Cma Tanzania

Cma Tanzania

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Cma Tanzania, Government Organization, CMA Headquarters, 3 Zimamoto Street, 41102 Viwandani, Dodoma.

07/04/2026

Mkurugenzi, Menejimenti na Watumishi wote wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) tunaungana na Watanzania wote katika Maadhimisho ya Miaka 54 ya Kumbukizi ya kifo cha Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


05/04/2026

Mkurugenzi,Menejimenti na Watumishi wote wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) tunawatakia Wakristo wote na Watanzania kwa ujumla Heri ya Sikukuu ya Pasaka.

Tunapoadhimisha ufufuko wa Bwana Yesu Kristo, tuyakumbuke na kuyaenzi mafundisho na matendo yake ya huruma, upendo, msamaha na kujitoa kwa ajili ya wengine.

Pasaka hii itukumbushe umuhimu wa kudumisha amani, kuimarisha umoja na mshik**ano wa kitaifa, ili tuendelee kujenga Taifa lenye fursa kwa wote, ustawi na maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho






tanzania

tanzania

03/04/2026

Tunawatakia Ijumaa Kuu njema.

26/03/2026

Mkurugenzi, Menejimenti na Watumishi wote wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) tunaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kwa ujumla kuomboleza kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe. William V. Lukuvi kilichotokea Machi 25, 2026 jijini Dodoma.

"Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe"



sbu

20/03/2026

Mkurugenzi, Menejimenti na Watumishi wote wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), tunawatakia Waislamu wote na Watanzania kwa ujumla Sikukuu njema ya Eid Al-Fitr.

Tuyaishi na kuyaendeleza mema yote tuliyojifunza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, upendo, huruma na kusaidiana, ili kuimarisha maadili na mshik**ano katika jamii zetu.

Tusherehekee kwa utulivu, tukidumisha umoja na kulinda amani ya nchi yetu, kwa kuwa amani ndio msingi wa ustawi na maendeleo ya Taifa letu.



19/03/2026

ZIARA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA USTAWI NA MAENDELEO YA JAMII KATIKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)

Photos from Cma Tanzania's post 19/03/2026

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA MAFANIKIO YA MFUMO wa e-Utatuzi

Na Mwandishi - CMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kuanzishwa kwa Mfumo e-Utatuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambao umeongeza ufanisi katika usimamizi wa mashauri ya migogoro ya kazi nchini.

Pongezi hizo zimetolewa Machi 18, 2026 wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mfumo huo ambapo imeelezwa kuwa idadi kubwa ya mashauri yaliyosajiliwa tangu mfumo huo uanze imeongezeka mara mbili zaidi ikilinganishwa na hapo awali.

"Tija ya mfumo tumeiona ni mara mbili ya kile kilichokuwa kinafanyika mara ya kwanza, ubora wa Mfumo umekuwa mara mbili yake" amesema Mwenyekiti wa k**ati hiyo.

Aidha ameongeza mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea ukuaji wa uchumi, kwani wafanyakazi na waajiri hawatalazimika tena kupoteza muda mwingi kwenye foleni au kufuatilia kesi zao kwa kusafiri umbali mrefu, badala yake watasajili na kufauatilia mashauri yao popote walipo na wakati wowote.

Awali akizungumza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe.Rahma Kisuo amemshukuru Mhe. Rais kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa mwaka jana katika Maadhimisho ya ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ya kuanzisha mfumo huo ambao umesaidia kutatua changamoto zilizopelekwa kwake za Wananchi na Waajiri kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za Tume, Kupoteza muda na gharama kufuatilia haki, Mrundikano wa Mashauri na ucheleweshaji haki na huduma za Tume kukosekana katika baadhi ya Wilaya ambazo hamna ofisi.

Amebainisha kuwa serikali ilikuja na mfumo huo k**a suluhusu ya changamoto tajwa kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa haki mahali pa kazi, kusogeza huduma karibu na wafanyakazi na waajiri ambao ni nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi nchini.

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw. Usekelege Mpulla, amesema kuwa Tume ina mkakati wa kuendelea kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari na majukwaa mengine ili kuongeza uelewa na matumizi ya mfumo huo kwa wafanyakazi na waajiri wengi zaidi.

MWISHO

Photos from Cma Tanzania's post 18/03/2026

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Mchafu, wakipatiwa maelezo kuhusu namna usuluhishi unavyofanyika kupitia mfumo wa e-Utatuzi na Msuluhishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Mhe. Catherine Kalinga, wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mfumo huo, leo Machi 18, 2026, jijini Dar es Salaam.

Mfumo huo unalenga kuongeza ufanisi, uwazi na upatikanaji wa huduma za utatuzi wa migogoro kwa njia ya kidijitali.


tanzania

tanzania


Photos from Cma Tanzania's post 18/03/2026

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Hawa Mchafu, akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa mfumo wa usimamizi wa mashauri ya usuluhishi na uamuzi (e-Utatuzi) jijini Dar es Salaam, Machi 18, 2025.

Mfumo huo ulio chini ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), wenye lengo la kuongeza ufanisi na uwazi katika utatuzi wa migogoro ya kazi nchini ni sehemu ya miradi ya maendeleo iliyotembelewa na Kamati hiyo ya Bunge kwa ajili ya kukagua maendeleo yake.


tanzania

Photos from Cma Tanzania's post 18/03/2026

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa ziara ya ukaguzi wa mfumo wa usimamizi wa mashauri ya usuluhishi na uamuzi (e-Utatuzi), jijini Dar es Salaam, Machi 18, 2025.



Photos from Cma Tanzania's post 18/03/2026

Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Mhe. Usekelege Mpulla, akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mfumo wa usimamizi wa mashauri ya usuluhishi na uamuzi unaotambulika k**a (e-Utatuzi), mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam, Machi 18, 2025.


tanzania
tanzania
@

Photos from Cma Tanzania's post 18/03/2026

HABARI PICHA

Matukio mbalimbali wakati wa ziara ya k**ati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya jamii ,walipotembelea na kukagua mradi wa mfumo wa Usimamizi wa Mashauri ya Usuluhishi na Uamuzi (e-Utatuzi) wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), leo Machi 18,2025 jijini Dar es Salaam.


tanzania
tanzania



Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

CMA Headquarters, 3 Zimamoto Street, 41102 Viwandani
Dodoma