mazingira rafiki.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada aliitaja baadhi ya miradi iliyofadhiliwa na ASAS katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwa ni pamoja na ukarabati wa jengo la ofisi ya Mstahiki Meya kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 150, na Jengo la ustawi wa jamii lililogharimu zaidi ya milioni 60.
Miradi mingine ni mradi wa soko la wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu k**a wamachinga ambalo liligharimu zaidi ya shilingi milioni 220 kwa ajili ya ujenzi wa vibanda, vyoo na eneo la soko la matunda.
Kwa upande wake Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Taifa aliwashukuru viongozi wa ALAT kwa kuthamini juhudi alizozifanya katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa na kuahidi kuendelea kushirikiana na Viongozi wa Jumuiya hiyo katika kusukuma gurudumu la maendeleo la Manispaa ya Iringa.
Amesema ziara ya viongozi wa ALAT imempa hamasa ya kuendelea kujitolea na imemuongezea wadau na kuahidi kushirikiana na ALAT katika shughuli zao.
07/03/2023
Kaimu Katibu Mkuu ALAT TAIFA Bw. Mohamed Maje akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mikakati na vipaumbele vya Jumuiya hiyo mara baada ya kukamilika kwa kikao cha k**ati tendaji kilichofanyika tarehe 7 machi, 2023 jijini Dodoma
16/08/2020
Katibu Mkuu ALAT akagua miradi ya maendeleo Mwanza Katibu Mkuu Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Elirehema Kaaya amekagua wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na ku...
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Dodoma
P.OBOX2049
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 15:30 |
| Tuesday | 07:30 - 15:30 |
| Wednesday | 09:00 - 15:30 |
| Thursday | 07:30 - 15:30 |
| Friday | 07:30 - 15:30 |

25/06/2020